Duru za Siasa: Matokeo ya Uchaguzi Marekani

kwakukusanya 234 naona Trump kawanyamazisha wapinzani wake ndani ya chama na nje ya chama. Na akishinda (nategemea ashinde) atafanya kazi yake ya Urais kwa uhuru zaidi kama Rais wetu Magufuli.
 
Kuna state ya Maine, hawa wana EV 1 ambayo ni muhimu sana hasa kwa Trump kwasababu inaweza kumfikisha 270 kama , narudia kama matokeo mengine yatabaki kama yalivyo

Maine inatoa EV kwa congressional district
 
Hakuna namna Clinton anaweza akapata tena ushindi...katika hali hii, natamka kwamba Trump ndiye Rais mteule wa Marekani! Clinton sasa akamate simu tu akampongeze Trump.
Mkuu unakumbuka hii?
SURA YA UCHAGUZI

Tukumbushe uchaguzi si idadi ya kura, bali viti (Electral vote) au EV katika state
Kuna solid and Red Sates ikimaanisha zinajulikana zitakuwa Republican au Democrat

Kuna state zitakazoamua nani awe Rais kwasababu hazitabiriki, hizo ndizo swing au battle states

Macho kesho yatakuwa katika state zifuatazo (Kundi 1)
Nevada EV 6
Florida EV 29
Ohio EV 18
NC EV 15
Hampshire EV 4
Pen state EV 20
Iowa EV 6

Halafu kuna state ambazo hazieleweki kutokana na hali ya uchaguzi
Utah EV 6 Hii ni kutokana na kuwepo kwa mgombea binafsi Evans M
Arizona EV 11 Kutokana na kuwa na Latino
Maine EV 2 Kutokana na kuwa na congressional district
Georgia EV 16 Kwasababu hii ni red state lakini kura za maoni zipo karibu sana
Michigan EV 29 , lead ya Clinton imepungua 11 hadi 4, ambayo ni within margin of error

Hizi zinaweza kuwa chafuzi tu kwa wagombea ingawa ni unlikely zinaweza kuwa na impact hiyo
Muhimu ni kundi la kwanza kwasababu hizi

Kwa mujibu wa track poll (si lazima ziwe sahihi) Magic number inayogombewa ni 270
Hillary Clinton anasimama na EV 268 na Trump 204

Kwa minajili ya mjadala the EV baseline ni 204, hivyo wagombea wanatakiwa kufikia 270
Kama polls na uchambuzi ni sahihi bila mishaps kutoka kundi la 2 hapo juu, then

Clinto akiwa na 268 atahitaji EV 2 kutoka popote kama New Hampshire EV au Iowa
Donald Trump 204 atahitaji EV 66 na hizo lazima zipatikane kutoka kundi la 1 hapo juu

Inaweza kuonekana ni mlima mrefu kwa Trump kupanda, lakini huu ni uchaguzi lolote laweza kutokea. Ingalikuwa rahisi kiasi hicho Clinton asinge kampeni

Kwa mfano, BREXIT ilibashiriwa ushindi UK kubaki EU. Kilichotokea kila mmoja anakijua
Kwanza, wengi hawakujitokeza kupiga wakiamini kambi ya Remain itashinda.
Kambi ya exit ikapiga kura na mwisho ikashinda

Pili, katika primaries Hillary Clinton alikuwa anaongoza kwa asilimia 9-11 Michigan. Kwa mshangao Bernie Sander akashinda

Tatu, hakuna aliyetarajia 2004 George Bush angerudi madarakani kwa kumshinda Kerry

Nne, kuna factors nyingi zinafanya kazi katika uchaguzi tutajadili bandiko lijalo

Inaendelea
 
Trump ameshinda Iowa

Kama tulivyosema mwanzoni, Ohi na Iowa zitakwenda Trump na hivyo ndivyo ilivyo
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Pennsylvania imebadilika na sasa ni kwa Trump

Trump akishinda hii, tayari anakuwa president elect

Hali kwa Dem ni mbaya kuliko ilivyotarajiwa kwani Pen haijaenda Republican tangu 1992
 
Hakuna namna Clinton anaweza akapata tena ushindi...katika hali hii, natamka kwamba Trump ndiye Rais mteule wa Marekani! Clinton sasa akamate simu tu akampongeze Trump.
Mkuu naungana na ww no way, jamaa hata hizo state zilizobaki anongoza pia, ngoja tusubiri final results, ni maajabu tu Clinton kushinda
 
Main Stream Media na kura za maoni zilimdanganya HRC!! na yeye akadanganyika!! Wamarekani waliiona hatari iliyokuwepo ya 'Mama' kuiporomosha Marekani kwa mwendokasi wa ajabu!
 
Utah Trump atashinda kutokana na namba zilizopo.

Nevada Clinton atashinda kutokana na namba

Minnesota Clinton atashinda

Arizona Trump atashinda

Maine congressional district bado ni tight kuna EV 1

Hizi hazijawa projected ni kutokana na tofauti ya namba tunazoona. Zisichukuliwe kama final tafadhali
 
Masoko yametetereka kama ilivyokuwa Brexit ambapo Dow J imepoteza 4.5%
 
Wanajamvi

Kutokana na namba zinaoonekana Trump atashinda Pennyslavania

Kwa mantiki hiyo na kwa kuangalia Wisconsin na Michigan :

DONALD TRUMP IS PRESIDENT ELECT

Hakuna namna Hillary anaweza ku recover

Hesabu ni kama hizi
New Hamshire Trump anaongoza na hakuna mahali Dem watapata kura. EV 6
Michigan ina EV 18. Wisconsin 10. Jumla ni 34.

232 + 34= 268

Hapa kuna Arizona yenye EV 10 na hivyo kuwa na EV 278
 
Jambo linalowaumiza Clinton kampeni ni moja
Kwamba Trump angeshinda swing state zote bado asingekuwa Rais.

Walichotaka ni kushinda New Hampshire tu.
Hii ingewekana kama wangelinda Wisconsin na Michigan

Uchaguzi umeamualiwa na blue state, hilo watajiuliza na watalia nalo sana

Pamoja na hayo kuna mambo yatakayotokea

Kutetereka kwa masoko kwasababu market hazitaki uncertainty

Comey atakuwa mjadala kuelekea mbele

WikiLeaks iliyoingilia democrat na si Republican itakuwa katika mjadala

Kwa upande wa Democrat

Kwanini wameruhusu mchezo kuchezewa 'maeneo yao' kama WI na MI

Bernie Sanders factor 'Bernie or bust' itakuwa katika mjadala

Lag time kabla ya Comey ilikuwa obvious kwani hawakufanya mikutano mingi

Kwa upande wa race

Swali litakalojadiliwa, Latinos wana impact gani pamoja na expolisions kule FL

Je, hii ni rebellion ya white kwamba Rais wao anachaguliwa na competition ya race (black/Latinos)

Je, wananchi wamechoka na 'the establishment' ?

Baadhi ya haya yatakuwa katika mjadala, lakini kwa sasa President elect Trump atakutana na incumbent president Obama siku ya Alhamisi

Kwamba uchaguzi umeisha hilo halina mjadala tena, na kwamba Trump kashinda uchaguzi
 
Tathmini , maoni, mafunzo yataendelea katika bandiko hili

Hakuna ukweli mwingine isipokuwa ukweli kuwa Trump kashinda.

Dunia imeshangazwa lakini ndiyo demokrasia ya wenzetu inavyofanya kazi.

Kwenda mbele kuna mambo yatakayojitokeza haraka

- Je, Rep waliomkataa Trump watafanya naye kazi?

- Trump atapitishaje agenda zake kukiwa na resentment

- Atafuta Obama care katika siku 100

- Atajenga ukuta kama alivyoahidi?

-Atabadili mikataba ya biashara?

-Ataondoa majeshi ya Marekani yaliyoko nje?

Haya ni mambo yanayomkabili akiwa na divided Republican. Shaka hapa ni kuwa kama hakuwaunganisha wakati wa uchaguzi ataweza mbele ya safari?

Kinachofanyika sasa ni postmortem na way forward kwa ulimwengu kutokana na matokeo ya Taifa lenye nguvu za kila aina duniani
 
Back
Top Bottom