Kama sio msemaji wa Chadema unahusika vipi hili kaa kimya.Amani iwe nanyi wanaJF!
Ndugu zangu wanaJF na wapenzi wa mabadiliko nchini kwa ujumla....!
Hivi kama Dr Slaa amehudhuria vikao vyote vya kamati kuu ya chama na waliafiki na kuridhia kumpokea ndugu EDWARD LOWASA,Wakaweka msharti ya kumpokea ikiwemo ni pamoja na kukuueleza umma ukweli juu ya kampuni hewa ya Richmondi na sababu ya kujiuzulu kwake uwaziri mkuu mwaka 2008.
Lowassa alikubaliana na masharti hayo na akatekeleza! Je, Dr Slaa kama mtu mwenye akili timamu na uelewa wake tunavyoujua alikua na sababu ipi ya msingi kususia wenzake! Kama ingekua ni kweli si angeiangikia kamati kuu barua juu ya kutokukubaliana na suala hilo?
Ninyi msiokua wanachadema nani kawapa mamlaka kujua na kumfuatilia Dr Slaa anafanya nini na yuko wapi? Anawahusu nini? Je, kama mwenyekiti anawaambieni anawasiliana naye mnataka nini zaidi? Mnajua wanawasiliana nini viongozi hao wakuu wa CHADEMA!
Mimi sio msemaji wa CHADEMA lakini sioni sababu ya msingi ya Dr Slaa kususa.
Hakika wanaomtukana DR.#Slaa wataalaniwa na #Mungu kwani ni mjinga na mpuuzi pekee yake ambaye hawezi kuona mchango mkubwa na kazi kubwa aliyoifanya Dr.Slaa kwa faida ya chama pamoja na taifa kwa ujumla.
Lengo letu ni kuiondoa ccm madarakani bila mchango wa Dr.#Slaa hatofanikiwa kabisa .Dr.#Slaa watu wengi tuna imani kubwa na wewe tunakusubiri tumeambiwa kwenye utashiriki kwenye vikao vya kamati kuu ya chama tunakusubiri kwa hamu kwa hamu kubwa tunakuombea kwa #Mungu afya njema ,ulinzi wa #Mungu siku zote tunakuhijitaji sana tuna imani kubwa na wewe .dada Tetty umepitia huku?
Dr slaa yupo lakini Kwa sasa yupo na Nape na Membe wamemficha kwao wanamhesabia Dola nyingi toka kwenye yale mapesa lundo ya Marehemu Gadafi kisha watamsaidia namna ya kutorokea italy mafichoni au hata marekani , ccm wapo busy wanabuni mbinu za kuwafarakanisha Ukawa huu ni Mgodi mkubwa wengi watavuna pesa nyingi kupitia huu Mladi waliobuni yaani bajeti ya mabilioni ya kuwachakaza wapinzani hizo pesa zitakuwa zinapitia mikononi mwa Nape anapiga cha juu kabla ya kwenda Kwa waliyemkusudia, Nape anasali usiku na mchani Dili litiki Apate pesa Kwa mgongo huo wa kuwavuruga Upinzani
Ni ngumu kwa wakati uliopo. Usisahau mmeambiwa lowasa kaja na mamilioni ya wanachama, mamilioni hao wanachojua ni lowasa. Ndiyo maana wote kama makondoo sasa mnaimbishwa tuna imani na lowasa.WanaJF na hasa wana CHADEMA wenzangu tuwe makini sana na maandishi yetu hapa jukwaani kuhusu huu ukimya wa DR SLAA, tafadhalini sana, DR ni kiongozi mkubwa sana anastahili kuheshimiwa, wale wenye uchungu na CHADEMA na tunaofahamu tulipotoka hatuwezi kumkashifu huyu mtu, kwa lipi hasa ? Acheni kabisa jambo hilo, sikupenda kuandika jambo hili maana linaweza kuendeleza malumbano zaidi lakini nimelazimika kuliweka kama angalizo.
Mzee Slaa apumzike sasa, kama amefikia hatua ya kufichwa na Mchumba wake, hafai huyo!
Vipi mkuu ile biashara yako ya unga inaendeleaje?
Naona CCM wanashindwa kumdadi Magufuli na baadala yake wanaparamia mambo ya CDM.
Teh teh teh!!
Laki si Pesa, anatoa tamko kuwa Dr.Slaa awapishe kwenye chama chao Chadema.
Siasa hizi tutasikia mengi.
wana jf.
Kesho vikao vya kamati kuu ya chadema vinaendelea ili kupanga mikakati ya kuhakikisha ukawa inapata ushindi wa kishindo october .
Ili mikakati ya ushindi kwenye uchaguzi mkuu october iende vizuri, wajumbe wote wanatakiwa wawepo akiwemo katibu mkuu wa chama dr. Wilbroad slaa ambae mpaka sasa hivi hajulikani alipo, endapo dr. Slaa hatahudhuria kikao kesho naomba kamati ya maadili imchukulie hatua kali za kinidhamu ili kulinda kanuni na maadili ya chama.
chadema sio mali ya mtu binafsi ,ni mali ya watanzania wote, na hakuna mtu mkubwa kupita chama.
Asietaka ukombozi wa nchi october atupishe.
Inasikitisha sana Slaa amefichwa mpaka simu zake zote kazima.
Mkuu mimi nilikuwa shabiki wa huyu babu lakini baada ya kujua kwamba mshumbushi ndio mwenye remote ya huyu padri nimemdharau sananaunga mkono,huyu hafai hata kushika nchi maana atatuletea yaleyale ya mke toka mtwara na watoto ake wa msoga kujimilikisha chama na kumzidi mume na baba yao katika maamuzi yenye tija na nchi. Slaa kaonyesha udhaifu mkubwa sana maana unapo milikiwa na mwana mke wewe hufai katika jamii.
Mwenzake lowassa anamsimamo hata marafiki zake na mkewe walipo jaribu kumshauri abakie ccm na awe mnafiki akaliona hilo na kukataa. saa mfumbuzi bin slaa ana mremote contol slaa wake
Kweli CCM mmeishiwa sera! Hivi Magufuli mtamnadi lini?
jamani mjue kuwa yule ni padre do kaweka mfungo na kajifungia. Kuna ule mfungo wenyewe wakatoliki huwa ukifungu huruhusiwi kuongea na mtu