Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri

KAMATA KAMATA, VUNJA VUNJA VINATUSAIDIAJE?
NINI KIPAUMBELE CHETU KATIKA UJENZI WA TAIFA

Rais Magufuli amenukuliwa mara nyingi akisema 'Maendeleo hayana chama'.
Kwamba, maendeleo iwe kubuni, kutatua matatizo au kuendeleza hakuna uchama

Kauli hii ina maana sisi ni wamoja, tunajenga taifa moja kama Taifa na Rais
Tofauti ya itikadi za kisiasa isiwe chanzo cha kuzorotesha nchi kimaendeleo

Kuna mwendelezo wa kukamata watu na nyakati nyingine kuwaachia bila kuwafungulia mashtaka. Jambo hili ni ukikwaji wa haki za Raia na matumizi mabaya ya madaraka

Siasa za vyama vingi zina robo karne nchini na ni jambo jema hakujawahi kutokea matatizo yanayosababishwa na wanasiasa.

Yametokea matatizo kutokana na kukiuka haki za msingi za wananchi hasa za kukutana

Majuzi viongozi wa Chadema wamekamatwa Ubungo kwa amri ya DC.
Hakuna sababu zozote za kutishia usalama isipokuwa tu ni hoja za taratibu kutofuatwa

Hatudhani wapinzani wanaoongoza sehemu ya jamii yetu hawana haki ya kujadili maendeleo ya wananchi kama alivyosema Rais.

Kama maendeleo hayana chama kuna tatizo gani kila mmoja kuchagiza maendeleo?

Madiwani wamekamatwa Arusha. Hakuna maelezo ya kuridhisha bali uwepo wao chini ya vyombo vya dola. Kama kuna tukio lenye kutishia amani kwanini haisemwi?

Hiyo ni mifano michache tukilinganisha na matukio ya kamata kamata na mengine ya kuvunja maeneo kama mashamba au uwekezaji kwasababu tu wahusika ni Wapinzani

Kuvurugwa kwa shamba la M/kiti wa Chadema imeelezwa ni kulinda vyanzo vya maji. Ulinzi wa vyanzo vya maji ni muhimu sana na ni tatizo kubwa nchini.

Kushughulikia tatizo ni jambo jema, namna gani linashughulikiwa ni jambo jingine

Hatuamini kama viongozi wanAotenda hayo wamemwelewa mh Rais na kauli mbiu ya Maendeleo. Imefika mahali wananchi wanahisi kuna 'maagizo' zaidi kutoka kwingine

Viongozi wanaotenda hayo kwa utaratibu usiofaa wanachonganisha serikali na wananchi, wanapanda chuki katika jamii, wanakiuka desturi na taratibu zinazozingatia utawala wa sheria.

Kinachoshangaza viongozi hawalioni hilo kama tatizo kana kwamba kuna ''baraka zao''
Wakati huo huo viongozi wa CCM wakiendelea kutenda bila kuguswa na vyombo dola

Tuna matatizo makubwa kama ujambazi kule Rufiji unaotishia amani na usalama wa wananchi na vyombo vya dola.

Ujambazi umesababisha vifo vingi kuliko matatizo yanayotokana na siasa kwa muda mrefu sana. Haya ndiyo kipaumbele chetu

Katika miezi sita tumepoteza Askari wetu zaidi ya 10 kwa matukio ya ujambazi
Katika kipindi hicho hakuna askari hata mmoja aliyepata tatizo kutokana na siasa

Hivi tunawawezaje kuamini kuwa siasa na wanasiasa wanaotembea mitaani , wanaoishi nasi na tunaowajua wamekuwa tatizo kubwa kuliko majambazi yanayoumiza Raia na Askari kule Rufiji! Je, tunatumia rationale gani kutoa vipaumbele kwa matatizo yetu!

Tusitumie muda na akili kwa mambo yasiyosaidia Taifa bali kujenga chuki na uhasama

Mambo ya siasa yasifike mahali yanavuruga nchi ,hayaruhusu shughuli za maendeleo, yanakiuka haki za binadamu na yanachagiza matumizi mabaya ya madaraka

Tatizo lililopo mbele yetu ni usalama hasa Rufiji, si wanasiasa wanaokutana kujadiliana tu

Tusemezane
 
UKUBWA WA MATATIZO TULIYO NAYO

VICHWA 15 VISIVYO NA MWENYEWE!

Kauli ya Mh Rais ya uwepo wa vichwa 15 vya treni bila kujulikana mmiliki inatisha

Ukubwa wa vichwa vya treni na gharama tu inatosha kuamini hilo si kwa bahati mbaya

Hatari ni bandari kupokea mzigo wasiojua unatoka kwa nani/wapi unakwenda kwa nani/wapi

Kituko hicho kinachunguzwa,lakini kinashughulisha akili za mtu yoyote aliyeamua kuzitumia

1. Hivi bandarini hakuna mfumo wa kujua meli gani inakuja na imebeba nini.

Kwa utaratibu kuna nyaraka zinazoruhusu mzigo kupakiwa melini nakala zake hupatikana unapokwenda. Je, kwa vichwa 15 nyaraka hizo zilikuwepo?

2. Upakujai wa mizigo mizito kama vichwa vya treni unahusisha 'crane' kubwa

Je, walioendesha crane hizo hawakuwa na nyaraka za kuonyesha wanapakua mzigo gani, na kama zilikuwepo nyaraka zilizoonyesha mzigo huo ukiwa na maelezo gani

3. Uongozi wa bandari unawekaje takwimu , na takwimu hizo huonyesha maelezo gani.

4. Vichwa vilihifadhiwaje,wanaohifadhili waliambiwa ni mali ya nani inakwenda wapi na lini.

Haya ni maswali rahisi ya mtu wa kawaida asiye na utaalam anayeweza kuyaauliza.
Kitaalam kuna maswali yanayoshtua mtu sana

Uongozi wa bandari umebadilishwa mara kadhaa kutokana na uzembe.
Tunajua bandari zilivyokithiri matukio ya ajabu, lakini hili linatisha na si kusikitisha

Linatisha kwa kutambua kuwa bandari ni lango muhimu la kuingia na kutoka nchini
Usalama wake haulinganishwi na maeneo mengine kwa ukaribu wowote

Ikiwa vichwa 15 vimeingia nchini bila mmiliki, nini kinashindikana kontena moja la bidhaa hatari kama silaha kuingia tu na kupotea bila kujulikana limetoka wapi na kwenda wapi?

Kuna eneo linalohitaji kuangaliwa kwa ukaribu kama chanzo cha tatizo hili, usalama.
Vyombo vya usalama bandarini vilijua nini na kwa wakati gani na kwanini havikuzuia tukio.

Haya ndiyo mambo yanayopaswa kushughulisha vyombo hivyo kwa ukubwa wake
Kushughulikia na watu wasio na athari kunaondoa focus ya matukio ya kutisha kama hili

Bandiko lililopita tulizungumzia kuhusu usalama, na tunarejea tena kunasihi, vyombo vya usalama vihangaike na matatizo ya kweli na viache kupoteza focus kwa kukimbizana na watu ambao pengine kuwaacha tu walivyo kisingeharibika chochote

Tusemezane
 
VIJANA WANAVYOLIANGUSHA TAIFA

'ULEVI WA MADARAKA NA SIASA ZA CHUKI NA VISASI'

Ile dhana ya vijana kuweza wakiwezeshwa imepoteza maana, na ujana si hoja tena
Tangu teuzi zimezingatia 'ujana' yanayoendelea sehemu mbali mbali ni aibu kwa Taifa

Vijana wanatumainiwa kwa uwezo wa kufikiri kwa kina, kuchanganua na kupambanua
Dunia ya leo fursa ya vijana kujifunza kutoka kwa wenzao ni kubwa kuliko siku za nyuma

Uwezo huo unasaidiwa na elimu ambayo ni kiungo muhimu cha kuunganisha fikra

Ilitegemewa vijana kwa mmoja mmoja au katika makundi yao kuibadili nchi kimaendeleo
Kwamba, wawe mstari wa mbele katika kuleta fikra mpya za kisayansi na kijamii

Kinachotokea si fikra mpya bali ulevi wa madaraka na siasa za chuki na visasi na 'kupendeza'
Ili kijana aonekane anafaa inabidi ajipendekeze au afanye mambo ya 'kupendeza'

Ni nadra sana vijana wa Tanzania kuja na kitu cha kubadili maisha ya wananchi
Taifa linakabiliwa na matatizo ya elimu, ujinga na maradhi yanayohitaji majibu ya haraka

Inashangaza katika zama hizi hakuna anayefikiri kuongoza mapambano dhidi ya ujinga , elimu na maradhi kwa mbinu za kisasa bali mwendelezo wa siasa zisizo na kichwa wala miguu

Vijana waliokulia katika jamii zetu na wajuao ugumu wa kupata maji, usafiri , ughali wa maisha na ugumu wa huduma za elimu na afya ni kana hawakuwahi kuyaishi maisha hayo

Ni ulevi uliokithiri wa madaraka unaochangiwa na siasa zisizo na tija maana wala mantiki. Matumizi mabaya ya madaraka ni sehemu ya ulevi huo bila kujali matatizo yanayoikabili jamii

Vijana wanasahau vyeo ni dhamana waliyopewa na jamii na kwamba ipo siku watayaacha. Mbegu wanazopanda za kutowajibika, kuchukiana na visasi ni mbaya kwa mustakabali wa taifa

Ni wakati wenye fikra pevu wafungue macho na midomo
Ni wakati tuwaulize vijana nini cha maana walichofanyia taifa kwa wiki, mwezi au mwaka

Wananchi wasiposimama kuwauliza vipaumbele vyao, ulevi wao una madhara kwao

Na muhimu ni kuwaambia vijana waache siasa za majitaka, watumie elimu na fursa walizopewa kutoa majibu ya matatizo yanayoikabili jamii

Tumechoka! si Bungeni , si wilayani, mikoani au ndani ya vyama ni uozo tuu wa vijana

Hapana, wakati umefika wa kuwawajibisha kwa kuwataka watueleze nini wamefanya katika kumkomboa Mtanzania na si kipi wamefanya katika kutekeleza azma na masilahi binafsi

Tusemezane
 
Tunawawajibishaje? Ni kweli ulevi wa siasa chafu umewaathiri wengi. Swali, TUNAWAWAJIBISHAJE?
Hoja nzuri sana na niliitegemea. Hatuwezi kuwawajibisha kimamlaka kwasababu wananchi hawana nguvu hizo


Kuwawajibisha kuna namna nyingi ndani ya uwezo wa wananchi.

Kwanza, kuwakemea wanapofanya siasa majitaka na kuwaeleza hicho si kipaumbele
Hilo litasaidia watakapobaini utoto umeonekana na hakuna anayeushabikia au upenda

Pili, kuwakalia kooni kwa kuwahoji nini walichokifanya katika kupambana na matatizo yanayowakabili au kuchagiza maendeleo.

Hilo wana uwezo nalo.Kwamba uwepo ulinganifu wa nini wanafanya na upuuzi wanaoufanya
Waonyeshe kwa uwazi wamefanya nini na kwa muda gani na kwa kipaumbele gani

Leo wananchi wakipaza sauti zao kueleza yale muhimu kwao na yanavyowasumbua bila msaada itasaidi mawaziri, RC, DC kuelewa umma haujali upuuzi unajali matatizo yaliyopo

Inawezekana wananchi wakisimama na kuwauliza viongozi wahusika awe waziri,RC, DC au mkurugenzi ya kuwa tendo moja alilolifanya kisiasa limeleta suluhu gani katika maisha yao

Viongozi watabaini hawana umma na watalazimika kurudi na kujikita na matatizo yaliyopo na kuokoa muda wa kushughulika na mambo trivial and travesty yasiyosaidia wananchi

Tatu, wananchi wazieleze mamlaka ikiwa hawatapewa watu wa kuwasaidia kusukuma maendeleo mbele, basi ile 'haki yao' ya kuweka mamlaka hizo wataitumia vema

The bottom line ni kuwa wananchi wasizungumzie trivial zinazoofanywa na hawa vijana, wazungumzie nini wanataka kufanya na kwanini vijana wanawakwaza.

Kauli tu inatosha kuwatenga vijana hao na wao kujua umma hauhitaji mambo yasiyo na maana, unawahitaji kufikiri kwa kina na mantiki , busara na hekima katika madaraka yao

Wananchi wa focus katika kuwaweka sawa kwa matatizo na maendeleo wakikemea aina nyingine ya siasa majitaka, za visasi na za chuki ili vijana hao waelewe umma haukubaliani nao.
 
Hoja nzuri sana na niliitegemea. Hatuwezi kuwawajibisha kimamlaka kwasababu wananchi hawana nguvu hizo


Kuwawajibisha kuna namna nyingi ndani ya uwezo wa wananchi.

Kwanza, kuwakemea wanapofanya siasa majitaka na kuwaeleza hicho si kipaumbele
Hilo litasaidia watakapobaini utoto umeonekana na hakuna anayeushabikia au upenda

Pili, kuwakalia kooni kwa kuwahoji nini walichokifanya katika kupambana na matatizo yanayowakabili au kuchagiza maendeleo.

Hilo wana uwezo nalo.Kwamba uwepo ulinganifu wa nini wanafanya na upuuzi wanaoufanya
Waonyeshe kwa uwazi wamefanya nini na kwa muda gani na kwa kipaumbele gani

Leo wananchi wakipaza sauti zao kueleza yale muhimu kwao na yanavyowasumbua bila msaada itasaidi mawaziri, RC, DC kuelewa umma haujali upuuzi unajali matatizo yaliyopo

Inawezekana wananchi wakisimama na kuwauliza viongozi wahusika awe waziri,RC, DC au mkurugenzi ya kuwa tendo moja alilolifanya kisiasa limeleta suluhu gani katika maisha yao

Viongozi watabaini hawana umma na watalazimika kurudi na kujikita na matatizo yaliyopo na kuokoa muda wa kushughulika na mambo trivial and travesty yasiyosaidia wananchi

Tatu, wananchi wazieleze mamlaka ikiwa hawatapewa watu wa kuwasaidia kusukuma maendeleo mbele, basi ile 'haki yao' ya kuweka mamlaka hizo wataitumia vema

The bottom line ni kuwa wananchi wasizungumzie trivial zinazoofanywa na hawa vijana, wazungumzie nini wanataka kufanya na kwanini vijana wanawakwaza.

Kauli tu inatosha kuwatenga vijana hao na wao kujua umma hauhitaji mambo yasiyo na maana, unawahitaji kufikiri kwa kina na mantiki , busara na hekima katika madaraka yao

Wananchi wa focus katika kuwaweka sawa kwa matatizo na maendeleo wakikemea aina nyingine ya siasa majitaka, za visasi na za chuki ili vijana hao waelewe umma haukubaliani nao.

Uko sahihi Mkuu, lakini ni ukweli kuwa, HAYO YOTE YANAHITAJI UMMA UNAOTAMBUA WAJIBU WAKE NA KUUTANGULIZA BADALA YA MIHEMKO YAKE.

Tunakemea na Kukosoa tunakopaswa kuunga mkono wakati Tunaunga mkono tunakopaswa Kukemea na Kukosoa. MIHEMKO.

Wapumbavu wanatumia mihemko hiyo kujihakikishia maslahi yao binafsi, werevu wachache wanashindwa kutumia huo mtaji.

Umma umekosa sifa kuu ya kutambua nafasi yake katika Taifa, matokeo yake ni kushindwa kutimiza Wajibu wake, na kuishia kutumika na wanasiasa.

TUFANYE NINI KUUTOA UMMA HUKO? Umma ni lazima utambue pasipo wao Ikulu ni kazi bure. Tufanye nini?

Anaita sasa.
 
Umma umekosa sifa kuu ya kutambua nafasi yake katika Taifa, matokeo yake ni kushindwa kutimiza Wajibu wake, na kuishia kutumika na wanasiasa.

TUFANYE NINI KUUTOA UMMA HUKO? Umma ni lazima utambue pasipo wao Ikulu ni kazi bure. Tufanye nini?
Nianzie ulipomalizia, nini kifanyike?

Jibu ni kuendelea kuufahamisha umma adui yupo ndani yao kwa jina la kutojitambua
Kwamba umma usiendelee kulalamika unapotumika na wachache kwa masilahi yao

Kuueleza umma nafasi yake katika Taifa na kwamba Taifa ni wao

Kwamba umma una nafasi ya ku shape destination na ndio ume hold future yake

Umma ujitambue, kwamba wanaodhani ndio umma wafike mahali wauogope umma.
Nimetoa mfano wa jinsi vijana walioko madarakani wanavyovurunda nchi hii

Mambo wanayofanya vijana yanatisha na kusikitisha.
Kutwa kucha ni kutafuta ni kupendeza wanaotoa mkate na si kusaidia umma

Kiongozi anashughulikia na mambo ya kipuuzi huku umma unaomtegemea ukiteseka

Viongozi wamepewa zana za kazi ikiwemo sheria na mamlaka kusukuma maendeleo, kupunguza dhiki za wananchi na kujenga mazingira ya Taifa la kesho

Badala ya kutumia zana kwa manufa, wanatumia katika upuuzi.

Kukimbizana na vitu trivial kabisa huku wakijivuna 'nina madaraka, nina mamlaka , sheria inaniruhusu nikutendee kadha wa kadha, nitakuweka mahuhusu n.k.''

Ni amri ya fulani atendewe hivi au vile badala ya amri ya kuimarisha usafi wa maeneo, kilimo elimu na afya, ni udumazi wa hali ya juu ya fikra

Wananchi wanawashangilia viongozi vijana walioshindwa majukumu yao.
Kila uchao wananchi wanajadili upuuzi walioufanya.

Hawana uthubutu wa kuwaambia si kipaumbele na wala hawahitaji ujinga na upuuzi
Wananchi hawana muda wa kuuliza jana kiongozi huyo amefanya nini.
Wanajadili upuuzi wa kundi la vijana wasiojitambua linaloufanya umma usijitambue

Ili kufikia hatma njema , wananchi wakemee vijana wanao abuse madaraka, wanaofanya kazi za kufurahisha na si matokeo kwa umma, wasio na ubunifu bali udunifu

Ni kuwaeleza umma hauhitaji siasa ,visasi, itikadi na amri za kipuuzi zisizomsaidia mwananchi kwa lolote, unahitaji maendeleo.

Umma hauhitaji kusikia nani anaitwa nani, unahitaji kuona matokeo kutoka kwa fulani

Kundi hili la vijana lianze kukemewe na kutengwa.
Lisisikilizwe kwa upuuzi, lishangiliwe kwa ujinga,lisijadiliwe linapoendekeza utoto

Ni kundi la vijana wasio na innovation au mission. Wakitoka hutasikia la kujivunia
Vijana hao watengwe na umma kwanza, ili tupate watu wenye maono na fikra!

Kwa mfano, hatuhitaji vijana wanaotoa amri za kupeleka watu mahubusu, kesho yake wanampokea balozi wa Japan kwa msaada wa ujenzi wa vyoo vya shule !

Tusemezane
 
KAULI YA MBUNGE KUHUSU TEUZI ZA Mh RAIS

Mbunge wa upinzani amezungumzia teuzi ambazo wanawake 'wameachwa' kando

Kauli ilitegemewa kuleta malumbano , kinyume chake ukimya umetanda

Ukimya hauna maana ya kumpuuza au kukubaliana naye, ni ishara hisia tofauti

Awamu ya nne, ilikuwa kawaida kuwa na uwiano katika nafasi za teuzi kijinsia

Hilo lilikwenda mbali na hata kuzingatia tofauti nyingine zilizopo katika jamii yetu

Sheria zilizotungwa na bunge lenye jinsia na tofauti zote za kijamii ndizo zinatumika

Sheria zinazolazimisha uwiano wa jinsia zimeeleza ni kwa namna gani utekelezwe
Tuna mifano ya chaguzi ndani ya vyama katika nafasi za Ubunge n.k.

Ipo sheria inayomwelekeza Rais kuteua wasaidizi bila kigezo kingine chochote
Kuteua jinsia moja au kucanganya kwa uwiano ni utashi, ''hafungwi'' na sheria yoyote ile

Rais Aweza teua wanawake wote, halikadhali kuteaua wanaume wote kwa mantiki ile ile

Kusema kuwa Rais hajali au hapendi jinsia fulani si sahihi kwa mujibu wa sheria zetu

Kwa upande mwingine, jamii yetu imejengwa na mchanganyiko wa itikadi za imani, jinsia, rika na chochote unachoweza kufikiria kuwemo katika jamii ya watu milioni 45

Hata pale ambapo sheria busara ni kitu muhimu

Tusifike mahali tukaielekeza jamii kuhisi kuna tofauti au mapungufu miongoni mwetu

Tunaamini kwa dhati Tanzania ya leo ina watu weye uwezo wa elimu, busara na hekima
Tanzania inawezekana kupata mtu kutoka eneo lolote la jamii kutekeleza majukumu

Tusipotumia busara kuangalia jamii na upana wake tunaweza tia ufa wa umoja wa Kitaifa

''Ushahidi'' utakuwepo hata kama si kweli kwasababu upo na unawezatumiwa vibaya

Tusemezane
 
VIJANA WANAVYOBORONGA KATIKA UONGOZI

Mabandiko 383 na kuendelea tumeongelea hoja ya vijana kuliangusha Taifa kutokana na uwezo dhaifu au kutokuwa na maono . Ni tatizo kubwa nchini kuliko matatizo yaliyopo

Mfano, kulinda vyanzo vya maji ni jambo zuri sana lililowekewa sheria.
Kila mmoja anapaswa kufuata sheria ili kulinda mazingira na hasa vyanzo vya maji

Kuna shauri moja limemalizwa kwa mkuu mmoja wa eneo kushindwa kesi aliyosimamia akiamini kufanya hivyo ni 'muhimu'

Nia ya kiongozi huyo kijana ni njema kabisa, jinsi gani anateitekeleza inashangaza

Shauri la kwanza limemamlizika kwa kiongozi huyo kutakiwa alipe fidia huku akiomba mwanasheria mkuu ashirikishwe shauri la madai kwani alitekeleza majukumu ya nchi

Hoja si kutekeleza majukumu bali namna gani anatekeleza majukumu.
Serikali haikumwagiza kufanya mambo bila weledi kwa mgongo wa kutimiza majukumu

Kiongozi huyo alitakiwa kushirikisha timu ya wanasheria, kusimamia zoezi kwa ukubwa wake na haki na si kwa mtazamo wa kisiasa au chuki. Hakufanya na kashindwa mbele ya sheria

Kuna matatizo ya watu kuvamia vyanzo vya maji makubwa kuliko anayoshughulika nayo
Kuna matatizo makubwa yanayowakabili wananchi yanayohitaji suluhu ya pamoja

Katika mwezi mzima tatizo la mtu mmoja limeonekana kama ndilo tatizo la eneo lake

Kesi ikiendelea kuna gharama nyingi nchi inaingia achilia mbali muda uliopotea

Tujiulize, katika mwezi mmoja, miwili , mitatu au mwaka kiongozi huyo amefanya lipi la maana zaidi ya hili ambalo limeonekana halikuwa na sababu za msingi?

Ndivyo kiongozi mmoja alivyokimbizana na mtu mmoja kumweka mahabusu.

Tutakapomuuliza kiongozi huyo kijana katika miezi 3,6,12 amefanya nini kwa wnananchi hatakuwa na jibu. Katika kipindi hicho amebuni nini eneo lake, hana jibu

Mifano ni mingi inatosha kusema vijana ni tatizo kubwa sana la maendeleo ya nchi yetu
Viongozi wanaolitia Taifa hasara hawatufai, ni vema wakaondolewa

Na wala ujana usiwe sifa ya uongozi, tunaona wanavyoliangusha Taifa kila siku

Tusemezane
 
UTARATIBU WA MPYA 'MAHABUSU' UNAVYOSHIKA KASI
CCM HAIWEZI KUKWEPA LAWAMA

Mwanzo wa mabandiko baada ya uchuguzi tulisema hakuna kazi ngumu na muhimu kama kuliunganisha taifa baada ya 'majeraha' yanayotokana na uchaguzi

Hakuna mafaniki ikiwa taifa limegawnayika, halielewani na linaishi kwa hofu na visasi
Kazi ya kwanza kulileta Taifa pamoja ni kuhakikisha habari ni za maendeleo ya wananchi

Kumalizika kwa uchaguzi si kumalizika kwa shughuli za siasa nchini au pengine
Msajili wa vyama anaendelea na kazi, tume ya uchaguzi inaendelea na kazi

Uwepo wa taasisi hizo ni kielelezo cha uendelevu wa shughuli za siasa nchini
Hakuna sheria ya nchi inayosema kumalizika kwa uchaguzi ni mwisho wa msimu wa siasa

Matukio yanayoendelea nchini yanatishia uhai na ukuaji wa demokrasia nchini.
Wimbi la kukamatwa viongozi wa upinzani au kuandamwa umeshika kasi

Kukamatwa hutumia sheria inayotoa fursa kwa mamlaka mbali mbali kama RC au DC
Aghalabu kukamatwa 'pattern' ikionyesha siku za mwisho wa wiki

Kukamatwa mwisho wa wiki kuna tatizo la kupata waendesha mashtaka, mahakimu n.k.
Hii maana yake, katika masaa 48 yaliyopo kisheria mtu aweza kamatwa tu kwa matakwa

Hatuamini viongozi wa upinzani ni wasafi kama tusivyoamini ni wachafu
Kitakachotusaidia kupata jibu ni kufuata mkondo wa sheria

Ikiwa kuna makosa ni wajibu kutumia njia za kisheria kuwafikisha mahakamani.

Ikiwa si sivyo njia nyingine za kuwataka kufika mbele ya sheria zinaweza kutumika.
Kwa mwendo uliopo masaa 48 na baadhi ya nyakati bila kesi ni kawaida

Haya ni matumizi mabaya ya madaraka. Matumizi mabaya hayana maana ni mkaosa bali matumizi mabaya yenye kukiuka haki za msingi za Raia kwa kutumia sheria zilizopo

Matukio hayo yanazidi kujenga ufa miongoni mwa wananchi, CCM na serikali yake
Haiwezekani kuitenga CCM na serikali kwani kwa mfumo wetu ni ''baba na mtoto

Ikiwa shughuli za siasa zimeharamishwa, ni vema tangazo likatoka kwa mujibu wa sheria, na kuzitaka taasisi zinaziohusika kusimamisha kazi zao hadi itakapotangazwa tena kisheria

Hali ilivyo, kuna chuki inajengeka katika jamii na kuhusisha CCM na serikali yake. Haiwezekani CCM ikaruhusiwa kuendelea na siasa vyama vingine vinatishiwa

Taswira ya nchi inachafuka na chuki zinatawala jamii badala ya upendo na haki

Kwa yanayotokea CCM na serikali yake zinaiweka nchi katika mgawanyiko usio na ulazima
Matukio hayo yana mkono wa CCM na haiwezi kukwepa lawama hata kwa bahati mbaya

Katika nchi masikini na yenye matatizo lukuki kama TZ haya ya kukimbizana wenyewe kwa wenyewe yanatusaidiaje? Yanatatu kero zipi ?
Kwanini yanafanyika ? Wahusika hawayaoni?

Tusemezane
 
Kazi na dawa! vivyo hivyo na kwa wakati mjadala huu muhimu ukiendelea naomba tupumzike kidogo tusikilize kibao hiki cha Dr. Remmy (R.I.P) kisha tuendelee na mjadala. Karibu

 
UTENDAJI HUU UNA MASHAKA JUU YAKE

Kuna tukio la kukamatwa mbunge, bado hajafikishwa mahakamani na hilo libaki kama lilivyo

Katika tukio hilo kumetokea mambo mawili yanayoshangaza na kutia shaka juu ya utendaji
Mbunge aliyekamatwa alipelekwa kwa mkemia mkuu ili apimwe 'mkojo'

Tuhuma za mbunge husika hazina 'uhusiano' na kupelekwa kwa mkemia mkuu
Pamoja na kazi nyingine za mkemia mkuu, moja ni kuhakiki vipimo kubaini aina vilivyomo

Hata kama mtuhumiwa anashukiwa kuwa na vitu vinavyohitaji ithbati ya mkemia kuna taratibu za kufuatwa. Kazi ya Polisi ni kusimamia utii wa sheria na kufuata sheria kama zilivyo

Polisi kama eneo jingine la kazi linashirikiana na vyombo vingine kubaini au kupata ushahidi
Vyombo hivyo ni kama wataalam wa afya wanaosaidia kupatikana kwa majibu ya tatizo

Polisi wanapohisi kuna mwananchi asiye katika hali ya kawaida, jukumu lao ni kumfikisha kwa daktari atakayeamua ni aina gani ya uchunguzi na vipimo vitakavyoweza kutoa majibu

Ndiyo maana Polisi hupeleka watuhumia majeruhi hospitalini, Mahakama huomba ushauri wa kitatibu ili kuweza kutoa haki kwa haki, vidhibiti na ukweli

Kitendo cha kumpeleka mtuhumiwa kwa mkemia mkuu kina maana moja.
Kwamba Polisi wana utaalam wa kubaini (preliminary diagnosis) na wanachotaka kupata ni laboratory investigation ili waweza kufikia diagnosis ya mwisho wao wenyewe!!!

Huku ni kuingilia mamlaka ya taaluma nyingine. Ikiwa Polisi walihisi mhusika anaapaswa kupimwa, ni wajibu wao kupata ushauri kwa watalaamu kama vipimo husika vinahitajika

Mkemia mkuu (Chief chemist) anatoa majibu ya sample kitaalam kwa kuanisha aina vitu(contents) zinazopatikana katika sampuli (sample) na kiwango chake

Kazi ya kuoanisha sampuli na mwendendo au maisha ya mwanadamu ni ya daktari.
Daktari ndiye anaweza kutafsiri mahusiano ya kilichoonekana kwa mkemia na hali ya mhusika

Inaendelea
 
UTENDAJI HUU UNA MASHAKA JUU YAKE (II)

Wengi wanadhani mkemia mkuu anatoa taarifa za sampuli flani ina ( 'bangi,heroine n.k)

Mfano wa mjadala, mkemia mkuu anaweza kusema sampuli ina Cannabinoid inayoweza kupatika katika vitu vingi ikiwemo Cannabinol yenye Cannabis

Kazi ya kuunganisha kemikali hizo ni ya Daktari kwa kuelewa ufanyaji kazi wa mwili wa mwanadamu , maingiliano ya kemikali za ndani na za nje n.k.

Mtu asiye na utaalamu akiambiwa sampuli ina Cannabinoid au Steroid , hawezi kutafsiri ni kitu gani wala kuhusianisha na mwili wa mwanadamu au kubaini tatizo lina uhusiano gani

Kosa la pili ni kudhani mtu atendaye vitu visivyo vya kawaida ni mgonjwa wa akili
Yes anaweza kuonekana hivyo lakini si lazima awe hivyo.

Nyakati za nyuma wagunduzi wakubwa duniani kama Galilei , Newton n.k. walionekana ni wendawazimu ingawa leo tunajua ''wendawazimu'' ni wale walioshindwa kuwaelewa

Hata ikitokea mhusika ni mwendawazimu (psychiatric) bado kuna mengi ambayo Daktri pekee ndiye mwenye uwezo wa kuyabaini na kuyaeleza kitaalamu.

Maradhi ya akili yanaweza kutokea kwasababu nyingi kama kurithi, mazingira n.k.

Sampuli ya mkojo peke yake hata kama ina kemikali zisizoruhusiwa haielezi ugonjwa wa mtu wala matukio anayofanya au chochote kile, isipokuwa tu kwa ushauri wa kitaalamu

Wenye kesi nzito za mauaji, Mahakama hujiridhisha kuhusu uthabiti wa akili zao kwa ushauri wa wataalam na si kwasababu sampuli zao zimekutwa na kilevi au la

Hii maana yake, sampuli za kilevi peke yake hazielezi afya ya mtu.

Sampuli haziwezi kumtia au kumtoa mtu hatiani hadi pale wanasheria watakaporidhika pasi na shaka na ushauri wa wataalam wa fani nyingine zikiwemo mkemia au afya.

Siyo lazima mwendawazimu awe mtumiaji wa vilevi ingawa vilevi vinaweza kuchangia sehemu ya tatizo. Wapo watu wenye maradhi hayo ingawa hawatumii vilevi

Dhana ya magonjwa ya akili yanatokea kwasababu za matumizi ya vileo ni potofu

Tumeeleza na mifano michache kuonyesha kuwa tukio la Polisi kumfikisha mtuhumiwa kwa vipimo vya mkojo halikuwa sahihi, lina mapungufu, wala lisingetoa matokeo yoyote

Ni tukio la kuchukua mamlaka za taaluma nyingine likishindwa kisheria moja kwa moja.

Vipimo vilivyoagizwa na Polisi kwa mkemia mkuu haviwezi kutumika katika kesi yoyote kwasababu havikufuata taratibu

Tukio linatia shaka na nia yake, kama Watendaji walifahamu nini wanataka na mwenendo mzima wa utendaji wa wahusika

Hata hivyo tukio hilo linatueleza kitu kimoja, kwanini serikali inashindwa kesi nyingi licha ya watuhumiwa kukamatwa na ushahidi. Ignorance of law is no excuse

Tusemezane
 
VIPIMO VINGETOA MAJIBU GANI KWA MASHTAKA HAYA?

Mabandiko mawili yaliyopita tumeongelea vipimo vya mkojo kupata picha ya nini maana ya vipimo
Tulisema shauri hailijazungumzwa na ni mapema mno kujua nini shtaka linasema

Kesi bado ipo mahakamani, suala hilo likiwa mbele ya sheria haliwezi kujadiliwa
Kinachojulikana ni shtaka linalomkabili mhusika lililosomwa na ambalo si siri

Shtaka linahusu uchochezi, na kama tulivyosema hatujadili shtaka

Tunachoweza kujadili kwa uchache ni mahusiano ya vipimo vya mkojo na shtaka la uchochezi

Pengine upo utaalam mpya wa kisasa tusiofahamu, swali letu ni moja matokeo ya vipimo vya mkojo yanawezaje kuonanishwa na shtaka la uchochezi? Uchochezi ni kauli na vipimo hutoa matokeo ya kikemikali, kuna uhusiano gani?

Tusemezane
 
KWAHILI LA SaMPULI, POLISI WAJITATHMINI

Tunaliongelea suala la sampuli la kesi ya 'uchochezi' mtuhumiwa akitakiwa kupimwa mkojo
Ni suala zito si kwasababu ya mhusika au kipimo, bali uaminifu wa Jeshi (credibility)

Kumekuwepo na tuhuma sehemu mbali mbali duniani Polisi kupandikiza ushahidi kwa watuhumiwa
Yapo mataifa Polisi wanalazimika kuvaa kamera wakiwa katika mjukumu
Hatua hizo zinachukuliwa makusudi kurudisha heshima na uaminifu wa majeshi kwa umma 'credibility'

Malalamiko ya kupandikiza ushahidi, kufungua mashtaka yasiyolingana na kosa yamekuwepo nchini

Tunaamini kwa dhati kauli ya jeshi la polisi inapaswa kuwa thabiti na ya kuaminika

Kwa suala hili na kipimo cha mkojo kwa kesi ya uchochezi inasikitisha

Polisi kama taaluma nyingine wanapaswa kufuata sheria na taratibu wakiongozwa na weledi

Haieleweki waliotaka kupata kipimo cha mkojo kwa mtuhumiwa wa uchochezi walilenga nini hasa

Ikiwa lengo lilikuwa kudhalilisha mhusika kwa sababu zozote zile hilo linatokea kwa gharama ya jeshi
Wahusika wangejitokeza na kuueleza umma nini kilitarajiwa katika sampuli kuhusiana na uchochezi

Kama hakuna majibu, kuna upungufu wa weledi, utendaji wa jazba na watakaoamini ukiukwaji wa maadili na haki za watuhumiwa bila sababu yoyote

Waliotaka sampuli kwa mtuhumiwa hawatalitendea haki Jeshi la Polisi ikiwa hawatafafanua nini walikusudia

Hili si kuwa linawaweka mahali pagumu kiutendaji na kimaadili bali linaondoa uaminifu (credibility ) ya jeshi

Kesho itakapotokea shauri linalohusu sampuli, wananchi wataliangalia kwa jicho la tukio hili
Kesho Jeshi litakapotoa kauli wananchi wataiangalia kwa jicho la mashaka

Wahusika hawakuliendea Jeshi haki, wamelifedhehesha na kuliondolea heshima na credibility unless wajitokeze na kufafanua yaliyotokea. Kukaa kimya hakutasaidia pengine ni bora kuomba radhi ikibidi

Tusemezane
 
''YA BUNGE NA CUF''

TUNAENDA MBELE KAMA BOYA

Baada ya tukio la kupima 'mkojo' lililofedhehesha Jeshi la Polisi, inatosha kusema upo umuhimu kwa Jeshi kujitenga na wahusika wa tukio lile.

Tunaamini katika weledi wa Jeshi, makosa ya mtu au kundi wasilipake matope.

Habari katika dunia ya leo zinasomwa kila kona
Kama zinavyoandikwa habari za Tanzania duniani ndivyo habari za Jeshi zitaandikwa.

Kesi inamvuto, ikisomwa kesi ya sedition inachunguzwa kwa mkemia mkuu, hatudhani taifa litakuwa limetendewa haki.

Katika mtiririko wa matukio Mh Spika amethibitisha kuvuliwa ubunge wabunge 8-CUF
Ni baada ya taarifa kutoka baraza kuu lililo chini ya Prof Lipumba

Inaeleweka kuna mgogoro wa uongozi ndani ya CUF ulipopelekea kuvunjika kwa amani Ubungo
Kundi la Mwenyekiti lilivamia mkutano wa chama kingine na kufanya vurugu

Tukio hilo halikuzungumzwa kwa ukubwa wake wa uvunjifu wa amani wala taasisi husika kama Msajili wa vyama na Jeshi la Polisi ''kutilia maanani''.

Ilionekana ni tukio la ''kawaida'' tu la kisiasa licha ya watu kuumizwa
Wiki iliyopita Msajili alikemea CUF na CHADEMA kwa malumbano yanayotishia usalama

Alifanya hivyo akibeba dhima ya ofisi yake na masilahi maPana ya nchi na Taifa

Malumbano ya CUF na CHADEMA ''yanahusiana'' kwa sehemu 'na mgogoro wa CUF
Mgogoro upo mbele ya mahakama na si muafaka kuuzungumzia

Kitendo cha Spika kukubali maagizo ya ''baraza'Prof Lipumba yanaamsha hisia na udadisi

Mh Spika anajua mgogoro ndani ya CUF,kwamba sheria haijakamilika katika maamuzi

Inakuwaje anakubali barua ya upande mmoja wa shauri lililoko mahakamani?

Je, Mh Spika ameangaliaji uhuru wa mihili mitatu ya nchi katika utendaji wake?

Hisia zinazotanda miongoni mwa watu hazijengi umoja wa kitafia, zinaondoa imani na zinaleta hisia zisizo na ithibati kuwa mgogoro wa CUF na 'msaada' nyuma yake

Wanaodhani hivyo pengine wanaongozwa na hoja ya lini shauri la mahakani likafanyiwa maamuzi nje ya utaratibu kwa maana kabla ya shauri kumalizika.

Kwa tukio hili,Mh Spika na Msajili wa vyama watalitendea haki Taifa kwa kufafanua ni utaratibu gani Wabunge wamefutwa Ubunge likiwa mahakamani.

Tusemezane
 
TUKIO LA TANGA SIYO USULUHISHI NI UPATANISHI
MITANDAO ISIBADILI MAANA NA ASILI YA TUKIO

Kwanza tufafanue kwa kadri maneno mawili.
Usuluhishi inatokana na neno suluhu 'reconciliation'

Katika mchezo wa soka dakika 90 zikimalizika bila kufungana hiyo ni suluhu
Ikitokea timu zimefungana 2-2 au 4-4 hiyo ni 'Sare' siyo suluhu

Kwa mantiki ya kiswahili inapotokea tatizo ambalo pande mbili zina hoja zenye uzito kinachotafutwa ni suluhu si upatanishi

Pili, inapotokea upande mmoja umeghadhabishwa kutokana na upande mwingine, na ule wenye ghadhabu ukawa na haki, kinachotafutwa ni upatanishi si suluhu

Suluhu ni kuridhiana baina ya pande, upatanishi ni msamaha kwanza unapolekea kuridhiana

Tumeeleza haya kutokana na tukio la Tanga ambapo Mh Rais aliwaita vijana vawili, Ruge na RC aliyesusiwa na vyombo vya habari na kuwasihi 'wapatane na wayamalize'

Mh Rais hakusema watafute suluhu bali wapatane kwa maana tuliyoeleza hapo juu

Takribani wiki na mwezi zimekuwepo jitihada mitandaoni za kutaka habari za RC ziandikwe
Hoja zinazojengwa ni dhidi ya jukwaa la wahariri kuendelea kususia habari zake

Wapo walioenda mbali na kusema jukwaa la wahariri linafanya makosa, si sehemu ya siasa
Tukio zima lilikuwa la 'kihalifu' si la kisiasa, kusema ni jambo la siasa ni kupotosha umma

RC alikwenda katika nje ya ofisi ambako aliweka kompyuta zake akifanya kazi na hata 'kuandaa' habari zitangazwe kama anavyotaka na si kama taaluma ya habari inavyoeleza

Kitendo cha kuwa na kompyuta nje ya eneo la kazi tena kwa chombo binafsi si jambo jema

RC ni mkuu wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, kuna uhakiki gani habari nyeti zinaweza kuhifadhiwa katika chombo binafsi ? Hili tu kwa kuanzia ni kosa

Clouds wana kosa la kutofuata maadili ya kazi. Kumpa RC dawati ni kwenda kinyume na maadili na miiko ya kazi inayowataka kutenda haki kwa kila mtu na kusikiliza pande husika

Ugovi wa Askofu na RC hauwezi kutendewa haki na Clouds ikiwa kuna ofisi za mmoja wao ndani. Hili ni kosa la kimaadili tu ambalo linajadilika kimaadili na haki

RC kwenda Clouds na kuzua sintofahamu iliyopelekea hata mahasimu wa biashara kuungana na kulaani tendo si jambo linaloweza kupewa haki katika mizani yoyote ya fikra na ukweli

RC kukataa kushirikiana na tume na kupelekea waziri kupoteza kazi yake si jambo la busara. RC alifanya hivyo akijua huenda kuna 'nguvu' bila kujali haki au uzito wa kosa alilotenda

Jukwaa la wahariri halikususia habari kwasababu ya ugomvi wa RC, Clouds au Askofu
Lilifanya hivyo katika 'spirit' ya kulinda taaluma na hasa kuzuia mamlaka nyingine kuwakwaza

Inaendelea....
 
TUKIO LA TANGA SIYO USULUHISHI NI UPATANISHI
MITANDAO ISIBADILI MAANA NA ASILI YA TUKIO

Kususiwa habari kumeleta athari kwa RC kwa kutompa nafasi 'dysfunctional'

Pili kumeibua hoja nyingine mbali ya zile zisizo na majibu hadi sasa
Haya yanaondoa uaminifu wake mbele ya jamii 'credibility' na anabaki na nguvu za ofisi

Mh Rais ameona athari hizo na kutumia lugha laini ya kupatanisha kwa maana ile ile ya kwamba kuna mkosaji na mkosewaji wapatane akimuombea Mkosaji 'msamaha'

Ni katika kutafuta upatanishi na jukwaa la wahariri Mh alisifia media kwa kuzitaja.
Hapa anaviomba vimalize mgomo dhidi ya RC kwa kumuombea 'Msamaha' kiutu uzima

Ni makosa kwa baadhi ya watu waliotumwa mitandaoni kugeuza suala hilo kama Suluhu
Hakuna suluhu inayotafutwa hoja ipo wazi, yupo mkosaji na mkosewaji 'clouds'

Vurugu zilitokea clouds si ofisini kwa RC na wala clouds hawakuwahi kujibizana kwa hilo
Clouds wakikubali matumizi ya neno 'suluhu' wamekubali kufanya makosa! hakuna

Clouds wakikubali upatanishi kwa maana ya kukosewa, watakuwa wamekubali 'msamaha uliombwa na Mh Rais' jambo jema kabisa.

Hata hivyo nao wanawajibu wa kulimaliza suala hilo kwa busara kama walizotumia za kupuuza majibazano na RC katika kipindi chote cha timbwili

Ili kumaliza kwa busara, Clouds washirikiane na wadau wenzao wa TEF si kutangaza suluhu bali Msamaha' alioombewa RC na Mh Rais

Inaendelea...
 
Back
Top Bottom