Dr.Slaa live ITV akichambua hotuba ya Kikwete

Dr.Slaa live ITV akichambua hotuba ya Kikwete

kazi gani kafunga? Nakuhakikishia ndo kwanza ameifungua, kama rais bila ushabiki amewaangusha watanzania, tulikuwa na matumaini makubwa na mh. Rais, lakini ametuangusha.

Wewe umeangushwa nini wewe? kama kweli una uzalendo acha kutumia umeme, ulitaka umeme wa bure? maana Habinder anazalisha umeme mpaka dakika hii, na michuzi inaingia.

Babu kapiga porojo, sikuona alipoonesha nani kaiba na nini kimeibiwa. Au wewe umesikia hilo?
 
Kweli mdau, kama Rais hakubaliani na ushauri ama maazimio ya Bunge Katiba iko wazi. Atekeleze ama avunje Bunge!
Na ajiulize kipi chenye manufaa kwa Taifa kuvunja Bunge ikiwa ni pamoja na gharama za kuandaa uchaguzi mwingine au kutekeleza maazimio ya Bunge? Kipi chenye gharama rahisi?

Kwa nini tulembe? Kwa nini Rais ulembe?

Bunge ndiyo sauti ya Wananchi, kwa mantiki hiyo kama wamekushauri hivyo wewe Raisi kwa nini usitekeleze maamuzi ya Wananchi? Gharama zitokanazo na utekelezaji wa maazimio hayo ya Wananchi si watabeba wananchi wenyewe?
Naunga hoja mkono
 
vyombo vya usalama visicheze mbali na huyu mzee kwani ni wazi kuwa hatakubali kushindwa safari hii.
security lazima wamuweke under surveillance tangu sasa just incase.
hata huko marekani ama dubai wanakonunua nyumba za kukimbizia family zao iwapo wataanzisha vita,pelekeni maajent from now as a pre empt.ama sivyo huyu babu ataharibu
haa haa,yaani badala ya vyombo vya ulinzi na usalama kukamata kina chenge, ruge, ngeleja na mafisadi wengine waliochota mamilioni ya shilingi pale mkombozi benki, wahaingaike na mzalendo dr. Slaa? Utakuwa usalama wa lumumba na sio usalama wa taifa huo.
 
Hivi slaa anadhani naye kunasiku anaweza kuwa kiongozi wa taifa hili,anachekesha kweli huyu mzee.

anasema anataka kujaribu mara ya mwisho,napo ataangukia pua tu
 
weka picha vile amebeba lumbesa or it didnt happen
ndo tatizo la lumumba, yaani sijui mnafikiri kwa kutumikia mak.alio ama! Pccb ni taasi ya serikali imethibitisha hayo. Nani mwingine wa kukanusha haya? Jk nchi imemshinda, anapaswa kwenda kupumzika msoga.
 
Kweli mdau, kama Rais hakubaliani na ushauri ama maazimio ya Bunge Katiba iko wazi. Atekeleze ama avunje Bunge!
Na ajiulize kipi chenye manufaa kwa Taifa kuvunja Bunge ikiwa ni pamoja na gharama za kuandaa uchaguzi mwingine au kutekeleza maazimio ya Bunge? Kipi chenye gharama rahisi?

Kwa nini tulembe? Kwa nini Rais ulembe?



Bunge ndiyo sauti ya Wananchi, kwa mantiki hiyo kama wamekushauri hivyo wewe Raisi kwa nini usitekeleze maamuzi ya Wananchi? Gharama zitokanazo na utekeleza
HUWEZI KUMSHINIKIZA RAIS afanye utakavyo wewe

Maazimio ya bunge yepi ambayo hayajatekelezwa? la kutaifisha? hilo sahauni, hakuna mwendazimu ataeiingiza nchi kwenye hilo tatizo, hamkumbuki yaliyotukuta Nyerere alipotaifisha? au hamkuwepo? hata kanda mbili tukawa hatuna tunavaa makatambuga.

Huko Kikwete kishasema NO. Ujamaa wa kutaifishana na kujiingiza kwenye matatizo tuliachana nao zamani.
 
Maazimio ya bunge yepi ambayo hayajatekelezwa? la kutaifisha? hilo sahauni, hakuna mwendazimu ataeiingiza nchi kwenye hilo tatizo, hamkumbuki yaliyotukuata Nyerere alipotaifisha? au hamkuwepo? hata kanda mbili tukawa hatuna tunavaa makatambuga.

Huko Kiwete kishasema NO. Ujamaa wa kutaifishana na kujiingiza kwenye matatizo tuliachana nao zamani.
mawazo mgando siwezi kukulaumu sana kwa sababu uwezo wako wa kufikiria ndo umefikia mwisho hapo
 
Umeona eeeh! Nashangaa kuona Padre Mzinifu anakuja na bla blaaa nyingi pasi na ushahidi wowote

siasa za namna hii ccm walidhani zinaweza kuwasaidia watz wakasema noo tumechoka na uhuni wenu..... Zamani vijana walikuwa wanaandaliwa wawe na hoja za kujibu matatizo wa watz siku hizi sifa kubwa ya kupewa uongozi ni UWEZO WAKO WA KUTUKANA UPINZANI NA KUWATUKANA WAZEE NA WAASISI WA TAIFA KM WARIOBA TENA MATUSI YA NGUONI. ccm hawana tofauti na mbwa
 
Msikilize Dr.Slaa live ITV akiongelea sakata la Escrow na hotuba ya Kiwete.

Dr.Slaa, anamlaumu raisi Kikwete kwa kukosa uzalendo kwa jinsi anavyoshughulikia sakata hili la Escrow na kumlaumu kwa kuvunja katiba.

Dr.Slaa amlaumu Kikwete kwa double standard.Yaani kumuondoa Tibaijuka kazini na kumuweka kiporo Muhongo.Pia, amehoji utaratibu wa kumuweka mwanasiasa kiporo.

Dr.Slaa anasema Kikwete anapuuza bunge na kwamba hivi sasa ni serikali inayolisimamia bunge na si bunge linaisimamia serikali.

Dr.Slaa anasema Seth anastahili kuwa amekamatwa kwa kugushi nyaraka na pia kutolipa kodi na kwamba raisi anafumbia macho.

Dr.Slaa anasema singasinga huyu ana uhusiano na Ikulu kwa muda mrefu na ndio maana hachukuliwi hatua.

Pia,Dr.Slaa ameishaangaa polisi kupewa msaada wa fedha na singa singa.

Dr.Slaa pia anashangaa raisi kuwasiliana kwa email na mtuhumiwa mmoja na huku mtuhumiwa huyo akimwita raisi "dear".

Dr.Slaa anungana na maaskofu kutaka uwajibikaji wa watuhumiwa wa sakata hili na pia ameungana na wanaosema raisi anapaswa kujiuzulu(Deus Kibamba ni mmoja wa watu waliotoa kauli kuwa, kwa sakata hili,hata raisi anapaswa kuondoka madarakani-Tanzania Daima la leo).
......................................................................................................................................................
Dr.Slaa amemalizia kwa kusema hawana chuki binafsi na Muhongo wa raisi.


Escrow ni Tatizo, Tushughulikie chanzo chake. Tusihukumu dhamiri njema ya kumaliza tatizo hata kama kuna mapungufu yaliyojitokeza.

Watanzania wengi hawakulielewa vizuri hili sakata la ESCROW. Nami sitaweza kwenda hatua kwa hatua kuwaelewesha juu ya jambo hili. Nataka tu sisi wananchi wa kwaida tujenge hoja ya ufahamu kwa kuuliza maswali ya msingi. Wanachong'ang'anizwa kukikubali wananchi ni ile taarifa potofu ya wizi wa Bilioni 3.6 ambazo zilitakiwa kuweko kwenye accnt ya escrow. Wamekaririshwa maneno ya wizi na ufisadi ambayo yalikuwa na msisitizo wa propaganda chafu yenye lengo la kuharibu uhusiano wa CCM, serikali na wananchi wa Tanzania. Watanzania wakasitushwa na taarifa hiyo ya Wizi Mazingaombwe bila kujua kumbe matarumbeta hayo yalikuwa na dhamira ya kuchafua hali ya hewa kisiasa na kuwadungua Waziri Mkuu, Waziri Muhongo, Mwanasheria Mkuu na Katibu Mkuu Maswi. Na wote tunafahamu wangefanikiwa kwa kiasi kile walicholenga, wangekuwa wamefanikisha uharamia wa kisiasa ambao ungeitikisa nchi kisiasa, kiutawala na kiutendaji. Wangekuwa wametengeza mkakati na agenda ya uchaguzi wa mwaka 2015. Watu wote wanaoitakia mema nchi hii (bila kujali itikadi) wanalaani vitendo vyote vya wizi wa hazina ya uma bila kujali vimefanywa na baadhi ya watendaji wa serikali ya CCM, wanasiasa wa CCM, CHADEMA, Taasisi au mtu yeyote binafsi. Na katika hili la ESCROW, yeyote mwenye mchango katika kutengeneza tatizo hili anapaswa kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria na sio kwa mujibu wa wakosoaji wenye chuki za kisiasa na dhamira ya kutaka nchi hii nzuri isitawalike.......Wizi unapotendeka huwa kuna element ya kufanya vitu kwa ghiliba, kimyakimya na kutohusisha wadau muhimu (relevant stakeholders) wakati wa mchakato wa utoaji pesa. Ukiuangalia mchakato wa utoaji wa fedha kotoka ESCROW account, utaona consultations na mawasiliano mbalimbali baina ya taasisi muhimu husika hiyvo kufanya neno wizi likose sifa ya kutumika kwenye transaction hii... Pamoja na kupongeza kazi nzuri ya PAC, ningetegemea badala ya matumizi ya neno "wizi" labda wangebainisha taratibu zilizokiukwa(Kasoro) katika mchakato mzima wa utoaji wa fedha za ESCROW. Vilevile kiasi cha fedha zilizoluwamo kwenye akaunti hiyo ndio kingetajwa kwa usahihi wake badala ya kuwapandisha presha watanzania kwa kuripoti kiasi ambacho hakikuwepo akauntini humo. Vilevile ni vema tukakubaliana juu ya uwiano wa umiliki wa fedha hizo kati ya serikali na taasisi zake kwa upande mmoja na mwekezaji kwa upand wa pili.

Kwa Mujibu wa hotuba ya Mheshimiwa Raisi na vyanzo vingine, akaunti ya ESCROW ilifunguliwa ili kuweka pesa zilizokuwa zinalipwa kwa IPTL kama tozo ya Mitambo na uwekezaji. Malipo kwenye akaunti ya ESCROW yalitarajiwa yafanyike kwa kipindi cha mgogoro unaohusiana na kiwango (Rate) ya malipo ya tozo hiyo. Na ilitarajiwa kwamba baada ya maelewano juu kiwango cha kulipa kama tozo ya uwekezaji, IPTL angelipwa kutoka akaunti hiyo malimbikizo yote baada ya kukatwa kodi. Pia iwapo kiwango cha tozo kingepunguzwa, ile ziada ya malipo amabayo ingetokana na kiwango kipya cha tozo, nayo ingelipwa kwa TANESCO. Lakini pia ifahamike kuwa tozo hii ya sasa inayolalamikiwa na TANESCO, ni ile iyokuwa imepunguzwa na Taasisi ya Utatuzi wa Migogoro ya Uwekezaji kutoka Bil 3.6 mpaka Bil. 2.6.

Swali la kujiuliza ni kwamba je! Baada ya Chombo cha Utatuzi wa Migogoro ya uwekezaji kufanya hukumu ya tozo pungufu in favor of TANESCO, TANESCO waliridhika? na kama hawakuridhika, hatua walizochukua kushughulikia madai yao zilikidhi matakwa ya kisheria ambayo hatimae zingehakisha usalama wa mali na mtaji wa Shirika?(yaani TANESCO). Kwa Maoni yangu nadhani TANESCO haikuwa na mkakati madhubuti wa kisheria wa kushughulikia madai yao dhidi ya IPTL. Matokeo yake ni kuupokea ushauri wa mawakala /madalali wa upatanishi ambao walishindwa kuutatua mgogoro kwa miaka hiyo mingi. Na hiki ndugu zangu ndio kiini kikuu cha tatizo hili, yaani mgororo wa tozo ya mitambo/uwekezaji kati ya TANESCO na IPTL kutopatiwa ufumbuzi kwa muda wa zaidi ya miaka 5 kwa uchache wake. Tujiulize swali lingine; Je! Katika kipindi hiki chote, PAC au bunge kwa ujumla wake (Kama taasisi yenye jukumu la kuisimamia/kuishauri serikali; hawakuona huu mgogoro kuwa ni tatizo linalohitaji intervention kutoka kwao? Je! Pia kwa nini Bunge au hata Mheshimiwa Rais wasione haja ya kuwawajibisha waliolizalisha tatizo hili la mgogoro na kulilea kwa miaka zaidi ya kumi? Tutambue kuwa tatizo hili lina umri mkubwa kuliko account ya ESCROW yenyewe.

Kunaweza kuwa na shida katika mtiririko wa hisa za IPTL kutoka kwa mmiliki wa kwanza hadi kumfikia Habinder Singh. Nakubaliana na wazo la mheshimiwa Rais kwamba vyombo vyetu vitusaidie kujua fedha tulizopoteza kama kodi na tuzidai kwa nguvu zote. Lakini ukweli pia unabaki kwamba mkataba wa TANESCO NA IPTL hatuwezi tu kuutangaza leo kuwa null and void, mkataba huu unatambuliwa hata na vyombo vya usuluhishi vya kimataifa. Hatuwezi katika hali ya kuwa hatukumlipa mtu haki yake (Capacity Charge) kwa miaka mingi hivi leo uamue tu kuvunja mkataba na kutaifisha mitambo yake.........kwa ndoto tu kwamba akienda kutushtaki sisi tutasimami hoja kwamba umiliki wake wa hisa una mashaka au usajili na utambulikaji wake BRELA ni debatable; Aaah! nyie wabunge, kweli huko mjengoni siku hizi wote ninyi ni wataalam, lakini mnayotuambia sisi wananchi mengine tunachananya na ya kwetu.....mbona hata hiyo mnayoiita natural justice inakataa......Mimi niwaombe ndugu zangu huko bungeni hili la IPTL tulimalize kiungwana tumelikoroga wenyewe kama Taifa. hakuweko wa kumsaidia mwenzanzake lilipokorogeka; Si Bunge, si Kamati(PAC), Si mwanasheria mkuu, na wala sio sisi maamuma wananchi.

Mimi kwa maoni yangu nimemtoa kabisa Rugemalila au Ruge kwenye sakata la ESCROW hata kama Singasinga' kalipia zile hisa walizouziana kwa hela ya escrow. Naamini kwa vyovyote kwenye escrow account lazima kulikuwa na hela IPTL hata kama siyo yote. Kwa hiyo singasinga katoa sehemu ya hela yake akamlipa Ruge. Tumwache Ruge.

Na huenda makubaliano /maamuzi ya serikali ya kumlipa IPTL kutoka ESCROW account kabla ya ku-resolve mgogoro yalizingatia hali mahitaji mwekezaji huyu ya kuimarisha uwezo wake wa kuendelea kutuzalishia umeme kwani amejitahidi kuzalisha umeme kwa hela za mauzo ya umeme (energy charges) peke yake na akawa analemewa. Na kwa kuwa uhai wa mkataba bado ni mrefu tu, kungekuwa na taabu gani kwa Serikali/TANESCO chini ya maelekezo ya Mwanasheria mkuu AG;kukubaliana kumlipa IPTL "Contractor wao" ambae aliendelea kuwazalishia umeme bila malipo ya tozo ya mitambo iliyokubaliwa kimkataba ili kupisha maelewano? Kama dhamira hapa ni (Preventive mechanism) ili IPTL asishindwe kuzalisha umeme kwa kipindi ambacho kimeonekana kuwa "fragile"kuepusha taifa kupungukiwa umeme. Uamuzi unaofanywa kwa dhamira njema kimahusiano ya kibiashara na huduma hata kama bado mgogoro haujatanzuliwa lakini road map to resolving the dispute is already drawn, kuna ubaya gani?

Shida imetoka wapi? Share holder mmoja Ruge akalipwa fedha za mauzo ya hisa zake akaanza kugawa kwa ngugu zake, viongozi wa dini, wtumishi wa uma majaji na mawazili. Kwa kutumia pesa zake (sio za ESCROW) akawaingiza watumishi na viongozi wa umma katika mgogoro wa kimaadili na rushwa.

Lakini je! hela za Singasinga (PAP/IPTL) zimegawanywa? No Singasinga Hakufwanya hayo....Sasa hizi ndio za Escrow, IPTL wanazitumia kuzalisha umeme kwa mujibu wa makubaliano yake na TANESCO. Na Anaamini dhamira ya upande wa pili ikiwa njema, isipoingiliwa na wanasiasa na wapinzani wake wa kibiashara ambao wanauza umeme kwa be kubwa hata kama ni wa gesi, isipoingiliwa na madalali wa upatanishi waliofukuzwa na Muhongo. Mahusiano ya IPTL na TANESCO siku zote yasingekuwa na shida.

Mheshimiwa Rais alisema tatizo ni wataalam/watendaji kuendelea ku-Manage Crisis na sio Ku-Resolve crisis.Ndugu yangu Mh.RAis; wanapo-endelea ku-manage crisis wanaendelea kulapo wenzioo....lakini waki-resolve lishe itaishapo......

Hivi ninyi PAC, kwa nini hela za Ruge mkaziita za escrow? mmetuchanganya. Halafu nyie niwabaya sana, kila waziri mkuu mnataka mumdungue....Ngweeeeuuuun... safai hii mmekosa.

Now seriously! PAC/Bunge muwe mnatusaidia kuchanganua mambo katika uhalisia wake. Mkitenganisha hili na lile, mkitoa mapendekezo ya haki kwani mapendekezo yenu ni hukumu kwa walengwa.

Pengine ni muhimu kasoro halisia za utoaji hela kutoka accnt ya escrow zibainishwe na dhamira ya utoaji itazamwe vizuri. Kwani kuendelea kuwepo kwa account ya escrow ambayo TANESCO walishindwa kuiwekea hela as required kuna umuhimu gani? ending it was a good Idea, Serikali itanzue kwa haraka mgogoro huu usiendelee kutoa ajira kwa watu, ndio; wapatanishi wamafaidika sana na mgogoro huu... ndio na inawezekana ndio yaliyokuwa maudhui ya ku-u-anzisha. Kasoro zilizojitokeza kama zipo zishughulikiwe, wahusika waadhibiwe.

PACna Bunge wamejiridhishaje kuona kwamba uamuzi wa serikali kwa maana ya Wizara husika na TANESCO wakisaidiwa na mwanasheria mkuu, waliusimamia mchakato wa kumlipa IPTL fedha zilizokuwemo kutoka akaunti ya ESCROW ili pengine kudhoofisha dhamira ya Habinder Singh Set kwenda mahakamani kudai ucheleweshwaji/malimbikizo ya Capacity Charges na riba na kesi zingine ambatanishi ambazo zingeigharimu serikali/ shirika iwapo ingeshindwa? Ikumbukwe pia wawekezaji wengine wote kwenye nishati ikiwemo Songas wanalipwa na TANESCO tozo hii bila kukosa. Kwa nini TANESCO hailalamikii makampuni hayo? Au hao hawatulalii na kwamba tunalipa Capacity Charge kiduchu tu kulinganisha na uwekezaji walioufanya? Maana kama hoja za namna hii hazina majibu basi IPTL anaweza kujenga mtazamo kuwa wawekezaji wanakuwa-treated tofautitofauti. IPTL akiona anazo kesi za msingi ataishitaki TANESCO halafu akishinda mseme ni mpango wa serikali/CCM ili hiyo hukumu/ faini waigawane vigogo. HIVI NI NANI MBAYA WETU ZAIDI! NI YULE ALIYEANZISHA MGOGORO ASIJUE NAMNA YA KUUMALIZA AU ALIYETHUBUTU KUUMALIZA HATA KAMA KWA NJIA ZA ZIMA MOTO? Mimi naamini kasoro zilizojitokeza katika utoaji fedha za ESCROW (kama zipo) zitazamwe kwa maana ya kuzuia kwanza hata uwepo wa hizo escrow account. PAC waendelee kufanya kazi nzuri ya kusimamia serikali na washirikiane na serikali kabla wananchi hatujaanza kuhoji credibility ya bunge na kamati zake pia. Tungekuwa na PAC makini, mgogoro huu usingedudumu kwa miaka ming yote hii. Wakati bunge huitaka serikali kurekebisha kasoro mbalimbali katika utendaji wake na sisi wananchi tunalitaka BUNGE na kamati zake kudhamiria kusimama kama "Noble Institution" isiyotiliwa shaka katika utendaji na maelekezo yake. Wananchi hatuwezi kuendelea kuona udhaifu wa kamati zetu za Bunge katika kutafsiri ripoti za kihasibu na uchunguzi kiasi cha umma kuanza kujenga dhana ya matajiri au maraisi tarajiwa kuwatumia wabunge kudhoofisha nguvu za wapinzani wao kibiashara au kisiasa.Na hatuko tayari katika nchi hii kuridhika na hali (phenomena) inayoweza kutafsiriwa kuwa "Tyrannic Parliament"au "Tyranny of the Parliament"

Tujiulize kwa nini mkazo au focus ya PAC na baadhi ya wabunge ilielekezwa kwenye hela za Rugemalila zaidi ya zile za IPTL zenyewe. Kwa nini wanasiasa na hao wataalamu wao hawakufafanua /bainisha kuwa hela za Rugemalila ni matokeo ya mauzo ya hisa zake halali hivyo kuzifanya pesa zake kuwa halali pia. Dhana ya kutakatisha fedha za Rugemalila ina mashiko gani kama sio uhuni na kufilisika kisiasa tu. Rugemalila angeweza kulipwa na Habinder Singh Sethi kutoka chanzo kingine/ akaunti nyingine yeyote ya IPTL. Wajibu wa Habinder Singh kulipa manunuzi ya hisa alizo nunua kwa Rugemalila (VIP) hauwezi kuhojiwa popote na mahakama yoyote duniani. Rugemalila alilipa kodi na TRA hawakusita kuchukuwa kodi yao kwa hofu kuwa hela hizo ni chafu.... Mwenendo wa matumizi ya fedha za Rugemalila (Ambazo sio za ESCROW na hazifungamani na ESCROW) ndio umetiliwa shaka pale ambapo aliamua kuwagawia fedha nyingi viongozi wa kisiasa na watumishi wa serikali. Lakini hili ni tatizo lenye sura ya ukiukwaji wa maadili/miiko ya uongozi na hisia za kuwepo kwa dhamira na utekelezaji wa kuto na kupokea Rushwa. Katika hili Msimamo wa chama cha mapinduzi ni kwashughulikia Mawaziri na Watendaji waliopokea fedha hizi. Na ndio maana tunaunga mkono maagizo ya Mheshimiwa Rais ya kuwataka Takukuru, Taasisi inayoshughulikia maadili ya viongozi na mamlaka za uajiri kukakamilisha chunguzi zao ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa mapema. Lakini uhuru wa Rugemalila kutumia hela zake apendavyo kwa watu wasio watumishi au viongozi wa uma hauwezi kuhojiwa. Rugemalila na VIP yake si sehemu ya mgogoro wa ESCROW, msipotoshe watanzania.

PAC na Bunge kwa ujumla wametuacha mahali ambapo tunaamini kuwa fedha za Rugemalila ndio Escrow na kwamba waliogawiwa ndio wezi wetu. Sikatai harufu mbaya ya Rushwa na ukiukwaji wa maadili ulioghubika mgawo wa Ruge. Lakini ndilo mlilolilenga peke yake? Hamkutoka na kingine kama vile TANESCO kutowa- treat contractors wake evenly na kuondoa kasoro katika management ya mikataba inayoweza kuwafanya washitakiwe na kushindwa hivyo kubebesahwa mizigo ya faini kwa watanzania wote kupitia bili za umeme? Rugemalila asingegawa hela zake, PAC wangekuwa na hoja gani nzito? Mimi niwaombe Bunge hebu fuatilieni mbegu iliyootesha huu mti maarufu wa ESCROW, huenda tukashughulika na wazembe wengine waliokwisha staafu ambao ni pamoja na Wakurugenzi na wanasheria wa TANESCO waliokuwepo mwanzoni mwa mgogoro, mwanasheria mkuu aliekuweko wakati huo, katibu mkuu wa wakati huo n.k.

Mwisho:

Ninyi watu wa Serikali; Mawaziri, Makatibu Wakuu, Wakurugenzi na Wakuu wa Taasisi. Muwe wawazi zaidi. Mgogoro huu ni wa miaka mingi lakini mlikuwa mnaujua peke yenu. Katika kutekeleza mising ya Good-governance, tranparency ni nyenzo nzuri na muhimu sana. Shirika kama TANESCO linaposhitakiwa au kushitaki, linapokuwa na mgogo wa kimkataba na Contractors na Consultants wake; kumbe kwenu ninyi wakubwa hii siyo habari ya kuwajulisha wananchi wenu? Mngekuwa mmetujulusha wananchi tangu mwaka 1998 mlipoanza kuzozana na IPTL juu ya Tozo ya Mitambo kupitia Press Conferences & Releases, tungekuwa tumejua escrow ni nini. Uamuzi wa kutoa hela kutoka escrow account mgetuambia na sababu za kufanya hivyo, hii shaida yote isingetokea. Lakini kwa kukosa uwazi kwa taarifa ambazo ni basic, gharama zake ndio hizi za kuunda baraza la mwaziri kila uchao. Badilikeni jamani huu ni wakati mpya...........

Mheshimiwa Rais! Pole sana, kwanza kwa kuumwa lakini pia hongera kwa matibabu na uponyaji. Hawa watu wako nina maana ya kusema mawaziri na watendaji ngazi zote wawe wanafunguka.... wanatoa habari/taarifa kwa mambo ya msingi. Waongee kupitia media...Au TBC wanawanyima Airtime. Chama na Serikali yetu Kwa hapa Africa, kimefanya mambo makubwa na kinakubalika. Awamu yako hapa nchini imefanya mengi na yanaonekana. Hatuna sababu ya kuwa wanyonge....Ni kundi /sekta gani katika jamii yetu litasema hakuna kabisa kilichofanyika, nani atasema haoni jitihada na utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapindizi.....Wanawake; 50/50, Huduma bora za Afya ya Uzazi, Biashara etc., Vijana/wasanii; Elimu ya juu, Talent Development, Wafanyakazi wa umma; Ongezeko la mishahara, favorable pension schemes, Media; Freedom of expression (tukana serikali mpaka basi) hata ikifanya mazuri, Magazeti, Radio, TV Kibao, Kilimo; Kilimo kwanza, ziada ya chakula, Ulinzi na Usalama; Tuko salama, Democracy;Tena hii imekuwa sifa, vyama kibao,maneno kibao, wanasaidia somehow wanatuamsha. Wafanyabiashara/ Wajasiliamali:Miundo mbinuya uchukuzi, Mawasiliano, Health; Maboresho na upanuzi wa vituo vya Afya ya msingi, Wilaya na Rufaa,Bima ya Afya, Sekta ya Fedha;Mabenki, huduma fedha mtandao, mitaji, Uwekezaji/Uwezeshaji;Uwekezaji mkubwa na mdogo katika sekta ya mafuta, gesi, madini, utalii na Kilimo. Ni mengi siwezi kumaliza. Basi Mawaziri wako wawe wanaongea......halafu hoja kama escrow ziwe zinajibiwa kwa ufasaha.
 
Back
Top Bottom