mwambunnyara
JF-Expert Member
- Sep 25, 2013
- 518
- 208
Nina rafiki yangu amekuwa akiishi Dodoma na msichana wake, the same room as Mr and Mrs japo hawajafunga ndoa.
Jamaa wangu amekuwa akimwamini sana msichana wake, kwasababu kiukweli ukimtazama shemeji yangu huyu ni mpole sana.
Kilichonifanya niandike uzi huu ni kilichonitokea kwa shemeji yangu huyu,hakika mpaka dakika hii siamini hata chembe.
Tumekuwa na mawasiliano ya kawaida sana kama mtu na shemejiye, kwa kipindi kirefu tu na sikuwahi kuwa na shaka naye wala jamaa hakuwahi kuonyesha mashaka kwa shemeji yangu huyu.
Jamaa wangu alikuwa akisaka ajira kwa udi na uvumba, Mungu kamjalia amepata kazi mkoa mwingine tofauti na Dodoma, hivyo ilimlazimu kwenda kazini j.tatu ya wiki hii.
Cha ajabu siku ya J.nne shemeji yangu alinipigia simu majira ya saa nne usiku, tulizungumza mengi,lakini sauti yake ilibadilika sana, ilikuwa yenye ishara ya mahaba mno,sikutilia maanani sana nkajua ni kwa sababu ni usiku,yawezekana ana usingizi mno.
Jana akanipigia tena usiku na kunambia Shem kesho natamani nije nikutembelee, (Mimi naishi Morogoro), ila usimwambie jamaa, nilishtushwa na hiyo statement, kwanini nisimwambie jamaa,akadai jamaa akijua itakuwa noma.
Niliishiwa pozi kwa ghafla, nikamwambia hapana, amsubiri jamaa akija ndo waje wote,lakini hakutilia maanani kile nlichomwambia, baada ya muda mfupi akanitumia ujumbe mfupi wa simu "Shem naomba usijali, sina nia mbaya najua unampenda sana (anamtaja jina mchumba wangu,)siwezi kukuharibia, lakini naomba unipokee tu,kesho nakuja").
Leo asubuhi kanitumia SMS, " Shem naenda stand kupanda gari ya kuja Moro,plz usimwambie (anamtaja jamaa wangu).
Nilijua huyu ananitania tu,lakini ajabu majira ya saa nane amenambia yupo msamvu stand, anaomba nimuelekeze namna ya kufika home, basi baada ya kumpa maelezo, amefika na nimemkaribisha home.
Baada ya kumwandalia chakula amekula,amekaa kwenye sofa anachart, nikamuuliza vipi una ndugu mwingine hapa Moro kajibu hapana.
Baadaye ananambia "ila Shem sio siri Leo nkwambie tu, namuonea wivu sana mpenzi wako, kwa muda mrefu nafikiriaga why didn't I meet you early".
Nimeishia kumuangalia tu usoni,coz nlikuwa simuelewi kabisa.Nimemuuliza shem unarudi saa ngapi Dodoma ananambia ataondoka kwangu by J.mosi,(na yupo comfortable kabisa kwenye sofa haonyeshi hata chembe ya woga.
Najiuliza,nifanyeje hapa,
1.Nimwambie jamaa yangu?
2.Ninyamaze na nikatafute Sehemu nyingine ya kulala nimwache alale peke yake?
Naombeni ushauri wenu wadau, maana siku ya leo naiona kuwa ngumu sana kwangu, daaaah baadhi ya wanawake wetu ni shida kwa kweli, I don't know why is it in this way?

Last edited by a moderator: