Mkuu wangu sijui unachokizungumza hapa zaidi ya kunichanganya zaidi.Mkuu kuna vitu viwili umechanganya,naomba nikuwekee sawa ili ujadili bila kupoteza unguli wako unaoheshimika jamvini.
Kuhusu umeme, hakuna msaada wa nje unaotumiwa kulipa bili za Tanesco.
Tanesco inafanya kazi Tanganyika na inakusanya mapato yake huko.
Zanzibar wana Zesco, inauziwa umeme na Tanesco.
Kwamba Zesco wanakusanya kwa unit sh ngapi hilo ni juu yao.
Tunachojua kwa unit moja znz inalipa chini ya Mtanganyika.
Deni la Zesco kwa Tanesco ni baina ya mashirika mawili. Zesco wanakusanya mapesa na hayajulikani yanakwenda wapi.
Kuna scandal ya bilioni 20 kutoweka kiaina huko Zesco ambayo imefukiwa.
SMZ inachukua deni la Zesco na kuitupia serikali ya muungano. Sasa mznz analipa umeme jibu ni hapana.
Laiti wangekuwa wanalipa basi wasingegoma kulipa deni la bilioni zaidi ya 70. Deni linatoka wapi kama wznz wanalipa?
Hapo utakuja na hoja kuwa Zesco wanakula pesa. Well,walipojiondoa Tanesco ilikuwa ni kuwa na shirika lao.
Sisi tunawauzia umeme wao na ndiyo maana SMZ inatakiwa ilipe.
Mgomo wa kulipa,walitaka walipe kiwango cha chini cha unit za Tanganyika. Hiyo ndiyo akili ya ZNZ.
Pili, SMZ ilikuwa inatumia milioni 800 kwa mwezi kwa umeme wa Pemba.
Kwa mujibu wa waziri wao sasa hali itakuwa njema baada ya kuungwa na Tanesco kutokea Tanga.
Hali nzuri maana yake ni ile ile, watagoma kulipa na deni litapelekwa JMT. Wanaogoma ni znz kumbuka.
Tatu, kuhusu suala la misaada, umeme wa kwenda znz wa mwanzo ulikuwa mkopo na msaada uliolipiwa na JMT.
Mwezi Jan 2014 wamepeleka umeme kwa msaada wa nchi za nje ambzo zimetoa kiasi bilion 39? na SMZ bilioni 5. Kiaisi kilichotakiwa ambacho SMZ haikuweza kukilipia ni bilioni 11 walizoomba kutoka JMT.
Hadi hapo unaona jinsi gani mikopo na misaada inavyowafikia. Hivyo usichanganye kati ya bill na gharama za kupeleka umeme.
Unatakiwa ujiulize, kama mambo yote ni ya JMT, ZESCO imeundwa kumhudumia nani na kwanini.
Haya yote ni katika narcissism na nepotism, kwamba wanataka kutumia ubinafsi kujinufaisha kwa gharama za wengine.
Haiwezekani SMZ yenye kila chomba ipitishe matatizo yake kwa Mtanganyika kwa kisingizio cha jina.
Ili kuondoa kuvaa koti, tunataka Tanganyika yetu tushughulikie umasikini wa Watanganyika.
Znz wabaki huru waende kukopa na wapewe misaada kama Syechelles, Mauritius, Comoro, Haiti, Vnanuata, Fiji na Jamica.
Sijui mkuu kwanini hutaki tuweke equation sawa sawa.
Tunasema kama tumevaa koti basi tunaomba tulivue ili wenzetu nao wapate upande wa kujifunika. Hilo hutaki.
Usipoanza na kuwalaani wznz kwa ujahilia wao wa kudharau katiba yetu, na kuandika katiba yao ya kibaguzi ya 2010, unapoteza nguvu za hoja za kuwasemea.
Kwavile kuna dana dana za kuwapendeza, sisi tunasema they will pay the cost. Wana nafasi moja tu, kukubali uwepo wa Tanganyika. Wakiichezea hiyo tutawataka watusaidie kuizindua Tanganyika kwa gharama zao.
Tanesco au Zeco yote ni mashirika ya Umma ambayo yanaendeshwa Kijamaa nikiwa na maana ya kwamba hayapati maipo halali kutoka kwa wateja wake. Na ukitazama miradi ya Mtera na Hydropower zote including za gas kina Richmond a.k.a Symbion yote ni mashirika mengine yanayofua Umeme kwa jina la Tanzania na kuwauzia Tanesco. Hivyo madeni yote ya Ufuaji umeme ni ya TAIFA hivyo bara tusipowalipa Tanesco, haina tofauti kabisa na Visiwani wasipowalipa Zeco. Swala hapa ni kwa nini wizara za serikali, nyumba za viongozi. bunge na taasisi mbali mbali za serikali ya JMT hazilipi madeni yao! huwezi kuchambua madeni ya zanzibar pekee pasipo mkutazama mlolongo wa list of shame toka serikali zote wasivyoweza kulipa madeni na kuwaweka wananchi na tanesco ktk hali ngumu.
Aidha nataka pia uelewe ya kwamba najua vizuri ya kwamba Zanzibar wanapata Umeme wao kupitia National grid, hivyo ingewezekana kabisa wao wakalipa mashirika ya ufuaji bila kupitia Tanesco kama Mambo yote yangekuwa ya Muungano.. Lakini tumechukua sisi jukumu la kuingia mikataba ya ufuaji kwa jina la tanzania lakini mikataba hiyo ni kwa ajili ya viongozi. Wewe na kundi lenu la mnashindwa kuutazama ukweli badala yake mnajiingiza ktk ukabila huku viongozi wa CCM wakiwacheka maana hata wao hawalipi kama unavyoitazama serikali ya Zanzibar. Kikulacho kii nguoni mwako hutaki kutazama!
Tazama mradi wa Rapid Transit wa Dar es Salaam, imekuwaje fedha za mkopo wa benki ya dunia kwa Tanzania nujenge barabara za dara kwa mabillioni halafu mradi huo uwe wa watu binafsi (Bakhresa na EL)?.. Deni hilo itadaiwa tanzania lakini watakao faidika na mradi mzima ni watu binafsi hii ni baada ya wananchi kupiga makelele kwa nini wananchi wazawa wasinufaike na miradi ya Taifa, sasa wajanja wamegundua njia ya kuchukua miradi ya taifa wao wenyewe.
Jiulize kwa nini mradi huu usiwe wa Manispaa ya Dar es salaam au mkoa wa Dar? kwa nini UDA usiwe mradi wa Dar, kwa nini usafishaji mji na majitaka usiwe mradi wa mkoa wa Dar ila unapewa watu binafsi ambao wameshindwa kuifanya kazi kutokana na uwezo wao mdogo ama ubakhiri wao ktk kununua vifaa vya kisasa. Ni kwa sababu mambo yote bado yapo mikononi mwa serikali ya CCM. Mawaziri ndio wenye kuendesha kila jambo la serikali ya Tanganyika au Tanzania, anayekumaliza wewe nani hapa?.
Sasa nini solution kwa mtazamo wangu. Unapofanya mambo yote kuwa ni ya Muungano, unazigawa kazi toka serikali kuu inakuwa na majukumu yake, serikali za nchi, serikali za mikoa, majimbo na hata wilaya na kata kote kila sehemu inafahamu majukumu yake ktk utekelezaji wa shughuli za selikari yao. Ufuaji umeme ni swala mla serikali kuu ambalo serikali hiyo inatakiwa kuwa na shirika lake kama Tanesco inayofua Umeme na sio kugawa umeme. Serikali kuu inaweza kuwa contract mashirika ya nje lakini chini ya shirika hilo na sio mashirika hayo kuwa independent na Tanesco shirika la Umma kuwa mteja wao!. Huu ni mfumo wa Kijamaa ambao bado tunaukumbatia kiasi kwamba tanesco inaendeshwa Kijamaa badala ya kuwa shirika Binafsi.
Na unapozidi kuzungumzia swala la Tanesco ni miujjiza mitupu kwani shirika hilo lilitakiwa lenyewe ndio chanzo cha ufuaji Umeme na kuwauzia mashirika binafsi ambayo ndio yatahusika na kusambaza umeme nchini. Huwezi kuliweka shirika la Umma (taifa) ktk hatua ya kufuatilia madeni ya wananchi, hii sio kazi ya serikal bali ni kazi ya mashirika binafsi ambayo yatauza umeme kutokana na Tanesco ku control bei za ufuaji, hivyo kuwa na sauti ktk bei ya usambazaji, serikali kujua kodi yao, profit and loss ya mashirika na kadhalika. Serikali kuu kazi yake ni kuweka miundombinu ambayo ufuaji wa umeme ni mojawapo! huwezi kuwapa mashirika binafsi kazi hiyo ilihali mikopo inachukuliwa na Taifa.. Huu ndio uhumi unaofanyika wewe unaitazama zanzibar wakati unaibiwa na viongozi wako wenyewe.