Dr Slaa: Mtwara wamepuuzwa!

Dr Slaa: Mtwara wamepuuzwa!

Hivi na wewe unafuata dini gani ambayo inakufundisha uwongo? Swala la kuchinja bila aibu unasema alichochea Dr.Slaa? Kwa huyo wewe unajilidhisha kuwa huyo unayemshabikia hana dhambi au makosa. Haya ndugu yangu lakini Mungu hufanya kazi kupitia kwa watu. Mnawatesa WanaMtwara badala ya kuwasiliza na kuwaelimisha pale walipopotoka. Hakuna maendeleo bila maelewano na malidhiano. Nguvu ni swala la muda tu
sina dini ila namwamini mungu mmoja wangapi mnaenda kanisani na misitini halafu waovu wakubwa.
 
Wewe ni walewale, badala ya kutatua tatizo unashari kuongeza tatizo. To hell maCCM

we umeona kauli ya slaa itatatua tatizo la mtwara ni kauli ya uchochezi na inatakiwa akamatwe haraka sana anamwaga petrol kwenye moto
 
kwanza anatakiwa akamatwe kwa uchochezi na kauli mbiu zake za uchochezi mfano nchi haitatawalika,mpaka kieleweke.slaa ni janga la kitaifa.[/QUOT

What are you waiting.

Hizi ni akili za Nchimbi na Kikwete,watu waliopoteza uzalendo ndani ya mioyo yao.

Tumesikia maneno ya ajabu,watu wanaotishia Amani wakamatwe wanangoja nini,kama watu hao wapo nje na ndani ya nchi.

Wanafikiri bado hii ni zama za kutawala watu kwa kuwapa vitisho
njia hii imepitwa n wakati.Wapo watu hapa kwa sababu wapo ili kupindisha ukweli daima wamekuwa wa kwanza kupindisha maneno.,
niseme tu.

HATIMAE HAKI ITASHINDA UOVU.
 
Umeshatubu kuhodhi fedha za ujio wa papa? ,, Pia tambua mdomo wako una madhara sana ktk Taifa hili unapotoa kauli ambazo zinapelekea kuvunjika kwa Amani.

Kama wewe siyo mwongo na mzushi tuambie ilikuwa sh ngapi? Alihojiwa na kikao gani? Lini? wapi? walimpa adhabu gani? Jibu hoja usilete uwongo, miaka 50 ya uhuru mmewafanyia nini watu wa mtwara? HIYO ndo hoja ya Dr Slaa.
 
Niende Chadema kwani mimi Kinabo au Kweka.

Kwa hiyo, yale majimbo waliyoshinda ccm pale moshi tuseme kuwa wanaccm walipigiwa kura na wakwere kwa kuwa akina kinabo na Kweka wako chadema wote.
Tuambie Kwa nini mmewasahau watu wa mtwara, ndo mada ya uzi huu.
 
huku pwani ni wewe na babako ndio hammkubali. Kwingine kote tunamkubali

Anazungumzia pwani ya wapi wakati Chadema imeshinda kijiji cha Mwanzo mgumu, kata ya Msimbu, wilaya ya Kisarawe mkoa wa pwani miezi michache iliyopita? Au hajui kwamba walichakachua jimbo la kibaha pwani mwaka 2010?
 
Watu wana protest mpaka wanakufa kudai haki zao wewe unasema hawajui haki zao, wapewe elimu.

Viongozi wetu wanapokosea ni kutudhania Wanachi ni majuha wa kutupwa, Kikwete anasema vurugu ni za kuchochewa, yani sisi wenyewe wananchi anaamini hatuwezi kupinga mambo fyongo mpaka tuamshwe, tuchochewe.

Slaa nae, ungedhani angekuwa na falsafa tofauti kuhusu uelewa wa Wananchi, lakini nae anasema Wananchi hatujui haki zetu tupewe elimu!


Kwenye elimu anayosema Dr.Slaa hana maana kuwa Wanamtwara hawajaelimika bali anasema serikali itoe elimu kuhusu maslahi ya Wanamtwara yatakayotokana na uvunaji gesi baada ya kuwasiliza kwanza na kukidhi matwakwa yao na sio kuwalisha yale ambayo hawajatamka. Serikali inabdidi iende kwa unyenyekevu eneo la tukio kuliko kutumi magazeti ambayo watu hawawezi kuyasoma, kuyaona achalia mbali lugha ngumu iliyotumika
 
Huu ni mtihani mwingine wa kifikra kwa slaa, hivi anadhani ataendelea kuwahadaa wananchi kupitia matatizo yao hadi lini??? Kwa hiyo anashangilia vifo vya askari na mali za umma zilizoharibiwa???

Hao askari washenzi wameuawa na Dr. Slaa? Si na wao walikuwa wanaenda kuua?
 
kutokana na udhaifu wa JK katika maamuzi ndiyo maana imefikia mahali hapa Tanzania kila mtu anaona kuwa anaweza kuwa Rais. Suala kama hili la Mtwara mbona lilikuwa rahisi sana, elimu tu kuhusiana na suala hilo la gesi na ahadi alizowaahidiwana wa Mtywara basi, tusingefika hapa tulipo.
 
Hizo kura laki 2 za znbar nazo unahesabu? Kwa taarifa yako jk aliiba kura zaidi ya million moja. Mimi naamini siri itafichuka tu huko tuendako.

Ni zaidi ya mil moja mkuu, ni nyingi, kwanza ushindi wake ni debatable.
 
Dr.m Slaa siwezi kumshangaa kwa kauli yake hiyo.

Lakini NAMLAUMU SANA JK KWA "UJINGA" WAKE WA KUDHANI KILA KITU NI KAULI INAYOPITA AU NI UPEPO UNAPEPEA NA UTAPITA.

MARA BAADA YA MATOKEO YA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA 2010. DR. SLAA ALIKUWA ANATOA KAULI NYINGI ZA KULETA UCHOCHEZI MOJA YA KAULI HIYO ALIWAHI KUSEMA KUWA ATAHAKIKISHA NCHI HII HAITAWALIKI" NA MATOKEO YAKE TUNAYAONA.

INGEKUWA NCHI YENYE RAIS MAKINI NA MWELEWA KWA KAULI YA DR. SLAA YA KUHAKIKISHA NCHI HAITAWALIKI NI UHAINI ANGEKAMATWA NA KUWEKWA KIZUWIZINI NA HATIMAE ASEME MAANA YAKE NINI ANAPOSEMA NCHI HAITAWALIKI. NA ANGEHUSISHWA KWA KILA JAMBO LINALOLETA MATATIZO YA KIULINZI NA KIUSALAMA KATIKA NCHI. LKN MASKINI RAIS WETU PENGINE ANADHANI UHAINI NI MTU KUCHIKA BUNDUKI NA KWENDA KUPIGANA VITA ILI APINDUE NCHI, MASIKINI RAIS WETU HAJUWI KAULI INA NGUVU KULIKO HIYO BUNDUKI.

Parochial thinking and arguing at the dimension of your nose. Kwanza unalazimisha timing na tamko la nchi haitawaliki ili ukidhi matakwa yako ambayo nachelea kuyahita devilish. Kuenedelea kugangania kauli ya nchi haitawaliki ni kutaka kuficha udhaifu wa serikali unaoonekana mchana kweupe. Kauli hiyo ndiyo inafanya polisi wambambike mtu kichwa cha mtu, wapakie bhangi kwa gari la polisi/umma, washiriki kusindikiza bidhaa ya magendo ili kukwepa kodi, wapige watu wasio kuwa na hatia virungu na mabomu? Nguvu nyingi ya vyombo vya dola inatumika katika vitu vya ajabu badala ya kutumi elimu, ethics na skills kulinda usalama wa raia. Nimesahau utoshwaji wa twiga na meno ya ndovu. Hii yote ni kauli ya Dr.Slaa? Kama ni kweli basi nchi hii haipaswi kuwepo
 
Kwa hiyo watu wasiokuwa watumishi wa kanisa au misikiti wamejitenga na mungu? ushauri wa Dr ndio suluhisho la kidiplomasia na si risasii..listen them! Kuwe na transparency kwenye mikataba watu waelewe faida zake...simple! USHIRIKISHAJI UMMA-Maendeleo kwa kila mtu!
au umesahau Mtwar wengi ni CUF na slogan yao inasema HAKI SAWA KWA KILA MTU!!

Wakoloni walipokuja Africa na kwa tamaa zao za kuzoa Mali za Waafrika zilipozidi,walitunga Mkakati wa kuwamaliza waafrika taratibu ili angalau kupunguza resistance ya kuwakataa.....ili wabaki waafrika wachache...na walifanya hivyo kwa kuja wenyewe na kuwaua waafrika,
Baadaye wakagundua njia ya Kisayansi zaidi,kuwagombanisha waafrika ili waanze kupigana wenyewe kwa wenyewe...wao wakawa wanasaidia hili kwa kutengeneza silaha na kuwauzia makundi yote mawili yanayopigana

Walipoona waafrika wanapigana wenyewe kwa wenyewe,halafu likaja na balaa jingine la kupunguza kizazi cha waafrika kutokana na maradhi hasa ya Ukimwi....wakaona sasa inatosha,haina haja ya wao kutumia nguvu sana za kuwaua waafrika,kwani sasa mnauana na mnajiua wenyewe na ngono zembe...lengo lao la kuhakikisha kizazi cha waafrika kinavurugika na kinapotea linatimia.

SASA HIVI,WAMEKUJA NA MBINU MAHSUSI ZAIDI,HASA KATIKA NCHI ZILE WANAZIONA ZIKO STABLE SANA UTAWALA WAKE....MBINU HIZI NI KUWAINGILIA BAADHI YA MAKUNDI YA WATU KUPITIA MIGONGO YA WANAHARAKATI,VYAMA VYA SIASA,WAFANYABIASHARA WAKUBWA,VIKUNDI VYA DINI NA TAASISI NYINGINEZO,KUWEZA KULETA VURUGU NA CHOKOCHOKO MBALIMBALI KILA KUKICHA,KWA JINA LA "KUTETEA MASLAHI YA WANYONGE"!

NINASEMA KWAMBA,DHAMBI HII YA KUPANDIKIZA CHUKI KWA WANANCHI DHIDI YA SERIKALI YEYOTE DUNIANI,HATA KAMA ITAFANIKISHA LENGO LA KUWAWEKA WATU MADARAKANI,KAMWE HAITATOKA KWA WANANCHI VIZAZI NA VIZAZI.....UKIINGIA KWA UPINDE UTATOKA KWA UPINDE...UKIIINGIA KWA DAMU UTATOKA KWA DAMU!

Watu wanawashawishi Wananchi kufanya mambo ambayo wao tu ndio wanajua malengo halisi,wakiwahadaa wananchi kwamba watapata maisha bora......

Sakata la Mtwara kuna Watu ambao wanalala usiku na mchana wakiombea likuzwe na kukuzwa ili labda machafuko yatokee nchini na kuonyesha serikali iliyopo madarakani haifai......ili labda wananchi wachukie serikali yao,katika hali hiyo,makundi hayo yatapata ULAJI katika patashika hizo.

Na kinachonitia wasiwasi...kuna wasemaji na waandikaji na wakumbushiaji wazuri sana wa suala la Mtwara kuanzia hapa jukwaani mpaka mitaani,ambao ukifuatilia thread zao,utajua kwamba wao ndio pia wahamasishaji wakubwa sana na wazuri wa vyama fulani vya siasa hasa kunapokuwa na mikutano ya vyama hivyo......hili ni lazima mtu kama mimi linipe mwanga kwamba kuna vyama viko nyuma ya sakata hili,na lengo lao kubwa ni kuchochea mgogoro huu kwa faida yao wenyewe.....

Nina hakika kwamba watu wenye nia OVU na Taifa letu watashindwa....wawe wanatoka serikalini,wawe wanatoka katika makundi mengine,watashindwa....Tanzania ni ya kwetu sote....Tanzania ni nchi ya Kidemokrasia,ndio maana kila mmoja anafanya kwa raha zake anachokifanya sasa hivi...lakini daima siku zote ukweli hushinda....kundi lililo na ukweli katika vita hii ndilo litakaloshinda....hatutaki vurugu Mtwara.
 
Back
Top Bottom