Dr Slaa: Mtwara wamepuuzwa!

Dr Slaa: Mtwara wamepuuzwa!

Tatizo lako wewe unaongea sana hebu tupe mchanganuo wa michango ya M4C toka muanze kuwachangisha wananchi mmekusanya kiasi gani ni matumizi yake.

Mimi nilikuuliza kwa nini serikali inaficha mikataba, wewe wewe ukatoa majibu haya in red abve. Kwa hiyo, kwa kauli yako, wewe umekubali kwamba kuna wizi kwenye mikataba inayofichwa na unadhani mimi nisihoji sana wizi wenu kwa kuwa unadhani na sisi tuko kama ninyi.
 
HUO WOTE NI UCHOCHEZI NA KILA ASIYEKUWA NA AKILI ANAUPOKEA NA KUUFANYIA KAZI MATOKEO YAK NI KUPOTEZA MUDA, KUKARIBISHA NJAA, KUUMIA NA MENGINE MNGI YA HATARI YA KUDHURU MWILI. DR. AMA PADRI WILBROAD SLAA HANA JIPYA NA HATEMBEI KATIKA NJIA ILIYONYOOKA, YEYE HUJIFICHA NYUMA YA MATATITIZO YA WATU.

TUWENI WAKWELI KUWA WANACHOKIFANYA WANA MTWARA KWA KUSHAWISHIWA SI SAWA MAANA WANAOWASHAWISHI HAWAKUWMO KWENYE VURUGU WAO NA HAWANA MAUMIVU YOYOTE YA MISULI YA KURUSHA MAWE NK WAO MIDOMO TU NA KUWATUMA WANYONGE AKAPAMBANE NA ASKARI. MATOKEO YAKE NI KUUMIZANA WENYEWE KWA WENYEWE NA KUJENGANA UADUI
Mfano.........Unachoma duka la mtu nyuma yako kuna mtu anakuona ambaye ni ndugu ama mwenye Duka baada ya vurugu kutulia utabaki salama NI lazima atalipiza ni kwa naman gani WEWE na MIMI hatujui. Unachoma Gari la wagonjwa, nyumba ya mtu ambaye mke wake ama hawala tu ni Askari..............anahusikaje????????? Watanzania hasa kama unaamini kuwa unazo akili timamu hayan si ya kushabikia. Toa wazo mbadala ili uwasaidie.

Inaelekea wewe huna akili na unaedneshwa kama roboti na watu wengine lakini kama unaakili zako na unaamua mambo yako fahamu kwamba wana mtwara hakuna anayewashawishi wameamua wenyewe wanataka serikali iheshimu wananchi,wanataka wafahamishwe deni la kujenga bomba litalipwa na nani,wanataka kufahamu kwa nini gesi akachatuliwe kinyerezi na isiwe mtwara,Serikali ingekuwa na busara ingetumia nguvu zake zote za ezengeaji, wangeandaa vipindi vya television na radio kuna FM nyingi hapo mtwara kila jioni wangeweka muda wa majadiliano ili anagalau wananchi wengi washiriki,wangeandaa mikutano kila kata kuongea na wananchi,serikali imewapuuza wananchi, na watu kama wewe unadhani kwa kuwa wao ni maskini,wengi hawakusema basi hawana maamuzi ya kutenda ,na kufanya
Mahala popote mwanadamu anapoona anadharauliwa,hasikilizwi,anapuuzwa,huwa anafanya kama waliyofanya wana mtwara na hakika serikali imejitakia kwa kuwa serikali Kiburi
 
Frankly speeking; Kwenye mikataba ya gesi ambayo ilishasainiwa kutakuwa kuna mambo ambayo waliosaini wanajua yakifahamika wazi kwa jamii itawagharimu na dhio maana pamoja na watu kushinikiza mkataba iwekwe wazi, serikali inakwepa na italikwepa hili mpaka tone la mwisho.Tusubirie!

Nina uhakika mpaka sasa serikali inatambua tayari mistake ambayo ilishafanyika lakini kazi ipo kwenye kurudisha mambo sawa na kuhakikisha yanakwenda vizuri bila kuvujisha kile kilichoko kwenye mikataba ili kuwanushuru waliosaini mikataba hiyo.Kwa hiyo mengine haya tu ni mbio za sakafuni ila tatizo sugu liko hapa.
hapa kuna suala la ujenzi wa bomba na pia suala la uchimbaji gas.kwamaana kuwa suala la ujenzi wa bomba halihusiani na la uchimbaji.

Kama inatakiwa mikataba ya uchimbaji gas iwekwe hadharani,ni vizuri,lakini mtu hawezi kurukia tu kwamba kuna namna kwenye hiyo mikataba bila kuwa na evidence.
 
Wanadhani suluhisho ni kupeleka wanajeshi waue raia!hao wanajeshi watakaa huko mpaka lini?ukiona serikali inatumia jwtz kuwadhibiti wananchi wanao dai haki zao,ujue imekosa uhalali wa kuongoza nchi.Tatizo hawa mafisadi wameshakula hela ya mchina (mradi ujenzi wa bomba la gesi)hivyo wanashindwa la kufanya.
hyaya ni mawazo mfu yaliyokosa uhai wa dhati,mbona hujaongelea chama kinachochea vurugu na kupanga mauaji kinauhalali gani wa kuendelea kuwa chama cha siasa.
 
huyu mzee anahangaika tu amechoka kuchochea suala la kuchinja sasa kahamia kwingine,swali dogo hivi mzee slaa na jk nani aliyejitenga na mungu,kwa sababu mzee slaa aliasi dini na kufanya uovu mwingi ndani ya kanisa sasa uko wapi uadilifu wa slaa.
Mkuu nilitegemea busara kutoka kwako kuchangia post hii. Sidhani kama wana mtwara na Watanzania wote tunahitaji suala hili la Mtwara kujibiwa kwa maneno ya kashfa na kejeli kama unazotoa. Wanachotaka wananchi wa Mtwara na Watanzania wote ni kujua namna watakavyonufaika kwani katika uwekezaji wowote wanufaikaji wa kwanza wanapaswa kuwa wananchi wote,
 
hapa kuna suala la ujenzi wa bomba na pia suala la uchimbaji gas.kwamaana kuwa suala la ujenzi wa bomba halihusiani na la uchimbaji.

Kama inatakiwa mikataba ya uchimbaji gas iwekwe hadharani,ni vizuri,lakini mtu hawezi kurukia tu kwamba kuna namna kwenye hiyo mikataba bila kuwa na evidence.
Mkuu unachoongea ni kweli ila kama mikataba ingekuwa streight foward; basi hata bunge lingepewa liweze kuidurusu bila ya usumbufu.Kuhusu kurukia kwenye bomba; kuna mambo mtamuka yanayowasukuma watu kurukia kuho ikiwemo kukosa taarifa sahihi, hasira za muda mrefu zinazosababisha na mambo kadhaa, msukumo makundi, Historia, siasa, na jinsi serikali inavyoishughulikia hali ya mammbo.
 
Tatizo lako wewe unaongea sana hebu tupe mchanganuo wa michango ya M4C toka muanze kuwachangisha wananchi mmekusanya kiasi gani ni matumizi yake.[/QUOTE]

Mimi nilikuuliza kwa nini serikali inaficha mikataba, wewe wewe ukatoa majibu haya in red abve. Kwa hiyo, kwa kauli yako, wewe umekubali kwamba kuna wizi kwenye mikataba inayofichwa na unadhani mimi nisihoji sana wizi wenu kwa kuwa unadhani na sisi tuko kama ninyi.
hivi sheria inasemaje kuhusu hiyo mikataba.sheria inataka mikataba iwekwe wazi au inasema nini?.
 
linalojengwa ni bomba la kupeleka gesi kwenda kutumika kwenye viwanda vilivyopo dar es salaam,na pia matumizi mengine kama kupikia wananchi na pia kuzalishia umeme utakaoingia kwenye grid ya taifa...sasa hapa mrahaba sijui mrabaha unatokea wapi?na gesi itakayopitia hilo bomba ni asilimia 6 ya gesi yote.

Pia ni wazi kuwa kama kutakua na sababu ya kuexport kupeleka nje meli zitapakia gesi hapohapo mtwara ,kwani itakua ni upuuzi gesi iende dar halafu ndo ipakiwe melini kwenda nje.
Sasa kinachonishangaza hapa ni kuwa ujenzi wa bomba unahusiana

vipi na mrahaba
.

Nilikuwa namaana hii.

1. Je tunaendelea kupewa asilimia za mrahaba chini ya 5% na 95% kuondoka na wawekezaji? -Migod ya madin nk

2. mkuu kobello unafahamu tutapata % ngapi kutoka mapato ya gesi/- Wananchi wanaozunguunka miradi hii

watafaidikaje? hatakama wamiliki watakuwa serikali bado wahusika wakuu ni wanachi wa maeneo husika

Mikataba ya madini inayofichwa - Mirahaba na faida zingine na gesi kwa upande mwingine kwapamoja kwenye mstari mmoja na kwa kifupi zaidi, haikuwa sahihi katika kuweka uwiano wa kueleweka vema

Asante kwa kuniweka sawa mkuu.
 
hapa kuna suala la ujenzi wa bomba na pia suala la uchimbaji gas.kwamaana kuwa suala la ujenzi wa bomba halihusiani na la uchimbaji.

Kama inatakiwa mikataba ya uchimbaji gas iwekwe hadharani,ni vizuri,lakini mtu hawezi kurukia tu kwamba kuna namna kwenye hiyo mikataba bila kuwa na evidence.


Mkuu

Evidence mwananchi atazitoa wapi? waanike mikataba then tujiridhishe na hapo ndipo penye evidence ya kuibiwa au hapana. Kwanini inafichwa? na kwa faida ya nani?

1. Je unafaham ujenzi wa bomba unagharama stahiki kulingana na standard za kimataifa kwa mita au kwa kilometer ni kiasi gani? tutajuaje kama tunalipa sahihi au gharama zimekuwa elevated kama za rada? nini mtazamo wako.

2. Nakatika kuchimba hiyo gesi je tumejenga mazingira gani ya

a) Kimapato kuhakikisha watanzania wanafaidika na uwepo wa wawekezaji hao au uchimbaji wa gesi hiyo?

b) Watanzania wanazunguuka maeneo hayo wanafaidikaje kwa uwepo wao na tunajiepushaje na uchafuzi wa mazingira haijalishi ni kwa vipi lakini lazima kutakuwa na athali za kimazingira hata kama hii ni gas.
 
Frankly speeking; Kwenye mikataba ya gesi ambayo ilishasainiwa kutakuwa kuna mambo ambayo waliosaini wanajua yakifahamika wazi kwa jamii itawagharimu na dhio maana pamoja na watu kushinikiza mkataba iwekwe wazi, serikali inakwepa na italikwepa hili mpaka tone la mwisho.Tusubirie!

Nina uhakika mpaka sasa serikali inatambua tayari mistake ambayo ilishafanyika lakini kazi ipo kwenye kurudisha mambo sawa na kuhakikisha yanakwenda vizuri bila kuvujisha kile kilichoko kwenye mikataba ili kuwanushuru waliosaini mikataba hiyo.Kwa hiyo mengine haya tu ni mbio za sakafuni ila tatizo sugu liko hapa.

Mkuu pesa ya USWIZI tayari ilionekana ilitokana na mikataba ya mafuta na gesi hakuna kupeppesa macho.serikali hata muwachinje kuweka hadharani mikataba ng'o hilo msahau.hiyo ni sawa na kuwakabidhi kisu halafu waambie wajichinje mmoja bada ya mwingine.May nguvu ya umma ifanye kazi
 
tatizo la macdm ni kujiona mnajua kila kitu,mawazo ya kibavicha.

Na tatizo la CCM ni kujiona hamjui kila kitu....ndo maana hata mwenyekiti wenu hajui kwa nini TZ ni maskini!
 
Huyu naye apunguze unafki kidogo,lakini ndiko kwenye siasa panamfaa, maana dini ilimshinda pinda alikwenda mtwara akaa nao na kufikia muafaka na rais ali adress issue hii kwa public through speech yake ya mwezi,sasa tunataka wafanye nini zaidi? Jk alisema kama kunakuwapuuza watu wa mtwara basi yeye atakuwa mtz wa mwisho kufanya hvyo. Huyu slaa aangalie sana kauli zake maana ikitokea bahati mbaya wakaingia ikulu watu wanataraji mabomba ya maziwa

Sent from my BlackBerry 9360 using JamiiForums

Jifunze kufanya utalii kwa kutembelea nchi yako ya Tanzania kisha nchi nyingine za Afrika na kutazama sehemu au miji ambayo ni kuna potential resources ikoje....nadhani utakuwa umefunguka kifikra!
 
Dr.m Slaa siwezi kumshangaa kwa kauli yake hiyo.

Lakini NAMLAUMU SANA JK KWA "UJINGA" WAKE WA KUDHANI KILA KITU NI KAULI INAYOPITA AU NI UPEPO UNAPEPEA NA UTAPITA.

MARA BAADA YA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2010. DR. SLAA ALIKUWA ANATOA KAULI NYINGI ZA KULETA UCHOCHEZI MOJA YA KAULI HIYO ALIWAHI KUSEMA KUWA ATAHAKIKISHA NCHI HII HAITAWALIKI" NA MATOKEO YAKE TUNAYAONA.

INGEKUWA NCHI YENYE RAIS MAKINI NA MWELEWA KWA KAULI YA DR. SLAA YA KUHAKIKISHA NCHI HAITAWALIKI NI UHAINI ANGEKAMATWA NA KUWEKWA KIZUWIZINI NA HATIMAE ASEME MAANA YAKE NINI ANAPOSEMA NCHI HAITAWALIKI. NA ANGEHUSISHWA KWA KILA JAMBO LINALOLETA MATATIZO YA KIULINZI NA KIUSALAMA KATIKA NCHI. LKN MASKINI RAIS WETU PENGINE ANADHANI UHAINI NI MTU KUCHIKA BUNDUKI NA KWENDA KUPIGANA VITA ILI APINDUE NCHI, MASIKINI RAIS WETU HAJUWI KAULI INA NGUVU KULIKO HIYO BUNDUKI.

Dr.Slaa hakusema atahakikisha nchi haitawaliki,ndo maana JK ajafanya utakayo...wewe ndo hujaelewa.
 
Dr.m Slaa siwezi kumshangaa kwa kauli yake hiyo.

Lakini NAMLAUMU SANA JK KWA "UJINGA" WAKE WA KUDHANI KILA KITU NI KAULI INAYOPITA AU NI UPEPO UNAPEPEA NA UTAPITA.

MARA BAADA YA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2010. DR. SLAA ALIKUWA ANATOA KAULI NYINGI ZA KULETA UCHOCHEZI MOJA YA KAULI HIYO ALIWAHI KUSEMA KUWA ATAHAKIKISHA NCHI HII HAITAWALIKI" NA MATOKEO YAKE TUNAYAONA.

INGEKUWA NCHI YENYE RAIS MAKINI NA MWELEWA KWA KAULI YA DR. SLAA YA KUHAKIKISHA NCHI HAITAWALIKI NI UHAINI ANGEKAMATWA NA KUWEKWA KIZUWIZINI NA HATIMAE ASEME MAANA YAKE NINI ANAPOSEMA NCHI HAITAWALIKI. NA ANGEHUSISHWA KWA KILA JAMBO LINALOLETA MATATIZO YA KIULINZI NA KIUSALAMA KATIKA NCHI. LKN MASKINI RAIS WETU PENGINE ANADHANI UHAINI NI MTU KUCHIKA BUNDUKI NA KWENDA KUPIGANA VITA ILI APINDUE NCHI, MASIKINI RAIS WETU HAJUWI KAULI INA NGUVU KULIKO HIYO BUNDUKI.

Naomba unieleweshe kwa vile binadamu tuna viwango tofauti vya kuelewa. Nilifuatilia sana uchaguzi wa 2010 na hata sasa mimi ni mfuatiliaji mzuri wa mambo ya siasa nchini. Hata hivyo, hata siku moja sikumsikia Dr. Slaa akisema kuwa 'atahakikisha nchi haitatawalika'. Labda katika ufuatiliaji wangu nilikosa fursa ya kusikia hayo. Unaweza kuniambia aliyasema hayo lini na wapi?
 
Msihukumu hapa msije mkahukumiwa hayo ya kuchambua watu, kama anakwenda msikitini au kanisani wala hayasaidii hakuna aliye msafi jamani.
 
Kwa hali ilivyo sasa hapa nchini, kuna viongozi kadha kwenye jamii zetu wameishiwa kabisa mawazo na hawana jipya kabisa, kutokana na hali hiyo wamebaki kujitutumua kwa kusikilizia matukio ili na wao waonekane bado wamo kumbe ni mfa maji haishi kutapatapa.

Viongozi hawa wanakaa kutwa nzima kuombea matukio kama haya ya kuatarisha amani ili tu na wao wajizolee umaarufu wa kisiasa na waonekane wapo upande wa wananchi, katika kutimiza azma yao hiyo wana hakikisha wana jenga chuki kati ya wananchi na viongozi wao.

Dr Slaa juzi hapa kwenye sakata la gesi huko Mtwara, badala ya kutoa kauli kama kiongozi tena wa chama kikubwa cha ushindani, ndio kwanza ana rudia ile kauli yake ya nchi haita tawalika. Huyu babu amedhihirisha kuishiwa mawazo mapya na anabaki kukukuruka tu kwa vitamko vyake visivyo na tija kwa taifa.

Dr Slaa kwenye sakata la gesi ukae kimya na uiache serikali iliyopo madarakani ambayo kimsingi ndio imeingia mkataba wa kulinda usalama wa wananchi na mali zao iweze kufanya kazi yake hiyo. Serikali hii ndio yenye jukumu la kusimamia raslimali za nchi na kuhakikisha zinafaidisha raia wote nchi hii.
 
Binafsi sikubaliani na dhana ya wananchi kupuuzwa na kwenda kuharibu mali za wenzao ambao kuzipata kwao ni kwa kuunga unga na kuua watu wengine. DR. Slaa pia anahusika kutokana na kauli zake na za chama chake katika kutia utambi wananchi, lazima akumbuke nchi ni ya watu wote na atabeba dhamana katika kila jambo linalotokea leo. Kama watu wanabifu na JK basi wawaambie wakachome nyumba zake na si za raia wasio na hatia.

Dr. Slaa na baadhi ya wabunge wa chama chake hawahubiri amani na kuona vurugu ndio mtaji wao kisiasa, lazima wakumbuke wanaweza chukua nchi bila chokochoko wanazozileta wao na washirika wao. Tunawaona na kukiona mnachokifanya mkumbuke na nyinyi hamtokuwa salama pia kikichafuka.

Kama hausiki alipaswa kuyasema hayo hakiwa Mtwara na sio kwao huko wanapopikia mizengwe kila mara.

Mbona kwenye 'pati kakasi' yenu mmesema Membe ndo anahusika? Au mnaweweseka kutafuta mchawi?
 
Huu ni mtihani mwingine wa kifikra kwa slaa, hivi anadhani ataendelea kuwahadaa wananchi kupitia matatizo yao hadi lini??? Kwa hiyo anashangilia vifo vya askari na mali za umma zilizoharibiwa???

"Kabla ya kutoa kauli hiyo Dk. Slaa aliwaomba wananchi wasimame kwa muda wa dakika moja, kuomboleza vifo vilivyotokea mkoani Mtwara."

Hapo waka kasema kafurahia askari kufa?

“Ni jambo la aibu kuwapiga mabomu wananchi wanaodai kunufaika na rasilimali za nchi yao hapa kunahitajika elimu ya kuwafahamisha haki zao ni zipi na siyo mabomu.,alisema Dr Slaa.


Hapo Slaa kaongea hadaa gani?

Acheni upuuzi wenu bwana kauli za Dr Slaa wapi zinaonyesha hadaa!! mmezoea kuwahadaa wananchi mnageuza geuza mambo! mlaaniwe!?
 
Sidhani kama kiongozi uliyemtaja anaendana na kichwa cha "thread" yako. Niakiangalia na kuchambua kutoka niliposimama namuona kama kiongozi anayewakilisha mawazo ya walio wengi (hata kama binafsi siyakubali) nchini na ndio maana amepata ufuasi mkubwa kila aendapo nchini.
 
laana kutoka kwa nani..?

Hivi bado mnadhani slaa alishinda ... Znz kura hazikutosha.. Miji ya pwani hana umaarufu.. Labda kaskazini huko

Naona akili zako hazina tofauti na Wassira zee la kulalala bungeni na kusema uongo. Muwache rais wetu Dr.W.Slaa atulie. Muda wenu ukifika wa kujielezea, mafisadi wote mtaozeana Jela tukianzia na huyu Kikwete na Mkapa.

Subirini Dr.W.Slaa aingie rasmi Magogoni kama hamjaikimbia hii nchi, na tutawafuata popote mlipo na account zenu zote za nje zitafungwa. Hiyo siku inakuja na haipo mbali
 
Back
Top Bottom