Duru za Siasa: Awamu ya 5 - Uongozi na Yanayojiri

SAKATA LA MCHANGA NA BUNGE LETU

Mh SPIKA KWA HILI LA LUSINDE NA MNYIKA KUNA KUPOTOKA

Mjadala unaondelea nchini ni hatua za Serikali kupitia kamati ya Prof Mruma-'wizi' wa mchanga wa madini

Mjadala umegawanyika maeneo mawili, wanaounga mkono kwamba ni hatua nzuri za kuanzia
Hoja yao ikiwa yaliyopita si ndwele tugange yaliyopo na yajayo

Pili,wanaosema tumechelewa , tuanze na wahusika waliotufikisha hapa, kisha twende mbele
Hawa wana hoja, hatuwezi kutenda makosa yale yale, bila kuangalia tulipokosea na kwasababu gani

Katika kundi la pili, kuna kunyooshewa vidole kwa watu na taasisi.
Kwanza ni kwa CCM inayounda serikali na taasisi zinazosimamia sekta ya madini

Eneo jingine ni Bunge. CCM yenye idadi kubwa ya Wabunge ilishindwa kusimamia serikali ya CCM

Hoja ya Bunge inaeleza mchango wa Wapinzani uliozimwa kwa sauti 'ya ndiyoo', kukubali kwa wingi na si mantiki

Sakata limerudi tena bungeni. Ilitegemewa kungekuwa na kujifunza kwa namna makosa yasijirudie

Majibizano ya Mbunge Lusinde na Mnyika yamepelekea vurugu ambazo busara ingetumika zisingetokea

Spika alipoombwa 'taarifa' alisema '..unamchokoza Lusinde' akibariki kauli za Lusinde bila kujali athari zake
Mnyika aliomba kufutwa kwa kauli ya Mwizi, Spika hakumsikiliza akitaka Lusinde aendelee!!

Spika amesahau kauli ya H.Mdee ilisikika katika vipaza sauti na alichukuliwa hatua
Je, utaratibu umebadilika lini hadi kuita Askari na kumtoa Mnyika katika dhalili ya kiasi kile

Ni dhahiri Spika alitaka kusikia alichokita na si kile kinachosemwa. Kauli za 'Mwizi' hazikuwa na ladha
Spika angetumia busara kusikiliza hoja kwa utulivu yasingetokea yaliyotokea. Inasikitisha sana

Spika hakutaka kusikia jingine zaidi ya sifa alizokuwa anazimwaga Lusinde kwa Serikali
Ni utaratibu huo ndio umetufikisha hapa pa tatizo la Mchanga na madini kwa ujumla

Hoja ya Mnyika tunaibiwa dhahabu na si mchanga peke yake ina mantiki na uzito.
Ilipaswa kujadiliwa ili kutafuta majibu.

Hoja ilikuwa nzito kuliko amri ya kutumia askari ikionyesha udhaifu na mapungufu ya busara

Tusipobadilika na kujadili hoja za nchi tutaendelea kuibiwa.

Matumizi ya nguvu ya Spika hayakulisaidia Taifa kwa bahati mbaya.

Kwa hili Spika aliingia katika mtego wa kujadili viroja badala ya hoja.

Tutaendelea kuibiwa,inasikitisha inauma sana

Tusemezane
 
WABUNGE MSAIDIENI RAIS KWA HOJA NA MANTIKI

Mikataba inayolalamikiwa imepitia katika Bunge kama chombo cha uwakilishi
Marekebisho au hoja zinazotokanazo hujadiliwa bungeni

Inatosha kusema, Bunge ni chombo cha kupanga, kuandaa na kusimamia masilahi ya nchi

Yanayoendelea ndani ya Bunge yanatia shaka kama kweli wawakilishi wetu ni 'serious'

Sakata la jana la Mbunge Mnyika halikupaswa kutokea. Lilitokea kwa uhaba wa busara

Kanuni za bunge zipo wazi, ima mhusika athibitishe kauli au afute kauli zake
Lugha ya bunge ina kanuni zake ikiwa ni pamoja na kutotumia maneno yenye karaha

Jana ilikuwa jambo rahisi, aliyesema athibitishe au afute kauli. Hilo lingemaliza mzozo
Kilichotokea ni kuita askari na kumtoa mbunge kindaki ndaki kwa jambo linalozungumzika

Tukio lingetokea katika serikali za vyuo lisingekuwa kama lilivyo. Busara haikutumika

Muhimu ni namna gani wabunge wanazungumza masuala mazito ya kitaifa
Wabunge ni watunga sheria na kusimamia serikali, wana fursa ya kusaidia Taifa

Kutoa pongezi si kosa, hata hivyo pongezi hazitoshi bila kuwa na 'substance'
Wabunge si watoe pongezi, wana nafasi ya kujenga au kuboresha

Bunge la CCM 'lina nyooshewa vidole' kwa mauza uza ya madini.
CCM kupitia msemaji wake wamekiri makosa siku za nyuma.

Je, si vema wabunge wakatumia fursa yao kusaidia kurekebisha makosa?

Wabunge wanatoa pongezi kwa katazo la mchanga. Huko migodini kuna madini ambayo hatujui nchi inanufaiki vipi. Vile viwanja vya ndege nani ana hakiki vinatumikaje?

Tulitegemea wabunge waseme tumefika hapa kwa makosa abcd ya kisheria
Nini kifanyike ili siku za baadaye yasijirudie

Wabunge wangejiuliza kwanini suala la madini halina ufumbuzi miaka mingi. Nini kifanyike

Kwa ufupi bunge lina nafasi kubwa sana katika kusaidia serikali kutimiza majukumu yake
Ukifuatilia mijadala ni wabunge wachache sana wanaojenga hoja kwa mantiki na weledi

Hivi kwanini tumefika mahali tunatumia askari kubebana mzobemzobe, hatuwezi kutumia sheria , kuziboresha au askari hao kupambana na wezi wa rasilimali za nchi wa ndani na na nje?

Wabunge, pongezeni zenu tumezisikia, mna nafasi ya vyombo vya habari kupongeza.
Swali mnalotakiwa kujiuliza, mumejenga hoja gani za kusaidia pongezi hizo kwa mantiki?

Kazi yenu ni nini mnapokuwa Dodoma? Mnatumiaje nguvu za kisheria kusaidia nchi?

Nani aliwaambia wananchi wana interest kuwasikia mkipongeza bila hoja ?

Tunalalamikia 'kuibiwa' tusisahau walioacha milango wazi wapo Dodoma, wakirushiana vijembe, wakibebana kama wezi. Hawana hoja nyingine zaidi ya kusimama na kupongeza

Wananchi wakinyooshea kidole bunge kwa matatizo yetu wanakosea wapi?

Tusemezane
 
UTEUZI WA WAPINZANI KATIKA NYADHIFA

WAPINZANI WAMEFIKIRIA?

Mabandiko mawili nyuma tumeeleza mzozo na matatizo ya bunge letu. Ni hali inayosikitisha
Kwanza, vikao chini ya wenyeviti matatizo mengi hayatokei. Kwanini yanatokea kwa Mh Spika na Naibu?

Pili, Mh Spika alipaswa kuongoza kwa kanuni akimtaka aliyesemwa 'mwizi' athibitishe au akanushe. Hilo tu

Tatu, Mh Spika aangalie kauli za kupandisha 'morali'. Kauli yake baada ya kuombwa mwongozo haikuwa na ladha

Kwa mtazamo wowote, Mh Spika aangalie video na atathmini kama yaliyotokea yanamhusu mwingine awaye!!!

Tukiondoka huko, tuangalie teuzi za karibuni ambazo wapinzani wameshirikishwa katika serikali ya CCM
Katika bandiko hili tulisema mwanzoni kabisa, Mh Rais ana kazi ya kuliunganisha Taifa kwanza kabla ya agenda

Teuzi hizi za wapinzani ni katika jitihada ingawa zimechelewa zikizingirwa na matatizo mengine yanayoepukika
Matumizi ya nguvu, marufuku ya mikutano, kuminya vyama vya siasa ni sehemu tu ya matatizo yenye makovu

Uteuzi wa wapinzani hauwezi kuunganisha Taifa bila kutoa uhuru wa kushirikia shughuli za kisiasa bila vikwazo

Kwa upande wa wapinzani, teuzi hizo zinapaswa kuangaliwa kwa jicho mujarabu

Uteuzi wa kiongozi mwandamizi wa ACT ulitetewa kwa hoja laini ya fursa ya kutumikia nchi kama katibu mkuu
Ukajengewa uzio kuwa ni kupandishwa cheo na kwamba ni nafasi ya kitaifa si ya chama

Imetokea tena mwenyekiti wa ACT kuteuliwa RC tena mkoa ambao upinzani una nguvu zaidi
Hakuna shaka viongozi wa ACT walifahamu na kutoa baraka kwa mwanachama mwandamizi kupokea uteuzi

Mkuu wa mkoa kwa hali ya kisiasa nchini ni mwanachama wa chama tawala 'by default''

Kuna maswali ya kujiuliza. Je, RC atasimamiaje sera za CCM bila kukinzana na sera za chama chake?

Kiongozi wa ACT bungeni aliwahi kulalamikia marufuku ya mikutano.
Je, akiwa Kilimanjaro atakuwa na msimamo gani? Atafuata maagizo ya RC au atasimamia hoja zake za mikutano?

Maswali ni mengi yasiyo na majibu. Kilicho dhahiri upinzani 'unatumiwa' kumaliza upinzani.

Kisiasa chama cha ACT kinapoteza fursa, taswira yake inatiliwa shaka kuliko uaminifu
Kwa teuzi zinazoendelea kutoka ACT, ni nini matarajio yao siku za mbeleni? Kwamba watafaidika na nini?

Mbele ya safari ACT watakuwa na kazi ngumu ya kujieleza badala ya kujieneza. Hili walitambue kuanzia sasa
Uaminifu wao miongoni mwa wapinzani utatiliwa shaka na huenda ukawa mwendelezo wa kuwatenga

Busara ni kitu muhimu kuliko uwezo wa kufikiri au kutenda. Busara ni uwezo wa kupima kwa mtazamo mpana

Kwa hili la ACT, viongozi wa chama chao wamekosa busara na maono ya muda mrefu. Muda utatuambia

Tusemezane
 
ACT WAZALENDO 'IT'S TOO LATE'

SPIKA: KUFUNGIWA WABUNGE NANI NI CHANZO?

Kwa mujibu wa gazeti moja la kila siku kiongozi mkuu wa ACT akiwa na Msemaji wamezungumzia uteuzi
Hoja yao inahusu teuzi zinazolenga kudhoofisha chama kwa kuchukua makada katika utumishi wa umma

Wamezungumzia hoja ya ACT kuonekana kama CCM-B jambo litakalo waaathirika katika uenezi
Viongozi wameeleza teuzi hizo kufanywa bila kuwasiliana nao kwanza, na kwa Mghwira yupo nje ya nchi

Wanategemea kuongea na Bi Anna ili kama atakubali uteuzi itabidi aachie ngazi katika uongozi
Mabandiko yaliyopita tuliwanasihi ACT kuhusu teuzi zinazoendelea na jinsi zitakavyowathiri kisiasa

Makosa ya ACT
Kwanza, ilikuwa kukabdihi sera baada ya uchaguzi uliokuwa na matatizo makubwa.
Hilo likawaweka tofauti na wapinzani wengine na kuwa karibu sana na CCM

Pili, kuruhusu Mshauri wa chama chao kuwa katibu mkuu kusimamia sera za CCM haikuwa sahihi
M/Kiti wa CCM alisema, baada ya utezi mteuliwa alikwenda kuchukua sera pale Lumumba.

Tatu, utetezi kuwa Mghirwa yupo nje ya nchi hauna mantiki. Teuzi hufanyika baada ya mawasiliano
Bi Mghirwa ana taarifa na chama kina taarifa. Kinachotokea sasa ni reaction kutokana na mtazamo wa jamii

Nne, kosa ni kutoa fursa kwa Bi Mghirwa kuamua ima chama au utumishi wa umma
Mghirwa hawezi kuwa RC umma ukamwelewa ni mtu tofauti na yule wa ACT.
Atabaki kuwa mwanachama wa ACT bila nyadhifa akitumikia sera za CCM akiamini za ACT. Upili wenye utata

ACT huwezi kumpa katibu mkuu benefit of doubt kama mtumishi, ukakataa RC kuwa mtumishi wa umma
Damage ni kubwa.Mnafanya damage control, tambueni ni irreversible itaacha kovu bichi

ACT is vulnerable as lone ranger. Wazalendo must brace for serious political ramifications

Tuangalie ya Spika na fukuza fukuza.

Inaendelea.....
 
ADHABU BUNGENI

Kuna kitu ambacho wengi hawakioni

Mbunge Mnyika alitaka aliyesema mwizi ima athibitishe au afute kauli

Wajibu wa Spika ilikuwa kuangalia mizania kwa kanuni

Laiti Spika angeruhusu aliyesema athibitishe kauli zake au afute haya mengine yasingetokea

Wabunge walio react ni kwasababu ya kutolewa Mnyika wakati akifuata taratibu

Hili likiangaliwa kwa jicho Mujarabu, kulikuwa na ukosefu wa busara hasa ikizingatiwa Spika alianza kuwapindisha mori wanaCCM wenzake. Hakukuwa na sababu zozote kufika lilipofika

Mh Spika anapolalamika kutusiwa, haitoshi. Mh ana wajibu wa kujiuliza kwanini wenyeviti wa bunge hawapati yanayomkuta yeye na naibu wake? Kwanini akina Msekwa, Sitta, Sapi haikuwa hivi?

Adhabu kwa wabunge hazikupaswa kuwepo kama busara ingetawala. Busara ni kitu muhimu sana kwa mtu anapokuwa katika hadhra. Busara haimfanyi awaye kuwa dhaifu

Inasikitisha sana kama ndio mwendo wenyewe

Tusemezane
 
Bunge linapobezwa wengi wetu hatushangai kwani i wazi limejipotezea heshima yake, na hili linaonekana wazi hata kwa watoto wadogo.

Kuna siku niliwahi kusema, HIKI SI KIPINDI CHA KUINGIA KWENYE MIVUTANO ISIYOKUWA NA LAZIMA. Ni jambo jema kuacha upuuzi mwingine upite, hasa pale unapojua ulimbukeni wa akutendeaye.

Laiti ningekuwa ni mimi, na kwa sababu sitarajii busara yoyote wala hekima ukumbini, ningesema niliyopanga kusema tu na kuacha upuuzi uendeshwe na wapuuzi wenyewe.

Mnyika anafukuzwa,, anafuatwa na askari anaombwa asindikizwe, bado anakaidi, anabebwa juujuu eti anaenda anarusha na kuzuia miguu kama mtoto mdogo, kwanini hakutoka tu kimyakimya? Haki gani aliyotarajia kupewa wakati Spika ameshaonesha ukaidi?

Simama pinga chochote kwa hoja, wakutusi wakuzomee, watz watakuwa wameshasikia hoja, usivutane na limbukeni, tutakuweka kundi moja nao.

Usitolewe kwenye mstari kirahisi hasa kama wewe unajinasibu kuwa mwerevu.

Bunge linatufanyia Maigizo makubwa mno hakika. Kamwe sitaliita Tukufu.


IPI NI NAFASI YA BOKSI LA KURA KATIKA KULETA MABADILIKO TUPASWAYO KUPATA?

Anaita sasa.
 
Bunge linapobezwa wengi wetu hatushangai kwani i wazi limejipotezea heshima yake, na hili linaonekana wazi hata kwa watoto wadogo.

Kuna siku niliwahi kusema, HIKI SI KIPINDI CHA KUINGIA KWENYE MIVUTANO ISIYOKUWA NA LAZIMA. Ni jambo jema kuacha upuuzi mwingine upite, hasa pale unapojua ulimbukeni wa akutendeaye.

Laiti ningekuwa ni mimi, na kwa sababu sitarajii busara yoyote wala hekima ukumbini, ningesema niliyopanga kusema tu na kuacha upuuzi uendeshwe na wapuuzi wenyewe.

Mnyika anafukuzwa,, anafuatwa na askari anaombwa asindikizwe, bado anakaidi, anabebwa juujuu eti anaenda anarusha na kuzuia miguu kama mtoto mdogo, kwanini hakutoka tu kimyakimya? Haki gani aliyotarajia kupewa wakati Spika ameshaonesha ukaidi?

Simama pinga chochote kwa hoja, wakutusi wakuzomee, watz watakuwa wameshasikia hoja, usivutane na limbukeni, tutakuweka kundi moja nao.

Usitolewe kwenye mstari kirahisi hasa kama wewe unajinasibu kuwa mwerevu.

Bunge linatufanyia Maigizo makubwa mno hakika. Kamwe sitaliita Tukufu.


IPI NI NAFASI YA BOKSI LA KURA KATIKA KULETA MABADILIKO TUPASWAYO KUPATA?

Anaita sasa.

Bunge limenajisiwa siku nyingi kutokana na kuendekeza ushabiki, uhasama na visasi visivyokuwa na maana. Bunge limekuwa ni sehemu ya kutupiana vijembe na kila aina ya bezo huku vikichekelewa hususani pale walengwa wanapokuwa ni wabunge wa upinzani. Kiti cha spika kimeonesha wazi kukosa busara na kutawaliwa na jazba na mihemko kwenye masuala ambayo yangeweza kutatuliwa kwa njia ya utulivu kabisa.

Sitaki kumtetea Mnyika kwenye hili lakini kulikuwa hakuna mantiki ya kupuuzia mwongozo wake na kumuacha Kibajaji aendelee wakati ametoa tuhuma nzito za rushwa. Laiti ingalikuwa ni mbunge wa upinzani ametoa tuhuma zile Jenista Mhagama au mwanasheria mkuu lazima wangesimama mara moja kuomba muongozo na wangesikilizwa... ambacho kingefuata ni kutakiwa kufuta kauli au kuomba radhi. Lakini spika ameonesha udhaifu dhahiri wa kuachia wabunge wa chama chake kutamba watakavyo.
 
Bunge linapobezwa wengi wetu hatushangai kwani i wazi limejipotezea heshima yake, na hili linaonekana wazi hata kwa watoto wadogo.

Kuna siku niliwahi kusema, HIKI SI KIPINDI CHA KUINGIA KWENYE MIVUTANO ISIYOKUWA NA LAZIMA. Ni jambo jema kuacha upuuzi mwingine upite, hasa pale unapojua ulimbukeni wa akutendeaye.

Laiti ningekuwa ni mimi, na kwa sababu sitarajii busara yoyote wala hekima ukumbini, ningesema niliyopanga kusema tu na kuacha upuuzi uendeshwe na wapuuzi wenyewe.

Mnyika anafukuzwa,, anafuatwa na askari anaombwa asindikizwe, bado anakaidi, anabebwa juujuu eti anaenda anarusha na kuzuia miguu kama mtoto mdogo, kwanini hakutoka tu kimyakimya? Haki gani aliyotarajia kupewa wakati Spika ameshaonesha ukaidi?

Simama pinga chochote kwa hoja, wakutusi wakuzomee, watz watakuwa wameshasikia hoja, usivutane na limbukeni, tutakuweka kundi moja nao.

Usitolewe kwenye mstari kirahisi hasa kama wewe unajinasibu kuwa mwerevu.

Bunge linatufanyia Maigizo makubwa mno hakika. Kamwe sitaliita Tukufu.


IPI NI NAFASI YA BOKSI LA KURA KATIKA KULETA MABADILIKO TUPASWAYO KUPATA?

Anaita sasa.
Albert Einstein once said: " A clever person solves a problem. A wise person avoids it."
 
Bunge limenajisiwa siku nyingi kutokana na kuendekeza ushabiki, uhasama na visasi visivyokuwa na maana. Bunge limekuwa ni sehemu ya kutupiana vijembe na kila aina ya bezo huku vikichekelewa hususani pale walengwa wanapokuwa ni wabunge wa upinzani. Kiti cha spika kimeonesha wazi kukosa busara na kutawaliwa na jazba na mihemko kwenye masuala ambayo yangeweza kutatuliwa kwa njia ya utulivu kabisa.

Sitaki kumtetea Mnyika kwenye hili lakini kulikuwa hakuna mantiki ya kupuuzia mwongozo wake na kumuacha Kibajaji aendelee wakati ametoa tuhuma nzito za rushwa. Laiti ingalikuwa ni mbunge wa upinzani ametoa tuhuma zile Jenista Mhagama au mwanasheria mkuu lazima wangesimama mara moja kuomba muongozo na wangesikilizwa... ambacho kingefuata ni kutakiwa kufuta kauli au kuomba radhi. Lakini spika ameonesha udhaifu dhahiri wa kuachia wabunge wa chama chake kutamba watakavyo.

Hiyo busara hakuna asiyejua kuwa haipo Bungeni, ndio maana tunasema Utukufu wa Bunge ni Batili leo hii.

Na ndio maana unaona ka very minor issue kamezua Tatizo kubwa zaidi. Madai ya Mongozo tu. Pande zote zime-act childishly, vile huwezi kusema mwerevu ni nani.

Anaita sasa.
 
Albert Einstein once said: " A clever person solves a problem. A wise person avoids it."
Ubarikiwe Mkuu.

Bado nasisitiza HII SI AWAMU YA KUINGIA NAYO KWENYE MIVUTANO ISIYO YA LAZIMA.

Yapo ya kusimamia kidete, lakini hayapiganiwi kwa nguvu kubwa hivyo Tunahangaikia mambo madogo. Ni lazima Siasa zetu zibadilike sasa.

Anaita sasa.
 
Na ndio maana unaona ka very minor issue kamezua Tatizo kubwa zaidi. Madai ya Mongozo tu. Pande zote zime-act childishly, vile huwezi kusema mwerevu ni nani.

Anaita sasa.
Mkuu, busara ilikosekana mwanzo na kuzua yote yaliyofuata
Mnyika aliomba mwongozo, wakati Spika anamwongoza kuna mtu alisema 'Mnyika ni mwizi'

Mnyika akaomba Spika amtake aliyetoa madai hayo ima athibitishea au akanushe. Yalisikika
Spika akaendelea kumwambia Kibajaji aendelee. That was an act of dis-contempt kwa Mnyika

Kumbuka mwanzo alipoomba mwongozo, Spika alitamaka kauli za kumtia Mori kibajaji

Ukichanganya na yaliyotokea, Mnyika kama mwanadamu ana haki ya ku react

Sasa kwanini hakutoka, hili ni katika kupinga 'resistance' ya uonevu aliofanyiwa

Spika hakuona busara kulimaliza suala kwa kufuata kanuni, aliongozwa kwa uchama tu

Kosa ni kamati kuwafungia wabunge wawili , mmoja akimsaidia Mnyika mwingine akizungumza nje

Again, hakukuwa na sababu zozote za kumtoa Mnyika kwa mabavu 'askari changamka'
Tatizo halikuwa mnyika au Kibajaji, bali kukosekana kwa mwongozo

Hii ni trvial matter lakini ikipata hamira inaumuka. Kwa maana hiyo, Spika aligeuka kuwa hamira na kullifanya jambo kuubwa bila sababu za maana kabisa. Ilikuwa busara kidogo tu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Mkuu, busara ilikosekana mwanzo na kuzua yote yaliyofuata
Mnyika aliomba mwongozo, wakati Spika anamwongoza kuna mtu alisema 'Mnyika ni mwizi'

Mnyika akaomba Spika amtake aliyetoa madai hayo ima athibitishea au akanushe. Yalisikika
Spika akaendelea kumwambia Kibajaji aendelee. That was an act of dis-contempt kwa Mnyika

Kumbuka mwanzo alipoomba mwongozo, Spika alitamaka kauli za kumtia Mori kibajaji

Ukichanganya na yaliyotokea, Mnyika kama mwanadamu ana haki ya ku react

Sasa kwanini hakutoka, hili ni katika kupinga 'resistance' ya uonevu aliofanyiwa

Spika hakuona busara kulimaliza suala kwa kufuata kanuni, aliongozwa kwa uchama tu

Kosa ni kamati kuwafungia wabunge wawili , mmoja akimsaidia Mnyika mwingine akizungumza nje

Again, hakukuwa na sababu zozote za kumtoa Mnyika kwa mabavu 'askari changamka'
Tatizo halikuwa mnyika au Kibajaji, bali kukosekana kwa mwongozo

Hii ni trvial matter lakini ikipata hamira inaumuka. Kwa maana hiyo, Spika aligeuka kuwa hamira na kullifanya jambo kuubwa bila sababu za maana kabisa. Ilikuwa busara kidogo tu

Na ukitaka kujua kiini cha tatizo angalia kama pamoja na kina Mnyika kuadhibiwa kwa "utovu wa nidhamu" ikiwa Kibajaji ametakiwa kuthibitisha tuhuma zake juu ya wabunge wa upinzani kuhongwa na Acacia. Immagine kama tuhuma hizi zingetolewa na mbunge wa upinzani kama kina Mh Jenista Mhagama wangekaa kimya...
 
TAARIFA YA PILI YA MADINI

UTHUBUTU SI KUTAJA BALI KUCHUKUA HATUA ZA DHATI NA WAZI

Baada ya kamati ya kwanza kuwasilisha taarifa kulikuwa na majadiliano mitandaoni kuhusu Acacia
Majadiliano yalihusu 'kilichoitwa uzalendo' kwa maana ya kuunga mkono hoja za Serikali dhidi ya Acacia

Baadhi walipinga hoja ya uzalendo, si kwasababu ya kutetea Acacia bali ilivyotumika kirahisi
Uzalendo 'Patriotism' ni uaminifu, utii, kujitoa na uchungu kwa Taifa lolote usio na shaka

Kushawishi watu tu kuunga mkono bila kujibu baadhi ya hoja ni upungufu wa fikra
1. Swali lisilojibiwa, Acacia alifanya kitu gani nje ya mkataba na serikali?
2. Nani aliona mkataba kiasi cha kudhani kulikuwa na matatizo kwa Acacia dhidi ya nchi?
3. Wako wapi wazalendo waliosaini mkatab kutueleza 'uhuni' wa acacia katika mkataba?
4. Kwanini wazalendo wa 'Bungeni' hawajadili hoja za Acacia ikiwa walipitisha sheria?

Majibu ya maswali hayo yalikuwa Rahisi 'wananchi wawe wazalendo' kwavile tu wanatakiwa wawe! Yaani kauli mbiu tu watu wawe wazalendo!

Kamati ya pili ya madini imewasilisha taarifa yake kuhusu sakata hilo hilo.
Kamati imebaini Watanzania kuhusika katika 'kudhulumu' nchi kwa kusaidiana na Acacia

Kamati imebaini dhuluma ipo kwa watu binafsi na taasisi zinazosimamia masilahi ya nchi

Kamati ikabaini mapungufu mengi ya sheria zilizotungwa na Bunge letu lenye Wazalendo

Kamati ikatoa mapendekezo takribani 20 kuimarisha sekta ya madini kwa faida ya umma

Hii ina maana moja kubwa, kwamba waliohoji 'uzalendo' kwa maswali 1-4 hapo juu walikuwa sahihi

Kamati imethibitisha na kujibu hoja zao kwa mantiki

1. Kwamba, Acacia 'hakuvunja' wala hawakuwepo nchi isivyo halali.
Kama wafanyabiasha walitumia fursa na uzembe kupata faida kama mwingine yoyote

2. Kamati imeona mkataba imekuja na maelezo ya mapungufu ya sheria za nchi yetu

3.Kamati imetaja, 'wazalendo' walioshirikiana na Acacia katika mpango mzima

4.Kwamba, wazalendo wa Bungeni walitunga sheria bila kuzingatia masilahi ya nchi

Waliohoji 'uzalendo' sasa ndio wazalendo kuliko waliofuata mkumbo tu bila kuhoji

Wapo wanaodhani kazi ya uzalendo imeisha leo, hapana! kilichotokea ni mwanzo tu wa kutakiwa kuonyesha uzalendo wa kweli. Hili litakuwa na mambo mawili

1. Kuadhibu wahusika kwa dhati bila kuoneana huruma, aibu au kuoneana

2. CCM, serikali yake na Bunge lake kuchukua dhamana ya kuomba umma radhi kwa hasara iliyotokea mbele ya uongozi, usimamizi na macho yao ikitendwa na watu wao

Makundi hayo mawili yanatakiwa kuonyesha uzalendo kwanza, kwa kuomba radhi kwanza kabla ya kuomba umma uzalendo.

Hakuna uzalendo nusu au wa majaribio, ni ima uzalendo kamili au hakuna!

Inaendelea....
 
NI WAKATI WA KUTEKELEZA 'UZALENDO' KWA VITENDO

Bandiko hapo juu tumeeleza makundi mawili yanayopaswa kutekeleza 'uzalendo' kwa vitendo
Ni kwa njia hiyo makundi hayo yatakuwa na uhalali wa kuzungumzia uzalendo na hata kushawishi

Kwanza, baada ya kamati mbili kutoa taarifa ni wakati wa hatua za dhati kuchukuliwa kwa wahusika
Kama tulivyosema, Acacia alipata ushirikiano wa kutosha kutoka kwa wazalendo waliopewa dhamana

Ipo haraka ya kutaka ''kuwashughulikia'' waliohusika kama tunavyosoma baadhi ya maagizo
Haraka hiyo itakuwa na matatizo mbele ya safari na itaondoa kabisa maana nzima inayokusudiwa

Kutoa adhabu ni fundisho kwamba wanaohujumu rasilimali watakumbana na mkono wa sheria sasa ,uzeeni au vitandani mahospitalini wakipigania roho zao

Itakuwa ni kosa kuanza kuzuia watu wasitoke au wasisafiri kwasababu tu wametajwa na kamati

Kamati inaweza kuwa imewataja lakini haimaanishi ni hao tu, bali kama kielelezo cha taarifa zao

Ni makosa kumchukulia hatua karani aliyehamisha faili kutoka bosi A kwenda Bosi B na kuaminisha umma karani ndiye mhusika. Huo utakuwa uonevu

Katika mabandiko haya tuliwahi kuisihi serikali kushughulikia suala la kiongozi anayetuhumiwa kwa mambo kadha. Tulisema kiongozi huyo atakuwa mzigo na ataipa serikali picha mbaya

Ni vema serikali ikatoka na taarifa ya uhakiki wa vyeti, majina na tuhuma zingine ili iwe na fursa

Kwa bahati mbaya ushauri huo haukuzingatiwa na zoezi zima la kutafuta vyeti feki na waajiriwa feki likagubikwa na utata wa kiongozi huyo.

Hata viongozi wanaoshuhulikia wakavunjika moyo kwa kujua ni 'uonevu' kumtimua fulani kazi wakati fulani mwenye tuhuma hizo akiachwa salama

Hapa tuna maana kuwa zoezi la kubaini waliotia taifa hasara lifanywe kwa uangalifu na umakini, wote waliohusika watajwe na kuchukuliwa hatua hadharani bila kificho au kusita sita.

Hilo litajenga heshima ya uzalendo na kuinasua serikali katika mtego kama wa kiongozi yule

Pili, washirika wa Acacia ni Watanzania, walichaguliwa au kuteuliwa na serikali inayotokana na CCM.

Ni chama kinachouza sera ikiwemo ya madini. Hakuna shaka serikali zilizopita zilisimamia sera za CCM

CCM ina dhamana na sakata la Acacia bila kuuma uma maneno

Zaidi ya hapo, CCM ilikuwa na wabunge waliopitisha miswada ya serikali inayojulikana ni mibovu leo Hapa kuna maana kwamba, CCM inabeba dhamana ya Serikali na Bunge lake kwa pamoja

Ni jambo la muhimu CCM kuonyesha uzalendo kwanza.
Uzalendo si kuzungumzia wapinzani wanasema nini, si kuzungumzia Acacia inafanya nini.
Uzalendo wa CCM ni kubeba dhamana waliopewa kuunda serikali na kupitisha sheria kwa Bunge

CCM wanatakiwa kusimama mbele ya umma na kuomba radhi kwa dhati kwa makosa yaliyofanywa na serikali zake na mabunge yake, taasisi zilizoongozwa na watu wake

Hili halikwepeki kwa kusema ni 'mafisadi'. Hapana
Mafisadi walikuwa wanachama wakitetewa na CCM na serikali zake pamoja na Bunge lao.

Kuwakana ni kudanganya umma

CCM iliwahi kuchukua sifa kwa mteuliwa wa kiti cha naibu katibu mkuu wa UN kwa kauli ya kuwa ni mwanachama wao na anawakilisha chama katika ubora wake.

Kauli iliyotolewa na aliyekuwa katibu mkuu wakati huo pale ofisi za Lumumba

Kwa mantiki hiyo hiyo wahujumu ni wanachama wao waliobeba dhama hata kama ni mbaya kwa niaba ya chama chao. Hakuna namna CCM inaweza kushawishi uzalendo bila ya kusimama na kuomba radhi

Hasara ya madini ni mzigo tuliotwishwa na CCM, si wapinzani wala Acacia. Waombe radhi kwanza

Tusemezane
 
Duh!
Mkuu Nguruvi3, mbona kama hukututendea haki wanajukwaa? Au ni mimi tu?

Ni kweli kuwa juu ya Ripoti zote mbili hasa hii ya jana umeona hili tu la porojo za kugombea jina la uzalendo kiasi cha tulifanye kuwa mjadala humu?

Kuna tija yoyote kubwa ya kujua nani anastahili kuitwa Mzalendo kuliko kujua Uhalali ama Ubatili uliomo kwenye ripoti?

Mbona kama tunaingia kwenye mitego ya usiasa?

Ninafikiri tuna nafasi ya kujadili hoja nyingine na kuaacha huu ulimbukeni wa wanasiasa wetu kugombea jina la uzalendo.

Mkuu umetaja hadi issue za vyeti humu, CCM /UPINZANI, ni lini tutajadili haya nje ya vifungo vya siasa uchwara za wanasiasa wetu?

Uhalali wa ripoti upoje?

JE, HATUNA NAFASI YA KUANZA UPYA KATIKA MADINI? Je, huu hauwezi kuwa Mtaji kwetu?
Anaita sasa.
 
"JingalaFalsafa, post: 21595709, member: 81123"]Duh!
Mkuu , mbona kama hukututendea haki wanajukwaa? Au ni mimi tu?

Juu ya Ripoti zote mbili umeona hili tu la porojo za kugombea jina la uzalendo kuwa mjadala humu?
Kuna tija ya kujua nani anastahili kuitwa Mzalendo kuliko kujua Uhalali ama Ubatili uliomo kwenye ripoti?Mbona kama tunaingia kwenye mitego ya usiasa?
Mkuu nimetenda haki kwa kujadili uzalendo. Hii si dhana niliyoanzisha, ipo na inatumika vibaya.

Tulichokifanya ni kuiweka sawa kwa muktadha wake. Pili, kwamba hili si suala la kisiasa si kweli. Wahusika waliotunga sheria mbovu ni wanasiasa. WalioteuA wataalam wa mikataba ni wanasiasa n.k.

Kwanini tumeongelea uzalendo? Kama utakumbuka taarifa ya kwanza iliambatana na kibwagizo cha kuungwa mkono ili watu wawe wazalendo. Waliojaribu kuhoji walionekana 'si wazalendo'

Kamati ya pili imekuja na majibu ya hoja zote tulizosema.
Kwamba, Acacia hawakuiba, hawakuvunja, walikaribishwa na Wazalendo.

Pili, kwamba, sheria zetu zilizotungwa na Bunge la CCM na serikali yake ndizo zimetufikisha hapa.
Hao ni wazalendo wanaotuambia tuunge mkono tu kwa kusikia
Tatu, kamati imetoa mapendekezo ikionyesha udhaifu wetu uliotumiwa vema na Acacia

Hoja ya uzalendo inatumika kufunika madudu ya waliotufikisha hapa.
Ndio maana tunasema, uzalendo si kuunga mkono ni pamoja na kukosoa na kujikosoa.

Waliohusika si watu wachache ni kundi kubwa hivyo linapaswa kutuomba radhi.

Kundi hili ni CCM, Bunge lake na serikali yake.

Hatuwezi kuendelea kuimba uzalendo ili kufuni madudu yaliyofanywa na hao wanaotushawishi

Lakini pia angalia mkutano wa Ikulu. Makundi mbali mbali hadi ya viongozi wa dini na sala yalikaribishwa kwa maombezi n.k. Hii lilifanywa katika ku 'harness' hoja ya uzalendo

Hakuna tatizo kwa yaliyofanyika, muhimu ni kutotumiwa kufunika ukweli wa wahusika

Unaweza kuita hoja ya uzalendo namna unavyoona, cha kuzingatia ni kuwa hoja inaingizwa na tunachokifanya ni kueleza kwanini kuna matumizi mabaya ya hoja na nia yake ni nini
Mkuu umetaja hadi issue za vyeti humu, CCM /UPINZANI, ni lini tutajadili haya nje ya vifungo vya siasa uchwara za wanasiasa wetu?
Nimeyataja hayo nikikotoa hoja muhimu ya 'uonevu'.

Kwamba zoezi la vyeti n.k. limepoteza maana kwasababu tu halikufanywa kwa 'uadilifu'

Nilichotaka kusema walioshirikiana na Acacia wawajibishwe bila kuoneana haya ili zoezi zima lisiingie nyongo kama lile la vyeti

Kuhusu wapinzani, hakuna siri walisimama na madini kwa miaka mingi.

Ndani ya Bunge walidhihakiwa, tukutanwa na kufukuzwa ka jambo linaloonekana dhahiri shahiri leo
Uhalali wa ripoti upoje?
Uhalali wa ripoti hauna shaka.

Katiba inatoa mamlaka kwa wahusika kutunda kamati.
Labda kama unataka kusema uhalali wa 'contents' za kamati. Hilo ni jambo tunaloweza kulijadili. Kumbuka, hakuna uhalali mwingine alio nao mwananchi kwa katiba iliyopo
JE, HATUNA NAFASI YA KUANZA UPYA KATIKA MADINI? Je, huu hauwezi kuwa Mtaji kwetu?
Kuna kitu kinaitwa 'insanity' yaani kufanya jambo lile bila matokeo na kulirudia

Tulikuwa na kamati ya Bomani na mwisho wake unaujua. Hakuna anayejua matokeo ya kamati hiyo
Imekuwepo mijadala bungeni hakuna kinachoonekana ku solve tatizo la madini

Leo kunapendekezwa sheria mpya kurekebisha zilizotufikisha hapa na hasara yote.

Wanaotakiwa kurekebisha sheria hizo ni wale wale ''CCM , serikali yao na Bunge lao la ndiyoo'.
Tusipoangalia namna ya kuziba ufa tutaendelea kujenga kuta kila uchao

Nafasi ya kuanza upya kwa hili la madini si kusahau yaliyopita.
Ni ujinga mzuri sana kama utajikwaa kila mara bila kuangalia kwanini unajikwaa na nini kinakukwaza

Kwa mantiki hiyo pa kuanzia ni kuhakikisha wahusika wawe wazima, wagonjwa au wafu wanajulikana
Kisha adhabu ziwafuate huko waliko , kama ni makaburini kizazi kichape makaburi ishara ya kuwalaani

Baada ya hapo tunahitaji wahusika waombe radhi. Kuomba radhi ni njia ya kiungwana ya kuleta umma mezani ili ujadili hatma ya madini upya.

Hatuwezi kuanza tukiwa na watu wale wale waliotufikisha hapa bila hata ya radhi tukitegemea maajabu. Hiyo ni insanity

Baada ya hapo turudi mezani, tuwaambie CCM , serikali na Bunge kuwa rasilimali ni mali ya wananchi si
Viwanja vya michezo wamepora , rasilimali hapana! Kwamba, mikataba ipitiwe , iwe wazi wananchi washirikishwe kuamua bila mizengwa au miswada ya dharura saa 8 usiku Bungeni
 
UTHUBUTU UMEINGIA GANZI

PROF ATETEA KILICHO WAZI NA KISICHO NA UTETEZI

Bandiko 374 tumeeleza uthubutu wa kukabiliana na uharibifu wa rasilimali za nchi.

Tukasema kutaja majina mawili matatu si uthubutu na hakutaondoa tatizo lililopo.
Kinachotakiwa ni majina ya wahusika bila kuonea au kupendelea hadharani

Tulitoa mfano wa zoezi la vyeti limepoteza maana kwasababu ya kuoneana haya
Wapo wanaosamehewa na sheria ile ile inayohukumu wanyonge kwa kuwatoa kafara

Hili la madini linaanza kuingia ganzi.
Waziri wa katiba akisema viongozi wastaafu wasizungumzwe hawakutajwa katika ripoti.

Prof anaamini waliotajwa katika ripoti ndio wahusika na washirika wa Acacia

Utetezi wa profesa ni hafifu na dhalili.Ripoti haikutaja kila mmoja na uhusika bali majumuisho

Profesa haileweki ni kutojua , kupotosha au alidhamiria kitu gani kwa kauli hilo.

Viongozi wa kitaifa wana dhamana ya Mikataba mikubwa kwa kuridhia kabla ya kuanza

Inashangaza profesa anapoaamini kwa dhati kabisa kuwa kama kuna asiyetajwa huyo hahusiki ili kukinga vifua kwa viongozi waliostaafu.

Hapa ndipo tatizo linapoanza , kwamba, hakuna atakayeshtakiwa!
Wahusika watashtakiwa vipi ikiwa idhini ya mwisho uilitoka kwa mamlaka ya juu?

Watanzani waelewe, woga umeshaingia, iganzi imetitia sasa wanarudi nyuma kwa kasi .

Kuna kuoeneana haya na kinachofuata ni kutafuta watu wachache watolewe kafara la kisiasa ili kulinda wakubwa pengine waliohusika na kashfa nzito za madini

Ndio maana kulikuwa na nguvu ya ziada ya kutangaza uzalendo ili kusahaulisha umma waliotia saini mikataba ni wazalendo , walioingiza taifa hasara ni wazalendo ambao leo baadhi yao wanawekewa kinga za maneno na maprofesa

Itashangaza kama tutafanikiwa. Mwenmdo wa kulindana hausaidii bali ni aina ya ulaghai

Prof anatetea viongozi kwa kusema wametumikia taifa, nchini kwetu viongozi wanastaafu na kuongea na maneno ambayo ukiyaweka katika mantiki utabaini profesa analazimika kusema tu kinachokuja kinywani!

Hivi watu wanawezaje kuingiza nchi nhasara ya trilioni 200 kwa mfano, watu hao wakasemwa wametumikia taifa kwa heshima.

Mikataba mibovu waliiona, walikuwa na uwezo hawakufanya , uadilifu wao upo wapi?

Zoezi zima la madini lieingia doa, linakosa uadilifu na ni vema likamlizwa.

Itashangaza umma kama kutakuwepo atakayeshtakiwa, huo utakuwa 'uoenvu'.

Wote waachwe huru tusitafute wanyonge ili kufunika madudu ya wakubwa

Hatuwezi kuwa na sheria moja ya nchi zikatumiwa tofauti kwa makundi ya jamii.

Tunafeli kila siku kwasababu ya double std, kulindana kwasababu tu ya mwaga mboga nimwage ugali. Wanajuana nani atamfunga paka kengele?

CCM na serikali zake na Bunge wanajuana, hakuna msafi anayeweza kuwarushia mawe wenzake!
 
BUNGE : MUUNGENI MKONO RAIS KWA VITENDO
KUUNGA MKONO KWA MANENO NI KUKWEPA WAJIBU WENU

Kumekuwepo na kauli ndani ya bunge za kutaka kuunga mkono jitihada za Rais kuhusu madini
Ni bunge hilo hilo lilipitisha sheria za dharura mwaka 1997/98 ambazo matokeo yake tunayaona
Ni bunge hilo hilo liliazimia kumtimua Mbunge Zitto mwaka 2007 kwa hoja za madini

Sheria nyingi zinapitishwa katika hali ya kushangaza. Inakuwaje suala lililopo miaka nenda rudi lifanyiwe marekebisho ya sheria kwa hati za dharura?

Lengo la hati za dharura si udharura bali kuzuia mijadala mipana itakayoibua au kutibu 'mipango'
Tunaposikia wabunge wakitoa kauli za kumuunga mkono Rais inashangaza sana na kutia shaka

Bunge halipaswi kutoa kauli za kuunga mkono, bali kuunga mkono hoja kwa vitendo na udhati
Kuunga mkono kwa vitendo ni kuhakikisha wabunge 300 wanaelewa, wanakosoa, wanachuja wanapima na wanakubaliana kuhusu mswada unaofikishwa mbele yao

Kupitia njia hiyo, serikali itakuwa na kioo cha kutazama miswada ambayo huishia kuwa sheria mbovu

Hoja za wabunge zijikite katika kutafuta suluhu. Ili suluhu ipatikane ikiwa na tija kwa umma, wabunge wakubali kuacha uchama pembeni na kuweka masilahi ya nchi kwanza

Hili litasaidia miswada kutopitishwa kwa njia ya 'ndiyoo' kwasababu tu chama tawala kimetaka
Tukitazama nyuma na hasa wabunge wa CCM hakuna namna wanayoweza kusema wanaunga mkono

CCM na Wabunge wake ndilo chimbuko la hasara tunayoona. Leo wanaunga mkono kitu gani ikiwa hawawezi hata kutamka samahani Watanzania kwa hasara tuliyowasababishieni?

Tusemezane
 
CCM MAANADAMANO YA NINI?

Kumekuwepo na habari za kuhamasisha ''maandamano'' kumuunga mkono Rais kwa suala la madini

CCM wanapaswa kutambua rasilimali za nchi si za chama na hakuna mwenye umiliki kwa vikundi
Maandamano yanayosemwa japo hayajatokea ni vema kama mpango upo ukafutwa mapema

Maandamano yataligawa taifa zaidi kwa kuamini CCM wanafanya hivyo kama chama na si suala la taifa

Matatizo yatajitokeza katika kueleza dhana nzima ya maandamano

Kwanza, ni sera za CCM za madini zilizotekelezwa na CCM ambao wengi bado wapo zimetufikisha hapa
Hoja ya awali ni ya CCM katika 'maandamano' walaani CCM waliolitia hasara taifa kwanza

Pili, maandamano ni kwenda kinyume na agizo la serikali la kuzuia mikusanyiko kama inavyotokea siku za karibuni. Makongamano , semina na hata shughuli za dini za nje zimekatazwa kwa 'usalama'

Kama mpango wa maandamano utakuwepo kuna maswali yatajitokeza

1. Polisi wanachagua vipi 'maandamano' yenye amani na yale yanayotishia hali ya usalama?
Kwanini CCM waruhusiwe, 'walemavu' wapambane na dola bila huruma au kusikilizwa?

2. Serikali ilipiga marufuku mikusanyiko ili kutoa nafasi kwa wananchi kufanya kazi
Je, nafasi ya kufanya kazi ni kwa shughuli za wapinzani au za Watanzania kwa ujumla?

Ingawa haijasemwa rasmi, ni muhimu kutambua maandamanotija kwa taifa
Pongezi zinaweza kutolewa kwa njia za vikao vya vyama na kufikishwa zinapostahili

Rasilimali ni mali ya umma, pamoja na ukweli kuwa hasara iliyopo imeletwa na uzembe wa CCM na sera zake za madini, kuendelea kulifanya suala hilo kuwa la kichama ni kuendelea kuligawa Taifa ambalo hadi sasa umoja wake unahojiwa kutokana na makovu ya uchaguzi na kushindwa kuyapona

CCM wasisahaau pia maandamano yataruhusu mijadala ya kitaifa na 'wastaafu' watakuwa kati kati ya mijadala hiyo.

Tujadili rasilimali za nchi kama Taifa hayo ya chama yabaki huko huko katika vyama

Tusemezane
 
SPIKA : ''WANYIMWE PESA ZA MAENDELEO''
KURA BUNGENI NI HAKI, SI UTOVU WA NIDHAMU

TUNALIGAWA TAIFA KWA MAMBO YASIYO NA MSINGI

Kura ndani ya bunge kuhusu bajeti au jambo lolote ni suala la kanuni na taratibu
Wakati wa chama kimoja, bunge lilipitisha bajeti, wabunge walikuwa na fursa ya kukataa

Tunakumbuka wakati wa Nyerere Mbunge wa Mbeya aliwahi kutoa shilingi katika bajeti
Mbunge huyo hakutishwa, hakutukanwa, alisikilizwa ni kwanini alitoa shilingi

Katika vyama vingi duniani hilo ni jambo la kawaida na hutokea kila mahali

Demokrasia ya vyama vingi inaruhusu maoni mbada kwa bajeti mbadala za wapinzani
Maana kubwa ni kuyaangalia masuala ya kitaifa kwa mitazamo na angle tofauti

Mbunge ni mwakalishi wenye dhamana ya kumwadhibu kwa uwakilishi ni wana jimbo

Bajeti ya serikali hutokana na kodi za wananchi bila kujali maeneo au itikadi za vyama

Spika anaposhauri mawaziri wa serikali yenye dhamana kwa waanchi wote wasitoe pesa kwa waliokataa bajeti, ana anawaadhibu wapiga kura na walipa kodi kwa ujumla wao

Spika anakwenda kinyume na kauli ya Mh Rais kuwa 'maendeleo hayana vyama'
Rais alisema uchaguzi umekwisha sasa ni kujenga nchi. Je,Mh Spika imesaidia Rais?

CCM inajinasibu ni chama cha wanyonge na watu wa hali ya chini.
Spika anaposhauri wanyimwe haki za kodi zao anasaidiaje kauli mbiu ya CCM?

Spika anaweza kutumia Bunge kuwaadhibu wabunge,hana haki ya kutumia chombo hicho kupendekeza 'adhabu kwa wananchi' ambao wengine hawajui hata kinachoendelea

Wengi wakiishi kwa dola moja,wakijifungulia watoto juu ya matenga ya basikeli wakililia roho kwa kukosa dawa n.k.. Hawa wanahitaji msaada si'adhabu' anayopendekeza

Wabunge wanasimama bungeni kwa alama ya Taifa bila kuj

Kauli ya Spika imetisha na imesikitisha na kuzua maswali kama Taifa tunaelekea wapi!

Ni kauli inayojenga chuki kati ya wananchi na serikali yao

Eneo litakaloachwa nyuma kwa sababu zozote litahisi mgawanyo wa keki ya taifa si kwa kutumia busara hekma na maarifa bai adhabu ya viongozi wa vyama na hapa CCM

Mh Spika, endapo itahitajika kura ya jambo linalohitaji kukabiliwa na Taifa kama adui wa ndani au nje, kwa kauli zako unawezaje kuwaweka wabunge wakawa kitu kimoja?

Tunamshauri sana Mh Spika arudi bungeni afute kauli yake na aombe radhi.

Kauli yake si inaligawa Taifa, inakiuka haki za kidemokrasia, inachonganisha serikali, inawanyima wananchi haki, inawadhalilisha na ni hatari kwa mustakabli wa Taifa.

Hatuwezi kujenga Taifa tukiwa vipande vipande, tutajenga Taifa tukiwa wamoja.

Tusemezane
 
Back
Top Bottom