Sikonge
JF-Expert Member
- Jan 19, 2008
- 11,550
- 6,062
Nina uhakika kuna wengi wetu wameshaangalia sinema au kusoma vitabu vya kijajusi ambavyo Wapelelezi wa aina mbalimbali waliweza kupelekwa sehemu na kutulia kwa miaka mingi huku wakifanya kazi zao (Double Agent) au kutokufanya kitu chochote cha Kipelelezi na wakawa wanasubiri amri itoke ili waamshwe na kuanza kufanya kazi yao ambayo ni ya muda mfupi sana kutoweka (Sleeper Agent).
Kuna kesi nyingi hasa za Wauza madawa ya kulevya au Majambazi, Mafia nk ambapo Polisi na hasa FBI kwa USA, Scotland Yard wa UK nk walipeleka mtu wao ambaye na yeye alikuwa akifanya kila kitu kama jambazi. Alijenga uaminifu na hao majambazi hadi wakamuamini na wakawa wanampa siri zote za ndani. Kali zaidi kutokea ni lile tukio la miaka ya 90 ambapo FBI walienda kuusambaratisha mtandao hatari ndani ya POLISI wa New Orleans. Mapolisi hawa walikuwa wakitumia kofia ya Polisi kuuwa watu, kutesa watu na kuuza madawa ya kulevya nk.
Hawa Ma-agent au Wapelelezi wanaolazwa, mara nyingi ni NATO vs Russia, India vs Pakistan, North Korea vs South Korea, China vs USA nk. Hawa huja nchi wanayoitaka wakiwa vijana wakitokea nchi tofauti na yao. Wakifika sehemu wanapotakiwa kuishi wakisubiri amri, huweza kuanza maisha, kuzaa watoto na kushirikiana na Wenyeji wao vizuri tu hadi muda ukifika ndiyo hufanya kazi yao na kukimbia. Kuna mashirika au makampuni makubwa pia huibiana Techonology kwa kupeleka vijana kwenye shirika la upinzani.
Tumeshuhudia kwa miaka mingi sana vyama vya siasa vinapoanza kuwa maarufu, watu walewale waliokifanya chama kuwa maarufu huanza fujo na kukikimbia chama chao huku wakikiacha kikiwa kimemeguka. Cha ajabu ni kuwa hao hao watu ukiwachunguza sana, utagundua kuwa umaarufu wao ni kama ulikuwa umetengenezwa na Waandishi wa habari kwa uangalizi mkubwa sana. Wengi wao miaka ya zamani walirudi CCM.
Wote akina Mrema, Kabourou, Masumbuko Lamwai et el walitangazwa sana kwenye vyombo vya habari hadi wakajipatia umaarufu wa kutisha. Zitto Kabwe na Dr. Slaa pia siyo siri walitanganzwa sana hadi kila mtu akawafahamu. Pamoja na kupata upinzani kidogo wa hapa na pale kutoka kwa watu kama Shonzah na genge lake, upinzani huo walihakikisha haufanyi madhara makubwa. Mtu kama faizaFozxy alihakikisha kila wiki anamtaja Padre wake ili watu wasimsahau. Katika dunia hii, hakikisha unatajwatajwa sana iwe kwa mabaya au mazuri. Kama wewe hawakutaji, basi umekwisha kisiasa. Mti wenye matunda.... ndiyo msemo wao.
Tuje kwenye listi ya Mwembeyanga. Yale majina sijui nani aliyatoa ila tunaona hadi leo, anayetajwa ni mmoja tu Lowassa ingawa waliotajwa walikuwa 11 na bado wapo CCM. Hiyo listi ambayo Tundu Lissu anadai ndiyo aliiandaa, ndiyo iliyokuja kumpa umaarufu sana Dr. Slaa. Pia Dr Slaa alikuja kuwa hadi anatamba wazi kabisa kuwa nusu ya usalama wa Taifa (TISS) wanatoa ripoti kwake, mhhhhh!!!
Dr Slaa na Mzindakaya ukiwachunguza sana, unaona wanafanana. Wote walipewa majina na Skendo ili wazilipuwe.
Upande mwingine tuna Zitto vs Kafulila. Alichokifanya Zitto ni kuibua khashfa ya Madini na hapo vyombo vya habari vyote vikawa ni Zitto tu kila sehemu. Bungeni akasimamishwa kwa wiki kadhaa kufika kwenye vikao na kuanza kutembezwa nchi nzima kama shujaa. Alichofanya Zitto ukikiangalia sana, hakikuwa na madhara yeyote makubwa zaidi ya rasha rasha za hapa na pale.
Alichokifanya David Kafulila ni kilekile kwenye kesi ya Escrwo. Ila kwa Kafulila, hili halikuwa limemapangwa na madhara yake yakawa makubwa sana. Kafulila hakupewa umaarufu wowote na kibaya zaidi akawa kama vile anaminywa kabisa kwenye vyombo vya habari. Siku hizi amebaki yeye kujisifu tu ila Media hazisemi kabisa. Kama hiyo haitoshi, Zitto akadandia hilo treni na kusema hizo habari za Escrow ni yeye ndiyo alimpa ili mradi kupunguza umaarufu huo wa David Kafulila .
Kwa sasa hivi siyo siri tena kuwa Zitto yupoyupo tu na ni kama Agent aliyefumuliwa kabla ya muda na sasa hivi wanamuangalizia Plan B ili asije kuwekwa uchi zaidi. Anaweza kuwa hapo na baada ya uchaguzi, yeye na ATC wakawa wanapewa umaarufu hadi wawe chama maarufu cha upinzani, tayari kwenda kuwavuruga wapinzani wengine.
Kinachonisumbua hadi leo kwangu mimi ni:
- Kwa nini Mzee Slaa kaacha Chadema na kuingia CCM kwa mlango wa nyuma kama alivyoingia Serena Hotel?
- Je alikuwa kazini siku nyingi akiwa amelazwa akisubiri muda tu?
- Je Zitto hakuwa Agent wa CCM kama tulivyoaminishwa hapa ila alibebeshwa Mikoba yote ili watu wamuone yeye tu na kutokumfikiria kabisa Dr Slaa kama Msaliti wa kweli?
- Au ni kweli Mama Josephine alimfukuza ndani na akalala kwenye gari na baada ya hapo akawa kashikishwa adabu na akapiga magoti kutii amri za Josephine? Yaani kama usaliti ndiyo ulianza na ilibidi asalimu amri kwa kuchagua kushikamana na Josephine au kuisaliti Chadema na kwenda CCM.
- Je mtu aliyesemwa hana KIPATO kwenye ule Waraka wa Prof. Mkumbo au Samson Mwigamba na wakakataa katakata kumtaja na wengi wakidhani ni Zitto, alikuwa ni Dr Slaa?
- Kwa nini Tundu Lissu na Kafulila pamoja na kazi kubwa walioifanya bungeni, hadi leo hawajapewa umaarufu wa Zitto na Dr Slaa?
- Kwa nini wizi wa Escrow na madudu mengine hayasemwi ila Richmond peke yake ingawa inamhusisha Kikwete moja kwa moja? Je baada ya uchaguzi, watu wataendelea na Richmond na hasa ukichukulia Mkubwa hatakuwa badi Mkubwa?
- Je ni kweli Dr. Slaa kaamua kuimaliza Chadema na hasa Lowassa au ni Double Agent wa Chadema huko CCM? Tumtegemee wiki kadhaa kabla ya uchaguzi arudi Chadema na kuanika yote aliyofanyiwa na CCM? Hadi leo hakuna jipya sana alilolisema ambalo watu hawalijui kuhusu Lowassa. Labda ya Chadema.
Kama kweli Dr wetu alikuwa ndiyo Silaha ya mwisho ya CCM ndani ya Chadema ambayo walikuwa wakiitegemea, basi inabidi kumpa hongera sana Mbowe kwa mchezo alioufanya. Kama angelibaki na Dr Slaa kama mgombea wa Chadema, basi Magufuli alikuwa kashajishindia siku nyingi na akibaki kuapishwa tu.
Je CCM wana mtu bado ndani ya Chadema? Kwangu mie aliyebaki pekee marufu ni Mbowe ingawa na yeye ni kama vile kuna mtu anahakikisha anadharaulika sana nchi hii. Tishio pekee kwa siku za mbeleni ni Mnyika na Lissu ila na wao pamoja na juhudi zote, wanahakikisha habari zao haziandikwi sana.
Mwisho nikiri kuwa Usalama wa Taifa wa Tanzania (TISS) kuna mijitu ina VICHWA, laiti vingelitumika kujenga UCHUMI?
Mungu Ibariki Tanzania.