Dulla Mabala ni msanii wa singeli kutokea nchini Tanzania ambaye alijizolea umaarufu kupitia wimbo wake wa makabalia uliopelekea kuwa sehemu ya jina lake.
Madai
Katika baadhi ya mitandao ya kijamii kimeibuka kipande cha video kinachouonesha msanii wa singeli Dullah Makabila akitumbuiza kwenye moja ya mikutano ya hadhara, huku miongoni mwa mashairi yake yakiwa yamebeba maneno yenye ukakasi.
Mathalani mtumiaji mmoja alichapisha kipande hiko cha video katika
mtandao wa youtube kisha akaambatanisha na ujumbe kuwa
“Dulla Makabila ni msanii wa ajabu sana”
Uhalisia wa madai hayo
JamiiCheck imefuatilia kipande hicho cha video na kujiridhisha kuwa kimehaririwa.
Ufuatiliaji kwa kutumia utafutaji wa marejeleo ya picha kupitia google reverse search umebaini kuwa video halisi ilichapishwa Aprili 05, 2025 na Dj Erick kupitia
mtandao wake wa TikTok huku ikiwa na sauti halisi inayosikika;
“Bora nikae bachela nitaoa hata mwakani
Dullah mke wa koa nahisi nimekosa
Nchimbi kanishauri nioe Mnyakyusa
Mnyakyusa mwenzenu simtaki mbinafsi
Anapenda kujitenga kama nyama za mishikaki”
Aidha ufuatiliaji zaidi umebaini kuwa sauti inayosikika kuwa ni ya mashairi yenye ukakasi iliimbwa katika eneo tofauti na siku tofauti hivyo haikiwa katika mkutano huo. Vile vile unaweza kuzingatia mjongeo wa video ulikuwa tofauti na sauti iliyokuwa inasikika na hivyo kudhihirisha kuwa video inayoonekana haihusiani na sauti inayosikika.
Video halisi ilikuwa ni ya tukio la April 03, 2025 wakati Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi
alipofanya mkutano wa hadhara Namtumbo, Mkoani ruvuma