E. Kezilahabi: Rosa Mistika

Kimechapishwa na udsm Press 1988 naamini ukienda maktaba zao udsm hasa kitivo cha sanaa ama kiswahili unaweza kupata kipo pia mtandao wa amazon usd 86
 
Kimechapishwa na udsm Press 1988 naamini ukienda maktaba zao udsm hasa kitivo cha sanaa ama kiswahili unaweza kupata kipo pia mtandao wa amazon bei yake
usd 86
 
Kimechapishwa na udsm Press 1988 naamini ukienda maktaba zao udsm hasa kitivo cha sanaa ama kiswahili unaweza kupata kipo pia mtandao wa amazon bei yake
usd 86
maktaba ya udsm vipo vichache hivyo wanaoruhusiwa kuvitumia ni wale wanaofanya tasnifu,kwa ngazi ya bachelor hawaruhusu sio tu kuazima hata kusomea palepale.
nitajaribu optional ya pili,thanks mkuu
 
Niliwai kuambiwa kwamba sababu kubwa ni kuusisha na maswala ya dini hasa dini ya kikatoriki....kwamba muhusika rosa kwatabia yake....hakupaswa kupewa jina lile la kikatoriki....kufanya vile ni kuidhalilisha dini hiyo....xo iyo nisehemu ya arguement za washikaji zilizo changia kuzuiliwa kwa kitabu hcho....japokua sasa hvi zinasomwa chuo kikuu.
 
Ninayo riwaya ya Rosa Mistika ila ngoja Nimalize kufanya UE ya semister hii nitakufanyia mpango ukipate
 
Wadau naomba kuuliza, kwa wale wanaopenda kufuatilia kazi za riwaya za Prof. E. Kezilahabi watakuwa wanafahamu riwaya ya Rosa Mistika. Nimekisoma sana kitabu hiki ila sifahamu ni kwa nini serikali ya Tanzania ilikipiga marufuku kitabu hiki kusomwa. Noambeni maelezo kwa mwenye kufahamu.


E.Kezilahabi ni mmoja wa watu waliokumbana na kinachoitwa udhibiti wa kazi za fasihi. Udhibiti huu ulianzia Amerika ya Kusini na mtu wa kwanza kudhibitiwa huko alikuwa mtunzi mashuhuri wa mashairi Pablo Neruda ambaye alianza kupingwa baada ya kubadili utunzi wake na kusema maovu ya tabaka tawala. Rosa Mistika cha E. Kezilahabi kilipigwa marufuku kwa kuwasema wakubwa akiwemo Deogratias aliyekuwa bwana maendeleo kwa kutembea na wanafunzi akiwemo Rosa, ili kudhiti siri za wakubwa kuwekwa wazi serikali ilitafuta visingizio vya kukipiga marufuku kitabu hicho na ikawa kama ifuatavyo:
1. Ilidaiwa na serikali kuwa kitabu hicho kinaharibu maadili kwa kuanika hadharani mambo machafu yasiyoendana na maadili ya mtanzania.

2. Wanawake nao wakaja juu kwa madai kuwa wamedhalilishwa kupitia matendo ya Rosa yaliyoandikwa kitabuni, inadaiwa kuwa mama mmoja aliwahi kuzimia baada ya kumkuta binti yake akisoma kitabu hicho.

3. Kundi la tatu ni kanisa Katoliki ambalo lilikuja juu kwa madai kuwa Mistika ni moja wapo wa sifa za Bikira Maria mtakatifu, hivyo ni udhalilishaji kumpa Rosa jina hilo hali ni mchafu wa matendo kiasi kile.

Kimsingi pamoja na udhibiti huo E. Kezilahabi alizidisha utunzi wake kwa kutumia lugha ngumu sana isiyoeleweka kirahisi hasa kwa msomaji wa kawaida.

Watunzi wengine walokumbana na udhibiti kama huo kwa Afrika ni Peter Abraham (Makhumazhan), David G. Mailu (My Dear Bottle), Ngugi wa Thiong'o ( I will Marry When I want - ambacho alikiandika upya kwa lugha yao kikaitwa Ngaaika Ndeenda), kwa ujumla hofu ya tabaka tawala ndio msingi wa udhibiti wa kazi za fasihi.
 
Ninayo riwaya ya Rosa Mistika ila ngoja Nimalize kufanya UE ya semister hii nitakufanyia mpango ukipate
dah we noma,m nakitafuta kwa ajili ya UE we unasema,,,,,,,,,,,,but sio mbaya nikikipata pia nitashukuru
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom