Familia ya Zorro miongoni mwa familia zilizotunyima kolabo kali

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,011
9,878
FAMILIA YA ZORRO MIONGONI MWA FAMILIA ZILIZOTUNYIMA KOLABO KALI.

Sikumbuki ni nani alikuja na wazo la kutengeneza albamu iliyoitwa BABA NA MWANA! Ilikuwa ya moto sana na ilikuwa na ladha TOFAUTI.

Nakumbuka Francis Nguza na Nguza Viking almaarufu Papii Kocha na Babu Seya waliurudia wimbo wa SEYA (Wengi HAWAJUI kuwa ni remix) na naweza kukiri kuwa SEYA NDIYO REMIX BORA KWA VIWANGO VYA DUNIA NZIMA.

Humo ndani kulikuwa na ngoma ya upendo wa familia ambayo walifanya Dully Sykes na baba yake, Abby Sykes. Dully aliimba kwa KIREFU huku mzee akimalizia vionjo mwisho wa wimbo.

Mzee Hamza Kalala na mwanaye, Kalala Junior walifanya remix ya NIMEKUSAMEHE na ikatoka ikiwa poa kama ilivyokuwa ngoma halisi.
Sasa nikirudi kwenye familia niliyojisikia kuiandikia, nina maumivu makubwa KUANDIKA haya.

Mzee Zahir Zorro ambaye alifanya Muziki wa dansi zama hizo, ama wengine huuita Muziki wa ZILIPENDWA, japo jina hili hupigwa vita na "wenye Muziki wao" ameshiriki kwa ukamilifu mkubwa kwenye ngoma za wasanii wa kizazi kipya Kama ifuatavyo;

1. RIPOTI ZA MITAANI - FID Q
2. SAFARI - WITNESS FT CP
3. WE MAKE IT ALRIGHT - ZIZZOU ARTISTS
4. FANYA MAMBO YAKO - BABY BOY
5. NYUMBANI - KIGOMA ALL STAR

Namkumbuka Banana yule niliyemsikia akiimba nyimbo za Westlife, nakumbuka Banana yule aliyefanya game ya RnB Bongo na mwanaye, Masiga, wakajiita B LOVE M na wakatambulika zaidi kwa ngoma yao ya moto iliyoitwa ANAKUDANGANYA.

Kundi likafa, Masiga akapotea japo nikaja kuambiwa kuwa ndiye mmiliki wa studio iitwayo KAZI KWANZA ambayo imepaishwa Sana na beats za MAXMIZER.

Banana akawaka na album yake Kali ya RnB na ngoma kali za mapenzi kama; WASIWASI, MAPENZI GANI, NINGEPENDA na SOGEA ambao ni wimbo wangu pendwa mpaka sasa.

Lakini kuna mtu asiyeikumbuka ile MAMA YANGU? Kuna aliyesahau ile vesi ya D Knob mle ndani?

Banana akaenda mbali zaidi na kuibuka na bendi yake aliyoiita B BAND na humo ndani kuna wakali wa masauti kama; Nuruelly, Ismail na baba yake mzazi mwenyewe, Zahir.

Banana amepamba VIITIKIO vya rappers/ MCs kibao Bongo, hii itaandikwa kwenye andiko lingine. Kuna ambaye ana mashaka na uwezo wa Banana? Mtu mmoja hivi ambaye SIJAWAHI KUSIKIA SKENDO YAKE HATA MOJA!!!
Oh Maundaaaa!! Nilimpenda kwenye ngoma zake mbili MAPENZI NI YA WAWILI na NIWE WAKO. Ngoma kali za hisia na sauti nyororo. Gone too soon! Hatunaye Tena na hatarudi.

Vuta picha ingefanyika hata albamu moja ya Zahir, Banana na Maunda, hebu niambie "huo muziki wa muziki huu"

Familia pekee iliyojitahidi kufanya collabos ni familia ya MZEE HAULE ambayo ina vichwa kama;

1 Mr. Teacher
2. Professor Jay
3. Tuff B
4. Black Rhyno
5. Simple X
6. Don Kolihombi.
Prof ameshirikiana na ndugu zake kwenye ngoma kama;
Nawakilisha
Hakuna noma
Piga makofi
Una
Na ngoma ya pamoja waliyoifanya juzi kati hapo inaitwa KAZA!!!

Familia ya MZEE Maxmillian Bushoke pia ambayo ina Max aliyeishi sana Sauzi, Ruta Bushoke na Ramso Bushoke wametudhulumu pia Kolabo maana Ruta na kaka yake walifanya ngoma moja tu Kali iliyoitwa WANASHINDWA LALA.
Lady Jay Dee na mdogo wake, DABO MTANZANIA wamefanya Kolabo moja tu kubwa baada ya miaka mingi kwenye game.

HARDMAD na dada yake, Fatmah (Cute Fettie) walifanya TAMARA peke yake.
Atuganile Bukuku "Enikah" na kaka yake, producer Roy Bukuku walifanya ngoma chache pia.

Nemo na binamu yake, Man Walter bado hawakufanya Kolabo nyingi kama ilivyotakiwa, sambamba na Messen Selekta na binamu yake, Pam D(Daffa)
Babuu wa kitaa hana ngoma yoyote na wadogo zake, Country Boy na Young Lunya.

DATAZ na kaka yake, SQUEEZER NDIYO FAMILIA PEKEE ILIYOTUBARIKI NA MANGOMA YA KUTOSHA.

Kwa wana HIP HOP, vichwa vilivyotubariki na kazi za kutosha ni MAPACHA, MAUJANJA SAPLAYAZ, wakati vichwa vilivyotunyima Kolabo ni vingi ikiwemo ADILI NA MAGAZIJUTO, ambao nao wametoa kolabo chache sana ikiwemo PEKE YANGU REMIX.

Ni familia gani nyingine unaidai Kolabo Kali?
Je miongoni mwa nilizozitaja, ni familia gani unaidai Kolabo zaidi ya nyingine?
LUAH.
MWANDISHI WA AINA YAKE.

331579646_890113048864487_8640053042980089545_n.jpg


330400280_5873058382810269_8694550965166425458_n.jpg

331415064_1670279020055650_2273219503749788074_n.jpg

331428094_572423074609649_255111798771229354_n.jpg
 
Papii Kocha na Nguza Viking bado nawadai,

Banana Zorro na Zahir Zorro bado wana nafasi nyingine,

Hardmad na Fatma bado wanaweza wakatupa kitu kikubwa zaidi ya Tamala,

Hanstone na Banza Stone walitunyima Kolabo au labda Hans alikua bado mdogo sijui umri wake,

Squeezer namkubali sana hasa ile ngoma yake ya NAJA, kile kisauti cha Nature kwenye chorus na ile michano ya mzee mzima na lile lisauti lake zito, dah arudi akiwashe tena, mziki umepwaya.
 
Hv kwenye lile kundi la b band ukiachilia kutoa album moja, wasanii mmoja mmoja hawakuwahi kutoa single kama solo artist?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom