Dr. Slaa bado anayo kadi ya CCM?

Dr. Slaa bado anayo kadi ya CCM?

Silly question..kwani zile zinazorudishwa kwenye mikutano hupelekwa wapi...pia zipo zinazochomwa moto zikirejeshwa.
je CcM wana kipengele kuwa ukiacha uanachama urejeshe kadi?
Kwa mfumo wa zamani na watu waliokuwepo miaka ya themanini kurudi nyuma kadi ya ccm ilikuwa ni kama shuruti hasa unapotaka scholarship na hata ajira lakini haikureflect mapenzi ya muhusika ktk chama
 
Kwa wafuatliaji wa siasa za hapa kwetu Tanzania, mtakumbuka ya kwamba Dr. Slaa alikuwa mwanachama mtiifu wa CCM kabla ya kuasi chama na kukimbilia CHADEMA.

Hata hivyo, mpaka leo hii Dr. Slaa hajawahi kukabidhi kadi ya CCM.

Nadhani jinsi dr Slaa anavyoichukia CCM hilo card atakuwa alilitupa chooni
 
Kwa wafuatliaji wa siasa za hapa kwetu Tanzania, mtakumbuka ya kwamba Dr. Slaa alikuwa mwanachama mtiifu wa CCM kabla ya kuasi chama na kukimbilia CHADEMA.

Hata hivyo, mpaka leo hii Dr. Slaa hajawahi kukabidhi kadi ya CCM.

kwa taarifa tu ni kwamba Dr bado analipia ada ya uanachama

Kwani wapi Nape kasema juu ya uanachama...uzezeta mwingine bhana hadimkinyaa, kauliza tu kadi ya CCM ya Dr. slaa aliirudisha lini na wapi basi......

Mkuu Kageuka, unaona Makupa alikuwa ameanzisha uzi kama huu mapema. Umeona alichokuwa amelenga?

Read between the lines!
 
Last edited by a moderator:
Naomba vuvuzela atuambie ibara gani ya katiba ya magamba inazungumzia kurudisha kadi
Pia atueleze katiba inasemaje iwapo mtu hatarudisha kadi
Dr slaa naamini kwa jinsi alivyoichukia ccm aliichoma hapohapo
 
kwani Nape karudisha kadi ya ccj?
Kwa wafuatliaji wa siasa za
hapa kwetu Tanzania, mtakumbuka ya kwamba Dr. Slaa alikuwa mwanachama
mtiifu wa CCM kabla ya kuasi chama na kukimbilia CHADEMA.

Hata hivyo, mpaka leo hii Dr. Slaa hajawahi kukabidhi kadi ya
CCM.
 
Hata mimi pia nimesikia kuwa Dr Slaa anashirikiana kwa siri sana na viongozi wa ccm hasa wale watumishi wa Umma waliompa nyaraka za EPA, uingizaji wa silaha za ccm, wizi wa kura zake na ule waraka wa kufuatilia watumishi wa umma wanaounga mkono chadema ili wafukuzwa.

Ni kweli kabisa nasikia wanakutana mara nyingi sana tena usiku. Wewe Nyaraka muhimu za kifisadi za serikali angezitoa wapi? Ni watumishi wa serikali ya ccm ambao ni wanaccm ndo wamempa? Wengi hawatakuelewa
 
ukisha jiunga na ccm shule yote inapotea ....jmosi nilimuona nape anajisifia kaenda geita kutoa leseni kwa wachimbaji wadogo...yaani alienda kusoma india kwa ajili ya kugawa leseni? kweli ni kitu cha kusimama hazarani km 2000 toka dar mpaka geita kwa ndege ya kukodi.
 
kwa hiyo tufanye nini sasa? kamuulize wasira ya NCCR aliipelekwa wapi?

Kwa wafuatliaji wa siasa za hapa kwetu Tanzania, mtakumbuka ya kwamba Dr. Slaa alikuwa mwanachama mtiifu wa CCM kabla ya kuasi chama na kukimbilia CHADEMA.

Hata hivyo, mpaka leo hii Dr. Slaa hajawahi kukabidhi kadi ya CCM.
 
  • Asema wengine wanaendelea kuzilipia mpaka sasa.
  • Ahoji Dr. Slaa ameirudisha yake lini..?
  • Awaita waganga njaa sio wanasiasa.


KATIBU wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Itikadi na Uenez Nape Nnauye, amerusha kombora kuwa vigogo wengi ndani ya CHADEMA wameendelea kuwa na kadi za CCM na wengine wanaendelea kuzilipia, jambo linalothibitisha unafiki walionao viongozi wengi wa upinzani nchini.


Akifungua mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Nyamagana, jijini Mwanza, leo uliokuwa na lengo la kupokea maazimio ya Mkutano Mkuu wa nane wa CCM na hotuba ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Kikwete, Nape amedai siasa kwa sasa imevamiwa na makanjanja wengi ambao kazi yao ni kuganga njaa na hivyo huishi kinafiki kwakuwa wakisemacho sicho wanachokiishi.


Sambamba na kombora hilo, Nape ameitaka CCM kuhakikisha inatoa uongozi mzuri ili kudhibiti uvamizi huu wa makanjanja kwenye siasa za hapa nchini.


"Siasa leo imevamiwa na makanjanja waganga njaa, ambao kwakweli wanachosema na wanachotenda ni vitu viwili tofauti, hawaishi maneno yao. Tunao viongozi wengi wa Chadema ambao kucha kutwa wanaishambulia CCM kwa maneno wakati tunawaona wakija kulipia kadi zao za CCM" alisema Nape.


"Kama nasema uongo, Babu Dk. Slaa ajitokeze aseme kadi yake ya CCM aliirudisha lini na kumkabidhi nani. Lakini ninayo orodha ya vigogo kibao wa Chadema ambao huja kulipia kadi zao za CCM kila mara. Huu ni unafiki mkubwa" alisisitiza Nape.


Nape alisema kauli ya Dk. Slaa kudai kwamba anataka kukisafisha Chadema kwa madai kuwa kuna viongozi wa chama hicho ngazi za chini ambao ni mamluki waliopandikizwa na CCM, ni kuweweseka vibaya kwa kuwa wenye kadi za CCM si viongozi hao wadogo tu, hata vigogo wa juu kabisa wa Chadema wana kadi za CCM, hivyo awe makini asije kujikuta anajifukuza na yeye kwa kuwa hakumbuki ni lini alirudisha kadi ya CCM.


Kuhusu DK. Slaa kuitupia tuhuma mbalimbali sekretarite mpya ya CCM, Nape anasema anamshangaa kushughulika na uongozi ndani ya CCM badala ya kujenga Chama chake ambako kinamsambarakitikia mikononi kila kukicha.


"Sana huyu Babu, hivi yeye badala ya kujenga chama chake ambacho kinamsambaratikia mikononi kila siku anaweweseka na sekretariete mpya ya CCM, nani kampa kazi ya kuitathimini sekretariti mpya ya CCM?" alishangaa Nape.


Nape aliwapongeza viongozi wa CCM wilaya ya Nyamagana kwa aina ya mkutano wa Halmashauri Kuu ya wilaya waliyoitisha katika mkakati wa kuendeleza yale yaliyoamuliwa na mkutano mkuu wa CCM taifa.


"Palianza kujengeka utamaduni wa baada ya kufanya maamuzi kwenye vikao hakuna utaratibu wa ngazi za chini kuyachukua maamuzi na kuweka mkakati wa kuyatekeleza, nyie Nyamagana mmefungua ukurasa mpya, nawapongeza na kuagiza wilaya zote nchini na ngazi zingine za chama kuiga mfano huu mzuri wa Nyamagana" alisema Nape.


Aidha amesisitiza agizo la Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kuwa ni lazima kuitoa CCM ofisini na kuipeleka kwa watu kama njia ya kuwa karibu zaidi na watu na kujua matatizo yao na kisha kuyatafutia ufumbuzi.


"Nasisitiza viongozi wa ofisini hatuwataki kwa sasa, lazima kutekeleza kwa vitendo agizo la katibu mkuu la kutoka ofisini na kuipeleka CCM kwa watu, mtaani kuwasikiliza, kujua matatizo yao na kuyatafutia ufumbuzi." alisema Nape.
 
Ndo maana wanamwita vu-v-zela
Hivi hata usiporudisha kadi Katiba ya CCM inasema hivi kuhusu uanachama:
7. (1) Mtu akikubali kuwa Mwanachama itabidi atekeleze haya yafuatayo:-
(a) Atatoa kiingilio cha Uanachama
(b) Atalipa ada ya Uanachama kila mwezi isipokuwa kama akipenda anaweza kulipa ada ya mwaka mzima mara moja.
(c) Atatoa michango yoyote itakayoamuliwa
(2) Viwango vya kiingilio, ada na michango vitawekwa na Halmashauri Kuu ya Taifa.
(3) Uanachama wa mwanachama utakwisha kwa:-
(a)Kufariki.
(b)Kujiuzulu mwenyewe.
(c)Kuachishwa kwa mujibu wa Katiba.
(d)Kufukuzwa kwa mujibu wa Katiba.
(e)Kutotimiza masharti ya uanachama.
(f)Kujiunga na Chama kingine chochote cha siasa.
(4) Mwanachama ambaye uanachama wake unakwisha kwa sababu yoyote ile hatarudishiwa kiingilio alichokitoa, ada aliyotoa wala michango yoyote aliyoitoa.

Nape, Katibu Mwenezi wa Chama anapaswa ajue haya.

My take:
Uongo na kuchafuana bado vinatumika kama mtaji wa kisiasa. Watu wameshaamka, tutumie mambo yenye maslahi ya nchi kufanya siasa.

Kama hajarudisha kadi, Nape anataka kuwaambia wana CCM kuwa Slaa bado mwana CCM?
Nnauye Jr, mtu akishaacha kulipa ada, au kujiunga rasmi na chama kingine si lazima arudishe kadi. Anakuwa si mwanachama kwa mujibu wa katiba ya CCM.
 
Duh yaani CDM kiboko wameanza kumchafua Dr. Slaa! Jana nilikuwa kijiweni na vijana tunakunywa kahawa nikasikia wanasema Dr. Slaa alitumwa na Nyerere kuingia upadri ili ajue huko mapadri wanafanya nini na hakuwa na utashi wa kweli. kwa kifupi wanasema alitumwa na serikali na ni mtu wao hadi leo. Vijana wakawa wanaonyesha wasiwasi juu ya Dr. Slaa na wakasema afadhali Mbowe. Leo naona hii post nimeshangaa. Naona mitandao ya Urais ndani ya CDM inafanya kazi kwa umakini mkuu.
wewe Kimbunga nilikuwa nakuona mchangiaji wa maana hapa JF kumbe ni walewale tu yaani unaenda kuokoteza habari za vijiwe vya kahawa uswahilini unaleta JF? shame on you! jipange au na wewe gamba??
 
kada mwenye kadi ya Ccm ni shibuda tu pekee ndani ya chadema!
 
Kwa hiyo watu wamekosa maji kwa sababu vigogo wa CHADEMA wana kadi za CCM? Au dawa hospitalini zimekosekana kwa sababu vigogo wa CHADEMA wana kadi za CCM? oh... na wengine wameficha hela Uswiss kwa sababu vigogo wa CHADEMA wana kadi za CCM?

Nape anaonesha kiini cha tatizo tulilonalo nchini - wrong people wamepewa madaraka. Watanzania kwa mamilioni wanaogelea kwenye dimbwi la umaskini, hawana maji, barabara mbovu, huduma za afya ni mgogoto mtupu, shule hazina walimu, watu wanalala kwenye mbavu za mbwa.

Nape haoni hayo, na wala hayamgusi kwa sababu anaingia kwenye shangingi na kufunga vioo, huku akihesabu posho! Haya ni madharau kwa wananachi. Haiwezekani kusimama mbele ya umma na kuongea hoja mufilisi kama hizo na kuacha kujadili mambo ya maana, kama kweli wewe unaheshimu watu.

Muda umefika sasa kwa wananchi kukataa kila mara wanapomsikia mwanasiasa anaongea mambo yasiyo na maana. Tanzania tunapitwa kwa kasi sana na nchi jirani, Nape bado anatumia muda wa wananchi kujadili mipasho.

Pengine kwa kumsaidia Nape, badala ya kutumia muda mwingi kuneemesha kitambi chake, angesoma katiba ya CCM hasa kipengele kinachohusu uanachama.


Mwisho, ndugu Kinana anatakiwa akae chini na kumfundisha maadili Nape. Si mara moja au mbili kumsikia Nape akitumia jinsia na umri wa mtu ili kumdhalilisha. Mara kadhaa Nape amekuwa anamuongelea Dr Slaa kwa kumuita 'babu au kibabu'. Sijui CCM wana tatizo gani na umri? Na kama umri ni tatizo, kwanini ndugu Kinana na Mangula bado wapo Lumumba? Kwa kiongozi kama Nape kuwa na lugha chafu kiasi hicho inaashiria kuporomoka kwa maadili ndani ya taasisi anayowakilisha. Ndugu, Kinana tueondeleeni hii fedheha.
 
Stupidity, haya magazeti yamekosa kabisa watu wa kuwapa coverage na kuandika habari za kijinga kutoka kwa mtu mjinga?

Hawa ndio Wahariri aina ya Absalom Kibanda, muda si mrefu nitaanza rasmi kusoma magazeti ya Kenya. naona Tanzania media haziko serious.
 
Huyu naye, Chadema itamkosesha usingizi sana hizo propoganda hazita isaidia Ccm milele
 
Mwenyewe hiyo ya CCM hana.. Jamani ..!! Siasa Za kwetu huku ni matopeni.com
 
Back
Top Bottom