Dr.Slaa live ITV akichambua hotuba ya Kikwete

Dr.Slaa live ITV akichambua hotuba ya Kikwete

Anaichambua hotuba ya rais

UP DATE;

Aeleza kuwa makosa ya Muhongo pamoja na mengine ambayo hayajawekwa wazi alisimamia masuala ambayo ambayo ni jinai.

Jinai kwa;
i. kughushi nyaraka
ii. kukwepa kodi

Aituhumu ikulu kuwa mhuusika mkuu katika sakata hili kupitia msimamizi mkuu wa ikulu Ngurumo

-Asema wakati bunge lindili Rugemalila alikuwa akimtumia e-mail Kikwete kwa kumwita Dear JK.

Salute sana
 
Mtasumbuka sana kupotosha, lakini ukweli ni kwamba hoja zake ni nzito naujumbe umeshazama.
 
mbona hajazungumza kuhusu maaskofu walionufaika na fedha hizo? Mbona hajazungumza kuhusu benki ya mkombozi iliyofanikisha utolewaji wa fedha hizo? By the way dr slaa dhambi ya uzinifu inamuandama. Hana uhalali wa kuhoji makosa ya mwingine. Kwa uzinifu anaofanya mahala pake ni jehannam tu


jadili hoja kiongozi, sio personal attacks, sizani kama wewe msafi kuliko wengine wote
 
wala msidanganywe na hawa kina saraly sleep,hawa nao wanafukuzia tuvyeo iwapo jamaa yao atakamata madaraka,ndo maana unamuona ameshupalia kila siku escrow escrow,ana interest zake binafsi wala msidhani eti ana uchungu sana na nyie.
ndo maana hata muhongo wakimtoa kesho usidhani ndo watanyamaza,hawa wanataka madaraka watabuni kitu kingine ili mradi attetion ya watu iwe kwao.
ajenda hawana zaidi ya kulalamika na kuipaka matope serikali
 
Msikilize Dr.Slaa live ITV akiongelea sakata la Escrow na hotuba ya Kiwete.

Dr.Slaa, anamlaumu raisi Kikwete kwa kukosa uzalendo kwa jinsi anavyoshughulikia sakata hili la Escrow na kumlaumu kwa kuvunja katiba.

Dr.Slaa amlaumu Kikwete kwa double standard.Yaani kumuondoa Tibaijuka kazini na kumuweka kiporo Muhongo.Pia, amehoji utaratibu wa kumuweka mwanasiasa kiporo.

Dr.Slaa anasema Kikwete anapuuza bunge na kwamba hivi sasa ni serikali inayolisimamia bunge na si bunge linaisimamia serikali.

Dr.Slaa anasema Seth anastahili kuwa amekamatwa kwa kugushi nyaraka na pia kutolipa kodi na kwamba raisi anafumbia macho.

Dr.Slaa anasema singasinga huyu ana uhusiano na Ikulu kwa muda mrefu na ndio maana hachukuliwi hatua.

Pia,Dr.Slaa ameishaangaa polisi kupewa msaada wa fedha na singa singa.

Dr.Slaa pia anashangaa raisi kuwasiliana kwa email na mtuhumiwa mmoja na huku mtuhumiwa huyo akimwita raisi "dear".

Dr.Slaa anungana na maaskofu kutaka uwajibikaji wa watuhumiwa wa sakata hili na pia ameungana na wanaosema raisi anapaswa kujiuzulu(Deus Kibamba ni mmoja wa watu waliotoa kauli kuwa, kwa sakata hili,hata raisi anapaswa kuondoka madarakani-Tanzania Daima la leo).

Dr.Slaa amemalizia kwa kusema hawana chuki binafsi na Muhongo wa raisi.

Tunasubiri sakata ya bomba la gesi. Hapa ataondoka tu.
 
Hapana, wacha kudanganya, pesa ya umma toka lini ikakaa escrow?

Fedha hizi mwenyewe nani, umma au IPTL
Nianze kuelezea ya Escrow ni kitu gani, ni tofauti kidogo na akauti zetu tatu tulizozizoea, na akauti maalumu na kazi maalumu pia ikiisha na yenyewe inafungwa, inasimamia na wakala na wakala pia anajukumu la kumlipa mwenye fedha wakati ukifika.

Akaunti ikafunguliwa BoT kwa ajili ya kuweka tozo ya uwekezaji, zinahifadhiwa ili kutoa nafasi kwa pande mbili kushughulikia tofauti zao lakini kabla ya hapo TANESCO walikua wanalipa moja kwa moja.

Kimsingi fedha hizi ni za IPTL,
katika swali pesa za nani, mdhibiti wa hesabu alisema humu yawezekana zipo za umma pia zipo za IPTL, Nilipomuuliza maana, akasema zamani walikua wanalipa moja kwa moja lakini baada ya mzozo walikubaliana kwanza waziweke BoT.

Kama mgogoro ungetatuliwa na madai ya TANESCO yakakubali ya tozo kupunguzwa, kiasi kilichopunguzwa kuna pesa za TANESCO ambazo lazima zirudi kwa kiasi kilichopunguzwa. Bahati mbaya miaka saba baadae halikuwa limefanyika.

Mama naona umeongezewa malipo hivi karibuni. Bunge zima la nchi limeona ESCROW ni utapeli wewe unakuja hapa kusema sio. Una tatizo kubwa la ufahamu!
 
haa haa kwa kitendo chake cha kumuweka kiporo muhongo na kumchukulia hatua tibaijuka, ni kitendo cha kibaguzi na kinyume na katiba ya mwaka 1977. Yako mengi kikwete aliyo yafanya ya kuvunja katiba.

Usijitie ujuha kwa kujichekesha bila mpango, umeulizwa "kavunja katiba kifungu namba ngapi ?"
 
Hakuna sababu yoyote ameamua tu ila ukweli unabaki pale pale kuwa ni pesa za IPTL mengine ujinga tu.
haa haa, kuna kitu kisicho na sababu? Je tangu lini CAG anakagua hela za binafsi? Rais kikwete kwa maamuzi haya ya escrow amethibisha pasipo shaka kazi ya urais imemshinda rasmi, ni afadhali atupishe watanzania, ili tumtafute mtu mwingine wa kuweza kuitetea nchi yetu na katiba yetu.
 
kuna watu hapa mnajidanganya eti hawa jamaa wakikamata madaraka mambo yatakuwa safi kila mtu maisha yatanyooka,vijana wote watapewa kazi,chuoni mtasoma bure etc,itakula kwenu nawambia na maneno haya mtayakumbuka.
kazi watapata hawa kina salal sleep na wengine humu hawafiki hata 10,kisha wengine sahauni.
wewe tafuta faranga kivyako na wala usidhani huyo slaa atakusaidia kwa lolote
 
Pesa zipi hazijalipiwa kodi?

Wacha kubwabwaja sana, sema pesa hizi hazijalipiwa kodi ili ueleweke na upata majibu.

Nyerere unaemtaja alitaifisha kama azimio la bunge linavyotaka, lakini tumejifunza kwa makosa hayo haypo aliyofanya Nyerere, baada ya kutaifisha tu, tukawa nchi omba omba hata kula hatuna, tunagawa sukari kilo moja kwa wiki kwa kaya.

Kikwete hilo kasema NO. Huturudii makosa ya Ujamaa wa Nyerere.

Ni nini usichokielewa tukusaidie.


Sasa mbona hata baada ya CCM kuanzia mwinyi kuuza kila shirika la uma bado kikwete anzunguka duniani nakiomba omba.
 
FAIZA FOXY. ..HUO NI UONGO WA MCHANA KWEUPEEE....NAJUA WEWE NI MSAKA TONGE NA UKO HAPA KUTETEA TUMBO LAKO..PLEASE HEBU KUWA NA UZALENDO KIDOGO NA NCHO YAKO...ESCROW NI PESA ZA UMMA HILO PIA WALILIKUBALI JAPO MWANZONI WALIJARIBU KUPOTOSHA....RUDISHENI PESA KISHA MUENDE JELA!!!!!! grrrrrrrrrrr


Pesa za umma zinakaa akaunti ya escrow? wewe si umma? unaweka pesa zako escrow account?

Kikwete huwa hakisii.
 
eti elimu itakuwa bure",wapi wewe hizo pesa za kusomesha bure wanavyuo karibu laki 2 unaitoa wapi?,au ndo unapanga kulipisha watu kodi hadi wauza machungwa
 
Pesa za umma zinakaa akaunti ya escrow? wewe si umma? unaweka pesa zako escrow account?

Kikwete huwa hakisii.
Bibie, ondoa kichwa ulichochimbia ardhini. Escrow ni kwamba hizo hela zilikuwa na ubishi. TANESCO ni kampuni ya umma na badala ya kuilipa IPTL moja kwa moja hizo hela ziliwekwa escrow mpaka ugomvi uliokuwepo baina ya IPTL na Tanesco kuhusu capacity charge utakapotanzuliwa mahakamani. Kwa hiyo in essence ni pesa za umma. Kiwete kasema uwongo kwa sababu yeye na familia yake wamefaidika kwa kuwa wabia 50% wa kampuni ya Singa Singa.
Watanzania wameamka.
 
Usijitie ujuha kwa kujichekesha bila mpango, umeulizwa "kavunja katiba kifungu namba ngapi ?"
nani akutafunie kila kitu? Kama una akili timamu umeshaelewa ni kifungu gani, sina haja ya kukiweka hapa,mesage sent!
 
Back
Top Bottom