Shukran ningekuomba wewe anzisha mada hiyo maana sielewi haswa unapokwazwa ama wanapokwazwa wengine. Maana ieleweke tu ya kwamba unapofanya mambo yote ya Muungano ina maana kila kitu kinaelezwa kwa ufasaha wake ktk Katiba ya nchi hivyo sheria za nchi zinapotungwa haziathiri sheria mama. Kuacha mambo mengine sio ya Muungano inaleta nchi moja inaweza kuandika na kupanga masharti wapendavyo ktk katiba yao maadam jambo hilo sio la Muungano.Mkandara,
Mimi naona kuna mjadala mpana sana kuhusu hiyo mifumo unayojadili au kupendekeza hapa. Kwani unaposema kuwa kila jambo liwe la muungano kuna mengi sana ya kujadili katika kuchambua faida zake na khasara zake kwa nchi hizo mbili huru zilizoamua kuungana.
Mjadala huo utajikita zaidi katika nyanja hizi:
1. Kiuchumi
2. Kijamii
3. Kisiasa
4. Kiutawala
Sasa mimi ushauri wangu kwako NI KUWA TUWEKE UZI MAALUM WA KUJADILI HOJA YAKO YA KILA KITU KIWE MAMBO YA MUUNGANO ili tupate muda na nafasi pana katika kujadili katika mada husika kuliko hapa katika uzi huu.
Kwani kwa kufanya hivyo nafikiri wengi sana watanufaika na kufaidia na mada hiyo. Na nataraji itakuwa ni moja ya mada bora sana katika barza hii kuhusu muungano kama watu wote watakaochangia watapunguza jazba, chuki na kuweka kando ushabiki na kujikita katika kutengeneza FACTS na hoja zenye mashiko.
Upande wangu insh'Allah japo nipo Ziara ya ibada hapa Madinat munawar lakin nitatafuta muda kuweka uzoefu na maoni yangu kuhusu utaratibu huo insh'Allah.
hayo ni maoni na ushauri wangu kuhusu hilo kwa nia ile ile ya kuilimishana na kuhabarishana ikiwemo kupeana mawazo na uzoefu mbalimbali kwa faida yetu sote.
Nikutakia siku njema.