Dr.Slaa live ITV akichambua hotuba ya Kikwete

Dr.Slaa live ITV akichambua hotuba ya Kikwete

vyombo vya usalama visicheze mbali na huyu mzee kwani ni wazi kuwa hatakubali kushindwa safari hii.
security lazima wamuweke under surveillance tangu sasa just incase.
hata huko marekani ama dubai wanakonunua nyumba za kukimbizia family zao iwapo wataanzisha vita,pelekeni maajent from now as a pre empt.ama sivyo huyu babu ataharibu

Ushaanza kudata. Aisee jipange maisha maana kitumbua kinaindia mchanga sasa hivi.
 
Dr. Slaa asikilizwe, alichokisema tukitafakari, na tupange mikakati ya kuwashughulikia wote waliothibitika kushiriki wizi wa Escrow na maovu mengine ndani ya serikali.
 
Kuna ushenzi zaidi ya padri kupora mke wa mtu na kumweka kimada na kumjengea jumba la kifahari kwa fedha zetu walipa kodi?

Kikwete yuko juu, mtabaki mnabwabwaja, leteni ushahidi wa huo ushenzi, wacheni kubwabwaja na kuhororoja bila mpango.

Kikwete ni Rais wa Watanzania zaidi ya Million 45, wamo Waislam, Wakristo, Mabaniani, Makadiani, Wasio na Dini, Wala nguruwe, wooooote hao yeye ndiye Rais wao, unaweza mfananisha na nani leo hii Tanzania hii?

Punguani wahed.
haa haa sio bure wewe, lazima umelamba au umelambishwa. Unatetea dhulma? Kweli nimeamini rushwa inapofusha wallahi. Ukweli utabaki palepale jk hajawatendea haki watanzania kwenye kadhia hii ya escrow. Kwa vile wewe unatetea mlo wako haya endelea.
 
2-slaa anamlaumu jk kwa double standard kumwondoa tibaijuka na kumwacha muhongo .

~~~ana kaondoka kwa kukiuka maadili ya kutopokea pesa bila kudeclaire wewe babu,muhongo kapokea nini na wapi?
justbecause mengi kakutuma haina maana kuwa utaforce we mzee na kama umekula pesa ya mangi yesu na maria utazitema usipodeliver
haa haa wewe ulichukua za kwenye lumbesa ama sandarusi? Jk kaudhalilisha sana urais, muhongo ndo alitakiwa awe wa kwanza kutimuliwa.
 
mropoko wa mwisho wa slaa.
--anataka rais ajiuzulu kwani hata kibamba amemtaka rais ajiuzulu pamoja na gazeti la tanzania daima.

-~~WHAT???,wewe mzee slaa we are you serious,yaani kibamba ndo amekua nani hadi...
punguza hamu ya urais we babu kama umeandikiwa utaupata kama ni no hata ufanye nini hupati ng'o
 
Safi sana Dr Slaa, hii itasaidia kikwete kuacha kutoa hotuba zisizo na mashiko..zilizo jaa mipasho , vijembe, uhuni dharau, kejeli, ulaghai na uswahili
 
Si vizuri kumtukana Dr Slaa humu jamvini. Ni vizuri ukajadili alichosema Dr Slaa. Kwa kuendelea kumtukana Dr Slaa ujue unaendelea kujidhalilisha na utadharauliwa na wafuasi wake na watanzania wenye akili timamu. Maisha binafsi ya Dr Slaa hayana nafasi katika maendeleo ya taifa letu. Hata hivyo kama msomi (sina hakika kama u msomi) unapaswa kutambua Dr Slaa alishinda kesi dhidi ya tuhuma za kumnyang'anya mke wa mtu; sasa tuhuma zako zinakuwa supported na nini? au ndio yaleyale ya kuunga mkono hoja kwa asilimia mia moja na kusema ndiooooooooooooo?
mkuu huyo mwana mama umsamehe bure, huyu muda wote kazi yake ni kutukana tu wapinzani na sio kujibu hoja. Pia hupenda kutumia dini ya mwenyezi mungu kama ngao ili kutetea mapungufu ya ccm/jk. Hana jipya zaidi ya kujifanya yeye anaijua dini kuliko wengine. Sijaona mwanamke wa kiislamu mwenye mdomo mchafu kama huyu mama wallahi.
 
mropoko nambari 3 wa slaa.
-S et anastahili kukamatwa kwa kugushi nyaraka na kutolipa kodi.
--wewe babu slaa unazeeka vibaya,seti amegushi nini na wapi?una,kamata vipi mtu ukiwa huna hata ushahidi si atatoka ndani ya dakika tu.kwamba hajalipa kodi,kodi ipi na kama kweli mbona yeye mwenyewe alidai kuwa tayari kulipa kodI
haa haa ndo madhara ya serikali kuwekwa mfukoni na mafisadi. Jk ni janga.
 
Dr. Slaa asikilizwe, alichokisema tukitafakari, na tupange mikakati ya kuwashughulikia wote waliothibitika kushiriki wizi wa Escrow na maovu mengine ndani ya serikali.
 
Kujiudhuru kwa AG ndiyo maana yake fedha si za IPTL?

Hivi hizi shule huwa mnakwenda kusomea ujinga?

Mimi simtambui kikwete kama ni rais , kwasababu term ya pili hakushinda bali aliiba kura...Kikwete hana personality ya urais yupo yupo tuu..
Kwa hiyo we kibibi cha magamba acha kutetea ujinga.
 
anaongea pumba HUYU MZEE ANACHOONGEA HAKIELEWEKI..UCHUNGUZI UNAENDELEA ANACHO JADILI NINI?

bora nimuanglie marin hassan TBC 1

Hapo kwenye RED unaweza kutuambia huo uchunguzi unafanywa na Taasisi, Kamati,Tume au idara ipi? na je umeanza lini na utaisha lini?
 
Mimi simtambui kikwete kama ni rais , kwasababu term ya pili hakushinda bali aliiba kura...Kikwete hana personality ya urais yupo yupo tuu..
Kwa hiyo we kibibi cha magamba acha kutetea ujinga.

Hiyo kazi kwako, ukimtambuwa usitambuwe.

Weka ushahidi wa kura aliyoiba, wacha kubwabwaja na kuhororoja bila mpango.

"nimetembea angani na ardhini Tanzania nzima sijaona Rais na serikali iliyotukuka kiutendaji kama hii ya KIKWETE." - Freeman Aikaeli Mbowe
 
Msikilize Dr.Slaa live ITV akiongelea sakata la Escrow na hotuba ya Kiwete.

Dr.Slaa, anamlaumu raisi Kikwete kwa kukosa uzalendo kwa jinsi anavyoshughulikia sakata hili la Escrow na kumlaumu kwa kuvunja katiba.

Dr.Slaa amlaumu Kikwete kwa double standard.Yaani kumuondoa Tibaijuka kazini na kumuweka kiporo Muhongo.Pia, amehoji utaratibu wa kumuweka mwanasiasa kiporo.

Dr.Slaa anasema Kikwete anapuuza bunge na kwamba hivi sasa ni serikali inayolisimamia bunge na si bunge linaisimamia serikali.

Dr.Slaa anasema Seth anastahili kuwa amekamatwa kwa kugushi nyaraka na pia kutolipa kodi na kwamba raisi anafumbia macho.

Dr.Slaa anasema singasinga huyu ana uhusiano na Ikulu kwa muda mrefu na ndio maana hachukuliwi hatua.

Pia,Dr.Slaa ameishaangaa polisi kupewa msaada wa fedha na singa singa.

Dr.Slaa pia anashangaa raisi kuwasiliana kwa email na mtuhumiwa mmoja na huku mtuhumiwa huyo akimwita raisi "dear".

Dr.Slaa anungana na maaskofu kutaka uwajibikaji wa watuhumiwa wa sakata hili na pia ameungana na wanaosema raisi anapaswa kujiuzulu(Deus Kibamba ni mmoja wa watu waliotoa kauli kuwa, kwa sakata hili,hata raisi anapaswa kuondoka madarakani-Tanzania Daima la leo).

Dr.Slaa amemalizia kwa kusema hawana chuki binafsi na Muhongo wa raisi.
Heshima kwenu wanajamvi !
Heri kwa sikuuu ya Xmas na Mwaka mpya 2015

Harbinder ameonesha ni namna gani alivyo mwananaume wa shoka,watu wenye dhamana wanaogopa kufanya maamuzi ya maana juu ya ESCROW kwa kwa kulinda maslahi ya Taifa, kisa ni huyu Singa na washarika walionufaika na Issue nzima ya IPTL/ESCROW.

Kwa namna ilivyo Harbinder Seith Singa ni mtu mwenye nguvu mpaka kiasi Dola inahofia,vyombo vyote ikiwepo Mahakama ,vimewekwa mfukoni na huyu mtu, watuhumiwa walio wengi wa hii Saga hii hawajaguswa.Kwa hoja hiyo huyu bwana anastahili kupokea pongezi,naam huyu ni mwanaume wa shoka,mpaka Serikali inamtetemeka ,na kuogopa hata kutekeleza maazimio ya Bunge!!!

Naam,Tanzania tu mambo haya yanawezekana,Ingekuwa China kwa issue kama hii tayari tungekuwa tunashuhudia misiba na maombolezo ya watu kunyongwa. Ila Tz kwa vile ipo kwenye AUTO PILOT mambo haya yanaonekana kama comedy ya akina JOTI na BAMBO.
Ningekuwa na muda wa kutosha ningetunga shairi la kumsifia Harbinder Seith Singa kwa namna anavyoichezea Serikali.

Congratulation Harbinder for keeping our government in your Pocket.But I wonder how great your pocket is? Enough to keep our government in your pocket ? Keep it up Harbinder.
Nawasilisha kwa kejeli moyoni naumia.
UKANA SHILUNGO,
Likizoni Masasi.
 
Back
Top Bottom