E. Kezilahabi: Rosa Mistika

MAKOLE

JF-Expert Member
Feb 5, 2012
618
280
Wadau naomba kuuliza, kwa wale wanaopenda kufuatilia kazi za riwaya za Prof. E. Kezilahabi watakuwa wanafahamu riwaya ya Rosa Mistika. Nimekisoma sana kitabu hiki ila sifahamu ni kwa nini serikali ya Tanzania ilikipiga marufuku kitabu hiki kusomwa. Noambeni maelezo kwa mwenye kufahamu.
 
nimekisoma huko, na hata sasa ninakisoma hapa ninapokuandikia hii sms, lakini sijui sababu ya kupigwa marufuku,

Mkuu hauna Soft Copy unipe,?

By the way, hicho kitabu kilipigwa marufuku kwa sababu inasemekana kilikuwa kinaukashifu ukatoliki,
hasa huyo Rosa anafananishwa na Maria mtakatifu,

Pia riwaya hiyo inaakisi maisha ya viongozi wetu wanavotumia madaraka na fedha kuwanyanyasa wasichana...
Ndipo Rungu likapita na kitabu kikapigwa marufuku
 
Kimeegemea kukashfu dini za watu na c unajua alichokifanya mkuu wa wilaya?nafkr ndo wakapga marufuku kiligusa tabaka tawala
 
Wadau naomba kuuliza, kwa wale wanaopenda kufuatilia kazi za riwaya za Prof. E. Kezilahabi watakuwa wanafahamu riwaya ya Rosa Mistika. Nimekisoma sana kitabu hiki ila sifahamu ni kwa nini serikali ya Tanzania ilikipiga marufuku kitabu hiki kusomwa. Noambeni maelezo kwa mwenye kufahamu.

Samahan hivi huku chuo mbona kinasomwa? Kimepigwaje marufuku? Au.sijaelewa?
 
Katika riwaya nlizozisoma nkiwa na umri Mdogo ni hii ya Rosa mistika....jitihada zangu za kukitafuta icho kitabu zimegonga mwamba kwa muda wote wa miaka 17....ntafurahi sana siku nkipata hata soft copy yake
 
waone wanafunzi wa chuo kikuu wanaosoma kiswahili. Mie nilikisoma wakati wife anasoma BA. softcopy siyo rahisi ila unaweza kutoa photocopy.
 
kitabu hiki mie nimekisoma miaka 1984 nilikipenda mno na nahitaji kukipata hata leo,hardcopy naweza kupata wapi?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom