Duru za Siasa: Marekani (U.S) Chini ya Donald J. Trump

MKUTANO WA G-20 (Sehemu ya IV)

Mkutano uliomalizika haukuwa na taswira nzuri kwa US. Nchi 19 zilisaini makubaliano kuwa maazimio ya Paris kuhusu climate change hayabadiliki miongoni mwao.

Ilikuwa ni 'kibao' usoni kwa Rais Trump aliyeiondoa US katika maazimio ya Paris.
Ilijibu hoja ya Trump, nchi 19 zinaamini maazimio ya Paris siyo alivyosema Trump Pittsburgh

Nchi za Japan, Ujerumani, India na nyingine zilisaini mikataba ya biashara baina yao
Ni linatokana na sera za 'America first' zinazotishia biashara na nchi hizo hivyo kuangalia namna nyingine ya ushirikiano nje ya US

Kwa mfano, Trump alitoa fursa kwa makampuni ya magari kurudisha utengenezaji US kutoka Mexico. Katika hilo aliacha nje makampuni ya Japan na Ujerumani

Trump alifanya hivyo kuwakomoa Mexico, kurudisha ajira US na kuleta makampuni ya nje

Nchi hizo nazo zimeingia makubaliano na Mexico ili ziweze kutengeneza bidhaa zao karibu na soko la US. Mexico nayo itatoa incentives ili kupata ajira kwa watu wake.

NKOREA:
Inasumbua US kwa sasa. Juzi Rais Trump aliilaumu China kuwa na biashara na Nkorea
Hapa alidhamiria kuweka shinikizo kwa China ili iiewekee vikwazo Nkorea.

Tarehe 29 serikali ya Trump ilidhinisha takribani Bilioni 1.4 za mauzo ya Silaha kwa Taiwan
China inatambua eneo hilo kama jimbo lake, jambo lililoiudhi sana

Mtakumbuka hili tumelijadili mwezi wa kwanza, kwamba Trump hakuelewa siasa za dunia

Kuibana China isaidie Nkorea kuacha silaha za Nyuklia inategemea mahusiano ya kimataifa

China inasema itasimama na UN ya vikwazo ingawa kuna 'negative' zinazojitokeza.
Hapa aliinyooshea US kidole kuwa ikiuza silaha Taiwan, China atamkubatia Nkorea

Korea Peninsulla haihusu China tu, kuna Russia, Iran na mataifa mengine. Vitisho havitoshi
Ingawa alimalumu sana Obama, Trump haonekani kuwa na mkakati kuhusu Nkorea kwa sasa

Kwa ufupi, mkutano wa Ujerumani umemalizika bila 'deal' kwa US. Kwa Rais aliyemsema mtangulizi wake vibaya na akijinafasi kama mfanya 'deal' hali si nzuri kwake hata kidogo

Kikubwa kilichoonekana ni US kupoteza uongozi 'leadership' katika uso wa Dunia.
Chancellor Angel Merkel ndiye anayeoonekana kama kiongozi wa 'free world' kwa sasa

Ushwaishi wa US katika siasa za duni unaanza kupoteza nguvu unless hali ibadilike mbeleni

Tusemezane
 
VUMBI VIUNGANI DC
TWEETS NA KAULI ZINAMRUDI RAIS
'RUSSIAN COLLUSION' YACHUKUA SURA MPYA

Rais Trump amerudi Wasgington,DC baada ya mkutano wa Hamburg ambako sehemu kubwa alishindwa kuonyesha makali yake kama 'Deal maker'

Jambo analozungumzia kupitia waziri wake Tillerson ni kusitishwa kwa mapambano kule Syria kutokana na mazungumzo kati yake na Rais Putin

Asubuhi na hadi jioni hii Rais Trump ametuma tweets nyingi zilizoamsha vumbi viunga vya DC
Moja ya tweet ni inasema 'it's time to move on' akimaanisha ameshazungumzia Russia collusion

Kauli hiyo imewaudhi watu wakimwemo wa chama chake na hasa maseneta waliyopinga vikali
Kinachosemwa ni kuwa haiwezekani Russia kuachwa tu kwavile ameshazungumzia

Kikubwa zaidi ni jinsi ambavyo kauli yake dhidi ya intel comm inavyozidi kudhalilisha taasisi hizo

Tweet nyingine ' wamekubaliana na Putin kuwa na cyber security unit' kuhakikisha hayajirudii.

Kauli imeudhi maseneta kama Rubbio 'haiwezekani kutengeneza 'unit' na jizi lililovunja nyumba yako'

Kauli hizo zinashadidiwa na hoja kuwa Trump hakukanusha kauli ya Putin ya kukubaliana naye
Kwa wachambuzi hilo wanaliona kama 'concessions' kukiri na udhaifu mbele ya Kremlin

Hali ya leo haikuwa nzuri, baada ya NY kueleza mkutano wa mtoto wa Trump, mkwewe Kushner na kampeni meneja wakati huo (June 20.. , 2016), Trump Jr alijitokeza kwa kusema alikutana na Lawyer kutoka Russia kwa mkutano kuhusu sheria ya adoption ya watoto

Gazeti la Washington post likatoka maelezo zaidi ambapo mtoto wa Trump akakiri kukutana na lawyer huyo kwa kile alichosema 'ana habari za kumharibia Clinton'

Trump Jr amekanusha kuhusu suala hilo kuhusishwa na baba yake na kwamba mzazi wake hakujua uwepo wa mkutano huo na Lawyer kutoka Russia

Mkanganyiko wa kauli za Rais Trump kuhusu Russia na tweets, matokeo ya mkutano wa Hamburg, kukosekana kwa diplomasia, kushindwa kukanusha kauli ya Putin na hili la Mwanae na Jared ndiyo habari ya DC kwa sasa na pengine wiki nzima ijayo

Ni kwanini hizi ni habari na zina ukubwa gani kisheria na kisiasa?

Inaendelea sehemu ya II

 
VUMBI VIUNGANI DC
Sehemu ya II

Tuzipitie hoja za bandiko [HASHTAG]#342[/HASHTAG] kwa undani wake

Rais Trump ameendelea na tweets akisisitiza kuliongelea suala la Russia hacking na Putin

Trump ametambua, kuliongelea kutaondoa utata wa kwanini hakuzungumza na Putin
Kwa njia hiyo litamsafisha na tuhuma za ushiriki wake katika sakata. Mkakati mzuri

Matatizo yanayomkabili
1. Kwanini alisema 'anauliza suala hilo kwasababu lina concern za wananchi wa US'?
Wanaohoji hili wanaunganisha na kauli zake katika mkutano wa Poland

Kwamba, ilikuwaje akazungumza na Putin ikiwa hakuamini intel community
Ilikuwaje akazungumzia hilo ikiwa anaamini kuna nchi nyingine zimehusika

2. Waziri Tillerson alisema Putin alielezwa tuhuma na kuzikanusha kama kawaida

Hoja: Kwanini Putin aliposema ' alikataa suala hilo na Trump alikubaliana naye' WH na Trump hawajakanusha? Hili linatoa picha alichosema Putin ndio ukweli

3. Rais Trump anasema wamekubaliana kuwa na timu ya cyber security kwa pamoja

Hoja: Kwanini anaunda tume na mtu anayetuhumiwa kuingilia uchaguzi wa Marekani?
Kwanini hakusisitiza vikwazo zaidi kwa Russia amekubali kuwa na tume

4. Rais Trump anasema '..move on' yaani watu waache hilo waendelee na mengine

Hoja: Ina maana uchunguzi wa Mueller, Senate na Congress visitishwe!
Je, kuna majibu gani ya kuzuia hali isijitokeze siku zijazo.Ni msamaha au ni kitu gani

5. Mtoto, Trump Jr ,Jared Kushner na Kampeni meneja Manufort walihusika katika mkutano na Lawyer Natali V kutoka Russia.

Kwamba, Lawyer alikuwa na habari za 'kumharibia' Clinton na baadaye kubadili topic

Hoja: Kwanini Trump Jr hakueleza hilo NY iliporipoti kwa mara ya kwanza.
Katika taarifa kupitia mwanasheria, Trump Jr alisema mkutano ulihusu ' adaption'

Kwanini taarifa ya pili aliyoitoa baadaye ilieleza kushiriki mkutano na Lawyer ambaye alikuwa na taarifa za 'kumvurugia' Clinton Kampeni

Hoja inayojitokeza ni kuwa Kushner mshauri WH alikuwepo katika mkutano.
Paul Manufort kampeni meneja alikuwepo kwenye mkutano

Manufort kwa wadhifa kama meneja aliingia vipi kwenye mkutano uliohusu 'adaption'

Ikiwa kuna mtu wa taifa la nje alitaka kuingilia uchaguzi wa US iweje Kushner, Trump Jr na Manufort hawakuchukua hadhari ya kuviarifu vyombo vya ulinzi na usalama!

Taarifa zilizopo, Lawyer aliunganishwa na timu ya Trump kupitia 'mwanadalizi' wa miss Universe, Russia,shindano ambalo CEO alikuwa Rais Trump.

Kisheria ni mapema mno kusema Trump Jr, Manufort na Kushner walifanya kosa.
Kukutana na Lawyer wa Russia haliwezi kuwa kosa ikiwa hakuna jingine zaidi ya hilo

Kisiasa sakata linachukua sura mpya na kuweka makazi WH na si washiriki binafsi

Pengine Trump hakushiriki,kauli zake zinachochea udadisi badala ya kumwepusha.

Trump aliwahi kusema 'Si yeye wala mtu wa kampeni yake aliyewasiliana na Russia'
Ilipofikia,washiriki wanaochunguzwa ni wa kampeni yake,hili la Trump Jr linaeleza

Iwe kuna ukweli au hakuna , Rais Trump anachochea moto pengine usio na sababu.

Ugomvi na Intel comm matokeo ni Intel comm kum'prove wrong' kwa taarifa walizo nazo.

Ugomvi na media ndio huu unaoibua matimbwili kila uchao

Mchawi si Intel comm, si media au Democrats, ni Rais Trump mwenyewe
Mwenzetu Mag3 aliwahi kusema ''mtu anatupiwa kitanzi na kujifunga mwenyewe''

Tusemezane
 
HABARI ZA UTATA ZINAONGEZEKA

''RUSSIA COLLUSION IMEPIGA KAMBI WH''

Awali, mabandiko mawili yaliyopita tulikumbusha kuwa hali iliyopo viungani DC ina usumbufu kwa Rais Trump, angependa kubadili maongezi kwa Mbinu zake zinazochuja

Baada ya sakata la mwanawe Don Jr kuhusishwa na mkutano wa Russia, Trump ali tweet kuhusu cyber security aliyosema ataanzisha na Russia.

Kauli hiyo ilitolewa na Sec Tillerson baada ya mkutano wa G-20.
Vumbi likatimka Dems na GOP likimchana wazi kuhusu mpango waliouita hovyo

Trump akalazimika ku tweet na kusema hilo halitawezekana akimtosa Sec Tillerson

Alifanya hivyo kwa mambo mawili, kukwepa madongo kutoka pande zote,pili kubadili maongezi ya Trump Jr na kundi lake ililoshiriki mkutano na Lawyer wa Russia Natalia V

Mbinu haikupunguza joto mitaa ya DC, mwanawe akikabiliwa na tuhuma nzito

Trump aka tweet kuhusu ugomvi na Comey kwamba ame leak classified information. Mbinu haikusaidia, Prof aliye leak information akasema hakupewa class. info

NYT ina ripoti watu 3 walioona email alizotumiwa Don Trump Jr zikieleza '' nia ya kukutana naye ili serikali ya Russia iweze kumsaidia katika kampeni''

Hakuna uhakiki wa email ingawa zinasemwa zimetoka katika source 3 tofauti.
Katika zama hizi za teknolojia ni mapema mno kusema ni kweli au la. Lakini ndiyo habari

NYT ndio waliomtoa Trump Jr kufafanua mara mbili katika akiwa na version tofauti
Habari hizi si nzuri ikiwa ni za kweli, ile link ya Russian collusion inaweza kupata njia

Habari zinavyotoka, ni kana kwamba kuna timing na hiyo ndiyo media house ya US
Ugomvi wa Trump na media si busara, kama tulivyosema watataka ku prove him wrong

Hadi sasa watuhumiwa ni wengi baadhi yao ni hawa

Sec Session aliyejivua wadhifa wa uchunguzi baada ya kukana habari a mwisho kukubali
M.Flynn aliyejiuzulu kama national security advisor baada ya kukana na kisha kukubali
Kuna Page Carter aliyetarajiwa huenda angekuwa sec of state
Na Bwa Roger ambaye ni mshiriki wa Trump

Watu wa karibu sana na Trump wanaotuhumiwa

Paul Manufort aiyekuwa kampeni meneja na aliyeshiriki mkutano na Lawyer Trump Tower
Jared Kushner, mshauri wa Ikulu ambaye pia ni mume wa Ivanka Trump
Na sasa Donald Trump Jr ambaye ni mtoto wa Rais Trump

Wote hao walikuwa washiriki wa Kampeni ya Rais Trump akyesema hakuna mtu anayemjua aliyeshiriki katika mahusiano na Russia

Nini kinajadiliwa? Inaendelea...
 
HABARI ZA UTATA (II)

Hakuna anayejua mkutano wa dk 20 wa Don Trump Jr, Jared Kushner na Paul Manufort ulihusu nini ingawa wanasema haukuwa na lolote baada ya Lawyer kubabaisha

Tatizo linalojitokeza ni Trump team ilikubali habari za m-Russia zinazomhusu Clinton.

Hakuna ushahidi wa uhalifu hadi sasa, lakini mazigira yanazua maswali

1. Baada ya kusikia kuna mtu wa Kremlin ana habari za Clinton kampeni, Trump Jr alitoa taarifa kwa vyombo vya usalama?

2. Kwanini story inabadilika kila mara. Mwaka jana alikana kuhusika na Russia akiita habari ni Phony. Mwaka huu akasema hana kumbu kumbu zozote kuhusu hilo

Baada ya NYT kuandika Juzi, Don Trump Jr akatoka na version ya kwanza.
NYT walipotoa tena naye akaja na version ya 2, na leo baada ya email amekuja na jingine

Ikiwa hakuweza kukumbuka mwaka mzima imekuwaje amekumbuka katika siku mbili?

Uwepo wa Email kama zikithibitika ni kweli una tatizo.
Kwanza, alijua alichoitiwa ikiwa ni kupata habari za 'kumdhuru' Clinton kutoka Russia. Je,ilikuwa sahihi ikizingatiwa ni Russia?

Pili, kwa mujibu wa email ambazo tunarudia hazijathibitishwa ilisema ' ... serikali ya Russia isaidie kampeni dhidi ya Clinton' .

Kauli hiyo itaingia nyongo kwa Wamarekani ikiwa ni kweli

Pamoja na hayo kuna mswada katika Seneti kuhusu kukaza vikwazo dhidi ya Russia
Mswada umerudishwa House ukiwekewa uzio kwamba vikwazo vikazwe zaidi

WH inataka vikwazo viligezwe. Hili tu linatia shaka, ikiwa mswada umeungwa mkono na Dem na GOP kwa 98 kwa 2 iweje Rais Trump pekee awe na 'huruma' na Russia?

Kauli ya '..move on' inatia shaka huku ikichagizwa na kauli ya cyber unit ya pamoja.
Ukiweka vyote kwa pamoja na ukivichambua, kuna shaka kuliko uaminifu anaoupata

Sakata linaendelea haijulikani litakuwa na matokeo gani ikiwa ni kweli au si kweli.

Inatosha kusema, sakata limepiga kambi WH na ikiwa habari ni za kweli, hali ya WH ni ngumu kuliko inavyotarajiwa

Tusemezane
 
Mkuu Nguruvi3, nilionya siku nyingi kuwa mambo ya Marekani hayataki kukurupuka na kwa hali ilivyo sasa ni kama vile wananchi wa Marekani wanatayarishwa kisaikolojia kuipokea grand finale. Hii haitatokea leo ama kesho lakini trust me kutokea itatokea tu watu wapende wasipende. Kuna info zinavujishwa makusudi ili kuwaandaa watu mapema wawe tayari kupokea ripoti ya Special Counsel itakapokamilika na nina wasi wasi kama itawaacha wahusika salama.

Tatizo la wahusika/watuhumiwa hawajui uzito wa ushahidi ambao umeshapatikana hadi sasa na hivyo kila tamko wanalolitoa ni hatari kwao kama halina ukweli na hivyo ushahidi kuzidi kujengeka. Bahati mbaya ni kwamba wameshindwa kufunga midomo yao na kukaa kimya, wanazidi tu kujitia kitanzi wanapotupiwa chambo na mwisho wa siku wanabaki wameduwaa. Huko WH watu hawalali na wanasutana na kulaumiana hadi wengine kutishia kujiondoa. Marekani naipenda.
 
DON,Jr, ATHIBITISHA EMAIL

MLOLONGO KUTOKA WH HADI KREMLIN UNAANZA KUJITOKEZA

Kijana mkubwa wa Rais Trum , Donald Trump Jr au Don Jr, ameachia emails leo
Hii ni baada ya siku nne za 'drip drop' kutoka gazeti la NYT

NYT ilimfikia Don Jr ikimtaka athibitishe email au watazichapisha. Don akawawahi akisema anataka uwazi
Emails ni kati ya Goldstone anayejulikana Russia akiwaunganisha Natalia V ambaye ni mwanasheria na Don

Kama yulivyoeleza awali, Natalia alikutana na Don, Jared na Manufort Trump Tower
Email zinaonyesha azma ya serikali ya Russia kusaidia Trump kampeni zikisema ni 'highly sensitive'
Don Jr alijibu ' kama ni hivyo nimependa''

Emails zinaonyesha mwimbaji Emin Agalarov ambaye baba yake ni real estate mogul kule Russia aitwaye Aras Agalarov wakieleza jinsi serikali ya Russia inavyoweza kumsaidia Trump

Aras akiwa real estate mogul waliwahi kukutana na Donald Trump katika biashara zao siku za nyuma
Mwanawe alishiriki kuandaa shindano la Miss Universe,Trump ndiye CEO wa taasisi hiyo
Wote wamewahi kujadili ujenzi wa majengo Russia, ni watu wanaofahamiana kibiashara

Email inaonyesha 'mwanasheria mkuu wa Russia' yupo tayari kutoa habari kwa wahusika zitakazowawezesha kumharibia Clinton na kumjenga Trump

Hii ina maana gani? Kwamba, Don Jr allikubali mkutano akijua nini kinaongelewa
Kwamba, yapo mawasiliano ambayo kwasababu alizosema Goldstone inabidi apitie kwa Don

Habari hizi zimezua vumbi zito viunga vya DC na kwingine ikizingatiwa Don Jr na baba yake Trump wamekana mara nyingi kutokuwa na mahusiano na Russia

Kwa hali ilivyo emails zimeonyesha 'Russia collusion' kwa namna fulani, swali ni je kuna nini katika mikutano mingine kati ya maafisa wa Russia na timu ya Trump?

Nini ushiriki wa Jared na Manafort katika mkutano unaosemwa Manafort aliapiga simu muda mwingi?

Natalia ametokea katika TV akisema si afisa wa Russia, hakutoa details nyingine

Tutajadili zaidi kadri habari zinavyojiri

Tusemezane
 
...

Ushwaishi wa US katika siasa za dunia unaanza kupoteza nguvu unless hali ibadilike mbeleni
Kwa mtazamo wangu Ni sahihi kabisa uliyoeleza kwenye hiyo post # 345 ya uzi huu.

Kama mtakumbuka nilisema HRC( mama) angeiangusha haraka sana US lakini Trump ataiangusha polepole. Uzuri, kwa haiba ya Trump, hata akiiangusha polepole he will get away with it. Mr. Putin katwambia Trump kwa kwenye TV siyo Trump wa kwenye makutano mahususi na wenzake. Trump 'mtata' kwenye mikakati ya kupata anachokitaka.
 
''FAKE NEWS ZINAPOKUWA REAL NEWS''

Kwa muda mrefu Rais Trump ameviandamana vyombo vya habari (baadhi) akisema habari za Russia collusion ni fake. Amefanya hivyo ndani na nje ya nchi yake

Wakati wa kampeni, Trump alizungumzia DNC ku rig election na kwamba atasusia matokeo ikibidi

Aliacha hali hiyo ikaendelea kwa muda mrefu. Leo inajulikana ni mbinu ya kuvielekeza vyombo vya habari nini wazungumzie wakati kampeni yake ikiendelea na 'mambo'

Kauli za fake news zililenga kuwaaminisha watu habari hizo si za kweli

Hapa jamvini tulijadiliana pia na kusema media za US ni tofauti, ni za kitaaluma

Trump alielewa lingewavunja waandishi nguvu ya kufuatilia kutokana na nguvu ya soko

Kuwavunja nguvu ili wasiendelee kufuatilia habari ambazo leo zinaanza kujitokeza

Uchunguzi unaendelea, ni mapema kuwa na conclusions
Kwa hatua ilipofikia kile alichokiita fake news sasa ni real news!

Sec Session yupo katika uchunguzi, ni fake news?
M. Flynn amejiuzulu nafasi yake, ni fake news?
Sasa Don Jr, Jared, Manafort wanakubali ''walitamani collusion'' , je ni fake news

Kama mtakumbuka, ujanja wa kuzua jambo kuhamisha mjadala ulifanikiwa wakati wa kampeni

Tulisema hapa wakati wa utawala hilo halitawezekana kwasababu anafuatiliwa kama kiongozi

Kila habari anayozua inajadiliwa kwa dk chache na waandishi wanarudi katika mada inayorindima

Rais ame tweet kuwa kijana wake ni transparent, ukweli, alichofanya ni pre preemptive baada ya kuambiwa na NewYork Times, wanachapisha emails kama ana lolote la kusema kabla hazijaenda hewani, akawahi

Hili la Don, Jr, limemweka Rais Trump mahali pagumu sana kusema fake news tena

Tusemezane
 
TRUMP Jr NA Emails

Emails alizotoa mtoto wa Rais Trump zimekuwa maongezi yalitawala anga za habari za US
Utetezi unaotolewa na Don Jr na maafisa wa WH umejikita katika mambo matatu

1. Kwamba Democrat walikuwa na kashfa ya Ukraine. Wasichoeleza FBI haikuona tatizo na kwamba kulinganisha na suala la Russia ni mambo mawili tofuati kabisa. Trump yupo katika uchunguzi wa FBI
Hoja haijibu hoja ya tatizo lililopo bali kufanya 'deflection'

2. Kwamba Rais Trump hakujua hadi majuzi. Picha zinazolewa zinaonyesha mahusiano ya karibu ya watajwa na Rais Trump wakiwa US na Russia kwa nyakati tofauti. Hilo haliwezi kumu 'implicate' Trump

Gazeti moja limeonyesha Trump alivyoshadidia uwepo wa 'dirt' baada ya mkutano wa Don na Natalia
Mlolongo wa kauli za Trump unaonyesha ni kana kwamba ''alikuwa anajua''

Pamoja na hayo ukaribu wa viongozi watajwa na Trump unatia shaka kama hakuwahi kudokezwa

3. Kwamba maongezi kati ya Trump na Natalia yaliisha katika dakika ishirini hakuna info zozote

Hapa ndipo hoja zilipo. Ikizingatiwa Trump Jr alihojiwa na TV moja mwezi mmoja baada ya email na kusema hakuna contact na Russia, na leo inajulikana tofauti ineleza 'credibility' yake

Hoja nyingine ni ya uchanga katika siasa Don Jr akisema akitazama nyuma leo angefanya vinginevyo.

Katika mkutano na Natalia, Paul Manafort, kampeni meneja alihudhuria akiwa na miaka 20 ya uzoefu katika mambo ya uchaguzi wa US. Ilikuwaje hakumshauri Don?

Jared Kushner alikuwepo naye kama Don ni mchanga katika siasa. Hata hivyo suala si uchanga bali weledi

Uwepo wa viongozi hao katika mkutano unaashiria ''ushiriki' na Russia

Je ilikuwa sahihi kuitikia wito na kutotoa taarifa hasa ilipobainika ni mahasimu wao wenye info?

Kamati ya bunge ya mambo ya sheria imemwita atoe maelezo chini ya kiapo.

Hapa pana mtego mkubwa, je, emails alizotoa ndizo pekee?
Je, atatoa maelezo mengine tofauti chini ya kiapo

Ieleweke, kudanganya kamati ni kosa. Ikiwa Don atatoa maelezo ikabainika amedanganya kamati ya Bunge adhabu haitakuwa mbali naye.

Suala lililobaki ni lini baba yake Rais Trump alijua hilo? kama alijua ni lini na alijua nini

Mtafaruku si wa Russia pekee, Jared Kushner ndiye aliyeamsha dude alipofanya marekebisho ya fomu yake ya security clearance na kueleza kukutana na Natalia, Don na Manafort

Haileweki emaili zilipatikana vipi lakini Intel community zinazoshughulika na security clearance zilijua
WH inamlaumu Jared kwani inaonekana kama ndicho chanzo cha timwbwili zima

Tusemezane
 
Duh...! Sijapita huku kitambo sana..ha haaa wachambuzi wetu naona bado mnaendelea...Haya wakuu kila la kheri.

Sent from my VF685 using JamiiForums mobile app
 
TRUMP Jr NA Emails...
Haileweki emaili zilipatikana vipi lakini Intel community zinazoshughulika na security clearance zilijua
WH inamlaumu Jared kwani inaonekana kama ndicho chanzo cha timwbwili zima
Kama tulivyotonya watu huko nyuma...hii inaitwa drip drip na kama wasemavyo Waswahili; matone matone hujaza ndoo (Haba na haba hujaza kibaba au Bandu bandu huisha gogo) Kila siku inavyovujishwa mpya watuhumiwa wazidi kujizika! Hizo za Emails ni utangulizi tu, zitafuata za audio na baadaye si ajabu zikafuata za video. Bahati mbaya kwao ni kwamba katika sheria utetezi wa ukilaza haukubaliki...Ignorance of the Law is no excuse!
 
RAIS TRUMP AKIWA PARIS

Maswali yanayohusiana na sakata la Russia yanamfuatakila alipo.

Akitoa 'utetezi' Trump alisema Kijana wake ni mwema alichofanya ni 'opposition research' ukachero dhidi ya mpinzani.

Rais akasema katika mkutano hakuna kitu kipya kilichojadiliwa kwa muda wa dakika 20
Kwamba, baadhi waliondoka na aliyebaki hakuwa na interest na maongezi

Akasema Don Jr alikutana na lawyer wa Russia ambaye si mfanyakazi wa serikali ya Russia

Mkuu Mag3 kasema huko ni 'kujizika'. Tunaona hayo kila siku kutokana na kauli tata

Tuangalie matatizo ya kisiasa kwa kauli za Rais Trump siku mbili baada ya ukimya siku nne

1. Kwanza, anasema alijua majuzi tu kuhusu mkutano wa Don na Lawyer
Mkutano ambao ulifanyika Trump Tower zilipokuwepo ofisi zake
Hoja inakuja ni kweli alijua majuzi? Ikibainika tofauti hilo litakuwa mjadala, kuna rekodi

Jared Kushner alishtukia emails June 21. Kukufanyika majadiliano kati ya FBI na Jared kuhusu security clearance Form. Wanasheria wa Trump na Jared walifahamishwa.

Je, hawakuwasiliana na Rais ambaye ni mteja wao?

2. Anasema hakuna kilichozungumzwa katika mkutano huo.

Don Jr alisema mkutano adoption kabla ya kubadili kauli mara mbili zaidi

Je, ana uhakika na hilo? Ikibainika tofauti taswira yake itachimba mambo zaidi

3. Anasema Don alikutana na Lawyer ambaye si mtumishi wa serikali ya Russia
Well, hakuna anayejua kwa uhakika kama alikuwa 'under cover' au la

Ikijulikana ni Russia operatives , Rais atakuwa katika hali gani!

Kwanini kauli tata zina matatizo
Tuhuma za Obama kufanya wiretapping Trump Tower zinamrudi sasa.

Ikiwa hilo baya wakati , kwanini lisiwe ni opposition research kama alivyoita suala la Russia?

Kauli kuwa Russian Lawyer Natalia V alipewa visa na AG wa Obama Loretta Lynch ina utata. Kwanza, alichosema ni 'Nasikia' kwa maana Rais wa USA anafanyia kazi kauli za 'mitaani'

Ikiwa Loretta alifanya ''kosa''Trump atawezaje kukanusha Lawyer si mfanyakazi wa Russia?

Ina maana kama Loretta aliruhusu mtu 'asiyefaa' Don aliongea na mtu asiyefaa.

Ndivyo ilivyokuwa kwa suala la Comey ambalo WH ilipanga aonekane amefukuzwa na Sec Session kwa ushauri wa Deputy wa DOJ.

Siku chache baadaye Trump akasema alipanga kumfukuza hata kabla ya Barua ya Session

Kinachoendelea sasa ni kuhusisha kufukuzwa kwa Comey na Russia investigation ili kupata ukweli kutokana na kauli tata.

Tumesema mara nyingi sana, vyombo vya habari vya USA vinafanya kazi kitaalam haswa.
Si eneo ambalo mtu ataweza kuongea lolote bila kujua kuna nini kinafuata

Kila kauli inachunguzwa kwa undani wake, si suala la kusema tu.

Tusemezane
 
Hivi aliyemsaidia kumuweka madarakani anaweza kuzungushwa hivi? MSM waache uchochezi
----------------
Moscow warned that it may take retaliatory measures and expel US Embassy staff unless Washington does something to break the stalemate in the closure of two Russian diplomatic compounds in the US.
Russian Foreign Ministry stated that it is hard to cooperate with the US in the light of diplomats’ repatriation and confiscated Russian property, which was under diplomatic immunity during its illegal seizure by the Obama administration in 2016.

“The seized objects have not been returned. Washington has not only failed to cancel the decision to expel our employees, but also refuses to issue visas to those who are to replace them,” Russian Foreign Ministry spokesperson Maria Zakharova said on Friday.

‘Time running out’: Moscow warns it may expel US diplomats over seized Russian property
 
Hivi aliyemsaidia kumuweka madarakani anaweza kuzungushwa hivi? MSM waache uchochezi
----------------
Moscow warned that it may take retaliatory measures and expel US Embassy staff unless Washington does something to break the stalemate in the closure of two Russian diplomatic compounds in the US.
Russian Foreign Ministry stated that it is hard to cooperate with the US in the light of diplomats’ repatriation and confiscated Russian property, which was under diplomatic immunity during its illegal seizure by the Obama administration in 2016.

“The seized objects have not been returned. Washington has not only failed to cancel the decision to expel our employees, but also refuses to issue visas to those who are to replace them,” Russian Foreign Ministry spokesperson Maria Zakharova said on Friday.

‘Time running out’: Moscow warns it may expel US diplomats over seized Russian property
Wewe endelea tu kumshabikia huyo dikteta wetu uchwara nchini Tanzania, ya Marekani naona yanakuzidi kimo. Ungejua namna Trump anavyohangaika...WH haikaliki wala kulalika. Uzuri wa Marekani Rais hawezi kuagiza hata mfagiaji tu wa ofisi kukamatwa na polisi na hata akilewa madaraka akathubutu kufanya huo ujinga anaweza kufutwa kazi. Wasiwasi uliotanda WH kwa sasa ni mkubwa kiasi hakuna anayemwanini mwenziye...si baba wala mtoto wala mkwe.

Kuna kinachoitwa pandora box na Trump kwa ujinga wake alilifungua siku ile alipotangaza ugomvi na vyombo vya habari akiviita fake news na sasa vita inaanza rasmi. Hii bado ni rasha rasha tu ya kutupiana risasi lakini mvua za vuli za mizinga ziko njiani na yako mambo yatakayoendelea kuvujishwa kwa dozi kila siku yatakayomwacha uchi kabisa. Ndiyo maana sasa wanatafutwa watu wa kumfunga luku asiendelee kuropoka ovyo na idadi yao inaongezeka kila kukicha!


maxresdefault.jpg


John I'm no snowflake Dowd.

ty-cobb-will-join-president-trump-s-legal-team-to-coordinate-the-response-to-the-russia-investigatio_365035_.jpg


Ty Cobb
Hawa wawili wameongezwa baada ya wanasheria wa Trump wa awali ama kupwaya kwa kushindwa kumdhibiti mkurupukaji-in-chief au kwa historia yao kuhojiwa. Kwetu hapa kauli ya mkulu ni sheria na vyombo vya usalama vipo kumlinda na kuhakikisha hakosolewi hata kama anatenda kinyume cha Katiba. Kwa kweli Tanzania kwa utaoji wa haki tuko zama za mawe na tusipoangalia kuna siku tupiga vigelegele tukimshanglia mtu akikata mtaa akiwa uchi wa mnyama, naam hiyo siku haipo mbali.

TUJITEGEMEE, mambo ni magumu kwa huyu pacha wake Magufuli...ni bahati mbaya yeye yuko katika anga la wastaarabu ambako upuuzi hauvumiliki hata kama mpuuzi mwenyewe ni Rais mwenye nguvu duniani kuliko wengine wote. Ajabu ni kwamba kama alivyo Magufuli anao mashabiki kama wewe ambao hata akiboronga kiasi gani wanaimba tu haleluya ila mbele ya sheria ushabiki wa kijinga hauwezi kuwa utetezi...sheria ni msumeno, haitazami sura!
 
Hivi aliyemsaidia kumuweka madarakani anaweza kuzungushwa hivi? MSM waache uchochezi
----------------
Moscow warned that it may take retaliatory measures and expel US Embassy staff unless Washington does something to break the stalemate in the closure of two Russian diplomatic compounds in the US.
Russian Foreign Ministry stated that it is hard to cooperate with the US in the light of diplomats’ repatriation and confiscated Russian property, which was under diplomatic immunity during its illegal seizure by the Obama administration in 2016.Time running out’: Moscow warns it may expel US diplomats over seized Russian property
Mkuu sina uhakika kama ulichukua muda wa kujua nini kinaendelea kuhusu suala hilo

Kwamba Waziri wa Russia kasema ni ushahidi wa mtafaruku na Trump ni myopic
Kwanza, Rais Trump amezungumza mabaya yoote ya nchi za dunia hii.

Aliisema China, Saudia magaidi, Ufaransa , UK,EU, NATO , Mexico, Canada. n.k.
Katika kusema hayo alitumia lugha za maudhi sana

Hakuna rekodi ya kusema jambo lolote la maudhi dhidi ya Russia, huku akisisitiza ushirikiano kumaliza migogoro ya dunia. Russia ni adversary namba moja wa US

Katika mkutano wa Hamburg Trump alinywea kwa Putin na majuzi kasema 'kakataa mlitaka nimpige ngumi' Hili ndilo lilipelekea aseme lets move on ililowekera Wamarekani

Pili, siku za karibuni congress imesisitiza vikwazo zaidi alivyoweka Obama.
Moja ya vikwazo ni kutorudisha jengo walilotumia Russia katika intelligence activities

Seneti ilipokea mswada na kuufanyia marekebisho kwa kukaza uzi wa Vikwazo
Mswada huo ulipitishwa kwa kura 98 dhidi ya 2 za hapana.
Hii inaonyesha Democrats na GOP ni wamoja kwa mtazamo wao dhidi ya Russia.

Mswada umekataliwa na WH kwa maana ya kutaka kulegeza vikwazo.
Moja ya ulegezwaji ni kurudisha jengo walilofukuzwa na Rais Obama 2016.

Hilo limelepekea hasira kwa Russia kutokana na article uliyoleta.
Russia wanahisi matumaini ya kutumia WH yamekufa kwa mswada wa 98 vs 2

Article inasema ' serikali ya Marekani' kinachosemwa ni Congress si WH inayotaka
Waziri wa Russia anaweka shinikizo na tishio kwa senate na house.

Nadhani hadi hapo utakuwa umepata picha labda kama unasoma kwa jicho la upendo

Mkuu Mag3 kuanzia Kapeni uchaguzi mkuu tulieeza vita ya Trump na intelligence community na Media haitakuwa nzuri na itamsumbua. Yanatokea

Wakati media zinachunguza tulisema zinazunguka tuu ni suala la muda mada itatua WH
Media zilikuwa na information, ziliandika na kuuliza maswali makusudi kabisa

Hoja ya kwanza media na Intel community walitaka ku prove ni 'Russia iliingilia uchaguzi'
Hoja ya Pili ni kwamba habari hazikuwa fake news
Hoja ya Tatu ni kuwepo kwa ushiriki ambao sasa wanaufanyia kazi kama ni kweli au la

Ukitaka kuona wana jambo, Trump akiwa njiani kutoka G-20 ikaletwa habari ya email. Don na Trump wakatoa kauli za mwanzo, pili na tatu. Media zikaweka kituo

Akitokea Paris kabla hajatua zikaja habari za watu 8, habari zilizofuta hoja zote zilizotangulia. Hiyo ni investigative journalism. Ikifika Ijumaa wiki ijayo kutakuwa na jipya
 
UPDATE ZA SAKATA LA RUSSIA

Bandiko hapo juu tulisema ikifika Ijumaa kutakuwa na habari mpya, leo tu zimetoka
Kwamba kampeni ya Trump ililipa dola 50K kumwekea Lawyer Don Jr

Hili lnaanza kujibu hoja kuwa Rais Trump alifahamu jambo hilo mapema kwa mujibu wa media

Mkakati uliowekwa ni kumtumia Lawyer wa Rais Trump kujibu hoja. Ingawa mwanasheria huyo anapoulizwa maswali husema ni mwanasheria wa Rais,ameingia 'kutetea' Trump teams.

Hoja ya mwanasheria,hakuna hakuna kifungu cha sheria kilichovunjwa.
Hata hivyo habarii kwa mujibu wa Don Jr ambaye amekaririwa mara nyingi akisema uongo. Mwaka jana alikana kuhusu tuhuma za kukutana na Russia kama alivyofanya mwaka huu.

Kinachoonekana ni kuwa lawyer amerudisha 'majeshi' nyuma badala ya ku charge kinachofanyika ni 'defensive'. Hii ni baada ya revelation ya mambo mengi yanayochanganya

Lawyer wa Trump amekaririwa akisema suala zima la Russia ni witch hunt.
Hata alipoulizwa kuhusu Mueller alisema ni kitu hicho hicho

Swali linaloendelea ni Rais alijua lini na alijua nini. Ukitazama habari za lawyer kukodiwa mwezi June na sakata zima kufumuka July kunahitaji maelezo na huko ndiko wanakoelekea

Chini ya kiapo hakutakuwa na udanganyifu, wataitwa wasiohusika ikiwa tu wataonekana wanajua habari fulani. Kuna watumishi wa WH watajikuta katika mazingira wasiyotaka

Kwa muda inaonekana ana ''control flow of information, kwa upande mwingine anachagiza habari zaidi. Again kabla ya Jumamosi kutakuwa na habari mpya 'drip drip'

Hata kama hakuna Russia collusion, kuficha habari kuna tia baadhi shaka
Kisiasa ni liability kwani mbele ya safari litaangaliwa kama ilivyokuwa emails za Clinton

Tusemezane
 
UPDATE YA SAKATA LA RUSSIA

Tulieleza kabla ya Jumamosi litatokea jingine, limetokea dogo masaa machache yaliyopita

Mwanasheria wa Rais Trump Bwana Jay Sekulowa amekuwa katika vituo vya TV akitetea suala zima la Don Jr na washirika Manafort na Kushner kuhusu na ugeni wa Russia Trump Tower.

Jay amesisitiza hakuna tatizo la kisheria kwa Don Kukutana na watu kutoka Russia

Katika hoja nyingine Jay alisema isingekuwa Rahisi secret service kuruhusu watu 'wabaya' kuingia Trump Tower na kama ilikuwa hivyo, kwanini Secret service wasilaumiwe kwanza

Siku za nyuma mwanasheria huyo alisema Don Jr alikuwa Raia na hakuna sababu zilizomzuia kujadili suala la adoption na watu kutoka Russia.

Hapa alikwepa sheria inayomzuia Raia kuongea mambo ya nchi katika nyanja za Diplomasia

Katika hali isiyo ya kawaida, secret service wametoa kauli. SS wanasema ' Don Jr alikuwa Raia wa kawaida, hawakuwa na sababu za kuchunguza nani anaingia nani anatoka Trump Tower

Kauli hii imezika hoja moja ya Jay kuhusu utetezi wake kwa Don ingawa anasema yeye si mwanasheria wake bali wa Rais.
 
SAKATA LA RUSSIA LINAENDELEA

''REPEAL AND REPLACE OBAMACARE( ACA)'' IMEFELI

Sakata la Russia na mkutano wa Don Jr limeendelea kwa namna nyingine. Mtu wa 8 kati ya washiriki amefahamika ni mwakilishi wa familia ya Agalarov (Rejea bandiko [HASHTAG]#347[/HASHTAG])

Hadi sasa upande wa Trump kampeni washiriki ni watu 3, Don Jr,Manafort na Kushner
Kwa upande wa Russia wapo watu 5 akiwemo Natalia, Goldstone na wengine 3

Don Jr katika mwanzo alisema wakuwepo watu 4, yeye, Natalia, Kushner na Manafort!!
Don Jr na mwanasheria wake wanataka kutoa 'statement' mbadala wa ya kwanza!

Sakata linaendelea kwa drip drip. Hakuna ajuaye mwisho utakuwa ni upi?

REPEAL AND REPLACE OBAMACARE IMEFELI

Muda si mrefu Senate Majority ametangaza kufeli kwa mswada wa kufuta ACA inayojulikana kama Obamacare. Hii ni baada ya kukosa kura za kutosha ndani ya seneti

Ieleweke Republican ndio wengi wakiwa na kura ya Makamu wa Rais ikitokea ufungano
Jana waliahirisha kura kutokana na maradhi ya seneta Mcain
Leo maseneta 2 wameungana na 2 wa mwanzo kuwa 4 wanaopinga mswada

Ni maseneta wa Rep. Kwa maneno mengine, GOP 52, Dems wapo 46 na Independent 2

Ukiondoa 4-GOP, wanaopiga watakuwa 46 sawa na Dem na mswada hautapita

Senate Majority amesema mswada wa kuondoa Obamacare umeshindikana, Rais Trump aki tweet kuwa sasa ni mswada wa kufuta Obamacare kwanza (Repeal) halafu watengeneze replacement wakishirikisha Dems

Tujadili kuhusu mswada ulioshindwa bandiko lijalo
 
KUSHINDWA KWA REPEAL & REPLACE OBAMACARE

Ni kauli mbiu ya Rais Trump kwa muda mrefu akisema Obamacare ni kitu kibaya sana

Nyuzi za uchaguzi tuliuliza Ilani ya ya Trump inasemaje kuhusu Healthcare?
Hakuna aliyekuwa na jibu

Trump aliaminisha watu atakuja na kitu kizuri kuliko Obamacare.
Kwa undani Trump ana chuki na sera za Obama, anataka kuzifuta bila sababu

Ndivyo alivyofanya kwa Azimio la Paris ambalo US iliongoza kuandika na kuungwa mkono na mataifa 150 yakiwemo yanayoongoza kwa uchafuzi wa mazingira

Azimio linaungwa mkono na Reps/Dems across. Kalifuta lisiwe legacy ya Obama.

Rais Trump alisema atafuta Obamacare siku ya kwanza kwani ni kitu rahisi tu.
Rais hakujua healthcare ni 6% ya uchumi wa US, ikigusa maisha ya wapiga

Miswada 2 imeshindikana, wakwanza ukikwama katika House na kisha kupitishwa kwa mbinde

Muda wote Trump na Reps walitegemea majority ndani ya Senate na House

Walichosahau, wapiga kura wanajali masilahi si masilahi ya vyama au wingi
Obamacare ni maarufu miongoni mwa watu ikiwa imesadia watu wengi sana

House na senate wanakubaliana Obamacare siyo perfect inahitaji kurekebishwa.

Wanapotofautiana, Dems wanasema muhimu ni kufanyia marekebisho Obamacare, Trump na Reps wanataka kufuta legacy ya Obama

Dems wameamua kukaa pembeni wakiwaachi mzigo GOP.

Mtakumbuka kuna mabandiko tulisema Rep watagawanyika (Reje nyuma)
Ndivyo ilivyotokea kwa kuwa na moderates na conservatives

Kugawanyika ni kwa maeneo na kuwalazimika kusimamia masilahi ya wananchi

Hakuna Democrats aliyeshiriki mjadala. Republicans wakagawanyika wakipingwa na wananchi. Obamacare ikawa maarufu kuliko mswada wa GOP

Trump aliahidi atafuta Obamacare na kuwaaminisha ni bingwa wa kufanya deal
Kilichotokea ni kukaa pembeni akiwaacha maseneta walumbane

Alipotoa kauli Trump alidharau kazi nayofanywa kwa maana ya kujitenga nao

Ni tofauti na Obama aiyefanya kazi na Pelosi kupata kura za kupitisha ACA

Trump alipumbaza watu wake na katika safu hii wakiwemo wenzetu walioshabikia 'atafuta 'kwa kalamubila kujua mswada ni mgumu kiasi gani.


Wenzetu waliimba bila ufahamu

Pendekezo la Trump kufuta kwanza (Repeal) Obamacare limelenga kuwafurahisha wapiga kura wake kwamba ametimiza repeal.

Tatizo ni kuwa ataulizwa, ame replace na kitu gani na wakati kitu hicho kinatafutwa nini itakuwa sheria inayotawala Healthacare?

M.McoNnel, senate majority aliwahisema ' I wish Obama fails' well,ndiye amefeli

Rais Trump kakutana na ugumu wa WH na utawala na si Trump Organization

Obamacare ya Obama imebaki sheria licha ya miaka 7 ya Reps kuipigia kelele

Tusemezane
 
Back
Top Bottom