WanaJF!
Katika hali iliyokuwa ikitazamiwa kutokea kwenye mkutano wa CHADEMA huko Iramba, sasa yametimia kwani mkutano umeanza takribani saa 1 lililo pita na matangazo ya kuhamasisha yamekuwa yakisikika kote hapa Iramba, ila mwitikio wa wananchi kwenye mkutano huo ni mdogo na hali hiyo imemfanya Dr Slaa kuduwaa na kubaki kukuna kichwa tu.
Jambo ambalo limemponza Dr Slaa na kumuingiza kwenye aibu hiyo, ni kufuatia kudanganywa na wapambe wake kuwa yeye ana kubalika Iramba na wananchi wanamtambua kama rais wao, badala yake Dr Slaa ameonekana kama kituko mbele ya wananchi ingawa alikuja na mbwembwe nyingi hapa kijijini.
Dr Slaa, CCM YATUTOSHA!
Hamy- D
Umeambiwa na watu zikiwekwa picha hapa usikimbie. Mara nyingi busara ya kawaida imekuwa ikitutuma hustahili kujibiwa wala kupata attention ambayo umekuwa ukiisaka kwa nguvu zote, kutoka kwa viongozi wa CHADEMA, kwa kuanzisha thread za uongo wa wazi kabisa huku ukitaja majina yao.
Mkutano wa leo kwa Wilaya ya Iramba ulifanyika eneo la Kiomboi. Ulikuwa mkutano mzuri sana kama ilivyo ada ya mikusanyiko inayohusu CHADEMA. Watu wa Kiomboi walikuwa na shauku ya kutoa maoni kwenye Rasimu ya Katiba Mpya, kupitia Mabaraza Huru ya CHADEMA yanayofanyika kwenye mikutano ya hadhara.
Wakati wewe unapiga porojo kwa ajili ya kujifurahisha kwa muda (comforting zone) kama ilivyo kawaida ya watu wa CCM, muda si mrefu utawekwa ushahidi hapa wa picha na namna ambavyo tayari simu namba 0782 248224, inayotumika kupokea maoni kwa njia ya ujumbe mfupi, inavyopokea msg kwa wingi kutoka Iramba.
Timu ya Katibu Mkuu, Dkt. Slaa tayari inakaribia kutua Singida, ambako mkutano mkubwa unaendelea kuwasubiri, baada ya wananchi wa Kiomboi, Iramba kupata fursa yao ya kutoa maoni kwenye mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Mjumbe wa Kamati Kuu, Mabere Marando na Dkt. Slaa.
Mind you, unaposema mwitikio ni mdogo ni kitu very very relative. Tukusaidie tu, ili usiendelee kuaibika mbele ya watu wenye akili kama hapa jukwaani, ungeweza kuweka idadi ya watu waliohudhuria mkutano huo Vs jumla ya idadi ya wakazi wa eneo husika, ili conclusion yako ionekane kuwa ni valid.
Vinginevyo ni mwendelezo wa watu wa CCM kutafutanhoha za kuokoteza kwa ajili ya liwazo la muda mfupi, wakati CHADEMA inazidi kushika kasi, kuongeza ushawishi na kusimamia masuala ya msingi kwa niaba ya wananchi, ikiwemo mchakato wa Katiba Mpya.