Dr. Slaa anastahili kuheshimiwa

Dr. Slaa anastahili kuheshimiwa

Nitakuwa wa mwisho kabisa kuubeza, kudharau mchango wa dr slaa ndani ya Chadema na taifa kwa ujumla katika safari ya mabadiliko. Kazi aliyoifanya 2010 ndiyo iliyozaa nguvu hii ya ushawishi wa mabadiliko kwa watanzania. Nasema nitakua wa mwisho kuungana na Mbowe, ati dr slaa apumzike. Nitakuwa mnafiki kufanya hivo na muongo kabisa. Naamini na nitasimama imara katika kufanya lolote kuhakikisha mabadiliko yanapatikana.lakini pia natambua nguvu ya Lowassa na umuhimu wake katika safari hii ya mabadiliko makubwa lakini pia kwa hekima kabisa ingekuwa vyema Mbowe angeeleza kwanza hoja iliyopelekea kuleta maamuzi hayo kisha tukamsikiliza dr slaa kwani nitamshangaa sana mwanachadema aliyeishangilia kauli ile bila hata kuuliza, kutafakari majibu, na kupima athari zake.
Tunayahitaji mabadiliko kwa gharama yeyote ile ila si kwa kukubali kuitenganisha nguvu tuliyonayo katika safari hii ya mabadiliko."mchango wa lowassa ni mkubwa katika safari hii ya mabadiliko lakini pia nguvu ya dr slaa ndiyo daraja kuu litakaloiunganisha nguvu ya chadema na nguvu ya Lowassa"
By Fikra mfumo.
 
Naanza kuamini kuwa Mbowe yuko Chadema kibiashara zaidi kuliko kutumikia wananchi; Slaa ndio nguzo ya chadema bila yeye mmekwisha na msijidanganye!!! Umaarufu wote wa chama hicho umejengwa na Slaa na yeye kujipumzisha ni kuwapa muda hawa mamluki ndani ya chadema wakiongozwa na Mbowe wajinyonge wenyewe kwani hakuna jinsi ya Lowassa kuingia Magogoni ; ataishia getini tu mtake msitake!!!!
 
Nitakuwa wa mwisho kabisa kuubeza, kudharau mchango wa dr slaa ndani ya Chadema na taifa kwa ujumla katika safari ya mabadiliko. Kazi aliyoifanya 2010 ndiyo iliyozaa nguvu hii ya ushawishi wa mabadiliko kwa watanzania. Nasema nitakua wa mwisho kuungana na Mbowe, ati dr slaa apumzike. Nitakuwa mnafiki kufanya hivo na muongo kabisa. Naamini na nitasimama imara katika kufanya lolote kuhakikisha mabadiliko yanapatikana.lakini pia natambua nguvu ya Lowassa na umuhimu wake katika safari hii ya mabadiliko makubwa lakini pia kwa hekima kabisa ingekuwa vyema Mbowe angeeleza kwanza hoja iliyopelekea kuleta maamuzi hayo kisha tukamsikiliza dr slaa kwani nitamshangaa sana mwanachadema aliyeishangilia kauli ile bila hata kuuliza, kutafakari majibu, na kupima athari zake.
Tunayahitaji mabadiliko kwa gharama yeyote ile ila si kwa kukubali kuitenganisha nguvu tuliyonayo katika safari hii ya mabadiliko."mchango wa lowassa ni mkubwa katika safari hii ya mabadiliko lakini pia nguvu ya dr slaa ndiyo daraja kuu litakaloiunganisha nguvu ya chadema na nguvu ya Lowassa"
By Fikra mfumo.

Naamini hatua ya kwanza kabisa ni kujua kama Lowassa au/na washirika wake wametoa fedha CHADEMA/UKAWA. Kama wametoa ni kiasi gani na kwa sababu zipi?

Hapo ndipo itakuwa rahisi kujua maamuzi ya Mbowe yanasukumwa na nini, uzalendo au biashara?
 
Watu wamekuwa wepesi zaidi ya kusikiliza na kukubali kuliko kutafakari hoja kuzipima na kufanya maamuzi
 
Dr Slaa baada ya kuzushiwa kuwa ana makubaliano maalum na chama, sasa anafunguka kuwaumbua
 
Attachments

  • 1438668659333.jpg
    1438668659333.jpg
    37.1 KB · Views: 96
Mchango wa Dr Slaa katika siasa ya vyama vingi Tanzania ni Mkubwa na kila mtu anaelewa hivyo. Mbowe hakumbeza Dr Slaa bali alikuwa anatoa ufafanuzi ni kwanini Dr Slaa hajaonekana kwa takribani wiki nzima, na mimi sikuona tatizo kwenye maneno yake.

Ikumbukwe aliyepeleka wazo CDM la kumchukua Lowassa endapo atakatwa CCM ni Dr Slaa, na wale viongozi wote mle wa CDM wanajua hivyo. Ikumbukwe pia siku ya tarehe 26 July 2015 siku ambayo Lowassa alikaribishwa rasmi na Kamati kuu ya CDM Dr Slaa alikuwepo na kama umeona picha, alikuwa ni mwenye furaha na amani katika hilo. Ni tarehe 27 July 2015 ndipo Dr Slaa aliacha kuonekana kwenye vikao, yaani kwa lugha nyingine ni masaa machache ya usiku wa tar 26 July 2015 yaliyombadilisha Dr Slaa. Nini kilimpata, yeye ndiye angetoka na kushirikiana na viongozi wenzie wa Chama.

Alichokifanya Dr Slaa kwa mtazamo wangu sio sahihi kwa chama, kamati kuu chadema, viongozi wote wa chama na sisi tuliowanachana na tusiowanachama. Ningemuelewa Dr Slaa kama maamuzi haya angeyafanya mapema wakati wa kyanza michakato ya kumpokea Dr Slaa.

Ninaamini bila Dr Slaa Lowassa asingekuwa CDM leo, ni ushawishi wa Dr katika chama uliopelekea CDM wamkubali Lowassa!

Ninamuheshimu Dr Slaa, lakini kwa hili anajipunguzia heshima aliyoijenga kwa miaka mingi. Nakushauri mzee wangu rudi ungana na wenzio katika kipindi hiki kigumu na muhimu kwa mustakhabari wa maisha yetu.
 
dah ama kweli shukrani ya punda ni mateke
 
Neno moja tu kwako mbowe bring back our Dr nakumbaka niliwahi mpigia simu aje homboro Dodoma tujenge chama na kweli akaja. na kugawa kadi za chama bila yeye kunijua lakin alitoa ushirikiano Wa Ku tosha kweli alikuwa na nia ya dhati. Sina mengine zaid ya bring back our slaa
 
Dr Slaa baada ya kuzushiwa kuwa ana makubaliano maalum na chama, sasa anafunguka kuwaumbua

Hizi zote ni Propaganda za CCM na TISS. Kwa taarifa yenu Dr hana access ya mitandao kwa zaidi ya wiki moja sasa!! Zaidi ya TV hakuna anachofuatilia! Yupo mapumzikoni akimaliza atarejea kazini
 
Ni kweli. Kwani hali hali ya wakati wa nccr ya mrema inataka kujirudia INAUMA SANA
 
Umma wa Watanzania utawahukumu Ccm October kwa kutengeneza mafisadi wanaopata sala ya toba Chadema

Mkuu hata wewe? Mungu ni mwema atawalipa usaliti wenu kwa Dr.Slaa na ni hapa hapa Duniani. Mungu hajawahi muacha mwenye haki. Damu za wtz zitawalaani vizazi vyenu kwani mmetusaliti. Bila Dr. Lowasa angejulikana fisadi na kutubu? Hakuna ushabiki kwenye mambo ya maisha na damu za Watu.
 
Hizi zote ni Propaganda za CCM na TISS. Kwa taarifa yenu Dr hana access ya mitandao kwa zaidi ya wiki moja sasa!! Zaidi ya TV hakuna anachofuatilia! Yupo mapumzikoni akimaliza atarejea kazini

Ingekuwa hiyo account anatumia mwingine zaidi ya Dr Slaa basi isingekuwa inapost vitu vya maana, ingekuwa inashambulia na kutoa kashfa na kejeli, Nia sikuchonganisha basi ingefanya kazi sawasawa kuchonganisha
 
WanaJF na hasa wana CHADEMA wenzangu tuwe makini sana na maandishi yetu hapa jukwaani kuhusu huu ukimya wa DR SLAA, tafadhalini sana, DR ni kiongozi mkubwa sana anastahili kuheshimiwa, wale wenye uchungu na CHADEMA na tunaofahamu tulipotoka hatuwezi kumkashifu huyu mtu, kwa lipi hasa ?

Acheni kabisa jambo hilo, sikupenda kuandika jambo hili maana linaweza kuendeleza malumbano zaidi lakini nimelazimika kuliweka kama angalizo.

simama ktk hoja kuu.mtasema mengi sana.kama ulishaapa kumtumikia Mungu kisha ukakengeuka:unadhani utafanikiwa kwa mengine?dhambi hiyo inazidi ile ya asili. dk atatangatanga sana ila mpaka kufa kwake hatakuwa na amani ktk maisha yake.sorry all of u,4 reallity.
 
Chedema inapendwa asikwambie mtu, ukipita mtaana ni gumzo kila mtu chadema hiyooo ikulu. 2015 hadanganyi mtu, tupo speed kubwa ukikaa barabarani utasagwa-sagwa. Ccm wanatapatapa wataishia copy and paste ya UKAWA.
 
Back
Top Bottom