Zinedine
JF-Expert Member
- Apr 9, 2011
- 1,187
- 694
Alichosema Dr Sezibera ni kwamba:
Tukianza na suala la liberalization of current account - makubaliano ni kwamba barriers & restrictions zote on the movement, sale, investment & payments of capital inatakiwa viondolewe; Vile vile kuna makubaliano ‘to remove all discrimination based on the nationality or on the place of residence of the persons or on the place where the capital is invested.' Ni kweli kwamba wenzetu Kenya, Uganda na Rwanda wameshafungulia haya, imebakia Tanzania na Burundi; Lakini pamoja na hayo, makubaliano ilikuwa kwamba Tanzania na Burundi wawe wametekeleza haya katika kipindi cha 2010 – 2015, kwahiyo tusubri tuone nini kitajiri ndani ya miaka miwili ijayo;
Tukija kwenye suala la work permit fees – makubaliano ni kwamba workers kutoka any partner state waruhusiwe kutafuta kazi katika nchi yoyote mwanachama wa EAC; Free movement of labour ni kwenye professions Fulani Fulani, sio professions zote, na professions hizi zipo listed wazi;
That said and done, lazima tuambiane ukweli kwamba pamoja na kwamba Tanzania ilikuwa mstari wa mbele baada ya uhuru kutafuta regional integration, katika kipindi cha hivi karibuni, tumejionyesha kuwa "shy partners'; kwa kweli hatujiamini, hivyo kufanya tusiwe na imani sana na EAC; Kuna vituko kadhaa tumevifanya in the past two years kuashiria kwamba hatuna genuine commitment – mfano kufunga mpaka wetu na Kenya Taveta (2012), kuzuia kuvusha mazao/nafaka kwenda nchi jirani(2011), kupingana na political federation and mutual defense pact (2011), na mahakama kuu Tanzania kuikingia kifua kampuni ya kitanzania (blueline) iliyofisadi;
Mbali ya haya, pengine hali yetu ya kusua sua pia inachangiwa Zaidi na hoja ifuatayo aliyotoa Waziri Mwakyembe mwaka jana wakati wa uchaguzi wa wabunge wa Tanzania to the EAC (Dodoma) ambapo alisema:
Maswali yanayofuatia ni je, ipi ni tafsiri sahihi kati ya hizi:
- Kusua sua kwetu kunatokana na ukweli kwamba suala la EAC integration tulikuwa tunaliendesha kisiasa Zaidi na sasa uchumi unapoanza kupewa prominence na kuanza kupambanishwa na wenzetu (hasa Kenya), tunagundua jinsi gani hatujajiandaa – both on the micro/household level, na pia macro – level, structure of the economy and how it affects the balance of trade kati yetu na wakenya?
- Ni woga wetu to share rasilimali na ardhi ambazo ni nyingi sana kuliko wenzetu?
- Ni ignorance juu ya compromise zinazokuja na regional integration?
Pengine kuna justification katika suala la ardhi, kwani makala moja inatusema kwamba:
Tanzania accounts for about 52% of East Africa's total land area, na ingawa we have the largest population in the region, bado there is is significant land available. Suala hili is both a THREAT and an OPPORTUNITY kwetu sisi katika muktadha wa EAC, na ukweli utaendelea kubakia hivyo;
Mwisho ni suala la passport – uraia – hapa pia tuna sua sua linapokuja suala la common passport tofauti na wenzetu; Katika hili, given given ukweli kwamba almost 33% ya population ya EAC region ipo Tanzania, tunahitaji kuwa waangalifu sana hasa ikizingatiwa kwamba wenzetu wanasukumwa Zaidi na population pressure & shortage of land kuliko chochote – kwa mfano population density Tanzania ipo chini sana ikilinganishwa na Burundi, Rwanda, Kenya na Uganda; we have 47 people per square Kms, the lowest in the regions, huku Uganda na Kenya wakiwa juu Zaidi, na Rwanda na Burundu wakiongoza, 430 & 301, respectively;
Inawezekana sijapanga hoja katika mtiririko mzuri, lakini mniwie radhi, ilikuwa ni suala la haraka haraka tu katika kuchangia hoja; Nitarudi kwa hoja Zaidi……
nakala JokaKuu, Nguruvi3
Mkuu@Machambuzi, wakati naendelea kulipitia kwa ufasaha bandiko lako nimeona hayo masuala niliyoweka red, ambayo nilikuwa na mawazo kama yako ya kuona ni uwoga wa Tanzania. Hata hivyo, nimefanyia utafiti zaidi na kubaini ukweli kadhaa.
1.Mutual Difense Pact: Katika suala hili, Tanzania ilipingana na kifungu kilichokuwa kikisema kwamba iwapo nchi moja ya Afrika Mashariki itaingia kwenye vita na nchi nyingine iliyo nje ya Afrika Mashariki, Nchi zote za Afrika Mashariki zishirikiane na kuchangia nguvu ili kumpiga adui wa mshirika wetu. (Kama mfano wa NATO Pact vile. Utafiti wangu umebaini mambo yafuatayo ambayo nahisi Tanzania ilikuwa right kufanya hivyo (not sure kama ndizo hoja walizotumia hizi ni hoja zangu za kitafiti)
a) Nchi nyingi za Afrika Mashariki yaani Rwanda, Uganda na Kenya haziko kwenye mahusiano mazuri na majirani zao na pia ni 'nchi chokozi kiasili" hivyo kitendo cha kuwa na "alliance" ya namna hii, ni kuongeza kujiamini kwa nchi hizo kuingia kwenye vita wakiamini kwamba nchi nyingine wanachama zita-bear cost ya vita hivyo. Hivyo uwezekano wa Tanzania kuingizwa kwenye vita isiyowahusu ulikuwa ni mkubwa sana iwapo wataridhia/wangeridhia kwa muktadha huu.
b) Tanzani ina mipaka na nchi nyingi ikiwa pamoja na DRC ambayo iko kwenye majaribu ya muda mrefu na Rwanda. Kusani kwa makubaliano haya maana yake ingetokea/ikitokea Rwanda kuingia kwenye vita na Congo DR, automatically, Tanzania ingebidi ishiriki kwenye vita ikipigana upande wa Rwanda na kumpiga Congo DRC, pamoja na kuharibu mahusiano ya kibiashara na Zaire, hii kitu ingetutia matatani kule SADC ambapo nchi kama Congo ni mwana SADC
3. Alliances za kijeshi chini ya muundo wa kikanda zina kawaida ya kusababisha kuenea kwa vita kwa eneo kubwa kama historia inavyotueleza kwenye WWI na WWII. EAC ikiwa na Alliance ya kupigana vita, na ile Jumuiya ya Afrika ya Kati (ikitokea) kuwa na alliance ya kivita, maana yake vita (let say) baina ya Rwanda na Congo ingesababisha vita ya nchi zaidi ya nchi kumi. Ukichukua model hii katika multiplier effect yake, utaona kwamba Bara lote la Afrika linaweza kuingia kwenye vita, just iliyosababishwa na migogoro ya nchi mbili tu. Kwa mfano, kwasasa huenda Tanzania ilipaswa kuwa na vikosi vyake Somalia-sipati picha kungetokea nini.
2. Kuhusu Shirikisho la Kisiasa, ni uroho wa hizo nchi tatu kwa sababu wao wanaamni kwamba, njia rahisi ya kuunda shirikisho ni kuanza na shirikisho lenyewe kisha shirikisho litumike ku-enforce Customs Union, Common Market na Monetary Union; kitu ambacho ni kinyume na Mkataba na pia ni kinyume cha Kanuni zinazotawala Jumuiya za Kiuchumi za Kikanda ambazo sababu zao kubwa ni Biashara wala si utawala na ndio maana zinasajiliwa WTO si Baraza la Usalama la UN.
Nina hakika, hata nawe ukifuatilia haya uta-withdrawa na hizi propaganda kwamba Tanzania ni "sleeping elephant" au "stumbling bloc" katika Jumuiya.
cc Nguruvi3, joka Kuu
Last edited by a moderator: