EAC Chief warns Tanzania on regional Integration

EAC Chief warns Tanzania on regional Integration

UK inatekeleza makubaliano yote ya EU isipokuwa la common currency. Usiwe mwepesi wa kupindisha ukweli.

Hata Tanzania ina mambo yake isiyoyataka, mfano kuingia nchini bila passport na ardhi kumilikishwa au kuuziwa wageni. Lazima muheshimu matakwa ya watanzania.
 
..Dr.Sezirabu kila akitoa tamko ni kuinanga Tanzania tu.

..sijamsikia akizinanga nchi nyingine.

..hatuwezi kuwa na EAC SG ambaye yuko biased against mmoja wa waanzilishi wa jumuiya hiyo.

Una muono kama wa kwangu.
 
.....ni Dr. Richard Sezibera ni Katibu mkuu wa EAC,Tanzania haiwezi kumtimua Dr kwa kuwa yupo kisheria na si mwajiriwa wa serikali ya TZ....
......ana uwezo wa kutuhumu na hata kushitaki mahamani nchi yoyote mwanajumuiya wa EAC pale anapoona haifuati utaratibu
.......Dr sezibera siyo Rwanda...sijajua umetumia nini (kichwa/tumbo)kufikiria na kuandika..."hivi kweli Dr.Seziraba/Rwanda inaweza kuituhumu Tanzania "
.......rwanda wameingiaje katika hizi tuhuma anazotoa katibu mkuu? Chuki zako zinazosababishwa na uelewa mdogo/uvimba macho sidhani kama zinakufanyia haki hata wewe mwenyew maana zinakufanya uonekane mp..umb...avu mbele za watu. mfano Rwanda imeingiaje katika hili?

Chuki walishaanza wasuti na Watuhu wa Rwanda ndio maana walipigana sana.
 
wavuta bangi hao kaka Koba umewasahau?unaona ameishaingiza Rwanda,baadaye kagame,kabla haijafika mwisho hii thread watakuwa wametaja na M23.....chuki itawatafuna wenyewe...

Watu wanapochangia usiwaite watu wavuta bangi! rwanda na uganda lazima itamkwe kwa vile wao ndio vinara wa kuitenga Tanzania.
 
Nafikiri ile fast-track walikuwa wana-shake ili TZ wapanic na ili tz iingizie kichwa kichwa kwa tahamaki. Sasa wamekuta ni unshakable ndo maana sahizi wameanza kutumia watumishi wa eac, maana pale awali walisema sio eac bali ni trio.

Wamekuta Tz ni kisiki cha mpingo. Waliokuja na mashoka walishindwa kuking'oa wao wanakuja na visu?
 
Kwa sababu kama hizi za kutudharau mara kwa mara ndio maana safari hii tunawaonyesha kiburi halisi cha Mtanzania--ardhi hatutoi, kuingia kiubwete ndani ya nchi yetu hakuna na zaidi ya hayo, hatutoki katika EAC na kutufukuza hawana ubavu!!

Big up mkuu. wape vidonge vyao. Maslahi ya Tanzania kwanza EAC baadae.
 
Vipi credentials? Naona unahofia competition kweli.

Ni nani wa kucomepete naye EAC? Uende kenya, uganda, rwanda na burundi Viwango ni vilevile ila tunatofautiana umahiri wa kutoa na kupokea rushwa! Kwa hili wenzetu wako juu.
 
nngu007 Seriously tunamtaka Waziri Sitta ajenge hoja ya kumkataa huyu jamaa kuendelea kuwa SG wa EAC--openly biased fellow! Mbona Juma Mwapachu hakuwa hivi?

soma aya hii "Museveni has also appointed his nephew, Joseph Ekwau (son of his younger sister Violet Kajubiri), Private Secretary to the President in charge of Medical Services (HIV//AIDS); his sister Miriam Karugaba as Administrator at State House (she is semi-literate) and her husband (therefore Museveni’s brother-in-law), Jimmy Karugaba, as Officer in Charge (OC) of the Accounts Department at State House. Museveni has also appointed his sister-in-law, Jolly Sabune, Executive Director of Cotton Development Authority, his niece-in-law, Hope Nyakairu, Undersecretary for Administration and Finance at State House, his cousin Bright Rwamirama, State Minister for Animal Husbandry, his other cousin, Faith Katana Mirembe, Assistant Private Secretary in charge of Education and Social Services and Justus Karuhanga, Private Secretary to the President in charge of Legal Affairs who is a nephew to Mrs Museveni"
sasa kweli hii fast tracking of the east african federation ndo linalenga kuwanufaisha wachache namna hii.Wa tanzania hatukubali kuongozwa na mtu mmoja chini ya kivuli cha familia moja kama hivi ni HATARI SANA KUWA FAMILY DYNASTY KAMAS HII .
 
Kitu nitakachomiss sana kwenye huu muungano ni Nov 1, mapumziko ya EAC. Otherwise hatuna cha kupoteza, watarudi tu.
do! bora umenijulisha nitakuwa napumzika mwenyewe hata kwa ruhusa kiukweli kwangu mimi ni blueband ambayo kiukweli na kilo zangu zilizo zaidi ya 115 sihitaji vinginevyo wao wanatuhitaji zaidi na sio sisi kuwa tunawahitaji na wanalijua hilo na kwa mazingira ya hawa jamaa wa alshabab(sifurahishi na tukio) lnaweza kuwafanya wafanya biashara wasikubali kutegemea kwa asilimia mia moja bandari ya mombasa kwa sababu za kiusalama hivyo bado wanatuhitaji.
kiukweli rwanda wanatuhitaji zaidi kuliko nchi nyingine yoyote iliyopo katika jumuiya hiyo kwa kuwa sisi ni shamba la bibi kwa kuwa ukiwa na tanzania chochote unaweza kufanya ndani ya nchi yao so we need tanzania kwa bei yoyote.
 
wao wasonge huko waendako tanzania ni moja,kwanza mfumo wetu wa maisha na wao upo tofauti,nyie mnao payuka hapa utadhani punda huko mwituni hamjuwi mfumo wa hawa wenzetu hamna mtanzania yoyote anaweza kupewa kazi nchini kenya uganda hata rwanda hata kama unashahada kutoka harvard university,huko hawatizami cv wanatizama ukoo wa mtu au kabila ukija upande wa ardhi huko wamegawana ardhi miaka mingi ambayo imepita hawana ardhi tena wakati nyerere akitaifisha ardhi wao kipindi hicho wanagawana ardhi kama keki ya xmasi leo hii hawana kitu zaidi ya slums kiswahili tunaita mitaa ya mabanda mtu unaweza kwenda hapo nairobi sehemu moja inaitwa kibera watu wanaishi kama mbuzi mazizini hiyo yote inatokana na ukosefu wa ardhi,kama ni bishara mbona mipaka iko wazi wanakuja kufanya hamna mtu ambae anawazuiya,nini kinacho wafanya hawa wenzetu kupayuka kama punda huko mwituni kusipo faida yoyote wao kama wanatuona sisi tunawakawiza wafanye mambo yao waachane na sisi, kipi ambacho wao kinawauma sana mpaka wajifanye wanatuonea huruma,wakwende zao huko bhana hiyo jumuiya kwanza sisi haituhusu kwa sana hivyo.
 
Alichosema Dr Sezibera ni kwamba:



Tukianza na suala la liberalization of current account - makubaliano ni kwamba barriers & restrictions zote on the movement, sale, investment & payments of capital inatakiwa viondolewe; Vile vile kuna makubaliano ‘to remove all discrimination based on the nationality or on the place of residence of the persons or on the place where the capital is invested.’ Ni kweli kwamba wenzetu Kenya, Uganda na Rwanda wameshafungulia haya, imebakia Tanzania na Burundi; Lakini pamoja na hayo, makubaliano ilikuwa kwamba Tanzania na Burundi wawe wametekeleza haya katika kipindi cha 2010 – 2015, kwahiyo tusubri tuone nini kitajiri ndani ya miaka miwili ijayo;

Tukija kwenye suala la work permit fees – makubaliano ni kwamba workers kutoka any partner state waruhusiwe kutafuta kazi katika nchi yoyote mwanachama wa EAC; Free movement of labour ni kwenye professions Fulani Fulani, sio professions zote, na professions hizi zipo listed wazi;

That said and done, lazima tuambiane ukweli kwamba pamoja na kwamba Tanzania ilikuwa mstari wa mbele baada ya uhuru kutafuta regional integration, katika kipindi cha hivi karibuni, tumejionyesha kuwa “shy partners’; kwa kweli hatujiamini, hivyo kufanya tusiwe na imani sana na EAC; Kuna vituko kadhaa tumevifanya in the past two years kuashiria kwamba hatuna genuine commitment – mfano kufunga mpaka wetu na Kenya Taveta (2012), kuzuia kuvusha mazao/nafaka kwenda nchi jirani(2011), kupingana na political federation and mutual defense pact (2011), na mahakama kuu Tanzania kuikingia kifua kampuni ya kitanzania (blueline) iliyofisadi na kukaribia kuifilisi east african development bank (EADB);;

Mbali ya haya, pengine hali yetu ya kusua sua pia inachangiwa Zaidi na hoja ifuatayo aliyotoa Waziri Mwakyembe mwaka jana wakati wa uchaguzi wa wabunge wa Tanzania to the EAC (Dodoma) ambapo alisema:



Maswali yanayofuatia ni je, ipi ni tafsiri sahihi kati ya hizi:


  • Kusua sua kwetu kunatokana na ukweli kwamba suala la EAC integration tulikuwa tunaliendesha kisiasa Zaidi na sasa uchumi unapoanza kupewa prominence na kuanza kupambanishwa na wenzetu (hasa Kenya), tunagundua jinsi gani hatujajiandaa – both on the micro/household level, na pia macro – level, structure of the economy and how it affects the balance of trade kati yetu na wakenya?
  • Ni woga wetu to share rasilimali na ardhi ambazo ni nyingi sana kuliko wenzetu?
  • Ni ignorance juu ya compromise zinazokuja na regional integration?

Pengine kuna justification katika suala la ardhi, kwani makala moja inatusema kwamba:
Tanzania accounts for about 52% of East Africa’s total land area, na ingawa we have the largest population in the region, bado there is is significant land available. Suala hili is both a THREAT and an OPPORTUNITY kwetu sisi katika muktadha wa EAC, na ukweli utaendelea kubakia hivyo;

Mwisho ni suala la passport – uraia – hapa pia tuna sua sua linapokuja suala la common passport tofauti na wenzetu; Katika hili, given given ukweli kwamba almost 33% ya population ya EAC region ipo Tanzania, tunahitaji kuwa waangalifu sana hasa ikizingatiwa kwamba wenzetu wanasukumwa Zaidi na population pressure & shortage of land kuliko chochote – kwa mfano population density Tanzania ipo chini sana ikilinganishwa na Burundi, Rwanda, Kenya na Uganda; we have 47 people per square Kms, the lowest in the regions, huku Uganda na Kenya wakiwa juu Zaidi, na Rwanda na Burundu wakiongoza, 430 & 301, respectively;

Inawezekana sijapanga hoja katika mtiririko mzuri, lakini mniwie radhi, ilikuwa ni suala la haraka haraka tu katika kuchangia hoja; Nitarudi kwa hoja Zaidi……
Mkuu Mchambuzi, ahsante kwa maoni yako.
Hapo juu umeonyesha kuwa miaka miwili Tanzania imekuwa haijiamini. Napenda kukuhakikishia kuwa kutojiamini ni tofauti na kutoaminiana.

Katika miaka zaidi ya mitano Uganda imepiga debe sana kwa Rwanda na Burundi kupewa uanachama kamili. Lengo lilikuwa Rwanda ili kuongeza nguvu katika mambo ''yanayokusudiwa''.

Ushirika wa sasa wa KKK haukuanza leo. NI mkakati mkubwa na Tanzania iliposhtuka ndipo ikaonekana kama haijiamini, ukweli ni kuwa inachukua tahadhari.

Waziri wa ushirikiano wa EAC mh Sitta amefanya kazi na Nyerere, Kenyatta, Obote, Moi na hawa wa sasa.
Hakuna mwenye uzoefu katika integration ya sasa na iliyopita kama yeye.
Huyu Sezibera hana uzoefu wowote labda kama ni kuongoza Genocide.
Hivyo kuna sababu muhimu sana za Tanzania kuchukua tahadhari.

Magazeti ya IPP ya jana yametoa siri kubwa sana inayounga mkono hoja zangu.(Nina nakala nitaweka hapa).
Chanzo cha habari ni cha kauaminika.
Kulikuwa na mpango wa kuunda jeshi la pamoja la EAC.
Taarifa za kuundwa kwa jeshi hilo alikuwa nazo Sezibera bila kujadiliwa na nchi wanachama.

Alichokifanya Sezibera ni kuweka mkakati wa kiuchumi halafu akachomeka kipengele cha jeshi.
Haiwezekani jambo kubwa kama hili lifanyike kihuni kwa kusainiwa na mawaziri bila mjadala wa maana.

Kumbe nyuma ya kifungu hicho kilichofichwa na Sezibera kulikuwa na mkakati wa Kagame na Museveni wa kuunganisha majeshi ili kuzuia majeshi ya Tanzania kuingilia mgogoro wa Congo wenye manufaa kwao.
Tanzania ilipokataa suala hilo likaahirishwa kwasababu maana nzima ilishapotea.
Hoja ilikuwa kuiweka Tanzania on the spot na kuendelea na ajenda zao.

Sasa ninapokuja katika maswali yako,unaposema kusuasua kwetu ni kutojiamini, woga au ignorance si dhani ni sahihi. Vipi kama ni tahadhari inachukuliwa hasa tukizingatia usiri na mkakati wa KKK dhidi ya Tanzania.

Mpango wao wa kujenga vitu kama reli si suala la siku moja ni mpango waliokuwa nao siku nyingi ilipoonekana Tanzania inachukua tahadhari wakaamua kwenda wenyewe kama njia ya kushinikiza.
Nadhani Zinedine #161 ameeleza mambo mengine yanayoshadidia hoja zangu

Kuhusu Tanzania kuchukukia integration kisiasa zaidi kuliko kiuchumi, mimi nadhani wengine ndio wanafanya hivyo.
Huwezi kuwa na nguvu ya kiuchumi bila kuwa na msingi imara wa kisiasa na kinyume chake.
Ni vitu visivyoweza kutengnishwa. Endapo wenzetu wangekuwa na fikra za kiuchumi zaidi kwanini basi wachomeke hoja za majeshi ya pamoja na wala si kuwa na benki kuu ya EAC kwanza?
Hivi hapa si siasa kweli na nani anafanya hivyo?

Leo wenzetu wapo makini kutuburuza tuamini kuwa hatujiamini huku wakiwa na ajenda za mambo kama ardhi, na jeshi ambayo hawayasemi bali wanampa Sezibira aandae vifungu vya siri na kuvichomeka kama sehemu tu ili tutakapokubali suala zima la uchumi basi na yale wanayokusudia tunayakubali.

Hebu tujiulize kwanini Kenya a Uganda walikataa suala la passport za EAC?
Jibu ni simple , passport zingezuia ajenda ya ardhi. Wakaja na ajenda ya vitambulisho kwa mlango wa nyuma.
Sasa Tanzania ikichukua hadhari kwanini ionekane inasuasua au ignorance.
Na hili la ardhi umekubali kuwa linahitaji hadhari ambayo wenzetu wanasema ni waoga wa ushindani.

Nadhani tuangalie nia za wenzetu na kinachoisumbua Tanzania sasa hivi ni kuwa na washirika wasioaminika na wenye nia za siri. Lazima hadhari ichukuliwe vinginevyo tunaweza kuunda EAC yaviongozi na si wananchi tukarudi kule kule kwa 1977.

cc JokaKuu zidane
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom