Dr Slaa: Mtwara wamepuuzwa!

Dr Slaa: Mtwara wamepuuzwa!

Hivi kwa nini mnataka kuleta machafuko? Kwa nini Dr Slaa anasema atahakikisha nchi haitawaliki?

Kwa hiyo nyie watu wakaskazini ndiyo mnawakumbuka watu wa Mtwara?

We Mwalimu, unadhani watu wa kaskazini hawapo kusini? too low, kasome, diploma yako ya uwalimu haijakukomboa...
 
Hata kama ni forum kuna utaratibu wa kufuata, huwezi kuleta michezo, mzaha au uchumi hapa, kuna majukwaa mengine humu.
Pili, hapa kuna mada kuhusu Mtwara na mada siyo mtu aliyetoa maoni yake. Swali la msingi ni kwa nini serikali imewatelekeza watu wa mtwara na kuwafichia mikataba ya uchimbaji wa gesi iliyoka ktk ardhi yao? Sasa hawajui watafaidikaje kwa kuwa mikataba ni siri ya jk na mawaziri wake. Je, hii ni sahihi?.
Ardhi yao au ya watanzania wote?Kile kipande cha Mnazi Bay hakimilikiwi na wana Mnazi Bay, au wana Mtwara , au wana Kanda kusini bali inamilikiwa na watanzania wote kwa ujumla.
Anza kwa kujifunza agrarian laws za nchi yako.....
Siasa nyingi mno hutandaza fikra. .... your whole thought process is corrupted,.
 
  • Thanks
Reactions: kix
Natamani ningekuwa na uwezo wa kufungua mioyo ya watu nione kama wasemalo ndilo lililo mioyoni mwao.
 
Hiyo gesi haiozi haraka ya nini? Elimu itolewe hata kwa zaidi ya miaka kumi, haraka ya nini? HAITOKI
 
laana kutoka kwa nani..?

Hivi bado mnadhani slaa alishinda ... Znz kura hazikutosha.. Miji ya pwani hana umaarufu.. Labda kaskazini huko

Matokeo ya kutumia tumbo kufikiri ndio haya! Kanda ya ziwa alikwenda mara tatu kimya kimya kufuata nn wakati kura zinahesabiwa!!!? Tuache hayo ...

JIULIZE KWA NINI HAWAKUSAFIRISHA MAJI KUTOKA MTERA KUJA DAR!!!?

MASWALI YA MSINGI KUTOKA MTWARA KWA SERIKALI jk ...

1. BANDARI YA MTWARA NI KIPAUMBELE KWA MAENDELEO YA NCHI YETU KWA KUENDELEZA UCHUMI NA IMEWEKWA KWENYE MPANGO WA KUJENGWA. jE!? HII YA BAGAMOYO IMEINGIA LINI KWENYE PLAN NA KWA MANUFAA YA NANI KAMA YA MTWARA INAPUUZWA!!!?

2. KM 48 ZA BARABARA IENDAYO MTWARA IMEPUUZWA KUMALIZIWA LAKINI KM 60 ZA MSATA BAGAMOYO ZIMEJENGWA, ZIPI ZILIKUWA NA KIPAUMBELE!?

3. ILISEMEKANA BUNGENI NA KWENYE MIPANGO MINGINE YA SERIKALI KUFUFUA VIWANDA MTWARA KUENDANE SANJARI NA UJENZI WA BANDARI, HII MIPANGO IMEPOTELEA WAPI!!!?

4. UWANJA WA NDEGE MTWARA BADO HAUNA KIWANGO CHA KUTOSHA, IWEJE LEO KUNA MIPANGO YA KUJENGA BAGAMOYO, JE WAPI NI KIPAUMBELE KWA MAENDELEO YA NCHI!!!?

5. KWA NINI KILA KITU BAGAMOYO NA MAMBO YA NTWALA YANAPUUZWA!!!?

6. JE!!!? MAKONDE CHI NTU!!!?

7. NAULIZA HIVIIII ... HAYO HAPO JUU NI CHAMA GANI CHA SIASA!!!?

8. JE!!!? UPUUZI WA ccm KWA NINI UNAHUSISHWA NA CHAMA CHA SIASA!!?
 
laana kutoka kwa nani..?

Hivi bado mnadhani slaa alishinda ... Znz kura hazikutosha.. Miji ya pwani hana umaarufu.. Labda kaskazini huko
My friend! Bado uko kwenye jinamizi la ukanda!
 
MUNGU HACHANGAMANI NA SHETANI!! Kinachotakiwa ni kumuomba Mwenyezi Mungu ateketeze kizazi chote cha kifisadi ili kuinusuru Nchi!!

Kama kweli M/Mungu ataamua kuteketeza kizazi chote cha mafisadi tutakao baki wachache sana na wengi watakuwa watoto wadogo,coz tz ya leo hadi viongozi wa dini nao wamo kwenye huo mkumbo wa mafisadi.
 
Dr. kasema itumike njia ya amani kutatua mgogoro wa Wanamtwara! Sasa wanaosema mchochezi, kachochea nini hapo! Ama kweli kuipenda serikali ya CCM, inahitaji uwe na moyo wa plastiki!!
 
Unatapatapa mithili ya mtu anayekata roho!! Yaani huyo Kikwete anayeua waandishi wa habari na kungo'a watu kucha na meno bado unamuona yupo karibu na Mungu? Mungu yupi? Mbona kila mtu anajua analindwa na majeshi ya majini ya Sheikh Yahya!!!

Mkuu huyo mwenyewe ni lipepo! Na ndo maana anamshangilia mtu wa tabia yake...
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1369378631504.jpg
    uploadfromtaptalk1369378631504.jpg
    61.6 KB · Views: 47
Ardhi yao au ya watanzania wote?Kile kipande cha Mnazi Bay hakimilikiwi na wana Mnazi Bay, au wana Mtwara , au wana Kanda kusini bali inamilikiwa na watanzania wote kwa ujumla.
Anza kwa kujifunza agrarian laws za nchi yako.....
Siasa nyingi mno hutandaza fikra. .... your whole thought process is corrupted,.

Kwani wanamtwara siyo watanzania? Malalamiko ya wanamtwara ni ya watanzania wote. Na mikataba tunayotaka yawekwe hadharani kama nilivyosema siyo ya mtwara tu bali nchi nzima. Kwa hiyo, swali langu liko pale pale, kwa nini ccm hawataki kuonesha mikataba ya uchimbaji wa gesi kwa wanamtwara na watz wote wakati yanachimbwa katika ardhi yao/yetu (sisi watz +wanamtwara pamoja na wewe kobello)
 
Jambo lolote limalozungumzwa sirini sio jema kwa umma.
Vivyo hivyo, mikataba yoyote ambayo terms and conditions zake zinafichwa na kufanywa siri si mizuri kwa umma
 
Kawakamate kwanza hawa!
 

Attachments

  • uploadfromtaptalk1369378997052.jpg
    uploadfromtaptalk1369378997052.jpg
    21.7 KB · Views: 59
Binafsi sikubaliani na dhana ya wananchi kupuuzwa na kwenda kuharibu mali za wenzao ambao kuzipata kwao ni kwa kuunga unga na kuua watu wengine. DR. Slaa pia anahusika kutokana na kauli zake na za chama chake katika kutia utambi wananchi, lazima akumbuke nchi ni ya watu wote na atabeba dhamana katika kila jambo linalotokea leo. Kama watu wanabifu na JK basi wawaambie wakachome nyumba zake na si za raia wasio na hatia.

Dr. Slaa na baadhi ya wabunge wa chama chake hawahubiri amani na kuona vurugu ndio mtaji wao kisiasa, lazima wakumbuke wanaweza chukua nchi bila chokochoko wanazozileta wao na washirika wao. Tunawaona na kukiona mnachokifanya mkumbuke na nyinyi hamtokuwa salama pia kikichafuka.

Kama hausiki alipaswa kuyasema hayo hakiwa Mtwara na sio kwao huko wanapopikia mizengwe kila mara.
 
Kwani wanamtwara siyo watanzania? Malalamiko ya wanamtwara ni ya watanzania wote. Na mikataba tunayotaka yawekwe hadharani kama nilivyosema siyo ya mtwara tu bali nchi nzima. Kwa hiyo, swali langu liko pale pale, kwa nini ccm hawataki kuonesha mikataba ya uchimbaji wa gesi kwa wanamtwara na watz wote wakati yanachimbwa katika ardhi yao/yetu (sisi watz +wanamtwara pamoja na wewe kobello)
Siyo mikataba yote ni lazima iwekwe wazi. Kibiashara baadhi ya makampuni hayataki kuweka mikataba yao public ....kuna mikataba ya kijeshi kati ya serikali (hao IMF na WB wanashupalia hili) na serikal au na mashirika binafsi, na haiwekwi public.
Hata hivyo, linalojengwa ni pipeline, sasa wewe unatyaka mkataba gani? Wakujenga pipeline?? AU WA MATUMIZI YA GESI?? Mimi bado sijaelewa tatizo ni nini hasa.
 
  • Thanks
Reactions: kix
DK.SLAA:Yanayotokea Mtwara ni matokeo ya umaskini ambao CCM imewaletea wananchi, Mtwarawanakumbuka ya Mwadui, Geita na North Mara.Wanayakataa. Wanapenda amani, wanaheshimu misingi ya Taifa letu lakini wanapinga gharama ya amani hiyo kuwa umaskini wa wengi na utajiri wa wachache.
 
Ni kweli kabisa wanajua kabisa hiyo gas ni kwa manufaa ya wakubwa ambao tiyari wameshachuka 10% zao ndio maana wanatumia nguvu sana.lakin hakuna jeshi litakaloweza kushida nguvu UMMA
 
DK.SLAA:Yanayotokea Mtwara ni matokeo ya umaskini ambao CCM imewaletea wananchi, Mtwarawanakumbuka ya Mwadui, Geita na North Mara.Wanayakataa. Wanapenda amani, wanaheshimu misingi ya Taifa letu lakini wanapinga gharama ya amani hiyo kuwa umaskini wa wengi na utajiri wa wachache.
JK anazidi kuweka historia kwa kutumia nguvu kupitiliza, wakati akiwa waziri wa madini, watu ambao ni wachimbaji wadogo wadogo takilibani 36 walikufa, kwa kufukiwa kwenye mashimo yao, Bulyankulu ili kuwapisha Barrick, mpaka sasa hakuna hata barabara ya Lami kuelekea kwenye mgodi huo 70km, sasa huu ndi uwekezaji gani?

Wanamtwara wasijekuwa kama wa Shinyanga, stand up for your right...
 
Back
Top Bottom