Dr. Slaa turns 70: Bado ni "think tank" wa CHADEMA?

Dr. Slaa turns 70: Bado ni "think tank" wa CHADEMA?

HAMY-D

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2011
Posts
7,146
Reaction score
3,830
WanaJF,

Kwa sasa Dr Slaa ametimiza miaka 70 rasmi lakini bado ameng'ang'ania nafasi kubwa ya kimaamuzi kwenye chama. Jambo ambalo ni hatari kubwa.

Kwa tafiti fupi iliyowahi kufanywa ilionyesha kuwa viongozi wengi waliowahi kuingiza nchi zao kwenye vita ni wale wenye umri mkubwa kama huo wa Dr Slaa.

Hivyo maamuzi ya CHADEMA kumtumia Dr Slaa mpaka sasa yanaweza kuhatarisha amani hasa kwenye kuelekea uchaguzi mkuu kutokana na maamuzi ambayo yanaweza kufanywa na Dr Slaa kutokana na umri wake.

Aidha, itakumbukwa miaka ya hivi karibuni Dr Slaa alikuwa akitoa kauli na ajabu ajabu na zenye viashiria vya kutaka kuleta uvunjifu wa amani. Sasa pata picha hali itakuwaje kwenye uchaguzi?

Ningependekeza Dr Slaa apelekwe kwenye baraza la wazee la chama na nafasi yake ichukuliwe na Tundu Lissu ili kukipa uimara chama ili kiweze kushiriki kikamilifu kwenye uchaguzi mkuu ujao.
 
WanaJF,

Kwa sasa Dr Slaa ametimiza miaka 70 rasmi lakini bado ameng'ang'ania nafasi kubwa ya kimaamuzi kwenye chama. Jambo ambalo ni hatari kubwa.

Kwa tafiti fupi iliyowahi kufanywa ilionyesha kuwa viongozi wengi waliowahi kuingiza nchi zao kwenye vita ni wale wenye umri mkubwa kama huo wa Dr Slaa.

Hivyo maamuzi ya CHADEMA kumtumia Dr Slaa mpaka sasa yanaweza kuhatarisha amani hasa kwenye kuelekea uchaguzi mkuu kutokana na maamuzi ambayo yanaweza kufanywa na Dr Slaa kutokana na umri wake.

Aidha, itakumbukwa miaka ya hivi karibuni Dr Slaa alikuwa akitoa kauli na ajabu ajabu na zenye viashiria vya kutaka kuleta uvunjifu wa amani. Sasa pata picha hali itakuwaje kwenye uchaguzi?

Ningependekeza Dr Slaa apelekwe kwenye baraza la wazee la chama na nafasi yale ichukuliwe na Tundu Lissu ili kukipa uimara CHADEMA haswa kwenye kuelekea kwenye uchaguzi.

Tunafurahi kwamba Dr. Slaa hakupi Amani wala utulivu, Usifikiri unamdhalilisha kwetu naona ndo unampandisha chati. Juzi tuliambiwa Mh. Samwel Sitta ametimiza miaka 71, na jana kateuliwa kuwa mwenyekiti wa Kudumu wa Bunge Maalum la Katiba.

Achana na siasa za Kijiweni,
Tulieni Sindano iwaingie taratibu tu
 
kwanza nimpe hongera dr.slaa kwa kula chumvi nyingi .. namtakia maisha marefu mzee wangu slaa. pili kwa jinsi taifa lilivyo na changamoto nyingi zinazolikabili namuomba tu apumzike mambo ya siasa na kujikita zaidi kuwa mshauri wa chama , pilikapilika za urais hataziweza kabisa zinahitaji vijana kama zito. mzee pumzika ule pensheni yako siasa zinakutesa tu
 
Inawezekana unachokisema ni sahihi!

Maana kadri CCM inavyoendelea kukaa madarakani(Sasa hv ina miaka 50) ndivyo uvunjifu wa amani UNAVYOZIDI!
 
Marehemu Mwalimu amefariki akiwa na miaka 77 tena sio kwa uzee bali maradhi. Na hakuna anayebisha kuwa ndiye alikuwa kiongozi wa CCM kutokea Butiama na CCM ile ingekuwepo leo hii hatungekuwa na sababu ya kutoa kwenye track. Sasa wewe umri huo unakusumbua nini? Kama baba yako ana umri huo na kesha poteza mwelekeo hayo ni matatizo ya kwenu kiukoo na ndio maana hata wewe katika umri wako mdogo umeshapoteza mwelekeo.

Sent from my iPad using JamiiForums
 
pata picha kwa umri huo hajaoa bado ana mchumba, sijui ni mfano gani kwa wajuku zake anaotaka kuwaongoza
 
ivi think tank au tuseme ID ya mtu inahusiana na umri?tuseme mwalimu kipindi ana umri wa 70 hakuwa tena mtu wa kusikilizwa?Mugabe ana umri gani?
 
miaka 70 na anaongeza mke, kweli nzi hufia kwenye kidonda.
Nenda kwenye histori ya Kenya Marehemu mzee Kenyatta alishawaambia wananchi wake pamoja na kua na umri wa miaka 75 lakini alichokua anamfanyia Mama Ngina usikua mpaka anaomba maji!
 
kwanza nimpe hongera dr.slaa kwa kula chumvi nyingi .. namtakia maisha marefu mzee wangu slaa. pili kwa jinsi taifa lilivyo na changamoto nyingi zinazolikabili namuomba tu apumzike mambo ya siasa na kujikita zaidi kuwa mshauri wa chama , pilikapilika za urais hataziweza kabisa zinahitaji vijana kama zito. mzee pumzika ule pensheni yako siasa zinakutesa tu

Mkuu,

Ni nani amekwambia Dr Slaa ana pensheni?

Hana lolote huyo mzee, yeye pamoja na mchumba wake hawapo kwenye mifumo ya mafao ya mfuko wowote ule.

Who knows, huenda hofu yake ipo hapo kuwa akipisha wengine, yeye ataishije?
 
Kwani katiba inakataza mtu mwenye umri kuanzia miaka 70 asiwe kiongozi wa hii nchi?
 
Back
Top Bottom