DSTV yalamba hasara ya bilioni 122, gharama za vifurushi zawakimbizia wateja 486,000

Replica

JF-Expert Member
Aug 28, 2017
1,447
7,822
Kampuni ya Multichoice inayomiliki visimbuzi maarufu vya DSTV imelamba hasara ya Tshs bilioni 122 kwa miezi sita iliyoishia Septemba mwaka jana sababu kuu ikiwa kupungua kwa wateja wake huku Afrika kusini pekee ikipoteza wateja zaidi ya laki nne.

Multichoice imedai kutekeleza malengo yake yote iliyoyapanga lakini mazingira inayofanyia kazi yametawaliwa na kukatika katika kwa umeme, presha kwenye gharama za kuishi na kushuka kwa thamani ya pesa katika nchi walizopo dhidi ya dola.

Mwaka huu channel maarufu ya michezo ya supersport itashindwa kuonesha michuano ya Afcon inayotarajiwa kuanza January 13 nchini Ivory Coast. Mwezi uliopita shirikisho la mpira wa miguu Afrika liliingia mkataba wa haki za matangazo kwa miaka miwili na kampuni kutoka nchini Togo ya New World TV iliyoanzishwa mwaka 2015.

Ni mwanzo wa mwisho wa utawala wa DSTV kusini mwa Afrika? Bado Multichoice ni moja ya nguli wa kurusha matangazo barani Afrika huku kampuni zake mbili za DSTV na GoTV zikiwa na visimbusi milioni 23 vilivyo hai kwenye nchi 50 barani Afrika.
 
Hata Cha kwangu, since last year February sijalipia, naona wananizingua tu,
Natafuta kile kifaa Cha kuweka filamu Cha GB 2000, nikiweka filamu zangu zikijaa natumia kuangalia hata miezi mitatu.

Sio mbaya kila miezi mitatu nikitoa elfu ishirini kuweka move mpya Library.
 
Hebu dadavua hapo kgd mkuu, maana namm ni mpanze wa movies....
 
Kampuni ya Multichoice inayomiliki visimbuzi maarufu vya DSTV imelamba hasara ya Tshs bilioni 122 kwa miezi sita iliyoishia Septemba mwaka jana sababu kuu ikiwa kupungua kwa wateja wake huku Afrika kusini pekee ikipoteza wateja zaidi ya laki nne.

Multichoice imedai kutekeleza malengo yake yote iliyoyapanga lakini mazingira inayofanyia kazi yametawaliwa na kukatika katika kwa umeme, presha kwenye gharama za kuishi na kushuka kwa thamani ya pesa katika nchi walizopo dhidi ya dola.

Mwaka huu channel maarufu ya michezo ya supersport itashindwa kuonesha michuano ya Afcon inayotarajiwa kuanza January 13 nchini Ivory Coast. Mwezi uliopita shirikisho la mpira wa miguu Afrika liliingia mkataba wa haki za matangazo kwa miaka miwili na kampuni kutoka nchini Togo ya New World TV iliyoanzishwa mwaka 2015.

Ni mwanzo wa mwisho wa utawala wa DSTV kusini mwa Afrika? Bado DSTV ni moja ya nguli wa kurusha matangazo barani Afrika huku kampuni zake mbili za DSTV na GoTV zikiwa na visimbusi milioni 23 vilivyo hai kwenye nchi 50 barani Afrika.
Dstv itafunga biashara mda sio mrefu monopoly walio kua nao Africa ilisha isha, ntu atalipia je kifurushi kwa 100k kuangalia chanel zote ni wixi ni gharama kubwa kushinda bill za uneme kwa mwezi
 
Back
Top Bottom