Unajua nimehuzunika sana,mpaka nikawa nawaza huyu mtu nimjibu au nisimjibu ?
Naomba unijibu maswali yafuatayo.
1. Hivi unaweza kunithibitishia kuhusu uhalisia wa hii nadharia ?
2. Tungamo ya Dunia na Jua unaipimaje ? Yaani ili kujua uzito wa kitu unatakiwa uwe na nini ?
3. Umbali wa jua na dunia unaupataje ? Yaani ili uujue wewe umbali kutoka Ubungo mpaka Kariakoo huwa unazingatia votu gani ? Hapa nimekufafanulia tu ili ujibu swali vizuri.
4. Huyo Mwanasayansi alijuaje kama kuna nguvu ya mvutano kati ya vitu viwili hivyo na alitumia kifaa gani kujua hilo ?
5. Katikati ya jua alifikaje na kujua kwamba hapo ndipo katikati ya Jua ?
6. Katikati ya jua ni wapi na katikati ya dunia ni wapi ? Je ili kujua katikati ya viwili ni sharti uwe katika viwili hivyo au unakadiria ? Kama unakadiria ni Ukweli wa nadharia hiyo ?
Ukijibu maswali hayo,nitakuuliza mengine.
Naendelea .....
Angalia list ya Wanasayansi wa kiislamu walioijua Qur'an kuliko wewe:-
(1) Avicenna (Abusina)----980 AD---1037
(2) Ibn al Hytham -965AD-1040.
(3) Al kindi -- ---873 AD.
(4) Al zahrawi- 936 AD --1013.
(5) Ibn al Baitar 1197-1248
(6) Abdus salaam 1926---1996
(7) Ibn Battula 1304-1317
(8) Toby Huff
(9) Ibn Sahl 940AD--1000
(10) Perez Hoodboy
(11) Maslama al Majrit 950AD-1007
(12) Abu dahl al Quln 940 AD- 1000
(13) Sl Farabi 872AD--980
(14) Hanayn Ibn Ishaq 809AD--873 AD
(15) Ismail al Jazar 1136--1206.
List ni ndefu sana, na kila mmoja alitoa mchango wake katika nyanja mbalimbali za sayansi, na walikuwa wanaijua Qur'an, sasa unakuja hapa kunajisi Elimu ya kweli ya sayansi.
Vyombo vinaonyesha dunia inajizungusha kwenye mhimili wake na inalizunguka jua, mwezi na dunia siku zote vimeambatana , giza na nuru ni matukio yanayotokea duniani, sasa kama mwezi unazunguka jua utakataaje kwamba dunia haizunguki.
Kitabu adhimu tulichokiteremsha kwako, chenye baraka ili wapate kuzitafakari aya zake, na wenye akili washike nasaha. (38:29).