Dr.Slaa live ITV akichambua hotuba ya Kikwete

Dr.Slaa live ITV akichambua hotuba ya Kikwete

Mama naona umeongezewa malipo hivi karibuni. Bunge zima la nchi limeona ESCROW ni utapeli wewe unakuja hapa kusema sio. Una tatizo kubwa la ufahamu!

Maazimio ya bunge ni manane yaliofikishwa kwa Rais wa Tanzania, nioneshe katika hayo maazimio manane linalosema escrow ni utapeli kama usemavyo wewe na Kikwete kalichukuwa hatua ipi katika hilo azimio lako la "utapeli".
 
huyu mtuhumiwa ni nouma sana,yani anamuita rais wetu Dear...!na anamshawishi asichukue hatua juu ya maazimio ya bunge.
 
kuna watu hapa mnajidanganya eti hawa jamaa wakikamata madaraka mambo yatakuwa safi kila mtu maisha yatanyooka,vijana wote watapewa kazi,chuoni mtasoma bure etc,itakula kwenu nawambia na maneno haya mtayakumbuka.
kazi watapata hawa kina salal sleep na wengine humu hawafiki hata 10,kisha wengine sahauni.
wewe tafuta faranga kivyako na wala usidhani huyo slaa atakusaidia kwa lolote
mkuu acha kujichekesha bure hapa mkuu, kwani kwa sasa vijana wote wamepewa kazi na serikali?
 
Maazimio ya bunge ni manane yaliofikishwa kwa Rais wa Tanzania, nioneshe katika hayo maazimio manane linalosema escrow ni utapeli kama usemavyo wewe na Kikwete kalichukuwa hatua ipi katika hilo azimio lako la "utapeli".

lakini hii ya "dear" unaionaje ustaadhat?
 
Msikilize Dr.Slaa live ITV akiongelea sakata la Escrow na hotuba ya Kiwete.

Dr.Slaa, anamlaumu raisi Kikwete kwa kukosa uzalendo kwa jinsi anavyoshughulikia sakata hili la Escrow na kumlaumu kwa kuvunja katiba.

Dr.Slaa amlaumu Kikwete kwa double standard.Yaani kumuondoa Tibaijuka kazini na kumuweka kiporo Muhongo.Pia, amehoji utaratibu wa kumuweka mwanasiasa kiporo.

Dr.Slaa anasema Kikwete anapuuza bunge na kwamba hivi sasa ni serikali inayolisimamia bunge na si bunge linaisimamia serikali.

Dr.Slaa anasema Seth anastahili kuwa amekamatwa kwa kugushi nyaraka na pia kutolipa kodi na kwamba raisi anafumbia macho.

Dr.Slaa anasema singasinga huyu ana uhusiano na Ikulu kwa muda mrefu na ndio maana hachukuliwi hatua.

Pia,Dr.Slaa ameishaangaa polisi kupewa msaada wa fedha na singa singa.

Dr.Slaa pia anashangaa raisi kuwasiliana kwa email na mtuhumiwa mmoja na huku mtuhumiwa huyo akimwita raisi "dear".

Dr.Slaa anungana na maaskofu kutaka uwajibikaji wa watuhumiwa wa sakata hili na pia ameungana na wanaosema raisi anapaswa kujiuzulu(Deus Kibamba ni mmoja wa watu waliotoa kauli kuwa, kwa sakata hili,hata raisi anapaswa kuondoka madarakani-Tanzania Daima la leo).

Dr.Slaa amemalizia kwa kusema hawana chuki binafsi na Muhongo wa raisi.

hapo kwenye nyekundu jamani.
 
Pesa za umma zinakaa akaunti ya escrow? wewe si umma? unaweka pesa zako escrow account?

Kikwete huwa hakisii.

Kama Yuda alimsaliti Yesu kwa vipande 30 vya fedha,basi si ajabu Faiza kutusaliti watanzania kwa mgao wa Escrow.
 
lakini hii ya "dear" unaionaje ustaadhat?

Asiyejuwa Kiingereza, neno "Dear" anaona ajabu sana.

Barua za Kiingereza za kibiashara karibu zote zinaanza na Dear. Cha ajabu ni nini?

Misukule mna taabu kweli kweli.
 
sipati picha siku slaa akishindwa kwa mara nyingine kwenye uchaguzi mkuu n sidhani kama rais ajae atamvumilia kama jk alivyomvumilia kwa miaka yote hii,kwani akileta za kuleta tena ataozea kizuizini,hii ndo nafasi ya pekee slaa kabakiza mwakani mida kama hii atakua kishasahaulika mda mrefu
 
Asiyejuwa Kiingereza Dear anaona ajabu sana.

Barua za Kiingereza za kibiashara karibu zote zinaanza na Dear. Cha ajabu ni nini?

Misukule mna taabu kweli kweli,
Mkuu JK anafanya biashara gani pale ikulu? Jamani nauliza tena huko ccm hakuna watu wasomi na wenye weredi wao wanaoweza kuitetea ccm hapa jamvini-hawa mapukupu akina Faiza,elungata na wengine mbona wanakizalilisha chama namna hii
 
Hahahaaa, Ticha bana, haifiki siku ukubali tu kuwa uliteleza? Hihihiiii.....

Heri ya Mwaka Mpya kwako na familia kwa ujumla. Mwaka wa mwisho wa Mpagani mpinga Kristo.

Naam, ananijuwa. Vipi, wewe hakujuwi?
 
sipati picha siku slaa akishindwa kwa mara nyingine kwenye uchaguzi mkuu n sidhani kama rais ajae atamvumilia kama jk alivyomvumilia kwa miaka yote hii,kwani akileta za kuleta tena ataozea kizuizini,hii ndo nafasi ya pekee slaa kabakiza mwakani mida kama hii atakua kishasahaulika mda mrefu

Unafikiri watamchaguwa agombee tena. Khaa, kwa lipi zaidi, babu ka flop huyo, kazi yake sasa hivi kuvizia na kudandia hoja.
 
Asiyejuwa Kiingereza Dear anaona ajabu sana.

Barua za Kiingereza za kibiashara karibu zote zinaanza na Dear. Cha ajabu ni nini?

Misukule mna taabu kweli kweli,

ustaadhat unaniangusha,kuna biashara gani kati Mhe. wa magogoni na mtuhumiwa wa Escrow?
 
Hayo matusi nilyoporomosha yako wapi?

Una tatizo binafsi? au ni chuki tu? Watanzania 80% juzi wameichaguwa CCM, umesahau, utaendelea kutuchukia sana tu lakini waliowengi hawaafikiani na wewe.

The first reaction to truth is hatred - Tertullian
Wanaichagua kwa ujinga tu na kutojitambua.Mimi naishi na mama yangu mzazi hapa nyumbani kwangu ila ukiongea nae kuhusu siasa atakueleza ccm imemlea.sasa jiulize kama ccm imemlea hapa kwangu anafanya nn? kwa mtaji huu utagundua wazazi wetu wanaichagua ccm si kwa kuipenda ila sababu ya ujinga tu.
 
Mkuu JK anafanya biashara gani pale ikulu? Jamani nauliza tena huko ccm hakuna watu wasomi na wenye weredi wao wanaoweza kuitetea ccm hapa jamvini-hawa mapukupu akina Faiza,elungata na wengine mbona wanakizalilisha chama namna hii

leo utaita hadi ukoo wako wote hapa,nashangaa sana injinia sijui na mwanauchumi unakua na upeo mfupi kiasi hiki.sasa unawaita ndo wakusaidie ama iweje?
unataka kila mtu aamini unavyotaka wewe,uende uishi korea ya kaskazin,hapa hapakufai
 
Back
Top Bottom