Dr Slaa na Zitto ni Double or Sleeper Agent?

Mahaba Niuwe........ Mama Josephine akiwa NUSU UCHI.....

josepjine-slaa-1.jpg
Wengine bado tunahuzunika hadi leo kwa unyama huo.


Bado hujaandika chochote kuhusu kisa kilichomuondoa Katibu Mkuu na Kipenzi chetu ndani ya CHADEMA.

Kwa nini hata kama alikuwa hakubaliani, asingelikaa kama Lipumba kwa kurudi kuwa Mbunge tu wa KARATU?

Utake usitake, kuna kitu kimemuondoa kutoka kwa RAFIKI yake Mbowe na kumtupa Mikononi mwa Mwakyembe.
Mkuu nadhani unataka mimi niseme kwa kutumia dhana yangu juu ya sababu za Dr. Slaa kuondoka Chadema (UKAWA)..

Yeye kazieleza kwa kirefu katika hotuba yake, sasa kama wewe hukubaliani naye isipokuwa unaamini ni matakwa ya mkewe haya! ila hata mimi kuingia tu kwa Lowassa kungeniondoa Chadema kama yeye.
Ni muhimu sana ifahamike tu kwamba watu wengi mnafikiri unaweza tu mtu ku cross chama hiki ukaingia chama kingine pasipo kuwa na imani ya mwongozo wao,misingi yao na kuwa muadilifu katika kanuni za chama hicho. Lowassa hafungamani na misngi wala mwongozo wa Chadema!

Kuna sifa za uanachama wa chama cha Siasa kiasi kwamba usiiingie katika Ujamaa huku unatangaza Ubepari ama kinyume chake. Matarajio ya Kisera, Ilani na ahadi lazima yafungamane na mwongozo na hivyo hutazami mtu gani
yupo huko ujiunge na unapopokelewa inatakiwa kuapishwa kwa kushikishwa katiba ya chama, sio kadi ya chama na kwamba utakitumikia chama kwa misingi iliyopo. Utaiheshimu katiba na kuwa muadilifu kulingana na Katiba. Lowassa amekabidhiwa tu kadi na kupewa Uongozi mkuu wa chama kama vile amenunua nyanya sokoni...

Kisha mkuu wangu nawashangaeni sana watu wa Chadema mnaposema Dr.Slaa angekaa tu UKAWA kama Lipumba, mbona huyo Lowassa hakukaa tu CCM kama wengine kakimbilia Chadema baada ya kuenguliwa? Hivi Lowassa alikuwa na haki gani kuondoka CCM walokuwa wakijivua magamba muone ni sawa, lakini huyu alokataa fisadi kuwa Supreme Leader wa Chama mnamuona ndiye mchawi?..

Dr. Slaa hakuacha urafiki na Mbowe kifupi hata mimi bado ni rafiki yake japo kabugi Step na habari za mujini zinasema haya mambo yaliandaliwa na wazee hivyo asingeweza kupinga, sasa iwe Dr.Slaa anamsikiliza mkewe na huyu anayemsikiliza baba mkwe tutasema nini? Hizo ndio habari za mujini kwa hiyo aidha zina ukweli ama uongo hazitakiwi kuwa hoja ama kero za kutangazwa sasa hivi badala ya sera. Wewe na mimi tutofautiane tu kwa sera na mtazamo lakini mambo ya mikakati ya vyama tuwaachie wenye vyama.

Swala la Mwakyembe ni rahisi kabisa kwa sababu Huyu Mwakyembe kapitia wakati mgumu sana baada ya swala la Richmond, inasemekana alilishwa sumu kenda kutibiwa India, akalalamika wanataka kumuua almanusura kaponea chupu chupu leo hii adui yenu kwa sababu ya Lowassa!. Hivyo yawezekana Dr.Slaa amepata mtu anayeweza kumshauri juu ya Uhalisia wa kisiasa, ajihadhari vipi na huyu kiumbe.

Hii ni dhana yangu tu lakini binafsi sioni ubaya kabisa kuwa na marafiki nje ya chama chako na hasa vyama hivi vilivyojaa unafiki mtupu.. Marafiki wa ndani ya chama kimoja huitwa Makundi na ukiwa nje wewe Msaliti sijui mnataka watu waishi vipi?..
 
Mwenendo wa siasa za Tanzania ni mgumu kwa kiasi chake. Ndiyo maana inakuwa vigumu kidogo kutengenezea kanuni yake. Njia ndefu ya kutengeneza kanuni ya mwenendo huo nilizama usome na kuelewa taarifa nyingi za uongo na taarifa kidogo za ukweli kuhusu siasa za Tanzania. Ukisha kuzielewa unaanza kuchambua kwa kina kila chanzo cha taarifa uliyosoma na kuelewa kwa kufuata "vigezo maalumu". Nilikuwa najaribu kutengeneza kanuni hii lakini Dr. Slaa kusababisha niongezee kigezo kingine maalumu katika kuchambua chanzo cha habari kiasi cha kuvuruga kiasi utaratibu niliokuwa nimejiwekea kupata kanuni hii.
 
Mwenendo wa siasa za Tanzania ni mgumu kwa kiasi chake. Ndiyo maana inakuwa vigumu kidogo kutengenezea kanuni yake. Njia ndefu ya kutengeneza kanuni ya mwenendo huo nilizama usome na kuelewa taarifa nyingi za uongo na taarifa kidogo za ukweli kuhusu siasa za Tanzania. Ukisha kuzielewa unaanza kuchambua kwa kina kila chanzo cha taarifa uliyosoma na kuelewa kwa kufuata "vigezo maalumu". Nilikuwa najaribu kutengeneza kanuni hii lakini Dr. Slaa kusababisha niongezee kigezo kingine maalumu katika kuchambua chanzo cha habari kiasi cha kuvuruga kiasi utaratibu niliokuwa nimejiwekea kupata kanuni hii.

Hili nalo ni fumbo la Imani...

Ni kweli siasa za Tanzania ni ngumu, ila kwa imani yangu si dhani kama Dr. Slaa alikuwa agent ila ukiniambia Mama Mshumbusi ninaweza kuunganisha dot kidogo kidogo na mwisho kutoka na kitu ambacho kinaweza kuelekea kwenye ukweli...
 
Back
Top Bottom