Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,427
- 31,475
- Thread starter
- #501
WHATTSUP, FACEBOOK ZATUMIKA KUKAMILISHA UHUNI
BORA LIENDE, TUMALIZIE MAJENGO YETU, KATIBA SHAURI YAO
NCHI INAELEA KAMA BOYA,KILA MMOJA KIONGOZI.
WENYE MAJUKUMU WAJIFICHA, WASUBIRI MWANYA WAENDELEZE UNAFIKI
Katika mahoka nzuri ndani ya bunge la Sitta linalokamilisha rasimu ya CCM ni hili la kupiga kura.
Dunia ilijua muda wa kwenda Hija kwa Waislam katika kalenda na taratibu za Dini kwa yoyote anayeshughulisha akili
Hilo lilipaswa lidahamike ili ratiba isiingiliane nalo. Vipi walijua uwepo wa bunge la bajeti, wasijue kuna ibada ya Hija?
Ili kukamilisha uhuni mjini Dodoma, Sitta akaamua Mahujaji wapige kura kwa kutumia Whattsup na facebook.
Hakuna anayejua huko whattsup nani ana verify kura hizo, achilia mbali ukiuakwaji wa sheria za nchi.
Sitta kaagiza, Pinda waziri mkuu akishuhudia tena kwa vimemo, na Rais wa nchi yetu akiwa safarini kusaka misaada
Kanuni za asili zikagoma kukubaliana na Sitta. Mbinu mpya ikatangazwa kuwa wapo wabunge wa UKAWA waliotaka kupiga kura.
Hili lilitangazwa baada ya kugundua kura za facebook na whattsup hazikamilisha azma ya uovu.
Waovu ni wazuri na mahiri wa mbinu. Sitta awali alisema walitaka kupiga kura ni UKAWA 25.
Jana wakati wanajadili uhuni, Sitta akasema zimepatikana kura 2. Hakusema katika 25 ngapi zimesema hapana.
Wait a minute! hapa kuna jambo pia, Sitta na CCM walitumia zaidi ya wiki 2 kukataa kura ya siri.
Baada ya kubaini facebook na Whattsup hazitaleta matokeo mema ya uovu, ndipo likaja suala la kupiga kura kwa siri.
Suala lile lile CCM ililokataa tena chini ya waovu kama Sitta na Chenge.
Leo wamegeuka eti wanahifadhi majina ya hao UKAWA. Samwel hana sababu za kuhifadhi majina, yeye alitakiwa asimamie kanuni za chama chake za kura za wazi ili katiba yao ya CCM itimie. UKAWA hawapo sasa kura za siri za nini?
Tena kura hizo za siri ni 2 ili kukamilisha uovu. Mzee Sitta ameshindwa kuelewa hata mtoto wa kidato cha II C, asingeweza kufanya mbinu za kitoto, kipuuzi na kihuni kama alivyofanya.
Hivi leo ni mwendawazimu gani ataamini kuna watu 2 walipiga kura ya siri.
Ingefaa kama angesema 30 wamepiga kura, au 75 maana hakuna wa kuthibitisha hilo.
Ni suala la Sitta kuamua anataka nini kukamilisha uovu wake.
Mtu kama Sitta anapotuma vimemo vya kutumia pesa za umma kununu kura, inaeleza bila kificho jinsi taifa hili linavyojiongoza kwa kutumia nguvu za jua na mizimu na si zakili za watu. Kuna akili gani katika ujinga uliokamilika Dodoma hata kama ni katiba ya CCM.
Rais wa nchi yupo kimya akisubiri kutoa vyeti kwa wahuni waliomaliza kazi ya kihuni kwa sababu ya uhuni wa CCM
Yote hayo yamefanyika ili kuzuia muundo uliopenedekezwa na tume.
Hivi nani alitegemea mtu kama Andrew Chenge akubali maadili ya uongozi?
Yeye akikubali tutarajie atatumia mbinu gani kuhamisha fedha kwenda visiwa wa Jersy!!
Katika kundi linalotia simamzi ni la vijana. Nao wameungana na wazee wahuni kufanya uhuni katika katiba ya chama chao.
Wamekubali kukaa kimya, wakasokomezwa matambara midomo! yes, tunaambia taifa linahitaji vijana. Ni hawa tuliowaona Dodoma.
Kama tunahitaji vijana wazoefu hawa wa Dodoma ni muhimu sana.
Wamepata uzoefu wa kufanya uhuni, kutumia teknolojia katika uovu, na hata mizimu kupiga kura, isipokuwa baadhi ya mizimu iliyopuMzika kwa amani na sasa inahangaika kuliona taifa likitumbukia katika sintofahamu kubwa.
Wengi wanasema Nyerere alifeli katika baadhi ya mambo, sasa jiulizeni angeweza kufaulu vipi ikiwa wananchi wanagundua waliokuwa wamemzunguka mwalimu na akina Sitta.
Hawa waliomba Mwalimu atoweke ili watimize haja zao ovu.
Leo wanashangilia na mizimu ya Nyerere inabubujikwa na machozi.
Laana hiyo haitawaacha salama. Mbele ya safari tunaweza kumsikia Sitta katika vichwa vya habari.
Tutamsikia wakati anakwenda kuungana na Charles Tailor kule the Hague.
Tunaweza kumsikia Sitta akiwa Nairobi ili kuungana na Rauto na wenzao kwenda the Hague
.
Na safari ya the Hague ikitokea(Mungu apishilie mbali madhara yake kwa wananchi) taifa hili litakuwa la majuha kama Sitta hatapewa ticket ya first class.
Uhuni wa CCM umekamilika, na wala hakuna tatizo.
Tatizo litakuja pale watakapotaka kuingiza uhuni huo kama nyaraka ya taifa. Hapo kutakuwa na tatizo.
Tusemezane