Dr. Slaa anastahili kuheshimiwa

Dr. Slaa anastahili kuheshimiwa

Dr.WILBROAD SLAA ALINUNULIKA,HILO LIKO WAZI,ILA SISI WATANZANIA:-

-TUTAMPIGIA KURA EDWARD LOWASSA NA SIO MAGUFULI. Hakika!

Mkuu unaushahidi na unayoongea kwamba Slaa amenunulika?
 
Baada ya wananchi kuona mafanikio yake, walimwomba agombee ubunge, na kweli akagombea kupitia CCM, CCM waliona kama ni mgeni katika siasa wakakata jina lake na kumpa mshindi wa tatu aliyekuwa mbunge wakati huo. Hivyo basi wananchi wakamshawishi kuhamia chama cha upinzani na kuwa wangempa kura, Dr Slaa akahamia CHADEMA wakati huo CHADEMA hakina umaarufu kama sasa, chama kilichikuwa maarufu kilikuwa ni NCCR mageuzi. Dr Slaa akashinda kwa kishindo na kuwa mbunge wa kwanza kutoka CHADEMA na Dr Warid Kabour kutoka jimbo la Kigoma mjini. Tangu mwaka huo Dr Slaa alikifanya CDM kuwa chama chenye nguvu kwa kupambana na CCM iliyokuwa na wabunge zaidi ya 80% kwa kusimamia alichoamini bila kuyumba, baade alipata support baada ya Mbunge kijana Zitto Kabwe kuingia bungeni hivyo CDM ikapata nguvu kwa kuwa ilijonyesha ndiyo CHAMA cha kutetea wanyonge. Dr Slaa hajapewa heshima stahili. tuache kumbeza.
Mkuu, hayo yote ni mema na yanafahamika. Ni kama vile tunavyowathamini wazazi. Kwa mapenzi yao wanatafuta mtoto, na akishazaliwa humtunza kwa gharama na kujinyima kukubwa. Wanayoyafanya wazazi ni mambo makubwa na magumu sana kiasi kwamba watu wengi hudiriki kusema kuwa wazazi ni miungu ya duniani kwa mtoto. Kati ya amri ambazo zinaweza kufupisha maisha ya mtu ni kuwadharau wazazi wake.

Hata hivyo ikitokea leo mzazi kaamua kumuua mtoto wake kwa sababu tu eti alipata shida sana kumtafuta, akataabika kumlea na kunfanya kuwa mtu mkubwa na maarufu, ni dhahiri matendo yote ya huyo mzazi yatasahaulika na hatua stahiki za kisheria kuchukuliwa dhidi yake. Hata kama Dr. Slaa aliifanyia mema CHADEMA, kitendo chake ni sawa na uuaji wa mtoto uliyemzaa. Hata kama ukijitetea kuwa ni wako sheria itachukua mkondo wake.

Kisiasa, kukusudia kuua matumaini ya chama, kuna kanuni zake ambazo hazina budi kuchukua mkondo wake. Kejeli badala ya hongera, kuzomewa badala ya kushangiliwa, kudharauliwa badala ya kuheshimiwa na kubezwa badala ya kuthaminiwa ni baadhi tu ya mikondo halali ya kisiasa dhidi ya msaliti wa aina yake. Hakuna m-badala na bahati mbaya hakuna aliye na kinga dhidi ya kanuni hizi.
 
Kuna CHADEMA ASILI na kuna CHADEMA LOWASSA. Hawa CHADEMA LOWASSA hawawezi kumuelewa Dr. Slaa alichosema, watamtukana na kumkashifu sababu hawa ni wahamiaji tu, hawajui uchungu wa CHADEMA. Hawajui mchango wa Dr. Slaa kwa CHADEMA.Hawa ni "friends of Lowassa" 4U MOVEMENTS; ni wahamiaji tu, hawa ndio kila siku wanaandika "ulipo tupo". Lowassa alipokuwepo CCM walikuwa nae. sasa hivi yupo CHADEMA wako nae. Lakini kuna kundi la wanachama, hawa ni CHADEMA asili. CHADEMA asili wanajua uchungu wa CHADEMA, wanamuheshimu Dr. Slaa kama CCM wanavyomuheshimu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere! Hawa CHADEMA asili wanaujua mchango wa Dr. Slaa kwa CHADEMA. Wanafahamu wazi kuwa Dr Slaa ndio aliyekijenga CHADEMA na kufikia hapo kilipo. Kamwe maisha yao yote hawawezi kumpuuza na kumdharau Dr. Slaa. CHADEMA asili ndio wanajua walipotoka na CHADEMA mpaka leo hii. Hawa ni vijana ambao kwao Dr. Slaa ni "hero". Hawa vijana ndio watakao washa moto usiozimika CHADEMA! ....."friends of Lowassa" ni wahamiaji tu, na hawana uchungu na CHADEMA. Kilicho wapeleka pale ni Lowassa tu. Hawa ni watu wasiomjua Dr. Slaa na kwao hana dhamani yoyote ile, hawa ndio watu tunao waona hapa JF wakimtukana Dr. Slaa kwa kila aina ya matusi. Viongozi wa CHADEMA dhambi hii itawatafuna siku zote za maisha yenu. Dhambi ya kuuza chama kwa "fisadi Lowassa" kamwe haitawaacha mkae kwa amani.

ushajiita mtoto wa gamba unataka tukusaidieje sasa
 
kujenga nyumba ni kaz kwan huwez ijenga kwa siku moja, lakin kuiboa nyumba hiyo si kaz kwan unaweza ibomoa kwa dakika kadhaa!! kwa hili alilolifanya hana mchango wowote kwa cdm ya sasa!! hi ni cdm mpya bila wasaliti na ndo mkombozi wa wananchi!!
 
Leo ni aibu kuona comment za kejeli na matusi ambazo wanachama wamekua wakimkosea heshima Dr Slaa.

Kwa namna mzee huyu alivyopambana kwa jasho na damu shukrani aliopatiwa haikumstahili, Hivi kama mti mbichi mmeutenda hivi je mti mkavu mtaufanyaje?

Hii ndio inayoitwa shukrani ya punda, Kwa namna chama hiki kinavyoongozwa kibabe ni wazi wengine wanaofikiri wamesimama basi na wajiandae.

L'su,mny'ka,na wengineo mjiandae siku yenu inakuja.

Naomba nikuulize swali moja kama ifuatavyo:-

Wewe umejenga nyumba nzuri tena kwa gharama kubwa na watu wakakusifia sana, je utakapoanza kuibomoa tena kwa makusudi na bila hata na kuwa na sababu maalum za kuibomoa nyumba hiyo je utaendelea kusifiwa kuwa umejenga nyumba nzuri kweli au utatukanwa na kuonekana hauna akili mbele za watu na jamii nzima?
 
Leo ni aibu kuona comment za kejeli na matusi ambazo wanachama wamekua wakimkosea heshima Dr Slaa.

Kwa namna mzee huyu alivyopambana kwa jasho na damu shukrani aliopatiwa haikumstahili, Hivi kama mti mbichi mmeutenda hivi je mti mkavu mtaufanyaje?

Hii ndio inayoitwa shukrani ya punda, Kwa namna chama hiki kinavyoongozwa kibabe ni wazi wengine wanaofikiri wamesimama basi na wajiandae.

L'su,mny'ka,na wengineo mjiandae siku yenu inakuja.
Huruma hii kwa CHADEMA inatoka wapi? Naona mbinu zenu chafu kuzuia mabadiliko zimeisha
 
Kila mtu anamapungufu yake, wacheni aseme anachijisikia, ila tambueni kuwa kama siyo yeye chadema leo isinge kuwa hapo ilipo.

Wengi inatuuma sana kuona amebadilika ila ni busara kumpa heshima yake, huenda sikumoja akabadilika.
 
Hiyo inakuhusu wewe na slaa. Heshima alipewa alipojiheshimu kashindwa kujiheshimu hakuna atakayemheshimu
 
Kila mtu anamapungufu yake, wacheni aseme anachijisikia, ila tambueni kuwa kama siyo yeye chadema leo isinge kuwa hapo ilipo.

Wengi inatuuma sana kuona amebadilika ila ni busara kumpa heshima yake, huenda sikumoja akabadilika.

Hata shetani mwanzo alikuwa malaika lakini alipomuasi Mungu alitupwa motoni mpaka leo
 
Kila mtu anamapungufu yake, wacheni aseme anachijisikia, ila tambueni kuwa kama siyo yeye chadema leo isinge kuwa hapo ilipo.

Wengi inatuuma sana kuona amebadilika ila ni busara kumpa heshima yake, huenda sikumoja akabadilika.
Kama una mahaba naye mfate huko mkale mihogo wote
 
Kila mtu anamapungufu yake, wacheni aseme anachijisikia, ila tambueni kuwa kama siyo yeye chadema leo isinge kuwa hapo ilipo.

Wengi inatuuma sana kuona amebadilika ila ni busara kumpa heshima yake, huenda sikumoja akabadilika.
Noted; mda mfupi ujao dr ataenda kula matapishi yake kwa mara ya pili.
 
Dr alifungiwa nje akalala kwenye gari kuamka asubuhi shingo,kiuno na mbavu zote zimekaza na maumivu makali akambiwa na Mama Mshumbuzi achague siasa au apigwe talaka rejea ?.Dr Mihogo akakimbilia Serena kubwabwaja akidhani atakuwa na impact ya maana kumbe wapi waTanzania wameamua safari hii ni mabadiliko.

Ukitaka kujua story zake muulize Gwajima atakupa full data za huyu Babu
 
Kila mtu anamapungufu yake, wacheni aseme anachijisikia, ila tambueni kuwa kama siyo yeye chadema leo isinge kuwa hapo ilipo.

Wengi inatuuma sana kuona amebadilika ila ni busara kumpa heshima yake, huenda sikumoja akabadilika.

Ataachwa vipi wakati anatumika mkuu, Dr. Slaa leo anatuambia tuchague ccm tukae kimya na tukubaliane tu kuwa ni sawa.

Na wewe tafakari mkuu ushauri wako siyo mzuri kabisa, angenyamaza tungemheshimu kweli lkn anatuambia tumchague Magufuli laa laa laa!!!!! aise hapana angesema Dotuvwa, H. Rungwe, Lema wa TLP au mama wa ACT ningemwuunga mkono.

ccm nitasema nooooooo!!!!!!!!!! siku zote.
 
Back
Top Bottom