Sir_Mimi
JF-Expert Member
- Jun 21, 2013
- 7,207
- 15,880
Ndugu zanguni,namshukuru sana,lakini pia nawashukuruni ninyi wadau mbali mbali kwa kunishauri katika hili,kipekee nimshukuru rafiki yangu karena,alinitia moyo na kuniongezea ujasiri ktk kuikabili hali ambayo sikuitegemea.
Hakika asubuhi hii nimefika nyumbani,sijamkuta mchumba wa rafiki yangu.
Nimeshtuka kwa mambo mawili ambayo kwa kweli sijui namna ya kuyakabili.
1.Jamaa yangu amenipigia simu asubuhi sana,anaonekana kupoa sanaaaa,kitu ambacho sio kawaida yake kabisa,(sijui amepata habari gani juu ya hii issue).
Mbaya zaidi ni ujumbe alionitumia huyu shemeji yangu,umenifanya nichanganyikiwe zaidi,naomba ninukuu ujumbe wake,then mniambie nini nifanye jamani,naomba mnivumilie tu ndugu zangu,
"Bahati yako we mwanaume,kutoka moyoni nawachukia sana wanaume,mwambie na rafiki yako,kwa maisha yangu ya sasa nalipa kisasi kwa mtu yeyote anaitwa mwanaume,I'M HIV POSITIVE,umenusurika but your friend unknowingly is already positive,mshukuru Mungu wako mshenzi wewe"
Nimeishiwa pozi kwa kwelinashindwa kuamini shemeji yangu mpole na mkarimu kweli kweli awezakuwa mnyama kiasi hiki.
Kinachoniumiza ni juu ya rafiki yangu,je,anajua hali hii??,nimwambie kilichotokea??au nimnyamazie tu??
Hakika duniani tunayo dhiki juu,daaah!!!
Damn!