Elections 2010 Dr. Slaa awe kiongozi mkuu wa Chadema kuelekea Uchaguzi Mkuu?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,476
39,995
Mojawapo ya faida alizonazo mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM kuelekea uchaguzi mkuu ukiondoa kuwa yeye ni Rais ni ukweli kwamba yeye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM. Hivyo, licha ya kwamba ni mgombea wa Urais aliyesimamishwa na chama Rais Kikwete vile vile ana ujiko na nguvu nyingine ya kutoa uelekezi kwenye chama kama Mwenyekiti wa chama. Ukweli huu vile vile unamhusu mgombea wa Urais kwa tiketi ya CUF Prof. Ibrahim Lipumba ambaye naye ni Mwenyekiti wa chama chake.

Kwa upande wa CHADEMA uamuzi wa kumsimamisha Katibu Mkuu wa chama chake kuwa Mgombea wa Urais na kumwacha Mwenyekiti ambaye atakuwa anagombea Ubunge unasababisha matatizo kadhaa ya kiuongozi ambayo naamini yasipojibiwa kwa haraka, kwa makusudi na kwa weledi wa juu yataamua kama Chadema inafanya vizuri kwenye kura za Urais au la.

Kwa mtindo uliopo sasa ndani ya Chadema bado Mwenyekiti ana nguvu zaidi za kutoa maelekezo na mwelekeo wa chama kuelekea kampeni ya Urais. Lakini hilo lingekuwa si tatizo sana kama Mwenyekiti asingekuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge vile vile. Lakini kwa vile ni mgombea basi maswali ya kiutendaji yanajitokeza na kama mfumo huu utaathiri mwelekeo wa kampeni.

Kwenye nchi nyingine za kidemokrasia yule anayekuwa mgombea wa Urais au Uwaziri Mkuu ndiye anakuwa kiongozi mkuu wa chama na viongozi wengine wote wa chama wanakuwa nyuma yake kufuata mwelekeo na maelekezo yake. Hivyo, Barack Obama ambaye alikuwa mgombea wa Urais alipopitishwa tu kuwa mgombea wa Urais viongozi wote wa Chama cha Democrati walikuwa nyuma yake kufuata maelekezo yake akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Dr. Howard Dean. Kule Uingereza kiongozi mkuu wa chama cha Conservatives ni Waziri Mkuu David Cameron.

Kwa maneno mengine, Dr. Slaa kuelekea uchaguzi Mkuu anatakiwa kuwa ndio kiongozi mkuu wa Chadema kwa maana ya kutoa mwelekezo, maelekezo, mtazamo, mikakati na maono ya chama kiwe vipi kuelekea ushindi. Yaani, Dr. Slaa hapaswi kuwa chini ya Mwenyekiti Mbowe bali anatakiwa kuwa juu ya uongozi wa kimuundo wa Chadema hasa ikizingatiwa kuwa akipata Urais bado atatakiwa kuwa kiongozi mkuu wa chama.

Hili hata hivyo utekelezaji wake ni mgumu.

- Je Mwenyekiti Mbowe yuko tayari kumuacha Dr. Slaa aonekane kuwa ndiyo kiongozi wa juu ndani ya chama?

- Je viongozi wengine wa Chadema kama Makamu wa Mwenyekiti, Zitto, na wengine wako tayari kujipanga nyuma ya Dr. Slaa, kumsikiliza na kufuata maelekezo yake ikiwemo kuwapangia majukumu au kuwaomba watekeleze mambo fulani ili kufanikisha kampeni?

- Je, wana Chadema ambao ni mashabiki wa mtu mmoja mmoja (kama mashabiki wa Mbowe au Zitto) wako tayari kuja nyuma ya Dr. Slaa kama mgombea wa Urais na kuondoa utii wao (loyalty) kwa watu "wao"?

- Je kwa kumfanya Dr. Slaa kiongozi mkuu kutasababisha kunyang'anyana madaraka kwamba sasa Mbowe, Zitto n.k hawana madaraka sana?

Maswali hayo yote yanahitaji majibu kwani ni wazi kwamba bila ya kuwa na unified command ambayo iko nyuma ya mgombea wa Urais ni vigumu sana kujipanga kupata ushindi. Faida kubwa ya kumfanya Dr. Slaa awe kiongozi mkuu ni pamoja na kuwafungua hawa viongozi wengine kuweka mkazo katika majimbo wanayogombea pasipo kuwa na wasiwasi na maswali ya kitaifa. Maanake matatizo ambayo tumeyaona hadi hivi sasa kuhusu wagombea na kura za maoni yangeweza kuelekezwa kwa Dr. Slaa na timu yake na kuyatolea maamuzi badala ya kusubiri uongozi wa kitaifa ambao mara kwa mara sasa utajikuta ukitawanyika kutetea majimbo.

Kwa mtu yeyote anayeweza kuangalia tunaweza kuona kuwa tayari Chadema wamefanya kosa moja kubwa (kama nilivyoandika kwenye Cheche wiki iliyopita). Lakini kosa la pili inaonekana linaendelea kufanyika na litawagharimu sana kama hawataamua kwa haraka na kwa makusudi kulishughulikia. Yaani, uongozi mzima wa Chadema ngazi ya taifa, uwe chini, nyuma na kuongozwa na mgombea wa Urais Dr. Slaa. Kwa kufanya hivyo wataichukua kampeni yao kutoka ilipo sasa na kuanza kuonekana wako tayari kwenda "kule".

Vinginevyo, tusiwasingizie CCM mambo yakienda kombo. Mengine yamo ndani ya wana Chadema kuyasimamia.

M.M.
 
Hata mimi hili swala nilikuwa najiuliza sana.
It doesnt make sense rais wa nchi awe anaripoti kwa boss mwingine (ambaye ni Mwenyekiti wa Chama)
Hapa ndipo mapungufu ya wazi (ambayo nadhani yataikosti CHADEMA) yanapoonekana.
Lakini najiuliza Katiba ya CHADEMA inasemaje juu ya Swala hili?
Katiba inaruhusu mwenyekiti abadilishwe kabla ya muda wake kwisha?
 
si lazima wabadilishe mwenyekiti; yaani mwenyekiti anaendelea kuwa Mwenyekiti lakini uongozi wa chama kimtazamo na mwelekeo unatolewa na mgombea wa Urais. Kwa hiyo hawahitaji kubadili Katiba ni makubaliano ya kimantiki tu.
 
I think hili linawezekana na muhimu likafanyika ili kumuwezesha mgombea Urais kuwa Msemaji wa Chama, kwamba Slaa akisema maana CHADEMA imesema
 
si lazima wabadilishe mwenyekiti; yaani mwenyekiti anaendelea kuwa Mwenyekiti lakini uongozi wa chama kimtazamo na mwelekeo unatolewa na mgombea wa Urais. Kwa hiyo hawahitaji kubadili Katiba ni makubaliano ya kimantiki tu.
umechoka fikra na mawazo! si lazma Mgombea awe Mwenyekiti au Mwenyekiti awe Mgombea kwani katiba ya Chadema inasemaje? na pia huoni ni mzigo mkubwa wa Dr Slaa (rais Mtarajiwa) kuongoza chama na wakati huohuo kuongoza serikali?
 
Hata wafanyeje CCM watafunika tu....

Nimeshasema huko nyuma kuwa CCM is a juggernaut. Haiwezi kuanguka mwaka huu, 2015, 2020, au hata 2025. Yahifadhini haya maneno yangu ikiwezekana myawekee sticky nyinyi akina Invisible, Silencer, Painkiller, etc.
 
Sijaona mantiki ya kuiacha wiki hii ya kwanza ya kampeni iishe kimyakimya wakati CCM wakiwa busy na kampeni, shime Chadema..muda hautoshi huu!!
 
kwa mantiki ya kawaida kabisa, CHADEMA hawafai kupewa nchi, maana badeo hawajajipanga kama walishindwa kuona jambo dogo hili basi uongozi wa nchi ni mkubwa zaidi, wabakie kujifunza kwanza.
swala hapa ni usalama wa nchi yetu na rasilimali hawa wachaga (mwanyekiti) watatuuza wakaishi Italy
 
Mojawapo ya faida alizonazo mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM kuelekea uchaguzi mkuu ukiondoa kuwa yeye ni Rais ni ukweli kwamba yeye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa CCM. Hivyo, licha ya kwamba ni mgombea wa Urais aliyesimamishwa na chama Rais Kikwete vile vile ana ujiko na nguvu nyingine ya kutoa uelekezi kwenye chama kama Mwenyekiti wa chama. Ukweli huu vile vile unamhusu mgombea wa Urais kwa tiketi ya CUF Prof. Ibrahim Lipumba ambaye naye ni Mwenyekiti wa chama chake.

Kwa upande wa CHADEMA uamuzi wa kumsimamisha Katibu Mkuu wa chama chake kuwa Mgombea wa Urais na kumwacha Mwenyekiti ambaye atakuwa anagombea Ubunge unasababisha matatizo kadhaa ya kiuongozi ambayo naamini yasipojibiwa kwa haraka, kwa makusudi na kwa weledi wa juu yataamua kama Chadema inafanya vizuri kwenye kura za Urais au la.

Kwa mtindo uliopo sasa ndani ya Chadema bado Mwenyekiti ana nguvu zaidi za kutoa maelekezo na mwelekeo wa chama kuelekea kampeni ya Urais. Lakini hilo lingekuwa si tatizo sana kama Mwenyekiti asingekuwa mgombea wa nafasi ya Ubunge vile vile. Lakini kwa vile ni mgombea basi maswali ya kiutendaji yanajitokeza na kama mfumo huu utaathiri mwelekeo wa kampeni.

Kwenye nchi nyingine za kidemokrasia yule anayekuwa mgombea wa Urais au Uwaziri Mkuu ndiye anakuwa kiongozi mkuu wa chama na viongozi wengine wote wa chama wanakuwa nyuma yake kufuata mwelekeo na maelekezo yake. Hivyo, Barack Obama ambaye alikuwa mgombea wa Urais alipopitishwa tu kuwa mgombea wa Urais viongozi wote wa Chama cha Democrati walikuwa nyuma yake kufuata maelekezo yake akiwemo Mwenyekiti wa chama hicho Dr. Howard Dean. Kule Uingereza kiongozi mkuu wa chama cha Conservatives ni Waziri Mkuu David Cameron.

Kwa maneno mengine, Dr. Slaa kuelekea uchaguzi Mkuu anatakiwa kuwa ndio kiongozi mkuu wa Chadema kwa maana ya kutoa mwelekezo, maelekezo, mtazamo, mikakati na maono ya chama kiwe vipi kuelekea ushindi. Yaani, Dr. Slaa hapaswi kuwa chini ya Mwenyekiti Mbowe bali anatakiwa kuwa juu ya uongozi wa kimuundo wa Chadema hasa ikizingatiwa kuwa akipata Urais bado atatakiwa kuwa kiongozi mkuu wa chama.

Hili hata hivyo utekelezaji wake ni mgumu.

- Je Mwenyekiti Mbowe yuko tayari kumuacha Dr. Slaa aonekane kuwa ndiyo kiongozi wa juu ndani ya chama?

- Je viongozi wengine wa Chadema kama Makamu wa Mwenyekiti, Zitto, na wengine wako tayari kujipanga nyuma ya Dr. Slaa, kumsikiliza na kufuata maelekezo yake ikiwemo kuwapangia majukumu au kuwaomba watekeleze mambo fulani ili kufanikisha kampeni?

- Je, wana Chadema ambao ni mashabiki wa mtu mmoja mmoja (kama mashabiki wa Mbowe au Zitto) wako tayari kuja nyuma ya Dr. Slaa kama mgombea wa Urais na kuondoa utii wao (loyalty) kwa watu "wao"?

- Je kwa kumfanya Dr. Slaa kiongozi mkuu kutasababisha kunyang'anyana madaraka kwamba sasa Mbowe, Zitto n.k hawana madaraka sana?

Maswali hayo yote yanahitaji majibu kwani ni wazi kwamba bila ya kuwa na unified command ambayo iko nyuma ya mgombea wa Urais ni vigumu sana kujipanga kupata ushindi. Faida kubwa ya kumfanya Dr. Slaa awe kiongozi mkuu ni pamoja na kuwafungua hawa viongozi wengine kuweka mkazo katika majimbo wanayogombea pasipo kuwa na wasiwasi na maswali ya kitaifa. Maanake matatizo ambayo tumeyaona hadi hivi sasa kuhusu wagombea na kura za maoni yangeweza kuelekezwa kwa Dr. Slaa na timu yake na kuyatolea maamuzi badala ya kusubiri uongozi wa kitaifa ambao mara kwa mara sasa utajikuta ukitawanyika kutetea majimbo.

Kwa mtu yeyote anayeweza kuangalia tunaweza kuona kuwa tayari Chadema wamefanya kosa moja kubwa (kama nilivyoandika kwenye Cheche wiki iliyopita). Lakini kosa la pili inaonekana linaendelea kufanyika na litawagharimu sana kama hawataamua kwa haraka na kwa makusudi kulishughulikia. Yaani, uongozi mzima wa Chadema ngazi ya taifa, uwe chini, nyuma na kuongozwa na mgombea wa Urais Dr. Slaa. Kwa kufanya hivyo wataichukua kampeni yao kutoka ilipo sasa na kuanza kuonekana wako tayari kwenda "kule".

Vinginevyo, tusiwasingizie CCM mambo yakienda kombo. Mengine yamo ndani ya wana Chadema kuyasimamia.

M.M.
Nina wasiwasi na usahihi wa hiyo red hapo maana najua Campaign team ndo ilikuwa inamuamulia Obama nini afanye na nini ajibu! sidhani kama ulichosema ni kweli na Hward Dean bado alikuwa superior na hata sasa ni superior kwenye chama!
 
ni wazi hujui siasa za Marekani. Kiongozi Mkuu wa chama cha demokrat ni Rais anayetokna na chama cha Demokrati yaani Barack Obama. Hii haiondoi au kunyang'anya shughuli za kiutendaji wa siku kwa siku wa chama unaofanywa na Howard Dean.
 
Hata wafanyeje CCM watafunika tu....

Nimeshasema huko nyuma kuwa CCM is a juggernaut. Haiwezi kuanguka mwaka huu, 2015, 2020, au hata 2025. Yahifadhini haya maneno yangu ikiwezekana myawekee sticky nyinyi akina Invisible, Silencer, Painkiller, etc.
Mbona hujajibu hoja ya MKJJ unarukia CCM kufunika.
 
ni wazi hujui siasa za Marekani. Kiongozi Mkuu wa chama cha demokrat ni Rais anayetokna na chama cha Demokrati yaani Barack Obama. Hii haiondoi au kunyang'anya shughuli za kiutendaji wa siku kwa siku wa chama unaofanywa na Howard Dean.
uache kuchemka angalia hapa halafu uniambie where is Obama in daily to daily running of the party? The Democratic Party
 
CHADEMA wasilaumiwe mambo hayawezi kukaa vizuri mara moja;

Ni mchakato wa muda mrefu. Nafikiri CHADEMA ni vema wakazingatia ushauri.
 
uache kuchemka angalia hapa halafu uniambie where is Obama in daily to daily running of the party? The Democratic Party

ndio maana nasema usome kilichoandikwa siyo unachofikiria kimeandikwa; ni wapi nimesema Dr. Slaa afanye "daily to daily running of the party"? Na niwapi nimesema Obama anafanya shughuli za kila siku za chama. Soma pole pole na taratibu (yaweza kuwa ni kitu kile kile) halafu utaona ninachosema hasa ni nini.
 
Back
Top Bottom