Dr. Slaa anastahili kuheshimiwa

Dr. Slaa anastahili kuheshimiwa

kwa maneno haya chadema inasafri ndefu inabidi ijitafakari kama wanachama ambao mbowe anasema atapata mamilioni inabidi ajitafakari sana

Mbowe atakuwa kapata wanachama mamilioni ambao hawana hata sifa ya kupiga kura.
 
Dr apumzike kwa amani kabisa tumesha choka sasa hakuna namna mkuu tunapigana na ccm dr apumzike kama ameamua atuachie ccm hawawezi sisi wana nchi tutapigana nao hata makonde kavu kavu!
 
Waswahili walisema penye udhia penyeza rupia hakika nimeyaona nimekumbuka yalipata Bw Yesu kwa yuda alipomsaliti leo chadema tunamsifu EL mtu safi Yesu wangu
 
Si wote wanaomtukana Dr. Slaa ni wanachadema. Wengine ni watu wa kitengo ili waonekane wanaCDM hawana shukrani. Kwa hiyo suala hili linatakiwa liache kufanyiwa kampeni ili muda ukifika Dr. Slaa ataweka wazi kama alivyosema.

asante sana mkuu .
 
We umeona wapi mgeni anakaribishwa nyumbani anaingia mpaka chumbani na kukabidhiwa familia aiongoze? Lowasa sasa hivi ndio kiongozi mkuu wa Chadema,, Akina Mbowe hawana chao tena wanasubiri maelekezo kutoka kwa Lowasa
natangaza rasmi kukudharau kabisa kwa kipindi chako chote kilichosalia hapa duniani .
 
Wanajf na hasa wanachadema wenzangu tuwe makini sana na maandishi yetu hapa jukwaani kuhusu huu ukimya wa DR SLAA , tafadhalini sana , DR ni kiongozi mkubwa sana anastahili kuheshimiwa , wale wenye uchungu na cdm na tunaofahamu tulipotoka hatuwezi kumkashifu huyu mtu , kwa lipi hasa ? acheni kabisa jambo hilo, sikupenda kuandika jambo hili maana linaweza kuendeleza malumbano zaidi lakini nimelazimika kuliweka kama angalizo .

CHADEMA asili hawezi mkashifu SLAA.,

hao ni wafa njaa.
 
Wanajf na hasa wanachadema wenzangu tuwe makini sana na maandishi yetu hapa jukwaani kuhusu huu ukimya wa DR SLAA , tafadhalini sana , DR ni kiongozi mkubwa sana anastahili kuheshimiwa , wale wenye uchungu na cdm na tunaofahamu tulipotoka hatuwezi kumkashifu huyu mtu , kwa lipi hasa ? acheni kabisa jambo hilo, sikupenda kuandika jambo hili maana linaweza kuendeleza malumbano zaidi lakini nimelazimika kuliweka kama angalizo .

Mkuu uko sawa Kabisa. Anayemdharau huyu Mzee ni maccm waliokatwa.
 
nyie mtakuwa wapuuzi kweli kweli, hivi akina mungi ndo wageni walikuja na lowasa? akina rockspider? acheni ujinga. fuateni ushauri wa red blood cell hapo juu.

umesoma comment za kina laki si pesa ambao ni kina pro lowasa?
 
Chama bila watu si chama naamini katiba na ilani vyamavyote ni safi shida ni watekelezaji tunaposema hatuna shida na mtu tunashida nachama kuna mantik gani.
 
mkuu uko sahii kabisa wanaomtukana ni pro lowasa ambao hawajaonja machungu ya Kuwa cdm

achana na hao, ukweli ni kwamba wanaoongoza kumtukana slaa humu ndani ni pro-magwanda tena wa siku nyingi. nimekutolea mfano kama akina mungi. achana na hao wa magamba wanafahamiaka siku zote. nashanagaa unazuia mwanga wa jua kwa ungo. sijui akili za wapi hizi,
 
Ataheshimika tu, naye ajue heshima yake inatokana na kusimamia nguvu ya umma na umma ndio sisi!
 
anastahili kuheshimiwa , wale wenye uchungu na cdm na tunaofahamu tulipotoka hatuwezi kumkashifu huyu mtu , kwa lipi hasa ?
Tunafahamu tulipotoka, tumetoka nae wapi, C.C.M?

Again, hakuna standard hiyo CHADEMA ya kusema tunaheshimu tulipotoka na mtu. Narudia, Zitto Kabwe amefukuzwa kama paka mwizi bila kujali alipokitoa chama hiki nyakati zile kina Wilbrood Slaa wakitokea C.C.M., na hata Dr. Slaa alipokuja CHADEMA kikawa bado chama cha kikanda, wakina Zitto wakakipeleka mipakani mwisho wa nchi Kigoma huko. Lakini akaja kufukuzwa kundini utadhani kaiba sadaka kanisani, kisa, kutaka kufanya mageuzi ya uongozi kwenye chama kilichohodhiwa na koo chache.

Kwa hiyo, tumtetee Dr. Slaa kwa yote lakini si kwa kusema amekitoa chama mbali. CHADEMA hatupendi mtu kwa kuangalia mchango wake kwa chama, hatuna standard hiyo.
 
Ni kwamba Dr Slaa kinachomtesa sio kukosa nafasi ya kugombea uraisi la hasha kinachomtesa ni mwanamke anaetaka kuwa firstlady mushumbusi hii inapunguza sifa kwa DR kuwa kiongozi kwa maana hana sauti kwa mwanamke sasa akiwa Raisi maana yake atatawala kwa maelekezo ya mwanamke, amwambie mke wake kuwa ata uchaguzi wa uraisi alioshiliki Dr alipendekezwa kugombea sio kwamba aliomba kugombea, mtaramu mbowe ndie aliekuwa nanafasi ya kugombea alikini alivyotumia watalaamu wa utafiti ilionekana Dr kwa wakati ule ndio alikuwa mpizani wa kikwete, lakini sasa ni makufuli Dr Sla ana ubavu wa kumzuia Pombe makufuli mwenye ubavu ni Lowasa tu ndie anaeweza kumshida pombe makufuli,mambo binafsi tuweke pembeni sisi wanachadema tunataka ushindi tu josefine akae pembeni asitualibie chama
 
Wana JF,

Kesho vikao vya Kamati Kuu ya CHADEMA vinaendelea ili kupanga mikakati ya kuhakikisha Ukawa inapata ushindi wa kishindo October .

Ili mikakati ya ushindi kwenye uchaguzi mkuu october iende vizuri, wajumbe wote wanatakiwa wawepo akiwemo Katibu Mkuu wa Chama Dr. Wilbroad Slaa ambae mpaka sasa hivi hajulikani alipo, endapo Dr. Slaa hatahudhuria kikao kesho naomba Kamati ya Maadili imchukulie hatua kali za kinidhamu ili kulinda kanuni na maadili ya chama.

CHADEMA sio mali ya mtu binafsi ,ni mali ya watanzania wote, na hakuna mtu mkubwa kupita Chama.

Asietaka ukombozi wa nchi October atupishe.
 
Back
Top Bottom