Hivi hata usiporudisha kadi Katiba ya CCM inasema hivi kuhusu uanachama:
7. (1) Mtu akikubali kuwa Mwanachama itabidi atekeleze haya yafuatayo:-(a) Atatoa kiingilio cha Uanachama(2) Viwango vya kiingilio, ada na michango vitawekwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.
(b) Atalipa ada ya Uanachama kila mwezi isipokuwa kama akipenda anaweza kulipa ada ya mwaka mzima mara moja.
(c) Atatoa michango yoyote itakayoamuliwa
(3) Uanachama wa mwanachama utakwisha kwa:-(a)Kufariki.(4) Mwanachama ambaye uanachama wake unakwisha kwa sababu yoyote ile hatarudishiwa kiingilio alichokitoa, ada aliyotoa wala michango yoyote aliyoitoa.
(b)Kujiuzulu mwenyewe.
(c)Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba.
(d)Kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba.
(e)Kutotimiza masharti ya uanachama.
(f)Kujiunga na Chama kingine chochote cha siasa.
Nape, Katibu Mwenezi wa Chama anapaswa ajue haya.
My take:
Uongo na kuchafuana bado vinatumika kama mtaji wa kisiasa. Watu wameshaamka, tutumie mambo yenye maslahi ya nchi kufanya siasa.
Kama hajarudisha kadi, Nape anataka kuwaambia wana CCM kuwa Slaa bado mwana CCM?
Nnauye Jr, mtu akishaacha kulipa ada, au kujiunga rasmi na chama kingine si lazima arudishe kadi. Anakuwa si mwanachama kwa mujibu wa katiba ya CCM.
Slaa rudisha kadi ya watu kama hii habari ina ukweli wowote. Huwezi kame kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja.
kweli shule na vyuo vyetu vina kazi sana kama ndio watu wanafikiri hivi. Kama hajarudisha manake kuwa anayo? Yaani hakuna uwezekano mwingine wowote ule? Mimi pia niliwahi kuwa na kadi ya CCM na hadi leo sijairudisha na sina mpango wa kuirudisha....
CLUE: Uanachama wa CCM unakomaje?
Oh My God!
Nape Nnauye Jr hata katiba ya chama chako huijui? Au unapotosha makusudi ili wapumbavu waendelee kukupigia makofi?
Hata mi naskia ivo na anashirikiana vizuri tu na viongozi wa ccm na serikali ila kisiri sana
Kwa wafuatliaji wa siasa za hapa kwetu Tanzania, mtakumbuka ya kwamba Dr. Slaa alikuwa mwanachama mtiifu wa CCM kabla ya kuasi chama na kukimbilia CHADEMA.
Hata hivyo, mpaka leo hii Dr. Slaa hajawahi kukabidhi kadi ya CCM.
nape hajui kazi yake akijua basi ccm itaendelea kutawala, mi navyothani jk alimchagua ili tu awe anamzungumzia dr slaa. Nape hapitishi wiki bila ya kumtaja dr slaa hata kama ni warsha ya serikali. kuwa kiongozi wa ccm lazima uwe mjinga ili uweze achana na ukweli ndo utaweza kuongoza, mi naamini hivyo.
Katibu Mwenezi wa CCM hajui uanachama wa CCM unaishaje!
Duh yaani CDM kiboko wameanza kumchafua Dr. Slaa! Jana nilikuwa kijiweni na vijana tunakunywa kahawa nikasikia wanasema Dr. Slaa alitumwa na Nyerere kuingia upadri ili ajue huko mapadri wanafanya nini na hakuwa na utashi wa kweli. kwa kifupi wanasema alitumwa na serikali na ni mtu wao hadi leo. Vijana wakawa wanaonyesha wasiwasi juu ya Dr. Slaa na wakasema afadhali Mbowe. Leo naona hii post nimeshangaa. Naona mitandao ya Urais ndani ya CDM inafanya kazi kwa umakini mkuu.
Kila mwenye akili zake timamu hapa, bila shaka yoyote kwa hii comment yako, anapaswa kukuelewa vyema. Aisee yaani it is extremely tooooooooooooooooooooo low and cheap mpaka kiasi cha mtu kufikiria mtu anayejiita GT anaweza kupoteza muda kuandika cheap kiasi hiki. Mwenzetu twaona kichwa watumia kuweka au kutunzia kofia kama unavyoonekana pichani. Pole mkuu Kimbunga, but honestly this is tooooooo low kwa mtu kama wewe hata kama bado unaamini katika CCMism au kuumia na CCMmonia.
Wewe unayejiita Great thinker, waliposema hivyo ukakubali? Na umeona hili ndilo la kushirikisha Great thinkers.Duh yaani CDM kiboko wameanza kumchafua Dr. Slaa! Jana nilikuwa kijiweni na vijana tunakunywa kahawa nikasikia wanasema Dr. Slaa alitumwa na Nyerere kuingia upadri ili ajue huko mapadri wanafanya nini na hakuwa na utashi wa kweli. kwa kifupi wanasema alitumwa na serikali na ni mtu wao hadi leo. Vijana wakawa wanaonyesha wasiwasi juu ya Dr. Slaa na wakasema afadhali Mbowe. Leo naona hii post nimeshangaa. Naona mitandao ya Urais ndani ya CDM inafanya kazi kwa umakini mkuu.
Slaa rudisha kadi ya watu kama hii habari ina ukweli wowote. Huwezi kame kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja.
Mimi siko CCM na ninazo kadi zao 5:........yaani bila kadi ulikuwa hupati haki yako....
- Niliyopewa nikiwa sekondari
- Niliyopewa nikiwa JKT
- Niliyopewa ili nijiunge Chuo Kikuu
- Niliyopewa ili nianze kazi
- Niliyopewa nilipo omba kiwanja