Duh! Wali Maharagwe umepanda bei, umefikia 1,500/=

Duh! Wali Maharagwe umepanda bei, umefikia 1,500/=

Leo mchana nimejongea kwa mama ntilie kupata wali maharage baada ya kumaliza kula nikampa buku, cha kushangaza akaniambia bado jero wali maharage ni buku jero.

Hii imenishangaza sana kwani nimezoea wali maharage ni buku buku. Wazee nimepigwa au ndo bei halisi kwa sasa wali maharage shilingi 1,500/=, huko kwenu ni shilingi ngapi wali maharage?
Mchele grade ya chini 1800 kwa kilo,super 2700
 
Duuh! Ndo yamefikia uko mbona huku wali maharagwe.Mchuzi wa nyama na mboga za majani tunaufinya kwa buku tu mkuu japo sijajua kama bei imepanda ntaenda kuuliza.
 
Buku jero kununua sahani moja ya wali maharage ni kuhujumu uchumi,matumizi ya siku yanatakiwa yawe hivi,asubuhi miogo ya 200 na chai ya 200tsh maji ya kunywa unagongea hapo hapo uliponunua chai imetoka hiyo,ikifika saa 9 unakula matunda ya buku sahani moja mchanganyiko wa tikiti maji tumbo linajaa kinoma huyo mdogo mdogo hadi ghetto,Asubuhi unaamkia na makande ya 500tsh
 
Chips dume bei ile ile, ni mwendo wa kugonga mihogo na chachandu ya brashi
 
Hii si ndo tangu kitambo bingwa? Chapati 4, chai nyeusi tii, cola baridiii, asubuhi imeisha! Kama usiku hesabu ilikuwa njema, supu chapati, cola baridiiii itahusika😄😄

Maisha ndo hivyo yani, ugumu wa nini sasa!
kwa jero ?hapo buku 3-5 inahusika
nilikua nakula kwa maza muuza kipindi flani basi namwambia we jaza mpunga nazi na mboga mboga tu maharage,spinach,mchicha plate likija rundo nikiongeza kuku robo tu yaani nakula mpaka naomba poo.
buku 5 tu nyingi.
 
Mpaka hii vita ya Ukraine iishe maji tutakuwa tunayaita 'mma'
 
Yaan bakery mkate wa 1200 saiv ni 1300 sambusa ya 500 ni 600 andazi la 300 saiv n 400 sasa chapati ya 500 utatamani ulie 😀😀😀
pale jk terminal 3 sambusa ilikua 1500 moja 4 years ago kwasasa itakua buku 3.2
 
Yuko sahihi sababu mafuta ya kula yamepanda bei, Akikuuzia kwa Buku anapata hasara.
 
Vitu vimepanda bei....Supu ya utumbo now ni buku jero,chapati 400/=
 
Yaan bakery mkate wa 1200 saiv ni 1300 sambusa ya 500 ni 600 andazi la 300 saiv n 400 sasa chapati ya 500 utatamani ulie 😀😀😀

Chapati inakuwa na wembamba kama Gazeti
 
Leo mchana nimejongea kwa mama ntilie kupata wali maharage baada ya kumaliza kula nikampa buku, cha kushangaza akaniambia bado jero wali maharage ni buku jero.

Hii imenishangaza sana kwani nimezoea wali maharage ni buku buku. Wazee nimepigwa au ndo bei halisi kwa sasa wali maharage shilingi 1,500/=, huko kwenu ni shilingi ngapi wali maharage?
Mkuu kipimo kimeongezeka kidogo au ni kile kile cha buku???
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom