Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

El Jefe amemuunga mkono Trump katika dai lake kwamba Russian collusion ni uzushi tu na witch-hunt iliyovaliwa njuga na Democrats kwa hasira ya kushindwa uchaguzi...!
Kosa hilo alilifanya Trump alipoambiwa Intel community 16 zina uhakika Russia ilifanya jambo kuhusu uchaguzi wa US

Intel hazikusema collusion, Trump akasema ni 'fake' kama ilivyokuwa silaha za maangmizi Iraq
Hapa hakujua kilichosemwa ni Russian influence si collusion. Akanunua ugomvi

Media zikachimba Russian influence .Kama ilivyo kwa Intel Trump akasema ni fake news

Kama unakumbuka tulisema ugomvi na media na Intel community hautakuwa mzuri , inatokea

Katika kutojifunza, kamtimua Comey kisha kashfa dhidi yake bila kujua amebeba nini kifuani

Intel na media zikaamua kuhakikisha si fake. Suala zima likawa Collusion na siyo influence. Matatizo yakaanza yakiwatafuta watajwa. Katika hali isiyo ya kawaida Trump tatizo

Sasa kuna Page, Flynn, Manafort, Rogger na leo Kushner

Haina maana wamehusika, kinachowaunganisha ni kauli ya Trump kuwa kampeni yake haikuhusika ili hali watajwa ni watu wa kampeni yake.

Trump akajikuta ameingia katika suala la Collusion kwa kulianzisha wala si media

Kinachoshangaza, kama Russia ilitaka kufanya mambo ya kijasusi ni kwanini Trump anataka uchunguzi uachwe? Ikiwa hakuna tatizo kwanini asisaidie jambo hilo likafika mwisho?

Katika kauli za ajabu, Trump akasema Kampeni, na yeye binafsi hasa, hahusiki na collusion. Alikazia binafsi, dalili ya kuwatosa wenzake. Je, nini kimetoke ikawa binafsi si la kampeni yake?

Inawezekana hakuna kitu collusion, hata hivyo kuna kila dalili ya kutaka jambo hilo life.

Kwa bahati mbaya 'wabaya' wake media na intel wamekamata mpini na haioenekani suala hilo kwisha leo au mwezi ujao. 'Drip drop' zinatishia

Trump kaweka mwanasheria binafsi kitu kinachotia shaka ni kwanini na kujiandaa na nini

Kuna baadhi ya washirika wanaaza kudoda kifedha, hoja yao kwanini kampeni isitumie rasilimali kuwawekea wanasheria ikiwa 'walikuwa' wanafanya kazi ya kampeni

Mkanganyiko huo unaongeza curiosity

Tusemezane
 
Breaking News: Russian ambassador told Moscow that Kushner wanted secret communications channel with Kremlin

Jared Kushner and Russia’s ambassador to Washington discussed the possibility of setting up a secret and secure communications channel between Trump’s transition team and the Kremlin, using Russian diplomatic facilities in an apparent move to shield their pre-inauguration discussions from monitoring, according to U.S. officials briefed on intelligence reports.

Ambassador Sergei Kislyak reported to his superiors in Moscow that Kushner, then President-elect Trump’s son-in-law and confidant, made the proposal during a meeting on Dec. 1 or 2 at Trump Tower, according to intercepts of Russian communications that were reviewed by U.S. officials. Kislyak said Kushner suggested using Russian diplomatic facilities in the United States for the communications.

The meeting also was attended by Michael Flynn, Trump’s first national security adviser.

The White House disclosed the fact of the meeting only in March, playing down its significance. But people familiar with the matter say the FBI now considers the encounter, as well as another meeting Kushner had with a Russian banker, to be of investigative interest.

Kislyak reportedly was taken aback by the suggestion of allowing an American to use Russian communications gear at its embassy or consulate — a proposal that would have carried security risks for Moscow as well as the Trump team.

Neither the meeting nor the communications of Americans involved were under U.S. surveillance, officials said.

Source: Washington Post

Mambo yanazidi kuwa makubwa kwa Donald Trump na sasa mkwe wake Jared Kushner imeripotiwa alikuwa anatafiti njia ya mawasiliano na Urusi ya siri bila Marekani kujua. Swali ni je ni mawasiliano ya namna gani hayo ambayo hawakutaka serikali yao iyafahamu? Drip drip drip, kitanzi kinazidi kukaza...!
 
WIKI KATIKA SIASA ZA US
Jared Kushner katika mazingira magumu
Je, Tembo kaingia Chumbani?


Jared Kushner mkwewe Rais Trump anafuatiliwa kwa ukaribu kutokana na kubainika 'maongezi'
Kushner anahusishwa na Flynn na Balozi Kisyalak kuwa na back channel na Kremlin

Kushner aliwasiliana na Sergey Gorkov, mfanyakazi mwandamizi wa Bank iliyowekewa vikwazo na US wakati wa Obama. Maongezi wakati wa transition haijulikana ni binafsi au ya Kampeni

Chenye utata ni miss Univ iliyofanyikia Russia miaka ya nyuma ikiwa chini ya Trump
Moja ya Sponsor alikuwa bank ya Sergey Gorkov mwenye uhusiano na Putin pia.

Wachunguzi wanaangalia uhusiano wa Trump. Kushner, Sergey na Putin

Katika hali nyingine Comey ata testify mbele ya kamati ya seneti.
Inatarajiwa ataeleza uhusiano wao, maswali yamezuka kuhusu wigo wa Comey kuzungumza

Kuna hoja Trump anaweza kumzuia kwa kutumia presidential privilege
Ni ngumu kuitafsiri kwa mazingira yaliyopo. Comey ni Raia, ni afisa wa zamani!
Presidential privilege inatekelezwaje katika mazingira yaliyopo?

Naye mwenyekiti wa kamati ya Bunge Bw Nunes aliye ji recuse kutoka investigations ameibuka na kutoa subpoena kwa washirika wa Trump na wa utawala wa Obama kwasababu ya 'leak'

Hayo ameyafanya bila kushauriana na wanakamati akiwa ameji recuse na sasa kurudi
Haitarajiwi kama yatakuwepo mabadiliko yoyote kwa kuchomeka hoja ya leak

Kwa ujumla hali ni ya hofu kwa WH kukiwa tayari na wanasheria wa kumtetea.

Kwa bahati yamekuwepo matukio yanayosaidia kupunguza joto na utawala unayatumia

Mfano, shambulio la Manchester lilipunguza joto dhidi ya Kushner, Kislayak, Sergey

Halafu ikaja hoja ya Climate change iliyobadilisha maongezi kwa muda

Na sasa kuna shambulio la London, yote yakififisha kwa muda habari zinazohusu WH

Inaendelea
 
WIKI HII KATIKA SIASA ZA US

Sakata la Russia linaendelea kuwa gumzo katika viunga vya DC na kuchukua nafasi kubwa

Juzi kumetokea shambulio kwa 'wabunge' wa Republican mazoezini kujiandaa dhidi ya Democrats

Raia wa Illinoi alifika katika viwanja vya baseball na kuuliza timu gani ilikuwa mazoezini
Alijibiwa ni Republican , kilichofuata ni kutoa silaha zake akimimina risasi uwanjani

Mnadhimu mkuu wa Republicans alikuwa na askari ambao kwa jitihada zao waliweza kuokoa watu
Raia aliuawa akimwacha mnadhimu mkuu mahututi na polisi waliojeruhiwa

Raia amejulikana ni mfuasi wa Bernie Sanders wa Democrats aliyekuwa na maduku duku
Hakupenda sera zinazoendelea ikiwemo suala la Healthcare ambayo GOP wanalifanyia kazi

Tukio limetokea muda mfupi baada ya Rais Trump kurejea DC akitokea ziarani alikozungumzia Healthcare Bill inayopendekezwa kwa kuiita 'mean' tofauti na chereko alizokuwa nazo alipoipokea

Healthcare bill ipo katika Senate ikiangaliwa kwa ukaribu

Russia: Sakata limechukua sura nyingine. AG Sessions amefanyiwa mahojiano na kamati ya seneti
Kwa sehemu kubwa alikwepa kujibu baadhi ya hoja akitumia 'presidential privilege '

Naye mchunguzi aliteuliwa Bwana Mueller anaendelea kusuka timu yake ya uchunguzi
Zilikuwepo habari za Rais Trump kumtimua, hata hivyo zimekanushwa na WH

Hilo lilitokana na uchambuzi wa magwiji wa sheria na siasa ulioonya kumfukuza Mueller kutatia nyongo suala la Russia kwa kile kinachoonekana 'kufichwa' kukiwa tayari na habari za kuzuia uchunguzi

Katika mahojiano Dir wa FBI aliyetimuliwa alielezwa alichoombwa na Rais kuwa 'loyal' kwakwe
Hiyo ni pamoja na viongozi wengine wawili wa Intelejensia akiwemo Bw Rogers

Picha iliyojitokeza katika mahojiano ya kamati na Comey, Sessions, Roger na Coats ilionyesha kuwepo dalili za kuingilia au kutaka kuzuia uchunguzi wa suala la Russia kutoka kwa Trump

Hali hiyo imepelekea Bwana Mueller kuanzisha uchunguzi kubaini iwapo Trump 'obstruction of Justice'

Masuala sasa ni mawili, Russia investigations na endapo kampeni ilihusika au la
La pili ni la obstruction of justice kwa Rais Trump.

Suala la Russia limemgusa mkwewe Trump Bw Kushner anayechunguzwa na Mueller

Hivyo Trump ana deal na mambo mawili, Russia na hili la Justice.

Kiwewe kimepelekea Trump kuweka wakili binafsi na VP Bwana Pence nayo imetafuta wakili binafsi

Tusemezane
 
Kwa kweli naipenda US wanavyoendesha mambo yao, hakuna kukurupuka...wanakuendesha taratibu huku wakikutupia kamba ujitundike hadi unajikuta unaanza kujinyonga kwa mikono yako mwenyewe. Masikini Trump, kama mzama maji sasa kajikuta anaanza kutapatapa na kuanza kupingana hata na wanasheria wake, kila moja akiropoka lwake. Tuliomshuhudia Nixon akijitia kitanzi ulifika wakati akaanza tumbua tumbua na kuanza kuweweseka hadi kujitumbua mwenyewe na kuachia ngazi.
 
Kwa kweli naipenda US wanavyoendesha mambo yao, hakuna kukurupuka...wanakuendesha taratibu huku wakikutupia kamba ujitundike hadi unajikuta unaanza kujinyonga kwa mikono yako mwenyewe. Masikini Trump, kama mzama maji sasa kajikuta anaanza kutapatapa na kuanza kupingana hata na wanasheria wake, kila moja akiropoka lwake. Tuliomshuhudia Nixon akijitia kitanzi ulifika wakati akaanza tumbua tumbua na kuanza kuweweseka hadi kujitumbua mwenyewe na kuachia ngazi.
Matokeo haya...yanatueleza mengi sana tena yasiyoya kawaida kwa baadhi yetu juu ya Uhusiano wa Wamarekani na rais wao Trump kwa sasa.

----
In a nail-bitingly close runoff special election, Republican Karen Handel has defeated Democrat Jon Ossoff for Georgia's 6th congressional district seat, which opened when Tom Price was appointed to be President Donald Trump’s health and human services secretary.
With 81 percent of precincts reporting, Handel was declared the winner with 52.5 percent of the vote, compared to Ossoff's 47.5 percent, according to the Associated Press.

Source:
Handel wins: GOP retains House seat in Georgia special election

The South Carolina fifth-district seat, vacated when Mick Mulvaney became Mr Trump's budget director, had been expected to be an easy win for Republicans.

The Republicans have so far staved off defeats by the Democrats this year.

In April they narrowly defended a deeply conservative Kansas seat vacated when Mr Trump appointed Congressman Mike Pompeo to lead the CIA.

Last month, Republican Greg Gianforte won a special congressional election in Montana, despite being charged with assaulting a UK reporter.
Source:
bbcnews.com
 
WIKI KATIKA SIASA ZA US

Wiki hii sec DHS amehojiwa na bunge na kuthibitisha Russia kufanya majaribio katika mifumo ya uchaguzi kwa state zipatazo 20. Hata hvyo alisema hakuna kura iliyoingiliwa na makachero hao

Kauli yake inashabihiana na ile ya Intel community 16 zilizosema Russia ilifanya majaribio

Mahojiano ni mwendelezo wa kamati ya House na Senate zinazofanya uchunguzi tofauti
Wakati huo huo mchunguzi Mueller naye akiendelea na shughuli zake za uchunguzi

Kamati ya House iliyomhoji James Comey wiki chache zilizopita ilitaka Comey awasilishe vimemo vya kumbu kumbu za maongezi yake na Rais Trump kama alivyodai
Kamati ikamtaka Rais Trump naye awasilishe kile alichokita 'tape' ya maongezi na Comey

Leo Trump ame tweet akisema hakuna tape na wala hajaanda. Kauli yake katika tweet inakinzana na aliyodai kuna tape na hivyo Comey awe mwangalifu wa kauli mbele ya kamati

Haya ndiyo mazungumzo yakihoji siku takribani 41 alizoulizwa kama kuna tape au la
Wacunguzi wanasema ikiwa alitoa kauli na alijua haipo kwanini alisubiri siku 41

Mjadala umejikita katika maeneo kadhaa. Kwanza, kauli ya uwepo wa tape ndiyo iliyomsukuma Comey kumtumia rafiki yake ku leak information katika magazeti

Kwa mujibu wa Comey, alichotaka ni kuundwa tume ambayo leo tunajua ni ile ya Mueller
Mueller si habari nzuri kwani uchunguzi unaweza kuja na kitu kingine zaidi ya Russia.

Kauli ya Rais Trump akidhani ni ndogo inampeleka mahali ambapo asingependa kuwepo

Pili, wengine wanasema hizi ni mbinu za Trump za kuhamisha umma kutoka katika hoja ya Healthcare.

Kwa wiki kadhaa senate GOP wamekuwa wanafanyia kazi Health act iliyopeleka na House kupitiwa na pengine kuwa na marekebisho. Healthcare act ni mwija mchungu kwa Republicans

Kwa sasa ndani ya senate kuna tofauti ya kura mbili tu, zaidi ya hapo mswada utakwama

Tatizo inalojitokeza ni uwepo wa Team Trump inayotaka ku repeal and replace Obamacare, moderates wanaotaka baadhi ya mambo ya Obama yawepo, na conservative wasiotaka jingine bali act mpya itakayokuwa kali zaidi hasa kwa wanyonge

Hivyo Tweet ililenga kuondoa watu katika maongezi, na huu ni mtindo ambao Trump ameutumia kwa muda mrefu kwa mafanikio wakiita distractions

Mtindo huo ulifanikiwa siku za nyuma lakini sasa unaelekea kumgeukia kwani maswali na hoja
anazotupa kupoteza umma zinabaki kuwa maswali muhimu yanyohitaji majibu

Kwa mfano, bado anaulizwa kama Kulikuwa na fraud katika wapiga kura uliofanywa na Obama
Pili, anaulizwa endapo anakubali uwepo wa Climate change
Tatu, kama anakubali Russia ilifanya udukuzi katika uchaguzi uliopita

Yote na mengine yameweka WH katika mtafaruku kila asubuhi wakifika mahali hata WH briefing zinafanyika bila Camera ili kuepuka kujichanganya zaidi

Hili linaonekana katika kura kuhusu utendaji wa Trump ambazo ni all time low kwa modern president zikiwa kati ya 35%-45% ukilinganisha na Marais wengine katika kipindi hicho

Inaendelea...
 
POLLS

Kura za maoni kuhusu serikali ya Trump zinaeleza kwa uchache nini kinaendelea USA.

Kama tulivyowahi kusema Trump ana kundi linalomwamini hata akisema nini
Hili ndilo linatengeneza 35-45% na halibadiliki kwa mtazamo au jambo jingine

Kusema ni all time low ni sawa, lakini kiuhalisia hajapoteza wala hajaongeza
Hata hivyo ukichanganya Republicans kwa ujumla umaarufu umeanza kushuka kwa kasi

Hili linachagizwa pia na chaguzi nne maalumu ambazo Republican wameshinda zote
Hii ina maana nyingi kwa mItazamo. Kushinda si hoja kubwa kwa kutazama majimbo

Nafasi zilizoachwa wazi ni zile ambazo wawakilishi wao wameteuliwa katika serikali
Kwa maana nyingine ni nafasi zilizoshikiliwa na Republicans

Ukitazama ramani maeneo kama Montana, Kansa na Georgia hizo ni red states
Hii maana yake ni kuwa ni maeneo salama ya GOP ambayo kushinda ni jambo rahisi

Mfano, mwaka 2012 Romney alimpiga Obama kule Georgia kwa point 20. Mwaka 2016 Trump alimshinda Clinton kwa point katika single digit. Hii ilionyesha kushuka kwa ushindi

Inapotokea maeneo salama kama Kansas,Montana na Georgia yanakuwa na ushindani inaeleza tatizo mbele ya safari.

Mgombea wa Democrats ameshindwa na Republican kwa point 5 katika eneo ambalo GOP walipaswa kushinda kwa asilimia 60-70 (Georgia au Montana)

Hoja hapa ni kuwa kushinda ni jambo la faraja kwa GOP lakini ushindi huo umekujaje?

Katika mtifuano mkali kule Georgia ni wazi Dems wanafanya 'inroads' kwa red states

Healthcare bill inayosubiriwa na ambayo huenda ikawatupa wengi nje ya mfumo wa afya itachagiza sana matokeo ya midterm election 2018 kama ilivyokuwa kwa Obama

Wanachokifanya Dems ni kutaka kumiliki kimoja kati ya House na Senate.

Unapochanganya na masuala ya tweets, GOP hawana raha na Trump.
Tweet kama ya leo si kuwa ni mbaya kwa maudhui bali kwa kitu kinachoitwa credibility

Kwamba, Republicans wanabeba mzigo wa Rais wao na huenda wakalipa gharama mbele

Wengi wanahoji dunia inaitazama vipi US katika mwendo wa 'damage control' kila uchao

Tusemezane
 
JARIBIO LA KUONDOA ACA LASHINDWA

Republican waparaganyika
Trump aonja machungu ya kutawala nchi si kampuni

Kwa miaka mingi Rais Trump yupo mstari wa mbele kupinga ACA inayoitwa Obamacare
Kwa miaka 7 Republican wamepinga Obamacare ambayo jana ilitimiza mwaka wa 7 rasmi

Kampeni yote 2016 ku repeal and replace Obamacare ilikuwa ni 'mantra' kila uchao
Jambo moja lililokuwa wazi, hakuna nyaraka iliyowahi kuonekana ikionyesha mbadala wa Obamacare

Rais Obama aliwahi kuhoji kama upo mbadala ili aweze kuunga mkono. Hakuna.
Trump wakatumia kauli nyingi kulaghai umma bila kuwa na mbadala wowote isipokuwa kelele tu

Uchaguzi wa ndani wa Republican wagombea karibu wote walikuwa na sera za namna ya kudeal na Obamacare kwa maana ya mbadala.

Trump hakuwa na hata ukurasa mmoja, lakini alikuwa mzuri sana wa kuponda Obamacare. Hapa jamvini tuliwahi kuhoji sana, kamaACA ni mbaya wapi nzuri ya Trump?

Baada ya kuingia WH Trump alisaini siku ya kwanza kitu kinachoitwa kupunguza maumivu a ACA
Ilikuwa ni kulaghai siku ya kwanza kafuta Obamacare na hapa jamvini wapo wenzetu waliamini

Katika kati ya siku 64 Trump akasema hakujua ni kitu complicated namna hiyo. Mbele ya safari akasema ilikuwa vema kuanza na tax cut kabla ya kufikiria kuiondoa Obamacare

Alichofanya ni kuacha Speaker Paul Ryan aandike bill kwasababu Trump hakuwa na kitu na GOP hawakuwa na blue print kwa miaka 7. Hivyo waliandika kuanzia mwanzo kama kitu kipya

Yote yalifanyika kwa haraka na kusahau factors nyingine zinazoweza kuathiri matokeo ya nyuma

1. Trump alikuwa na vita na 'the establishment' wakati wa kampeni akiwatukuna na kudai kubadilisha Washington. Hakuelewa nguvu ya the establishment ndani ya DC

2. Republican hawakuelewa nguvu na umaarufu wa Obamacare pamoja na mapungufu iliyo nayo

3. Trump hakuelewa Republicans wana makundi makubwa, kwanza, the establishmen,moderates halafu kuna Conservatives ambao ni far right.

Hawa conservatives sasa wanajulikana kama Freedom caucus, lakini ndiyo Tea Party waliompinga Obama na kumdahlilisha kila mara wakiongozwa na akina Hannity, Bannon na Breitbart, Rush Limb.
Hawa ni supremacist kweli kweli na ndio waliongoza sehemu ya kampeni ya Trump katika media

Kwanini wameshindwa kuondoa Obamacare?

Inaendelea........
Marejeo
 
ACA YASHINDWA (Sehemu ya II)

Katika kampeni Republicans walicheza vizuri sana kutoonyesha nini sera yao kuhusu afya
Walitumia Obamacare kuinanga na kuonyesha mapungufu bila mbadala. Walikuwa na sababu

Trump aliahidi kuifuta Obamacare siku ya kwanza, hakuwahi kuonyesha mstari mmoja wa sera yake

GOP na Trump walijua, Obamacare ambayo kimsingi ilijengwa katika misingi ya Republican imesukwa katika hali ambayo ni ngmu kuondoa kipande kimoja bila kuudhi sehemu ya jamii

Mategemeo yao yalikuwa kuifuta pindi wakipata WH, house na seneti amabazo sasa wanazimiliki
Obama aliwaambia Dems, waache GOP waifute wenyewe kama wanataka bila kuwapinga

Trump kama ''deal maker'' akaanza kuita GOP kwa makundi kuwashawishi.
Hii haikuwa bill yake bali imetengenezwa na house Rep chini ya Ryan

Rais Trump alijua jinsi ilivyo complicated akawaambia waahirishe hadi mwaka mmoja upite
Ryan akasema hii ndiyo nafasi wana majority house na seneti na kwamba itapita bila kutegemea 60%

Mswada unaomabatana na bajeti hupitishwa kwa simple majority na walitegemea kufanikiwa
Spika Ryan akatengeneza kinachoitwa America Health care act ili ku repeal and replace Obamacare

Tatizo
Rejea makundi matatu bandiko la awali. The establishment wana msimamo wa kati kwamba kuna mambo yatakayotakiwa marekebisho, lakini wanakubaliana na hoja ya ku repeal and replace
Ndani ya nyoyo zao wana reservation dhidi ya Trump na ubabe aliowafanyia, walimsubiri

Moderates wanatatizika, kwasababu repeal and replace ndiyo msimamo wa GOP.
Wanaona Obamacare inawasaidia hasa upande wa state ambako suala la medcaid ni maarufu

Tea party ambao ni Freedom caucus na ambao ni conservative hawataki kusikia kitu Obamacare
Kumbuka hawa ndio wenye vyombo vya habari na walikataa wazi wazi. Wanataka ifutwe yote

Trump anatambua watu milioni 14-20 watapoteza insurance na wapo wa medcaid, akina mama na wenye maradhi ya muda mrefu wanaonufaika na Obamacare.

Hataki kufuta anataka kbadilisha sehemu kadha wa kadha akiacha mazuri ya Obamacare

Hapo ndipo timwbili lilipoanzia na kuzima jaribio

Inaendelea
Bandiko la March 31 2017
 
  • Thanks
Reactions: dtj
TIMBWILI NA 'DEAL MAKER' (Sehemu ya II)

Walioangausha Ryancare ni freedom caucus na Trump.
Rais Trump alijaribu kufanya deal za kiutawala kwa mtindo wa deal za biashara zake

Haikuwa rahisi kama alivyodhani na alivyowahi kufanya kwa kuzuia makampuni kuondoka

Wananchi walikuja juu wakitaka kujua masilahi ya kila kundi katika mikutano ya wabunge na maseneta wa Rep. Hii ilikuwa na mkono wa Dems walioeleza wananchi athari zinazofuata

Wabunge na maseneta wa Rep waliona hatari katika miaka miwili ijayo na uchaguzi mkuu
Kuna hali ya kuchanganyikiwa kila mmoja aliona vema asimame na district yake

Najimbo yenye conservatives wengi yaliwalazimisha tea party au freedom caucus kusimama na msimamo wao vinginevyo wangepoteza midterm elections

Moderates na establishment nao walifuata misimamo ya district zao , wakitaka mambo kama ya family health, medcaid, insurance kwa familia yaangaliwe kwasababu yaliathiri district zao

Kuyaleta makundi hayo pamoja ku repeal and replace Obamacare haikuwa kazi rahisi
Trump alijaribu bila maafikiano. Ryancare ikishindikana wakisema ni dead on arrival

Rais Trump ameongea kwa unyenyekevu akieleza jitihada za wabunge wa Republicans na Spika Ryan.

Hakugusia nani waliohusika ikizingitiwa alihitaji Republicans 20 hadi 30 na waliokataa ni zaidi ya hapo. Deal alifanya na GOP hakusumbuka na Dems, GOP wanaweza kupitisha bila kura ya Democrats

Kwanini hakulaumu GOP aliwalaumu Democrats?

Trump alisema mswada umekwama kwasababu hakupa ushirikiano wa kura haa moja ya Democrats
Hili wapiga debe wote wanalizungumzia na kutupa lawama Dems ,mkakati tu wa kukwepa hoja

Trum amekuwa mwangalifu sana kuwaluamu Republicans kama freedom caucus akijua wana nguvu. Hakugusa the est. kwa ushwishi wala moderates, hahitaji upungufu wa kura katika mambo yajayo

1. Kuna tax cut ambayo inaelekea kufeli kabla ya kufika kama Obamacare.
2. Kuna infrastructure spending ambayo inahitaji kura kama Obamacare

Tea party au Freedom caucus au conservatives wanasema tax cut ni nzuri, pesa zitatoka wapi kuendesha serikali? Hawataki kukopa kwasababu deni la taifa ni sehemu ya mambo wasiyotaka

Infrastructure itahitaji trilioni na ushee. Kukiwa na tax cut kiasi hicho kitatoka wapi?
Vinginevyo denilitaongezeka. Hapa moderates na the establishment wataungana na freedom caucus

Mkakati wa kutupa lawama kwa Democrats ni mbaya.
Dems wanasema Trump hakuwafikianamna ya kuboresha Obamacare, kufeli ni mzigo wake.
Wanasema waliompinga Trump na Ryan na freedom caucus.

Kauli hiyo inazidi kuwachonganisha republicans.
Lakini baya zaidi, bado atawahitaji Dems katika kupitisha miswada mingine

Jana Spika Ryan kwa uchungu kaeleza wazi 'Obamacare remains the law in the land'

Pigo la nguvu kwa Trump. Inaendelea
Haya ndiyo yaliyokwamisha tena Trumpcare


Kwa kumbu kumbu tu, wenzetu waliambiwa na kuamini kwa dhati kabisa kuwa Trump 'ataifuta ACA' kwa kalamu. Hawa wenzetu katika jamvi hawakutuelewa, nadhani sasa watatuelewa.

Haya ni masuala yanayohitaji uchambuzi si ushabiki.

Republicans wapo katika wakati mgumu sana. Miaka 7 ya kubeza Obamacare ACA haijaweza kuifuta na kama itawezekana itabidi sehemu ya Obamacare ibaki. Neno ku repeal halitakuwa na maana iliyokusudiwa

Kama tulivyosema, Obamacare ilisukwa kiasi kwamba kuigusa lazima utagusa sehemu ya jamii
GOP wanaweza kabisa kuifuta kwa jina si kwa contents kwasababu kuna masuala 12 wamekubaliana wayaache, na hayo ndiyo yanawagawa

Kuna conservatives wasiotaka serikali ijuhusishe kabisa na masuala ya kusaidia Health
Kuna Moderates ambao kubomoa Obamacare kunagusa wapiga kura wao.

CBO wanatoa makadirio Obamacare bado inabaki kuwa bora kuliko zinazojadiliwa

Hawa ndio wanaotengeneza seneta wasiotkubaliana na Health act ya Trump ambayo yeye mwenyewe hakubali kuwa ipo sawa akiita 'mean'

Kinachofanywa na Trump sasa hivi ni kuhujumu Obamacare kwa kuzuia pesa ili ife yenyewe
Kwa bahati mbaya hilo limejulikana na wananchi wanaonekana kutokubaliana nalo

Chochote watakachokifanya kuhusu Obamacare, kitawagharimu GOP.

Tusemezane
 
Haya ndiyo yaliyokwamisha tena Trumpcare
Chochote watakachokifanya kuhusu Obamacare, kitawagharimu GOP.

trumpputincare-jpg.533366


Ha ha haaa...!​
 
ACA (OBAMACARE): GOP WANAFIKIRI REPEAL KWANZA REPLACE BAADAYE

Sehemu ya I

Maseneta wameendelea kugawanyika idadi ya wanaopinga kufikia 9 mbali na wasiotaka kujitokeza

Katika hali isiyo ya kawaida kundi la Superpack linalochangisha fedha za uchaguzi limemshambulia Senator Heller wa Nevada aliyepinga mswada wa kufuta ACA

Hoja ya senator Heller ni kuwa kuondoa ruzuku ya medicaid kutaumiza wapiga kura yake
Superpack wakamshambulia kama kitisho kwa maseneta wengine wanaopinga

Kuna maseneta kama Paul wanaotaka Obamacare ifutwe kabisa kitengenezwe kitu kingine ambacho serikali haitakuwa na mkono wa ruzuku wala mandate. Kila mtu na njia yake

Kundi la tatu ni la moderates wanaosema Obamacare ifumuliwe na kuacha baadhi ya mambo

Kwanini Medicaid na pre existing conditions?

Medicaid ni ruzuku kwa watu wa kipato cha chini. Pre existing condition ni kuwalinda consumers wasifanyiziwe na insurance Company.

Yaani ukiwa na maradhi insurance yako isiamuliwe na hilo
Na mwisho kuna suala la watoto kubaki katika insurance za wazee wao hadi umri fulani

Waathirika wa kufutwa kwa Medicaid ni watu wenye umri mkubwa wanaotegemea ruzuku kama wastafu. Katika kundi hili kuna wastaafu wa maeneo ya madini n.k.

Pre existing condition ni maradhi ya kudumu kama ya moyo, kisukari, kansa, kifafa, Multiple sclerosis n.k ambayo ni ya kawaida kwa jamii ya Wamarekani. Kila mmoja anaweza kuangukia hapo

Mwendesha show maarufu Jimmy Kimmel alipata mtoto aliyezaliwa akiwa na matatizo ya Moyo
Kimmel alisema, maana yake ni kuwa ana pre existing condition kuanzia alipotoka tumboni
Aliuliza, kwa wasioweza hilo ni tangazo 'la kifo' insurance itakuwa juu kwa miaka atakayoishi.

Tunayarudia haya kama yanavyojidhihiri ili kuelewa kwanini Trumpcare inagonga mwamba na kwanini itakuwa mwiba mkali mbele ya safari kwa hali yoyote iwayo

Senate Healthcare Bill inasemaje kuhusiana na hayo hapo juu na wapiga kura?

Inaendelea
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Sehemu ya II

Senate Bill inasema Medicaid iondolewe ili kupunguza gharama za uendeshaji na kukata kodi kwa kundi dogo la juu linalotoa kodi kuigharamia. Pre existing condition ibaki wakati kuna maseneta wanapinga

Hii ina maana gani kisiasa?
Kwamba kundi la matajiri wanaolipa kodi kufidia Medicaid litaendelea kumuunga mkono Trump
Kundi hilo litakuwa limepata tax cut kwani business ni nzuri

Kundi hilo dogo la asilimia isiyozidi 10 litafaidika na kufutwa kwa lazima ya kampuniyenye watumishi zaidi ya 50 kuwanunulia Insurance. Business haitakuwa na mzigo wa kuchangia bima ya mwajiriwa

Kundi hili la wafanyabiashara litachanga na kufanya kila jitihada Trump aendelee kwao ni ahueni
Trump atakuwa ame score political point kubwa na mtaji wa fedha za kampeni. Nzuri kwake

Upande wa pili, waathirika wa pre existing condition na Medicaid ni makabwela wa vijijini

Hawa hawakubaliani kabisha na mswada wa seneti na ndio wapiga kura wa Trump
Trump atakuwa amepoteza sehemu kubwa ya wapiga kura na itamwathiri sana

Ikumbukwe kuwa Rais Trump aliwaahidi makabwela kutoondoa Medicaid na pre existing condition

Mswada wowote utakaogusa hayo utamchanganisha na wapiga kura wake wengi kuliko matajiri

Hili ndilo limesababisha Trump akaita mswada huo 'Mean'

Kiitikadi akiwa tajiri na mfanyabiashara hataki dhana ya medicaid au pre existing condition
Kisiasa makundi yanayoguswa na vitu hivyo ndiyo wapiga kura wake. Yupo njia panda

Ushiriki wa Trump umekuwa wa kuingia na kutoka na kuvizia mafanikio.
Katika House mswada uliposhindwa lawama Spika Ryan, sasa anamtupitia senate majority McConnel

Mswada unaonekana kukwama si kwasababu ya Dems bali Republicans wenyewe kwa wenyewe

Trump amepata wazo kutoka kwa Conservative wanaopinga Senate Bill
Wazo hilo ni kufuta kwanza Obamacare, halafu muda upite ili Dems na GOP wakae pamoja

Je makakati wa kufuta Obamacare na kusubiri muda upite itengenezwe bill nyingine ni mzuri?

Tutajadili bandiko la III
 
  • Thanks
Reactions: dtj
Sehemu ya III

Obamacare ni maarufu licha ya mapungufu yaliyopo.
Imesadia wanyonge na makabwela.Kuifuta hakutaungwa mkono na Democrats hata kwa bahati mbaya

Dems wanasema, kinachotakiwa ni kufanyia marekebisho mapungufu ya Obamacare
Ni kwa njia hizo tu wataweza kukaa meza moja na GOP

GOP na Trumps waliahidi kuifuta Obamacare mara moja, wakapata House na Senate na Magavana

Kadri Rais Trump anavyohujumu Obamacare kwa kuzuia pesa za Medicaid ili ife,wananchi wanagundua uzuri wa Obamacare kwani wanaonja machungu

Mtihani mkubwa upo Republicans.
Kufuta Obamacare kutasubiri zaidi ya mwaka ili kupata kitu kingine

Conservative na Trump watafurahi kwani watakuwa wametimiza ahadi ya kufuta Obamacare tu
Moderates Republicans watakuwa na wakati mgumu kueleza wapiga kura nini mbadala wake

Katika kpindi cha mwaka tayari kutakuwa na midterm elections.
Wananchi watatoa hukumu kwa kuzingatia machungu ya kutokuwa na Healthcare insurance.

Republicans wanaweza kupoteza Senate au House.
Kupoteza kimojani kumweka Rais Trump katika wakati mgumu wa kueleza nini kimetokea ikiwa;
- Alisema ni deal maker, mbona deal zimekwama
- Alisema anabadilisha Washington, Mbona DC ndiyo imembadili
-Aliahidi Healthcare nzuri, itakuwa wapi wakati huo na kwanini alifuta kabla ya mbadala

Kuelekea 2020 Rais Trump atakuwa na mengi ya kujibu kuliko kueleza.
Healthcare inayochukua 6% ya Bajeti na inayoajiri itapoteza nafasi za kazi

Unaweza kuona madhara ya karata yoyote watakayocheza itakuwa na matatizo.
Obamacare ita define kwa sehemu kubwa legacy na hali ya baadaye ya uchaguzi wa 2020

Ukichanganya na matatizo ya dunia yanayoisubiri US kama Korea, vita Iraq, Afhganistan ,middle east na mengine ikiwemo mahusiano na washirika kama NATO n.k. utaona kwanini Rais Trump ni frustrated

Frustration kama za kuandika tweet na kubishana zinazomshushia hadhi na heshima ni kutokana na kukwama mambo mengi aliyodhani ni Rahisi tu akimuita Obama 'stupid'

Tusemezane
 
MKUTANO WA G-20 (Sehemu ya I)

Wiki mbili zilizopita Rais Trump alikuwa na mtafaruku na wanahabari kutokana na tweets zake
Mjadala uliotawala si sera bali nini anaandika na nani anabishana naye kila asubuhi

Huu ni mwendelezo wa 'mapambano' dhidi ya baadhi ya vyombo vya habari visivyo 'rafiki'
Tangu ameingia Ikulu mahojiano mengi amefanya na TV ya FOX kama chombo rafiki

Ametuhumu sana TV ya CNN na NBC kwa kuita habari zao ni 'fake' hata pale anapoanzisha habari hizo mwenyewe. Ukweli ni kuwa Rais Trump hataki vyombo vinavyoonyesha nini alisema siku za nyuma na nini anasimamia sasa akidhani vinamuumbua

Habari ya Russia inamtibua nyongo kwani imetawala zaidi kuliko sera zake ambazo nyingi hazieleweki zinasimamia nini.

Ugomvi wake na Intelligence community( IC) na Wana habari (media) ni wa siku nyingi

Akiwa Poland, Rais Trump alisoma hotuba iliyopokelewa vyema na pande zote za siasa
Hotuba anazosoma haziwakilishi mtazamo wa yeye anafikiri nini na kwa sababu zipi

Baada ya hotuba, alikuwa na mkutano mfupi sana na wana habari akiulizwa kuhusu Russia

Rais Trump kwa kujua au kutokujua alionyesha kukosa imani Intel community za nchi yake

Alisema, kuna uwezekano Russia wali hack au nchi nyingine, hakuna mwenye uhakika na hilo

Kauli ilipingana na Itel community zilizothibitisha mbele ya kamati za Bunge na Seneti Russia ilifanya hivyo bila shaka. Hizi ni intel comm zipatazo 16 kwa pamoja zikikubaliana na hilo

Kauli hiyo imemtia katika wakati mgumu hasa alikutana na Rais wa Russia V Putin

Kukutana na Putin lilikuwa jambo muhimu ambalo asingeweza kulipuuza kutoka na hali ya US
Uchunguzi unaoendelea na ambao wachunguzwa ni washirika wake ungezua utata mkubwa

Kwa kuelewa hilo, mazungumzo kati yake na Putin yalihusu Russia na uchaguzi n.k.
Rais Trump hakupenda alilazimika kutokana na wingu la Russia investigation lililotanda

Putin amweka kwenye Kona, DC yanazungumzwa mengi.

Inaendelea...
 
  • Thanks
Reactions: dtj
MKUTANO WA G-20 (Sehemu ya I)

Mkutano wa Trump na Putin ulihudhuriwa na mawaziri wa pande mbili wa mambo ya Kigeni
Wengine ndani ya mkutano ni wakalimani kutoka pande mbili

Taarifa za pande zote zinasema Rais Trump aliibua hoja ya Russia na uchaguzi katika mkutano
Alisema kwa masilahi ya wananchi wa nchi yake, anapaswa kumuuliza Putin kuhusu hilo

Hili ni jambo zuri sana kisiasa kwani limesaidia kwa sehemu kuonyesha kuwa pengine hahusiki na suala la Russia na uchaguzi ndiyo maana ameliibua. Alifanikiwa kupooza joto kwa wakati

Nje ya mkutano kauli zake zimechambuliwa na wachambuzi wa masuala ya kijamii na kuonekana kuna hoja na maswali zaidi, hivyo ukubwa wa tatizo la kauli umemweka pagumu

Taarifa ya waziri wa US aliyekuwa katika mkutano imeeleza kuzungumzwa jambo hilo na Rais Putin amekana kama kawaida. Tillerson alitaka kueleza umma jambo limezungumzwa

Waziri wa mambo ya nje wa Russia S.Lavrov ilisema Putin alimuuliza Rais Trump atoe ushahidi wa Russia kuhusika, Trump hakuwa nao. Taarifa ikasema Trump alikubaliana na hoja za Putin

Rais Putin alitumia udhaifu wa Rais Trump kutilia shaka intel community zake na kauli kuwa hakuna anajyejua nani amehusika , kumweka Trump kwenye kona aliyoshindwa kutoka.

Kushindwa kwa Diplomasia na inavyomgharimu Trump

Inaendelea.....
 
MKUTANO WA G-20 (Sehemu ya III)

Ni kawaida mikutano mikubwa kama wa G-20 viongozi huongea na wanahabari kuhusu 'position' zao juu ya masuala mengi yaliyojitokeza. Ni utamaduni wa wa mikutano yote

Ikumbukwe, Rais Trump katika ziara ya Uarabuni/Ulaya hakuongea na waandishi wa habari

Ndivyo alivyofanya katika mkutano uliokwisha ingawa aliongea na waandishi wawili wanaosemwa walipangwa mahususi kule Poland

Putin aliongea na waandishi akisema Rais Trump alikubaliana na hoja Russia haikuingilia US

Wakati anafanya 'timing' hiyo Trump na timu yake walishaondoka

Hili liliwakuta off guard ndani ya Air force one na hivyo dunia na US kwa ujumla kuelewa alichozungumza Putin ndicho walichozungumza.

Putin amemchongea Trump US bila majibu, ni udhaifu wa diplomasia wa serikali ya Trump

Maswali yanayomwandama sasa aliporejea US ni haya

1. Kwanini alivituhumu vyombo vya usalama Itel comm vya nchi yake mbele ya uso wa dunia
2. Kwanini alisema inaweza kuwa Russia au nchi nyingine ikiwa ana access na classified info
3. Kwanini alisema analazimika kueleza concern za wananchi, ikiwa yeye haamini katika hilo
4.Kwavile haamini ni Russia pekee, kwanini aliibua hoja katika mazungumzo na Putin
5. Kwanini hakuongea na waandishi kukubali au kukana kauli ya Putin kuwa alikubali hoja
6.Kwanini anamtuhumu Obama kutofanya lolote ikiwa haamini Russia iliingialia uchaguzi

Haya na mengine mengi yatatanda katika viunga vya habari za DC katika wiki hii.

Trump ni mtaalamu wa kubadili mada, haitachukua muda ata tweet jambo lenye utata kuzima hoja hizo. Hilo litatokea kati ya Jumapili hadi Jummane!

Kwenda mbele suala la Russia ni liability kubwa sana katika siasa za US.

Inaendelea..
 
Back
Top Bottom