Dr. Slaa bado anayo kadi ya CCM?

Dr. Slaa bado anayo kadi ya CCM?

Mimi nina kadi ya CCM hadi leo nimeiweka kama kumbukumbu kuwa kuliwahi kuwepo na dubwasha lilinyonya wananchi wake lililoitwa CCM, ni ya Tawi la Abjani -UDSM na alinipa Bwana Alfani mwenyewe pale Sinza enzi zile za Giza, kama wanaitaka wamtume huyo alienipa aje kuichukua.
Hata hivyo Nape haoni kuwa kudai kadi ni kupoteza muda na kupotosha hoja za msingi? Kadi inasaidiaje kujenga chama endapo itarushwa hata leo hii? hawana pesa ya kuprintia nyingine?
 
Waitara, kahigi, shibuda, taja na wewe wanaofuata usione aibu.
 
Tanzania my country very sory, hawa ndio viongozi wetu. Hapo hoja kuhusu Chadema ni ili iweje. Sera tunajadili watu. Real we hav a long way to go.
 
Yangu nilitupa chooni... atuambie yeye ya CCJ kapeleka wapi?
 
wewe Kimbunga nilikuwa nakuona mchangiaji wa maana hapa JF kumbe ni walewale tu yaani unaenda kuokoteza habari za vijiwe vya kahawa uswahilini unaleta JF? shame on you! jipange au na wewe gamba??

Mkuu OSOKONI vijiweni ndiko kuna wapiga kura. Hapa JF kuna wachambuzi. Usipuuze habari za vijiweni. Nakushauri uwe unajichanganya vijiweni ili uweze kupata habari nyingi ambazo huwa hazipatikani hapa JF.

Hii post ni ya siku nyingi kabla Nnape hajasema kuwa dr. ana kadi ya CCM!
 
Last edited by a moderator:
Yupi bora? ALIYEPOKONYWA kadi ya Uananchama na anaongoza chama pasipo kuwa mwanachama na ambaye HAJARUDISHA kadi ya uanachama ila unachama wake umekoma kwa mujibu wa katiba mara baada ya kujiunga na chama kingine cha SIASA na huko anaendesha harakati za wazi wazi dhidi yenu.
 
nape hajui kazi yake akijua basi ccm itaendelea kutawala, mi navyothani jk alimchagua ili tu awe anamzungumzia dr slaa. Nape hapitishi wiki bila ya kumtaja dr slaa hata kama ni warsha ya serikali. kuwa kiongozi wa ccm lazima uwe mjinga ili uweze achana na ukweli ndo utaweza kuongoza, mi naamini hivyo.
 
kweli shule na vyuo vyetu vina kazi sana kama ndio watu wanafikiri hivi. Kama hajarudisha manake kuwa anayo? Yaani hakuna uwezekano mwingine wowote ule? Mimi pia niliwahi kuwa na kadi ya CCM na hadi leo sijairudisha na sina mpango wa kuirudisha....

CLUE: Uanachama wa CCM unakomaje?
ukiondoa kufukuzwa na chama mi nadhani hata kuhamia chama kingine kunakufanya kuwa si manachama mwaminifu wa ccm,labda kama kuna katiba mpya ya ccm inayotambua hata watu waliohama chama kuwa wanachama wao
 
Hujui kufuatilia siasa,dr slaa alikuwa mwanachama wa ccm lakini baada ya kuenguliwa na ccm kura za maoni na kumweka qoro wa ccm,wananchi tukamwomba ahamie chama chochote naye akaenda chadema na akapita kwa kishindo hapa karatu.hiyo kadi unayosema imerudishwa muda mrefu baada ya kuhamia chadema na kupewa nafasi ya kugombea ubunge
 
kweli shule na vyuo vyetu vina kazi sana kama ndio watu wanafikiri hivi. Kama hajarudisha manake kuwa anayo? Yaani hakuna uwezekano mwingine wowote ule? Mimi pia niliwahi kuwa na kadi ya CCM na hadi leo sijairudisha na sina mpango wa kuirudisha....

CLUE: Uanachama wa CCM unakomaje?

Hivi hata usiporudisha kadi Katiba ya CCM inasema hivi kuhusu uanachama:
7. (1) Mtu akikubali kuwa Mwanachama itabidi atekeleze haya yafuatayo:-
(a) Atatoa kiingilio cha Uanachama
(b) Atalipa ada ya Uanachama kila mwezi isipokuwa kama akipenda anaweza kulipa ada ya mwaka mzima mara moja.
(c) Atatoa michango yoyote itakayoamuliwa
(2) Viwango vya kiingilio, ada na michango vitawekwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.
(3) Uanachama wa mwanachama utakwisha kwa:-
(a)Kufariki.
(b)Kujiuzulu mwenyewe.
(c)Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba.
(d)Kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba.
(e)Kutotimiza masharti ya uanachama.
(f)Kujiunga na Chama kingine chochote cha siasa.
(4) Mwanachama ambaye uanachama wake unakwisha kwa sababu yoyote ile hatarudishiwa kiingilio alichokitoa, ada aliyotoa wala michango yoyote aliyoitoa.

Nape, Katibu Mwenezi wa Chama anapaswa ajue haya.

My take:
Uongo na kuchafuana bado vinatumika kama mtaji wa kisiasa. Watu wameshaamka, tutumie mambo yenye maslahi ya nchi kufanya siasa.

Kama hajarudisha kadi, Nape anataka kuwaambia wana CCM kuwa Slaa bado mwana CCM?
Nnauye Jr, mtu akishaacha kulipa ada, au kujiunga rasmi na chama kingine si lazima arudishe kadi. Anakuwa si mwanachama kwa mujibu wa katiba ya CCM.

Katibu Mwenezi wa CCM hajui uanachama wa CCM unaishaje!
 
Mkuu OSOKONI vijiweni ndiko kuna wapiga kura. Hapa JF kuna wachambuzi. Usipuuze habari za vijiweni. Nakushauri uwe unajichanganya vijiweni ili uweze kupata habari nyingi ambazo huwa hazipatikani hapa JF.

Hii post ni ya siku nyingi kabla Nnape hajasema kuwa dr. ana kadi ya CCM!

Kimbunga, mkuu wangu. Jamaa anadharau watu wa vijiweni wakati hao ndio wapiga kura muhimu.
 
Last edited by a moderator:
Kinachonikera ni siasa zinazojengwa katika upotoshaji, uongo, vijimaneno n.k. badala ya mambo yenye maslahi kwa maendeleo ya nchi yetu!

Siasa hizi bado zinategemea upumbavu wa wananchi kuendelea kukubalika. Ndio mtaji ambao Nape anatumia.

Chama tawala kilipaswa kuonesha mfano katika hili jambo. Na wananchi wanazidi kuamka kwa kuona uongo na upotoshaji wa wazi kama huu.
Well said!
 
mara zote mambo kama haya huzushwa punguani kote duniani kama anvyofanya mlopokaji wa ccm NAPE,
Alitakiwa nape atuthibitishie kwa kuonyesha risit za Dr.kwamba hii ni risit aliyolipia mwaka jana au mwezi jana,
sio kusema tu kwamba hajarudisha kadi,si razima kurudisha kadi,uanachama ni zaidi ya kuwa na kadi.

Pili NAPE kama msemaji wa chama tawala,kadi ya dr haina uhusiano na utatuzi wa kero za wananchi,haina
uhusiano vile vile ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi wa chama chake,au utekelezaji wa ahadi hewa walizodanganywa
wananchi,achague maneno yenye maslahi na wapiga kura wa chama chake,kadi ya dr haina uhusiano na ujenzi wa ba
rabara,maji, shule bora na dawa ma madai ya watumishi wa afya mahospitalini.
 
Katibu Mwenezi wa CCM hajui uanachama wa CCM unaishaje!
Wengi hamjamuelewa Nape anamaanisha nini? ni kwamba ukienda kinyume na CCM basi urudishe ile kadi yao, ila kama haujarudisha wewe bado ni CCM. na wana CCM ni pamoja na hawa;

IGP, CDF, Jaji Mkuu, Mwanasheria Mkuu, Msajili wa vyama vya siasa, Mkuu wa Usalama wa Taifa, Mkuu wa TAKUKURU na wakuu wote wa taasisi nyeti.

Mkumbuke yeyote mwenye kushika cheo hicho kwa umri wake ni lazima atakuwa anayo kadi ya CCM kutokana na mfumo wa nchi ulivyokuwa chama kushika hatamu. sasa tuna kazi moja tu ni kuuvunjilia mbali mfumo huu.
 
Asee uko sawa kabisa bosi...magamba yameanza kutoa harufu xaxa wanamtafuta wa kumvika lawama...
 
Mbona nape anatumia sana nguvu nyingi kuitetea ccm mpaka sasa amekuwa kama mlevi fulani hivi je anazo idadi ya kadi ngapi za ccm zilizorudishwa kwao mbona anaitaka ya dr. Nape angefanya la maama kama angeikoronea serikali ya ccm irudishe hayo mabillion pamoja na vile vijisent huko uswiz labda tungemelewa ======= nape leo sio jana utatoka sana povu lakini husomeki
 
Mbona nape anatumia sana nguvu nyingi kuitetea ccm mpaka sasa amekuwa kama mlevi fulani hivi je anazo idadi ya kadi ngapi za ccm zilizorudishwa kwao mbona anaitaka ya dr. Nape angefanya la maama kama angeikoronea serikali ya ccm irudishe hayo mabillion pamoja na vile vijisent huko uswiz labda tungemelewa ======= nape leo sio jana utatoka sana povu lakini husomeki---mbona voda hawapigi kelele kuwa wnanchi wanalaini za airtel,tigo na zantel na wala hawajazirudisha pia sivibayo kuwa na cadi za ccm maana ikikuchosha we ni kuichoma na kupokea nyingine iwe cufau nccr au tlp hata ccj kama sio m4c
 
Back
Top Bottom