Registered_jf
JF-Expert Member
- Nov 27, 2024
- 939
- 1,491
Kwanini iwe abstract thinkingHujaelewa neno kidhahania, abstract.
Kufikiri nje ya box la kilichopo na kuweka dunia ambayo ingewezekana kuwapo.
Kwamba, dunia ingekuwa unapata nafasi ya kuchagua uzaliwe au usizaliwe, kabla ya kuzaliwa, mtoa mada asingechagua kuzaliwa.
Sasa mbona unalazimisha kufikiri ndani ya box la dunia iliyopo wakati ushaambiwa kuwa hii ni hoja ya kidhahania, abstract, ya kuangalia dunia ambayo ingewezekana kuwapo ambayo ni tofauti na hii?
Huelewi abstract thinking ni nini?
Dunia ni sehemu ya majaribu na mabadiliko, ambapo kila mmoja anapata nafasi ya kufanya maamuzi mwenyewe. Mungu alituumba na akatupa akili na uwezo wa kujitambua, we are meant to use these tools to navigate challenges.Kwanini Mungu aruhusu mbaya yatokee kwenye Dunia yake?
Yeye si mwenye uwezo wote na nguvu zote?
Kwanini akubali na aruhusu ushenzi utokee kwenye himaya yake?
Au Hana uwezo wote? Au
Hana Upendo na Nguvu zote kuzuia mabaya?
Duniani tunaishi Kwa kutegemeana sisi Kwa sisi, Kwa ufupi tunaishi Kwa kutegemea msaada wa mazingira.
Hakuna Mungu kwamba Yuko sehemu Fulani analinda Dunia na vitu vilivyomo.
Ukiwa mgonjwa, ukakosa matibabu ya madaktari au wataalamu wa afya, kinga zako zikawa dhaifu kupambana na ugomjwa wako, utakufa, Mungu hawezi kuja kukusaidia hata kukusogezea glasi ya maji.
Mungu hawezi kuhusika na maovu, ni binadamu ndo wanatumiwa vibaya kwa misingi ya itikadi.Amri za Mungu? Ni zipi hizo mkuu?
Mungu hawezi kunifanya chochote mkuu, Mungu siyo kitu halisi.
Anayeweza kunifyekelea mbali ni watu kama nyie wenye itikadi Kali za kidini.
Unamuua binadamu mwenzio huku unasema Mungu ndiyo kasema.
Ujinga mtupu
Yote yanatokea kwa sababu ya uhuru tuliopewa binadamu, huelewi nini?Mungu hajaachilia uovu, na Mungu hawezi kuzuia uovu.
Umesema Dunia ni Mali ya Mungu, ndiyo nikakuuliza kama Dunia ni Mali yake, kwanini aruhusu vita na majanga ya Asili yatokee kwenye himaya yake wakati yeye ni mwenye Upendo wote na nguvu zote?
Kwanini iwe abstract thinking
Kama ingekiwa HIVYO tufanye pia abstract thinking nani angekuwa anatoa option hizo au mikataba hiyo
Kifupi ni Imani AMBAYO unaikataa Imani inakufikirisha KITU mabacho jakipo Kwenye uhalisia kiwepo Kwa ImaniAbstract thinking inasaidia kuelewa matatizo vizuri. Inasaidia kuona kwa akili kisichoonekana kwa macho. Inasaidia kujua kitakachokuja kabla hakijafika.
Nitajie mifano ya option ambazo zipo BILA uwepo WA naniKwani haiwezekani options za kuchagua ziwepo bika kuwepo huyo nani?
Tunapompenda Mungu, tunafanya hivyo kwa sababu ya mapenzi yake kwetu na kwa ajili ya manufaa yetu wenyewe, sio kwa sababu ya kumtimizia ukamilifu wake.Mungu yeye si amekamilika? Anataka tumpende Ili apate faida Gani?
Au Mungu hajakamilika Kuna baadhi ya vitu anavitaka kutoka kwetu Ili akamilike?
Kumbe Mungu anatuhitaji Sana kuliko sisi tunavyomuhitaji
Nitajie mifano ya option ambazo zipo BILA uwepo WA nani
Binadamu tumepewa uhuru na nani? Uhuru wa Nini?Yote yanatokea kwa sababu ya uhuru tuliopewa binadamu, huelewi nini?
Hapa ninakubaliana na wewe. Mfano mzuri ni uvumbuzi wa ndege. Kabla ya Wright Brothers kugundua ndege, hakukuwa na mfano wa kitu kinachoruka kama ndege.Bado uko palepale.
Hili wazo la msingi katika swali lako pia ni kushindwa kufanya abstract thinking.
Umewaza ndani ya box la dunia ambayo kila kitu ni lazima kiwe na mfano uliokitangulia.
Ukiletewa kitu kipya ambacho hakina mfano uliokitangulia unakihoji kama hakiwezekani, kwa sababu hakina mfano.
Wakati hata hivyo vitu vyenye mifano navyo kuna wakati vilianza bila ya kuwa na mfano.
Kifalsafa hili tatizo linaitwa "the problem of induction" kaitafute uisome vizuri hii dhana.
Yani nikikwambia kuwa inawezekana kuna wakati jua lisiweze kuchomoza duniani, utabisha, kwa sababu katika uzoefu wote wa watu hakuna siku ambayo jua halijachomoza.
Bila kuelewa kuwa kuna vitu vipya huwa vinatokea bila ya kuwa na precedent wala mfano huko nyuma.
Bado unazunguka katika tatizo la failure in abstract thinking.
Uhuru tumepewa na Mungu.Binadamu tumepewa uhuru na nani? Uhuru wa Nini?
Sasa mkuu mimi kama binadamu sijakamilika, Kuna vitu nahitaji Ili nikamilike, ndiyo kama mfano uliyotoa hapo, Upendo n.kTunapompenda Mungu, tunafanya hivyo kwa sababu ya mapenzi yake kwetu na kwa ajili ya manufaa yetu wenyewe, sio kwa sababu ya kumtimizia ukamilifu wake.
Wewe kama ni mzazi bila shaka utakuwa unapenda kuwa na uhusiano mzuri na mtoto/watoto wako. Je nini faida ya kuwa na hayo mahusiano mazuri na nini hasara yake?
Seriously mkuu 🤣Uhuru tumepewa na Mungu.
Uhuru wa kufanya maamuzi na kuchagua bila shinikizo au kudhibitiwa na mwingine.
Fikiria mfalme mkubwa anayeishi kwenye falme yake. Mfalme huyu ni tajiri, ana kila kitu anachohitaji, na ni mwenye nguvu duniani, lakini, anafurahi sana pale ambapo wageni au watu kutoka kwenye taifa lake wanapokuja kwa heshima, kwa kujitolea, na kwa upendo wa dhati kumtembelea.Sasa mkuu mimi kama binadamu sijakamilika, Kuna vitu nahitaji Ili nikamilike, ndiyo kama mfano uliyotoa hapo, Upendo n.k
Sasa MUNGU mwenye nguvu zote na uwezo wote anahitaji Upendo wa KAZI Gani? Tusipompemda au tusipokuwa Upande wake anapungukiwa na Nini?
Uhuru wa kweli uko katika kuchagua upande wa Mungu kwa hiari, si kwa kulazimishwa. Mungu anataka watu waende kwake kwa mapenzi yao, si kwa vitisho.Seriously mkuu 🤣
Mimi sijapewa uhuru na Mungu bwana.
Ametoa vitisho kibao kwamba tusipokuwa Upande wake atatucjima moto kwenye Jehanam ya milele.
Sasa hapo Kuna uhuru Gani 🤣
Yeye angesema tu jamani wanaotaka kuwa upande wangu waje, na wale wanaotaka kwenda upande wa pili waende wakaishi maisha Yao.
Kwa Ufupi, Mungu anawahitaji wanadamu zaidi kuliko wanadamu wanavyomuhitajiFikiria mfalme mkubwa anayeishi kwenye falme yake. Mfalme huyu ni tajiri, ana kila kitu anachohitaji, na ni mwenye nguvu duniani, lakini, anafurahi sana pale ambapo wageni au watu kutoka kwenye taifa lake wanapokuja kwa heshima, kwa kujitolea, na kwa upendo wa dhati kumtembelea.
Mfalme huyu hawezi kupungukiwa na chochote, lakini anapohisi upendo kutoka kwa watu wake, anajivunia na anakuwa na furaha sana. Upendo huo ni ishara ya shukrani na uaminifu, na huimarisha uhusiano kati yake na watu wake.
Vivyo hivyo kwa Mungu, ingawa yeye ni kamili na hahitaji chochote kutoka kwetu, anapenda kuona upendo wetu, heshima yetu, na kujitolea kwetu kwake.
Hii inasimama kama ishara ya uhusiano wetu wa karibu na kumtambua kama mfalme wetu wa kweli. Mungu hapungukiwi na chochote lakini upendo wetu kwake huleta furaha na maana zaidi kwetu sisi tunapojiweka karibu naye mda wote.
HAPANA.Kwa Ufupi, Mungu anawahitaji wanadamu zaidi kuliko wanadamu wanavyomuhitaji
Jehanam unakubali kwamba ni eneo halisi lipo?Uhuru wa kweli uko katika kuchagua upande wa Mungu kwa hiari, si kwa kulazimishwa. Mungu anataka watu waende kwake kwa mapenzi yao, si kwa vitisho.
Hivyo, uhuru upo kwa mtu mwenyewe kuchagua, labda uniambie ni wapi Mungu ametoa vitisho , na kulazimisha watu kuwa upande wale?
Na unadhani kama angehitaji kulazimisha watu kuwa upande wake angeshindwa?
Unaelewa nini kuhusu uhuru wa kuchagua?