Elias Kamugisha
Member
- Mar 7, 2014
- 6
- 5
Ongelea mada iliyotajwa mambo ya kuongeza mke sio mada ya msingi
Dr. Slaa mchaga!!! Huu ni ujinga unaokaribia upumbavu.
mkaskazini basi
dr.slaa amezeeka sana. hafai kuwa rais hata wa TFF
Wewe kijana sana umefaa nini TZ, hata kibaka tu hujawahi kumkamata uanabwabwaja kama bata, Uzee wa Slaa unalindwa na Mandela na Mugabe; Ujana wako unatija ipi??? kama sio kutumika na wezi ambao Slaa na uzee wake anapambana nao???
Kwa hiyo ye yote anayetoka kaskazini hafai. Mtazamo wa hivi ni wa watu waliokosa hekima na busara.
Discuss issues not people.
pendekeza kwenye mkutano mkuu wa chadema. bila shaka utakuepo.WanaJF, Kwa sasa Dr Slaa ametimiza miaka 70 rasmi lakini bado ameng'ang'ania nafasi kubwa ya kimaamuzi kwenye chama. Jambo ambalo ni hatari kubwa. Kwa tafiti fupi iliyowahi kufanywa ilionyesha kuwa viongozi wengi waliowahi kuingiza nchi zao kwenye vita ni wale wenye umri mkubwa kama huo wa Dr Slaa. Hivyo maamuzi ya CHADEMA kumtumia Dr Slaa mpaka sasa yanaweza kuhatarisha amani hasa kwenye kuelekea uchaguzi mkuu kutokana na maamuzi ambayo yanaweza kufanywa na Dr Slaa kutokana na umri wake. Aidha, itakumbukwa miaka ya hivi karibuni Dr Slaa alikuwa akitoa kauli na ajabu ajabu na zenye viashiria vya kutaka kuleta uvunjifu wa amani. Sasa pata picha hali itakuwaje kwenye uchaguzi? Ningependekeza Dr Slaa apelekwe kwenye baraza la wazee la chama na nafasi yake ichukuliwe na Tundu Lissu ili kukipa uimara chama ili kiweze kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Jana na siku nyinginezo, kumekuwa na mjadala na kejeli juu ya umri wa Dr.Wilbrod Peter Slaa,Katibu Mkuu wa CHADEMA. Wapo wanaodiriki kumuita 'Babu'. Yupo mwana-JF ajulikanaye kama HAMY-D ambaye jana ameweka bandiko humu akisema kuwa Dr.Slaa amefika umri wa miaka 70 na kama bado Dr.Slaa ni tegemezi katika kujenga hoja ndani ya CHADEMA.
Mosi, Dr. Slaa hajafika umri wa miaka 70. Akizaliwa Oktoba 1948, Dr. Slaa atafikisha umri wa miaka 70 ifikapo Oktoba 2018. Inategemewa wana-JF waje hapa na hoja za kweli na si porojo kama za jana. Kwahiyo, si kweli kuwa Dr.Slaa amefika umri uliodaiwa wa miaka 70.
Pili, Dr.Slaa yuko katika rika la Rais wa sasa wa Tanzania Mh.Jakaya Mrisho Kikwete. Rais Kikwete kwasasa ana umri wa miaka 64 na Dr. Slaa ana umri wa miaka 66. Hivyobasi, Dr.Slaa hana umri wa kutisha kama inavyojengwa hoja nyepesi na wapinzani wake.
Tatu, ni juzi tu hapa Mh.Samwel John Sitta amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Bunge la Katiba. Isitoshe, Mh.Sitta anatajwa kama mmoja wa Wagombea watarajiwa Urais kupitia CCM. Kwasasa Sitta ana umri wa miaka 71 na Disemba mwaka huu anatimiza miaka 72. Hii ni kwakuwa amezaliwa Disemba, 1944. Huyu si mzee kama alivyo Dr.Slaa?
Nne, watanzania hawatahitaji umri katika kuchagua viongozi wao hapo 2015.Wataangalia uwezo wa mtu husika. Lakini,kujadilijadili umri wa Dr.Slaa na kumchora kama mzee asiye na uwezo wa kuongoza nchi ni upotofu na kukosa hoja. Rais wa zamani wa Kenya Mh.Mwai Emilio Kibaki aliingia madarakani akiwa na umri gani?
Tano,iko wazi kuwa Dr.Slaa ni mtu makini,mbobezi wa siasa na mjenzi mzuri wa hoja.Ni mwerevu,jasiri na anayeweza kuthubutu. Ni tishio katika siasa za nchi hii.Ndiyo maana haishi kutajwa midomoni mwa wapinzani wake hasa watokao CCM. Dr.Slaa amekuwa akipuuza hoja mfu hii ya umri wake na anasonga mbele!
ukiwa mzee akili inachoka inakuwa kama ya mtoto.
WanaJF,
Kwa sasa Dr Slaa ametimiza miaka 70 rasmi lakini bado ameng'ang'ania nafasi kubwa ya kimaamuzi kwenye chama. Jambo ambalo ni hatari kubwa.
Kwa tafiti fupi iliyowahi kufanywa ilionyesha kuwa viongozi wengi waliowahi kuingiza nchi zao kwenye vita ni wale wenye umri mkubwa kama huo wa Dr Slaa.
Hivyo maamuzi ya CHADEMA kumtumia Dr Slaa mpaka sasa yanaweza kuhatarisha amani hasa kwenye kuelekea uchaguzi mkuu kutokana na maamuzi ambayo yanaweza kufanywa na Dr Slaa kutokana na umri wake.
Aidha, itakumbukwa miaka ya hivi karibuni Dr Slaa alikuwa akitoa kauli na ajabu ajabu na zenye viashiria vya kutaka kuleta uvunjifu wa amani. Sasa pata picha hali itakuwaje kwenye uchaguzi?
Ningependekeza Dr Slaa apelekwe kwenye baraza la wazee la chama na nafasi yake ichukuliwe na Tundu Lissu ili kukipa uimara chama ili kiweze kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi mkuu ujao.
ukiwa mzee akili inachoka inakuwa kama ya mtoto.