Vipi ukienda lala hotelini demu akaona anaumbuka akafanya kitu kibaya kwako kama vile kunywa sumuBora umenisaidia aisee,SITAKI KABISA KUMSALITI RAFIKI YANGU,naona muda unazidi kwenda,shemeji yangu amesinzia hapa kwenye kochi,na mimi sijapata kujua haswa nifanye nini,jamani nikienda kulala hotelini nikamuacha hapa,yaweza kuleta madhara hasi??
Nina rafiki yangu amekuwa akiishi Dodoma na msichana wake,the same room as Mr and Mrs japo hawajafunga ndoa.
Jamaa wangu amekuwa akimwamini sana msichana wake,kwa sababu kiukweli ukimtazama shemeji yangu huyu ni mpole sana.
Kilichonifanya niandike uzi huu,ni kilichonitokea kwa shemeji yangu huyu,hakika mpaka dakika hii siamini hata chembe.
Tumekuwa na mawasiliano ya kawaida sana kama mtu na shemejiye,kwa kipindi kirefu tu,na sikuwahi kuwa na shaka naye,wala jamaa hakuwahi kuonyesha mashaka kwa shemeji yangu huyu.
Jamaa wangu alikuwa akisaka ajira kwa udi na uvumba,Mungu kamjalia amepata kazi mkoa mwingine tofauti na Dodoma,hivyo ilimlazimu kwenda kazini j.tatu ya wiki hii.
Cha ajabu siku ya j.nne shemeji yangu alinipigia simu majira ya saa nne usiku,tulizungumza mengi,lakini sauti yake ilibadilika sana,ilikuwa yenye ishara ya mahaba mno,sikutilia maanani sana nkajua ni kwa sababu ni usiku,yawezekana ana usingizi mno.
Jana akanipigia tena usiku na kunambia Shem kesho natamani nije nkutembelee,(Mimi naishi Morogoro), ila usimwambie jamaa,nilishtushwa na hiyo statement, kwanini nisimwambie jamaa,akadai jamaa akijua itakuwa noma.
Niliishiwa pozi kwa ghafla,nikamwambia hapana,amsubiri jamaa akija ndo waje wote,lakini hakutilia maanani kile nlichomwambia,baada ya muda mfupi akanitumia ujumbe mfupi wa simu "Shem naomba usijali,sina nia mbaya najua unampenda sana .......(anamtaja jina mchumba wangu,)siwezi kukuharibia,lakini naomba unipokee tu,kesho nakuja").
Leo asubuhi kanitumia SMS, " Shem naenda stand kupanda gari ya kuja Moro,plz usimwambie.......(anamtaja jamaa wangu).
Nlijua huyu ananitania tu,lakini ajabu majira ya saa nane amenambia yupo msamvu stand,anaomba nimuelekeze namna ya kufika home,basi baada ya kumpa maelezo,amefika na nimemkaribisha home.
Baada ya kumwandalia chakula amekula,amekaa kwenye sofa anachart,nkamuuliza vipi una ndugu mwingine hapa Moro kajibu hapana.
Baadaye ananambia "ila Shem sio siri Leo nkwambie tu,namuonea wivu sana mpnz wako,kwa muda mrefu nafikiriaga why didn't I meet you early". Nimeishia kumuangalia tu usoni,coz nlikuwa simuelewi kabisa.
Nimemuuliza shem unarudi SAA ngapi Dodoma ananambia ataondoka kwangu by j.mosi,(na yupo comfortable kabisa kwenye sofa haonyeshi hata chembe ya woga.
Najiuliza,nifanyeje hapa,
1.Nimwambie jamaa yangu?
2.Ninyamaze na nikatafute sehemu nyingine ya kulala nimwache alale peke yake?
Naombeni ushauri wenu wadau,maana siku ya leo naiona kuwa ngumu sana kwangu,daaaah baadhi ya wanawake wetu ni shida kwa kweli,I don't know why is it in this way????
Kufa sio kazi rahisi aisee,naamini hawezi kujiua akiwa nyumbani kwangu,MUNGU NA AEPUSHIE MBALI,nipo zangu hotelini,nimemuacha nyumbani!!!Vipi ukienda lala hotelini demu akaona anaumbuka akafanya kitu kibaya kwako kama vile kunywa sumu
Nimependa majibu yako. Safi sanaFanya kitendo ambacho kitamfanya rafiki yako awe proud na wewe wanawake wapo tunza heshima ya rafiki yako fanya maamuzi magumu ili hata siku za mbeleni ujiproud mwenyewe kwa maamuzi ya msingi na busara. Mwokoe rafiki yako
Sms ulizochat nae ndo ushahidi wako, sasa kama na wewe ulikua unamchombeza huko kwenye msg ndo utaisoma number LolNdugu yangu kusema ukweli,nashindwa kumwambia jamaa coz anaweza asiamini ntakachomwambia,jamaa anamwamini sana msichana wake,awezafikiri kuwa nawagombanisha tu,nathamini urafiki wetu,sipendi kugombana naye kabisa!!!
Yan apo miss chagga lazima tu kuna vijimazoea ambavyo walikuwa wamewekeana ivi kweli mtu afunge tu safar jaman mmh sijui kwakweli kwanza mimi nilivyo siwapendi mashemeji wanafiki sana hata ayo mazoea siwezi kujengaMfukuze haraka sana tena mapema
Acha mazoea mabaya na shemeji yako
Mrejesho ni muhimu...usije ukarudi ukasema shetani alikupitiaAhsante tatty!!!
Mrejesho?Ndugu zanguni,namshukuru sana,lakini pia nawashukuruni ninyi wadau mbali mbali kwa kunishauri katika hili,kipekee nimshukuru rafiki yangu karena,alinitia moyo na kuniongezea ujasiri ktk kuikabili hali ambayo sikuitegemea.
Hakika asubuhi hii nimefika nyumbani,sijamkuta mchumba wa rafiki yangu.
Nimeshtuka kwa mambo mawili ambayo kwa kweli sijui namna ya kuyakabili.
1.Jamaa yangu amenipigia simu asubuhi sana,anaonekana kupoa sanaaaa,kitu ambacho sio kawaida yake kabisa,(sijui amepata habari gani juu ya hii issue).
Mbaya zaidi ni ujumbe alionitumia huyu shemeji yangu,umenifanya nichanganyikiwe zaidi,naomba ninukuu ujumbe wake,then mniambie nini nifanye jamani,naomba mnivumilie tu ndugu zangu,
"Bahati yako we mwanaume,kutoka moyoni nawachukia sana wanaume,mwambie na rafiki yako,kwa maisha yangu ya sasa nalipa kisasi kwa mtu yeyote anaitwa mwanaume,I'M HIV POSITIVE,umenusurika but your friend unknowingly is already positive,mshukuru Mungu wako mshenzi wewe"
Nimeishiwa pozi kwa kwelinashindwa kuamini shemeji yangu mpole na mkarimu kweli kweli awezakuwa mnyama kiasi hiki.
Kinachoniumiza ni juu ya rafiki yangu,je,anajua hali hii??,nimwambie kilichotokea??au nimnyamazie tu??
Hakika duniani tunayo dhiki juu,daaah!!!