Dully Sykes-DHAHABU /Joselini v/s mr blue

Hatari sana aisee.. ngoma kali halafu wasanii ni Blue+Joslin na Dully moto sana hawa watu kipindi hicho.
Sjui Joslin yuko wapi.. huyu jamaa alikuwa na maneno flani ya swaga vijana wengi tuliyatumia kutongozea madem kitaa.. ngoma yake ya Pafyum hatar sana.
Huyo Blue sasa mpaka kesho ntazid kumuelewa... kosa tu apewe hata sekunde 30 kwenye songi anaua balaa.
 
Hatari sana aisee.. ngoma kali halafu wasanii ni Blue+Joslin na Dully moto sana hawa watu kipindi hicho.
Sjui Joslin yuko wapi.. huyu jamaa alikuwa na maneno flani ya swaga vijana wengi tuliyatumia kutongozea madem kitaa.. ngoma yake ya Pafyum hatar sana.
Huyo Blue sasa mpaka kesho ntazid kumuelewa... kosa tu apewe hata sekunde 30 kwenye songi anaua balaa.
Wadau wa JF wanasema Joslin anakaanga kiepe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kweli Ila sio kwa hii mkuu, mana ilikuwa kama nyimbo ya taifa vile yani.
Hapa nikikutajia nyimbo kama.
Wajua Kiba na Queen darlin
Distance ya Jadee
Latifa, Inamaana, waja za Mb doggy
Una Prof Jay
Ndugu zangu Afande sele
Zawadi Keisha
Agoust 13, mwanza mwanza za Fid
Zali la mental
N.k
Ukisema huzijui hizi nitakushangaa kidogo mkuu hapo itabidi tu nikuulize umri wako mkuu.
Mwaka huo nilikuwa Form one Morogoro secondary
 
U-lonely tena bye, mi nafurahi
Niko stimu za mjani, kichwani niko high
Namuona manzi maskani, yuko so fly
Mi nawahi, najigeuza Dully namfuata nampa hi
Nimeshaini kama Mully, kadata mtoto hakatai
(Heheh heheh)
Anang'aa kama gold (yeah, yeah)
Yeah, yeah, yeo-yeoh yeoh, yeo-yeoh
Anaita kama bling thing
Kama dhahabu, amefika kwa king
Queen wa Kheri Rajabu
Anakila sababu, asipate tabu
Nimezimika ajabu (sana tu)
Heheh
Yeoh, hapendi pesa, hapendi show
Ye anampenda Blue
Washamteta hasemi no
Ye anaona fool
Ndo mama Kabyser ajulikana mpaka kwetu
Steve unataka kumjua?
Master J twenzetu
Blue aliitambalizia hii verse kizazi sana
 
Kabla ya huu wimbo kulikua na hali ya 'bifu' ( sikuthibitisha) kati ya Mr Blue na Joseline, ikumbukwe Jose kamkuta Byser kwenye 'industry' lakini wakati Jose anaingia kwenye 'game' ni kama Blue alikuwa anapotea kwenye ramani.

Joseline akaachia mikwaju hatari kama Perfume, Mshkaji mmoja, etc... Later on Mr Blue akaja na NIPO feat Q Chilla bonge moja la wimbo huu. Sasa humu kwenye Nipo Blue ni kama alikuwa anafloo vile Jose anafanya. Kurap kwa Swags! Nafikiri tatizo likaanzia hapo.

Na ikumbukwe pia Mr Blue na Dully walikua washkaji sana wakati ule, marafiki walioshibana sana tu. Inasadikika Dully alipanga kuprove wrong watu kuwa Jose na Blue ni watu wawili tofauti kabisaa kwenye uandishi hata floo.

Japo nasikia wazo la hiyo 'Collaboration' Blue aliambiwa mapema tu hivyo alijiandaa vizuri tofauti na Joseline. Btw! Jose aliitendea haki nafasi yake kwa floo ambayo ilimtambulisha yenyw unyamwezi mwingi.

Blue nafikiri kwasababu ya kutaka kujitofautisha zaidi na Jose ikabidi azidishe swags sana kwenyw dhahabu ili ionekane kila mtu anapita njia yake. Kadri miaka ilivyokwenda ndio Rap Style ya Blue ilikua inabadilika hadi huyu wa sasa katika Pombe na Muziki.

Nimejaribu kurudisha kumbukumbu nyuma, moyo u radhi kurekebishwa.
 
Wote walikaza sana, ila dully kiboko japo alipambana na vijana wenye mitindo mipya ya kurap ila aliwakilisha vema. Hii collaboration inanikumbusha wimbo unaitwa NILIKATAA kutoka top band, TID, QChief ft Byser
Kabla ya kwenda kuingiza vocal Blue anakuambia alifanya mazoezi week nzima kama unavyojua zamani walikua wanazinatia sana...... Siku ya kurecord sasa pale MJ Rec Blue anaingia booth anapia averse yake, ile anamaliza tu watu wote waliokuwepo pale studio walisimama kupiga makofi
 
Mara ya kwanza nilikutana naye kitaani
Nikampa hi huku akinishika shavuni
I'm a Josline a.k.a mpendwa na watu
Kwasababu mi na-flow style zaidi ya tatu
Yeah kashtuka kanifagilia
Hakuamini kama "Perfume" niliwaimbia
Mshkaji mmoja hivi ndo uliofuatia
Mara akatikisa kichwa kifuani akaegemia
Ghafla akaanza kulia
Huku akinishika kwa hisia
Wasiwasi ukanijia, kumuona demu anan'lilia
Anadai anazimika navyo-flow
Namgusa mpaka mwisho, yaani namweka full, yeah
Hisia zangu kwenye muziki zinachoma
Ndo sababu kubwa iliyomfanya anipende sana
Mtoto mzuri ukimwona utampa heshima
Mi namuita dhahabu ndani ya kariakoo nzima
Woyiiioooooo piga kelele kwa joslin ake weweeee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Saana yani, hii ngoma ilikuwa kali Sana kwenye biti hapo Master J ameitendea haki kabisaa.
Kulikuwa na biti kali nazikumbuka kama ile ya
Nikusaidieje ya Prof Jay
Starehe
Kuna ile bembeleza ya Marlow
Ingewezekana ya Squeeze na Ray c
Balozi kwenye chati
Understanding ya banana na Jaydee
N.k
Biti la ngoma ya Ngwea A.K.A MIMI ni noma
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom