Huelewi nini? Unaishi wapi broda?
Ni kweli kabisa Watanzania ni watu wa ajabu sana. Yanapo kuja mambo ya msingi kama polisi kujichukulia sheria mkononi, watu kuiba raslimali za taifa, viongozi kushindwa kutimiza ahadi walizotoa wakati wa kampeni hakuna anayejadili maswala hayo kiundani. Yanapokuja mambo ya kipuuzi kama mtu kutangaza kutokewa na mwujiza, mtu kuwa na kadi ya CCM wakati yeye si CCM watu wengi sana wanaingia kwenye mjadala. Hili linatufanya tuibiwe mchana kweupe. Yaani ni shida maana vijana wote maskini wako kijiweni wanajadili mpira. Kweli aliyetuloga roho yake ilishaacha mwili muda mrefu sana.
Miongoni mwa viashiria vinavyo onyesha kuwa ccm inakufa ni propaganda za kijinga zisizo msaidia mtanzania kutoka kwenye lindi na mzingo wa umaskini huku ikitegemea watetezi wa propaganda hizo wawe watu aina ya Ritz na chama na muenda zake TUNTEMEKE.
Kinacho zidi kuipa heshima chadema na propaganda za ccm ni jinsi propaganda hizo zinavyojibiwa kwa nguvu za hoja na mashiko yaliyo jaa kauli mujarabu huku zikionyesha obwe la kiuongozi na mtindio wa ubungo kwenye nyuso za magamba.
Naanza kuamini ule usemi wenye ncha kali "Wanao tetea ccm wana akili za maiti".
Kwa nini?
1. Hawashupalii elimu bora kwa watoto wetu kwenye hizi shule za ukata (st kayumba), wao wanashupalia kadi.
2. Hawataki kukilazimisha chama chao kuwataja na kuwachukulia hatua wamiliki wa kagoda, meremeta, deep green finance, epa, rada na trilioni zilizo Uswis. Wao wanalia na kadi ya Dr slaa bila kujali kuwa ni mali yake.
3. Hawashinikizi chama chao kutekeleza ahadi za Trilioni 13 ili kuifanya Kigoma iwe Dubai ya Afrika, barabara za hewani DSM na Tanga jiji la viwanda, wao muhimu kwao ni kadi ya Dr slaa.
4. Mwenyekiti wao amekiri kuwa ccm iache kutegemea polisi, hawashinikizi polisi walio uwa raia wenzao wachukuliwe hatua. Wao chenye umuhimu ni kadi ya Dr slaa.
5. Hawashinikizi wajumbe waliopatikana kwa rushwa na yale magamba yaondolewe kwenye chama chao. Wao akili zinapinga mbizi kufikiria kadi ya Dr slaa tu!
Hivi kuna chembe ya shaka kwa hako ka usemi kwa mifano hiyo michache?! Kama jibu ndiyo hebu angalia orodha ya watetezi wa hoja zao.
1. ZeMarcopolo
2. Ritz
3. TUNTEMEKE
4. chama (angalau siku moja moja huwa anatumia kichwa kuwaza badala ya tumbo kama Ritz
5. Mwendazake Marilia sugu.
6. Mwendazake Faiza fox.
Ukisema hao watu wanatetea hoja za kadi kwa kutumia yale madude ya yule mayor wa darisalamu utakuwa umekosea sana.
*Samahani kama nitakuwa nimewakwaza bahati mbaya au kwa makusudi*
Kila jema na lenye kheri lisiwaponyoke na mbarikiwe hadi mpigwe na butwaa.
Wewe hata ukiambiwa siku zako na Chama chako za kufa zinahesabika utataka ushahidi wa saa dakika na sekunde ilhali unakufa. Rest in peace RITZ rest to he'll CCM
Huyu Dr. Slaa ni ndumilakuwili; CCM anataka na CDM anatamani
Nimejaribu kuangalia wapi Dr Slaa kakanusha sijaona.
kwa hiyo??!! Unataka kujilipua?Nimejaribu kuangalia wapi Dr Slaa kakanusha sijaona.
Kwa mujibu wa Star tv kuwa Dr. Slaa amewambia badala ya kujadili mambo ya kitaifa kama wizi wa nyara za serikali kama wizi wa tembo watanzania wanajaditi kadi, badala ya kujadili kwa nini watu wanalala njaa watu wanajadili kadi, watu wanauwawa na polisi watu wanajadili kadi.
Dr. Slaa kawauliza hivi hao wanaotoa matamko mmewachunguza na kuwajua ni kina nani??
Ukiwatazama watu hao ni mbumbumbu wa sheria na hawajui wanachokifanya na tunapoteza taifa kwa mambo ya kipuuzi tunaacha kujadili mambo ya kitaifa na mafisadi wanatumia mwanya huo kuiba zaidi raslimali za taifa
Mkuu, hakuna anayejua kila kitu, ni kumwelekeza atakuja kuwa jembe huko mbeleni. Na uhakika kuna wengine wengi tu wanapata maujanja kupitia hapa jamvini. Na pengine mazingira au sehemu aliyopo pamoja na kuwa kamaliza shule bado hakubahatika kupata kujifunza yaliyo nyuma ya pazia. Hivyo ushauri wangu ni kwake kuwa tayari kuchukua hizi kama changamoto za kujifunza zaidi. Otherwise, tumsaidie kijana ajifunze.Huyu Kisandu ana uwezo mdogo sana wa kujiongoza yeye mwenyewe,hajitambui,anazungumza kama vie ni monita wa arasa na sio kiongozi wa vijana katika mkoa,Sishangai kuona mkoa kama Tanga CDM haina ushawishi mkubwa kwa sababu watu wenye upeo mdogo kama Kisandu eti ndio viongozi!
Wameumbuka sana.Sasa yule kijana aliyejinadi kuwa ana digrii ya sheria sijui atakuwa katika hali gani.Tusikubali kutoka kwenye mstari.Hoja ni mabadiliko tu
Wapi kakanusha???Kwa mujibu wa Star tv kuwa Dr. Slaa amewambia badala ya kujadili mambo ya kitaifa kama wizi wa nyara za serikali kama wizi wa tembo watanzania wanajaditi kadi, badala ya kujadili kwa nini watu wanalala njaa watu wanajadili kadi, watu wanauwawa na polisi watu wanajadili kadi.
Dr. Slaa kawauliza hivi hao wanaotoa matamko mmewachunguza na kuwajua ni kina nani??
Ukiwatazama watu hao ni mbumbumbu wa sheria na hawajui wanachokifanya na tunapoteza taifa kwa mambo ya kipuuzi tunaacha kujadili mambo ya kitaifa na mafisadi wanatumia mwanya huo kuiba zaidi raslimali za taifa
Hauna uwezo wa kuona, mambo haya sio saizi yako.Nimejaribu kuangalia wapi Dr Slaa kakanusha sijaona.