Dstv yaondoa channel ya Emmanule Tv ya TB Joshua

Mjanja M1

JF-Expert Member
Oct 7, 2018
3,660
12,306
Kampuni ya televisheni ya Afrika Kusini ya Multichoice Africa imetangaza kuwa itasitisha matangazo ya Emmanuel TV, kituo cha kidini inayomilikiwa na marehemu Nabii Temitope Babatunde Joshua, mwanzilishi wa Kanisa la Synagogue Church of All Nations, kuanzia Januari 17, 2024.

Uamuzi huo unafuatia filamu yenye utata iliyorushwa na BBC ikielezea madai ya ukatili na uhalifu wa kingono uliofanywa na T.B. Yoshua.
 
DSTV wametumia kigezo gani kuifungia hiyo channel?

Wamewahi kumuhoji nani wa kanisa la TB Joshua ili kuthibitisha madai ya BBC dhidi yake?

Au kwao, uchunguzi wa BBC ndio final and conclusive usiotakiwa kuhojiwa na yeyote?

DSTV nao wamekurupuka tu, sitashangaa siku za mbeleni wakiirudisha hiyo channel.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Kampuni ya televisheni ya Afrika Kusini ya Multichoice Africa imetangaza kuwa itasitisha matangazo ya Emmanuel TV, kituo cha kidini inayomilikiwa na marehemu Nabii Temitope Babatunde Joshua, mwanzilishi wa Kanisa la Synagogue Church of All Nations, kuanzia Januari 17, 2024.

Uamuzi huo unafuatia filamu yenye utata iliyorushwa na BBC ikielezea madai ya ukatili na uhalifu wa kingono uliofanywa na T.B. Yoshua.
Heading iwe KUONDOA na si YAONDOA sababu bado hiyo channel ipo kwenye DStv.

Screenshot_20240111_180213_Edge.jpg
 
western media propaganda dhidi ya watu weusi na mambo mazuri yanayofanywa na weusi.

BBC, CNN na nyinginezo zipo kwa ajili ya maslahi ya watu wao na mataifa yao kwaa kueneza mitazamo yao, habari zao zipo bias sana na zime base kwenye one side story.

All in all siamini hao manabii ila pia western media zipo kwa ajili ya destruction zaidi kuliko kujenga.

Ulimwengu huu wa digital ni muhimu tujifunze ku control habari tunazotaka kuzisikia na ku ignore ambazo hatuhitaji vinginevyo tutakuwa wehu au kuishia kupata depression.
 
Hii kashfa kama ni kweli ni mbaya sana.

Tulikuwa na imani na TB Joshua, tulifuatilia sana tv yake hadi kuishika screen tukijua ni njia ya kupeleka maombi yetu kwa Mungu.

Waamini tumekufa ganzi sema tunajikaza tu hivyo hivyo.
😁😁 Mmekuwa kama wakatoriki na tamko la papa Fransis😀😀😀... Furahini tu mmejua what is behind the screen... Haiwezekani watu wote wale washuhudie mabaya yake kusiwe na hata moja la kweli... Na wengi wa azidi kujitokeza kusema yasioratibiwa na BBC... Kama huyu hapa aliekuwa mhariri wa habari wake👇
 
Back
Top Bottom