Duuuh, kweli wanawake wengine!

Duuuh, kweli wanawake wengine!

Ndugu zanguni,namshukuru sana,lakini pia nawashukuruni ninyi wadau mbali mbali kwa kunishauri katika hili,kipekee nimshukuru rafiki yangu karena,alinitia moyo na kuniongezea ujasiri ktk kuikabili hali ambayo sikuitegemea.
Hakika asubuhi hii nimefika nyumbani,sijamkuta mchumba wa rafiki yangu.
Nimeshtuka kwa mambo mawili ambayo kwa kweli sijui namna ya kuyakabili.
1.Jamaa yangu amenipigia simu asubuhi sana,anaonekana kupoa sanaaaa,kitu ambacho sio kawaida yake kabisa,(sijui amepata habari gani juu ya hii issue).
Mbaya zaidi ni ujumbe alionitumia huyu shemeji yangu,umenifanya nichanganyikiwe zaidi,naomba ninukuu ujumbe wake,then mniambie nini nifanye jamani,naomba mnivumilie tu ndugu zangu,
"Bahati yako we mwanaume,kutoka moyoni nawachukia sana wanaume,mwambie na rafiki yako,kwa maisha yangu ya sasa nalipa kisasi kwa mtu yeyote anaitwa mwanaume,I'M HIV POSITIVE,umenusurika but your friend unknowingly is already positive,mshukuru Mungu wako mshenzi wewe"
Nimeishiwa pozi kwa kwelinashindwa kuamini shemeji yangu mpole na mkarimu kweli kweli awezakuwa mnyama kiasi hiki.
Kinachoniumiza ni juu ya rafiki yangu,je,anajua hali hii??,nimwambie kilichotokea??au nimnyamazie tu??
Hakika duniani tunayo dhiki juu,daaah!!!

Hata kachai umezidishia sukari.
 
Nina rafiki yangu amekuwa akiishi Dodoma na msichana wake, the same room as Mr and Mrs japo hawajafunga ndoa.

Jamaa wangu amekuwa akimwamini sana msichana wake, kwasababu kiukweli ukimtazama shemeji yangu huyu ni mpole sana.

Kilichonifanya niandike uzi huu ni kilichonitokea kwa shemeji yangu huyu,hakika mpaka dakika hii siamini hata chembe.

Tumekuwa na mawasiliano ya kawaida sana kama mtu na shemejiye, kwa kipindi kirefu tu na sikuwahi kuwa na shaka naye wala jamaa hakuwahi kuonyesha mashaka kwa shemeji yangu huyu.

Jamaa wangu alikuwa akisaka ajira kwa udi na uvumba, Mungu kamjalia amepata kazi mkoa mwingine tofauti na Dodoma, hivyo ilimlazimu kwenda kazini j.tatu ya wiki hii.

Cha ajabu siku ya J.nne shemeji yangu alinipigia simu majira ya saa nne usiku, tulizungumza mengi,lakini sauti yake ilibadilika sana, ilikuwa yenye ishara ya mahaba mno,sikutilia maanani sana nkajua ni kwa sababu ni usiku,yawezekana ana usingizi mno.

Jana akanipigia tena usiku na kunambia Shem kesho natamani nije nikutembelee, (Mimi naishi Morogoro), ila usimwambie jamaa, nilishtushwa na hiyo statement, kwanini nisimwambie jamaa,akadai jamaa akijua itakuwa noma.

Niliishiwa pozi kwa ghafla, nikamwambia hapana, amsubiri jamaa akija ndo waje wote,lakini hakutilia maanani kile nlichomwambia, baada ya muda mfupi akanitumia ujumbe mfupi wa simu "Shem naomba usijali, sina nia mbaya najua unampenda sana (anamtaja jina mchumba wangu,)siwezi kukuharibia, lakini naomba unipokee tu,kesho nakuja").

Leo asubuhi kanitumia SMS, " Shem naenda stand kupanda gari ya kuja Moro,plz usimwambie (anamtaja jamaa wangu).

Nilijua huyu ananitania tu,lakini ajabu majira ya saa nane amenambia yupo msamvu stand, anaomba nimuelekeze namna ya kufika home, basi baada ya kumpa maelezo, amefika na nimemkaribisha home.

Baada ya kumwandalia chakula amekula,amekaa kwenye sofa anachart, nikamuuliza vipi una ndugu mwingine hapa Moro kajibu hapana.

Baadaye ananambia "ila Shem sio siri Leo nkwambie tu, namuonea wivu sana mpenzi wako, kwa muda mrefu nafikiriaga why didn't I meet you early".

Nimeishia kumuangalia tu usoni,coz nlikuwa simuelewi kabisa.Nimemuuliza shem unarudi saa ngapi Dodoma ananambia ataondoka kwangu by J.mosi,(na yupo comfortable kabisa kwenye sofa haonyeshi hata chembe ya woga.

Najiuliza,nifanyeje hapa,
1.Nimwambie jamaa yangu?
2.Ninyamaze na nikatafute Sehemu nyingine ya kulala nimwache alale peke yake?

Naombeni ushauri wenu wadau, maana siku ya leo naiona kuwa ngumu sana kwangu, daaaah baadhi ya wanawake wetu ni shida kwa kweli, I don't know why is it in this way?
Fanya maamuzi ya busara kaka, usijaribu kulala nae hata kidogo.
mwachie chumba tafuta sehemu nyingine ya kulala.
 
Fanya kitendo ambacho kitamfanya rafiki yako awe proud na wewe wanawake wapo tunza heshima ya rafiki yako fanya maamuzi magumu ili hata siku za mbeleni ujiproud mwenyewe kwa maamuzi ya msingi na busara. Mwokoe rafiki yako
HEMBU FAFANUA ZAIDI NAHISI KAMA HUJAELEWEKA VILE
 
Umenichekesha kweli
Huyo mtu toka unawasiliana naye anaonekana tu anataka dyudyu..Sasa we sijui ambacho haukukielewa ni kipi mpaka ukamkaribisha..Au ulikuwa unataka ushahidi???....We Dada kaa hapohapo usiondoke bila kupewa Dushe
 
Acha story iendelee lakini ukweli unaujua wewe binafsi naamini ushakula otherwise utakuwa bonge la lo.fa
Jamaa angu umesoma post yangu mpaka mwisho?including the finalizing one?hakika nkisoma comments za baadhi ya watu humu ndani,nagundua wengi wangekuwa tayari wamenaswa,halafu wakati mimi naona ni ushujaa kutofanya ngono hivyo,wewe unasema ni ulofa?hivi ulofa ni upi,kujifanyia ngono hovyo hovyo au kujizuia kufanya hovyo hovyo!!!?
 
Ulofa ni kucheza na hisia za watu kama ulishindwa kumzuia kuja moro sasa ulifikiri anakuja kupiga picha na wewe???. Ningekuona shujaa kama ungempigia boyfriend wake right after noticing evil plans
 
No love at all but just lies hao wanawake wana mapepo kabxa yan wewe cha mxingi jipigie show ulinde heshima yako ndo mpango
 
Vipi sir-mimi!mbona damn???

Hatari kaka...nimejaribu kufikiria kama ungekuwa kichwa panzi ukafuata baadhi ya shauri ulizopewa humu ukamsasambua kweli saizi ungekuwa ktk hali gani,mshukuru Mungu mkuu amekupa akili na hikma ya kujitafakarisha.
 
Mrejesho. Katoa huo

Hatari mkuu jamaa ana nyota ya #kakakuona ,huu mrejesho wake umenistua sana...pata picha angejifanya kidume cha mbegu akamkunja huyo mdada ingekuwaje.
 
Hatari kaka...nimejaribu kufikiria kama ungekuwa kichwa panzi ukafuata baadhi ya shauri ulizopewa humu ukamsasambua kweli saizi ungekuwa ktk hali gani,mshukuru Mungu mkuu amekupa akili na hikma ya kujitafakarisha.
Kiukweli,imenibidi nikatoe sadaka ya pekee kanisani,maana nashindwa kuamini kilichotokea.
Kwa sasa naumiza kichwa juu ya rafiki yangu,yatakuwa salama kweli?naanzaje kumwambia???ni kitendawili kigumu sana kinachonikabili kwa sasa!!!
 
HEMBU FAFANUA ZAIDI NAHISI KAMA HUJAELEWEKA VILE
Kwa kuthamini urafiki na uhusiano bora alio nao mtoa mada na jamaa, kwakutokubali kufanya zinaa na huyo dada pili kumuonesha dada kuwa anavalue zaidi uhusiano bora alionao na jamaa yake wanawake wapowengi wanaoweza kutimiliza mahitaji ya mwili wake incase akizdiiwa lakini sio huyo shemeji .Maamuzi haya yanaweza kumfanya baada ya kitambo kupita awe proud mwenyewe kwa kujiona mwanaume bora aliyeishinda zinaa kwa kuweka urafiki mbele na kuukana usaliti.
Awokoe rafiki yake kwa maana ya kuwa inawezekana jamaa ndio kajiwekezea hapo anaona huyo ndiyo mke wa kuweka ndani lakini kama ameweza kujirahisi hivyo kwa mtoa mada je kwa wengine ?Sio mwanamke mzuri
 
Hoja ni nzuri lakini tayari leo ni siku ya nne tangu aombe ushauri. Najiuliza je ushauri wangu wa leo utafanya kazi?

Nimechelewa kuuona huu uzi, hata hivyo, kwa faida ya wajao ni kwamba uzinzi huleta chuki na umaskini. Unadhani nani anafurahi kuona dada, mtoto, mama au mpenzi wake anaziniwa?

Muache huyo shem, mkimbie maana ni adui mbaya haswa.
 
Nashukuru kwa ushauri mzuri,japo kiukweli nkikumbuka mwili mzima unasisimka!!!
 
Hadithi njoo uwongo...njoo utam koleaaa,

Kuna sehemu naweza kukukamatia na kudhihirisha kuwa umetunga hii story.......btw heri ya mwaka mpya broh.
 
Last edited:
Nina rafiki yangu amekuwa akiishi Dodoma na msichana wake, the same room as Mr and Mrs japo hawajafunga ndoa.

Jamaa wangu amekuwa akimwamini sana msichana wake, kwasababu kiukweli ukimtazama shemeji yangu huyu ni mpole sana.

Kilichonifanya niandike uzi huu ni kilichonitokea kwa shemeji yangu huyu,hakika mpaka dakika hii siamini hata chembe.

Tumekuwa na mawasiliano ya kawaida sana kama mtu na shemejiye, kwa kipindi kirefu tu na sikuwahi kuwa na shaka naye wala jamaa hakuwahi kuonyesha mashaka kwa shemeji yangu huyu.

Jamaa wangu alikuwa akisaka ajira kwa udi na uvumba, Mungu kamjalia amepata kazi mkoa mwingine tofauti na Dodoma, hivyo ilimlazimu kwenda kazini j.tatu ya wiki hii.

Cha ajabu siku ya J.nne shemeji yangu alinipigia simu majira ya saa nne usiku, tulizungumza mengi,lakini sauti yake ilibadilika sana, ilikuwa yenye ishara ya mahaba mno,sikutilia maanani sana nkajua ni kwa sababu ni usiku,yawezekana ana usingizi mno.

Jana akanipigia tena usiku na kunambia Shem kesho natamani nije nikutembelee, (Mimi naishi Morogoro), ila usimwambie jamaa, nilishtushwa na hiyo statement, kwanini nisimwambie jamaa,akadai jamaa akijua itakuwa noma.

Niliishiwa pozi kwa ghafla, nikamwambia hapana, amsubiri jamaa akija ndo waje wote,lakini hakutilia maanani kile nlichomwambia, baada ya muda mfupi akanitumia ujumbe mfupi wa simu "Shem naomba usijali, sina nia mbaya najua unampenda sana (anamtaja jina mchumba wangu,)siwezi kukuharibia, lakini naomba unipokee tu,kesho nakuja").

Leo asubuhi kanitumia SMS, " Shem naenda stand kupanda gari ya kuja Moro,plz usimwambie (anamtaja jamaa wangu).

Nilijua huyu ananitania tu,lakini ajabu majira ya saa nane amenambia yupo msamvu stand, anaomba nimuelekeze namna ya kufika home, basi baada ya kumpa maelezo, amefika na nimemkaribisha home.

Baada ya kumwandalia chakula amekula,amekaa kwenye sofa anachart, nikamuuliza vipi una ndugu mwingine hapa Moro kajibu hapana.

Baadaye ananambia "ila Shem sio siri Leo nkwambie tu, namuonea wivu sana mpenzi wako, kwa muda mrefu nafikiriaga why didn't I meet you early".

Nimeishia kumuangalia tu usoni,coz nlikuwa simuelewi kabisa.Nimemuuliza shem unarudi saa ngapi Dodoma ananambia ataondoka kwangu by J.mosi,(na yupo comfortable kabisa kwenye sofa haonyeshi hata chembe ya woga.

Najiuliza,nifanyeje hapa,
1.Nimwambie jamaa yangu?
2.Ninyamaze na nikatafute Sehemu nyingine ya kulala nimwache alale peke yake?

Naombeni ushauri wenu wadau, maana siku ya leo naiona kuwa ngumu sana kwangu, daaaah baadhi ya wanawake wetu ni shida kwa kweli, I don't know why is it in this way?
Duh huo mtihani mkubwa kuliko mtihani wa shule. Ama ukipasi mtihani huo basi wewe kweli rafiki wa kweli. Manake rafiki zangu nakumbuka tulikuwa kila mtu anataka kumtafuna demu wa mwenziwe mpaka kuna siku tukataka kuzichapa. Ndio ukawa mwisho tukaanza kuwekeana mipaka.
 
Back
Top Bottom