DSTV Tanzania watoa onyo kwa watakaorusha matangazo ya ligi kinyume cha utaratibu

101 East

JF-Expert Member
Feb 25, 2015
1,040
2,121
MultiChoice Tanzania (DStv Tanzania) wametoa onyo kali kwa Watu wote wanaosambaza au kurusha kwa njia yoyote ile ikiwemo kwa njia ya waya (cable) matangazo ya ligi kama Premier league, UEFA Champions league, UEFA Europa league, UEFA Europa Conference League, UEFA Super cup league, Community Shield, Serie A, LALIGA, UEFA Youth League na FA msimu wa 2023/2024.

Taarifa kwa Umma kutoka kwenye kampuni hiyo imetoa onyo hilo kali kwa wote wanaofanya vitendo hivyo ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusema Multichoice na Washirika wake hawatosita kuchukua hatua kali za kisheria kwa yeyote atayerusha matangazo ya ligi hizo bila idhini kwani haki ya kufanya hivyo inahodhiwa na SuperSport International pekee.

"SuperSport International (Pty) Limited ni moja ya Kampuni tanzu ndani ya kundi la Makampuni ya Multichoice ambayo inasimamia huduma kwa Wateja wa Multichoice katika eneo la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kwamba matangazo ya ligi hizi yanarushwa kupitia chaneli za SuperSport pekee ambazo hupatikana katika kisimbuzi cha DStv, haki hizi ni za ukanda wa kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo Tanzania"

"Kwa minajili hiyo, kurusha au kusambaza kwa njia yoyote ile matangazo ya ligi hizi katika eneo tajwa bila idhini ya MultiChoice ni kinyume cha sheria, kanuni na makubaliano ya haki miliki, tunaujulisha Umma kuwa Multichoice na Washirika wake hawatosita kuchukua hatua kali za kisheria kwa yeyote atakayerusha matangazo ya ligi hizi bila idhini" #MillardAyoUPDATES
 
Wamepandisha bundles sisi tunafanyaje wakati Canal ukilipia 45 unacheki league zote.
Naomba mchongo huu ndugu yangu, maana jamaa wamepandisha lkn hata kwenye 60,000/= mechi kali za UEFA uoni. Yaani wizi mtupu, naomba saidia kama vipi zama Inbox
 
Sisi ambao huwa tunaangalia ligi ya bongo utopolo+ mikia hilo TANGAZO linatujazia tu server Wala halituhusu.
 
Back
Top Bottom