Kuzungumzia chadema ni nafuu uzungumzie ACT, Mambo waloyafanya ni ya ajabu sana sana, Dr. Hawezi kukubaliana na ujinga wa namna hiyo, ww umtukane mtu na ufanye hadi kapoteza uwaziri mkuu wake na unao ushahidi wa kutosha na unathibitishia watanzania na unasema kama Lowasa anabisha na aende mahakamani kwa kuwa ni kweli Lowasa hakuwahi kwenda mahakani. Maana yake kulikuwa na ukweli, Jana ulikuwa unasema Lowasa mwizi fisadi, leo unasema mwenye ushahidi na aende mahakamani, hivi wanaona ss mabwege sana na hatuna ufahamu kabisa.
Mimi nimesikia viongozi wakubwa wa ukawa wanasema kwamba ccm hawakumtedea haki Lowasa hadi walimkata na imekuwa ni ajenda kubwa sana sana, swali langu kwao je uchaguzi wa kumpata Mgombea wa UKAWA ulikuwa wa kidemokrasia? Kwani nn nasema hivyo sijaona wagombea wa vyama washirika ambao walipata nafasi kwenye vyama vyao wakichuana na Lowasa, kilichofanyika ni kumpachika Lowasa kugombea nafasi hiyo, na kama wao wanademokrasia kiasi hicho mbona hawajafanya mazungumzo na waasisi wa ukawa? Ss Lipumba kaondoka na Dr. Slaa pia. Tena Mbowe anawaaminisha wajumbe kuwa mzee tumeamua kumpumzisha, maana yake tu ni kwamba watu wasihoji, kuhusu Dr. Slaa.
Wenye ufahamu tayari nao wameondoka kimya kimya wala wao hawatangazi, ila mwaka huu UKAWA mlikuwa na bahati sana ya kuingia ikulu ss mtabakia kuitazama tu kwa ajili ya tamaa zenu za ajabu ajabu, mimi nawapa pole sana sana, watanzania tulio waengi tunatizama picha inavyokwenda japo kusoma hatujui.