Siyo mikataba yote ni lazima iwekwe wazi. Kibiashara baadhi ya makampuni hayataki kuweka mikataba yao public ....kuna mikataba ya kijeshi kati ya serikali (hao IMF na WB wanashupalia hili) na serikal au na mashirika binafsi, na haiwekwi public.
Hata hivyo, linalojengwa ni pipeline, sasa wewe unatyaka mkataba gani? Wakujenga pipeline?? AU WA MATUMIZI YA GESI?? Mimi bado sijaelewa tatizo ni nini hasa.
Mkuu [MENTION]kobello,[/MENTION] mbona hoja ya[MENTION] Mikael P Aweda[/MENTION] iko wazi.
Msome vizuri hasa kwenye red mkuu wangu.
By Mikael P Aweda![]()
![]()
Kwani wanamtwara siyo watanzania? Malalamiko ya wanamtwara ni ya watanzania wote. Na mikataba tunayotaka yawekwe hadharani kama nilivyosema siyo ya mtwara tu bali nchi nzima. Kwa hiyo, swali langu liko pale pale, kwa nini ccm hawataki kuonesha mikataba ya uchimbaji wa gesi kwa wanamtwara na watz wote wakati yanachimbwa katika ardhi yao/yetu (sisi watz +wanamtwara pamoja na wewe kobello)
Aweda ameweka kila kitu wazi.
1. Amekuuliza wanamtwara siyo watanzania? kama watanzania je hawana haki ya kudai kutekelezewa haki zao za msingi kutoka raslimali zinazopatikana katika mazingira yao kwanza na baada ya hapo zikawanufaishe na ndugu zao mikowa mingine. Serikali inapotosha kwamba wanamtwara wanazuia gesi huu ni uzushi na uwongo mkubwa.
2. swala la pili Aweda anauliza kwanini serikali inaficha mikataba? iwe ya madini, kubinafsisha ardhi au gesi?? nasiyo inawaficha wananchi tu bali inawaficha hata wawakilishi wa wanachi yaani wabunge wao! Aweda anapendekeza mambo yawekwe hadharani ilitufahamu tunapata nini kwanini tunapata hicho na siyo zaidi.
-Je tunaendelea kupewa asilimia za mrahaba chini ya 5% na 95% kuondoka na wawekezaji? mkuu kobello unafahamu tutapata % kutoka mapato ya gesi?
-Je tunalipa gharama shahihi za unzenzi wa mitambo na bomba kwa ujumla (Value for money related to the actual cost of the project) au tunaibiwa kwa kulipa mara kumi au zaidi ya gharama halisi??
-Je wananchi kwanza wa maeneo husika na pili wanzania kwa ujumla watapata faida staihiki au magumashi kutoka mikataba hii??
Haya ndiyo mawazo na matazamo wa mkuu Aweda, hujaelewa nini bwana Kobello?