Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Dr. Slaa amkosoa Rais Kikwete kuhusu Rwanda

Katibu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, amemkosoa Rais Jakaya Kikwete, kuhusu kauli ya kumshauri Rais wa Rwanda, Paul Kagame, kuzungumza na waasi wa serikali yake.

Dk. Slaa amesema haoni busara kwa Rais Kikwete kuwaambia viongozi wa Rwanda, akiwamo Rais Kagame, kuzungumza na wafuasi wa chama cha FDRL walioko Congo kwa vile wanatambulika kama wauaji.

Alisema hayo wakati akizungumza katika kongamano la vijana wa Chadema (BAVICHA) la uchumi na ajira lililofanyika jana jijini Dar es Salaam.

Alimshangaa kuwataka kuzungumza na watu ambao Kagame anawaita wauaji wenye asili ya kundi la jeshi la Nterahamwe, lililokuwa linaangamiza Watutsi.

“Rais Kikwete hapa nyumbani hawezi kuzungumza na wapinzani, hajachukua hatua dhidi wauaji wa mwandishi Daudi Mwangosi, alishauriwa amuwajibishe Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa Michael Kamuhanda, amempandisha cheo,” alisema.

Alisema Rais alitakiwa kuwaambia waje awapatanishe lakini si kuwaambia wazungumze na watu anaowatuhumu kuua Watutsi.

Kumezuka sitofahamu ya uhusiano wa kidiplomasia kati ya Tanzania na Rwanda, baada ya Rais Kikwete kutoa ushauri huo wakati wa mkutano wa Umoja wa Afrika (AU) uliofanyika Addis Ababa, Ethiopia hivi karibuni.

Ushauri huo ulionekana kumchukiza Rais Kagame, anayedaiwa kuhutubia mikutano kadhaa nchini kwake na kutumia lugha ya matusi, kejeli na dhihaka dhidi ya Rais Kikwete na Tanzania.


CHANZO: NIPASHE
Khaa!!! Ninamuheshimu Dr. Slaa, lakini kama kumkosoa JK ni kama hapa kwenye red na blue basi safari yetu hadi tufikie demokrasia ya kweli bado ndefu sana. Sidhani kama ni sahihi kwa kuwa ni chama upinzani basi maana yake kupinga kila jambo linalofanywa na serikali iliyopo madarakani. Ndiyo maana wakati mwingine tunakuwa tunalalamikia mambo mengine yasio ya msingi ilimradi tuwe tunapingana na serikali. Kwa akili yangu ndogo sana nadhani si sahihi. Nadhani si vyema kuwa na mawazo ya kupinga kila jambo eti tu kwa sababu ni wapinzani. :bored:
 
Of course, ni kuwa Dr. Slaa kama amesema hayo nae pia kateleza......! Hili suala kwa kweli sio la Kikwete ni la Tanzania na huo ndio msimamo wa nchi yetu, msimamo usio na kificho
AHAAAA hapo mkuu ndiyo hasa nilikuwa namaanisha yaani mtelezo kwa mtelezo sasa sijui nani atamtelezea mwenzake, msimamo umeshatoka wa nchi na raisi alisema hayo mbele ya hadhara ya waheshimiwa , kingine ambacho ni ziada ya hili ni kuwa usije ukakuta muheshimiwa ana ajenda na mataifa mengine kwa rwanda. nalisema hili nikiwa na hoja moja kagame tangu siku nyingi alikataa kuwa pamoja na hao FDRL ki masikilizano na baadhi ya mataifa yalimuunga mkono akiwamo baba wa taifa , iweje leo mtu anafufua kitu kilichozikwa siku nyingi , hapo ndipo naanza kuikubali hoja ya dr.slaa kwa upande mwingine utofauti wa kikwete na kagame usije kutuingiza katika vita. lakini kama nchi tuwe wamoja kwa hili
 
Nadhani Dr. Slaa hapa kakurupuka naye anasema mbona yeye kashindwa kushughulikia mambo yake ya ndani?? Mimi kwa uelewa wangu hii aimzuii kuongelea amani ya east afrika...mimi nadhani si kila kitu tupinge usalama wa east afrika una maana usalama wa tanzania...

J.K alikua sawa tu mtutu ukishindikana haina budi kurudi mezani.

I stand to be corrected

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

upuuzi huu.......
 
Nyerere alichafanya ni kila aliyemuona tishio kisiasa, "he was either liquidated or exiled". Baada ya hapo ilikuwa haiwezekani ku-organise uasi dhidi ya nyerere kwa sababu kuanzia padri, shehe, mwalimu mkuu mpaka daktari wa muhimbili alikuwa ni askari kanzu wa nyerere. Na hii ndiyo maana ya "authoritarian government". Nyerere hakufanya maamuzi kwa kuwashinda watu kwa hoja kwa sababu wenye hoja m-badala walikufa au walifukuzwa. Na kila mtanzania wa kawaida aliyekuwa na mawazo tofauti aliogopa kuyasema mawazo yake. Na ndiyo maana Nyerere aliwahi kuitwa "haambiliki".
Kuhusu JK kukutana na wapinzani, anafanya hivyo na kuna ushahidi wa hilo. Tatizo ni kwamba wapinzani wakishakutana na JK wanataka JK afanye wanayoyataka wapinzani. Kama yana maslahi kwa taifa JK anatakiwa afuate mawazo ya wapinzani. Na kama yana maslahi kwa chama fulani, JK anayo haki ya kuyakataa mapendekezo ya wapinzani.

Sasa nakuuliza wewe Ben Saanane: nini mtazamo wako binafsi kuhusu huu mgogoro wa Tanzania na Rwanda? na jee mtazamo umebadilika kutokana na kauli ya Dr. Slaa? au umebaki ule ule wa awali.

Mtazamo wangu uko pale pale maana nilitoa maoni binafsi.Kuhusu hoja ya kufanya dialogue na upinzani wa ndani hilo ni lazima tukubaliane.

Hoja ya Rais kwamba aliwahi kukutana na upinzani haikamiliki ikiwa rais hatekelezi makubaliano.Tuache upotoshaji.Hakuna mahali ilipolazimishwa kuwa ni lazima rais akubaliane na matakwa ya upinzani kwenye dialogue.Hoja ni kutekeleza walichokubaliana na inajenga utamaduni wa kisiasa katika ustaarabu tuliojipangia kama jamii ya watanzania au taifa lolote lile.

Hoja yako kuhusu Nyerere kufukuza waliopingana nae unathibitisha hoja yangu maana kuna ushahidi kuwa wapinzani wengi waliokimbilia exile miaka ile walikua hatari zaidi wakiwa huko kuliko wakiwa kwenye mataifa yao.Wengi wao walikuja kufanikiwa kupindua tawala zao kwa collussion na maadui wa serikali zilizokuwepo madarakani.Rejea historia ya Kagame,Rejea historia ya Museveni

Kwenye inyernational relations kwenye school of thoughts mara nyingi imeonekana kuwa ni ngumu kwa tawala nyingi kuwakatalia wanasiasa wa nchi nyingine wanaomba hifadhi ya kisiasa yaani political asylum kwa kuwa wanakua cautious kwamba itakuaje incase huyo wanayemkatalia atakuja kufanikiwa kuwa mtawala?

Leo hii ukiangalia Ishu ya MONUSCO ambako SA pia wametoa majeshi utaona jinsi ambavyo Kagame alipokasirika maana i'm sure ana hasira pia na Zuma kwa kuwa SA imempa political asylum General Kayumba Nyamwasa hasimu mkubwa wa Kagame na aliyekua rafiki yake na msaidizi wake wa karibu.
 
===>> Heee... I can't imagine ...Dr. Slaa as of this moment, day... to me ur USELESS, Mnafiki mkubwa.. hufai hata kuwa kiongozi of which anyway u hv never been... hujui UTAIFA NI NN...uko just to score political cheap popularity...

==> Slaa uliondoe BORITI kwanza ktk jicho lako ndipo uliondoe jicho la mwezio... kweli nyani ni nyani....hee...huyu ndio Slaa au..??

===>> Ntakudharau na kukuona mjinga sana kwa hili na nimejua ur inner most part.... poor Slaa...

===>> Kumbe ww Slaa wajiona UNAFAA SANA..MWEMA SANA...BORA SANA...WAJUA SANA...HODARI SANA... UNAJIDAI UNAFANYA RESEARCH B4 U SPEAK.... I*m rounding u to ZERO...0 KABISA... I will be against u to death for all in all...

===>> hv unaumwa nn Slaa..!!?? Rais wa nchi YAKO ANATUKANWA....ANATISHIWA NA MUUAJI KAGAME TENA PUBLICLY UNATHUBUTU TO OPEN UR DIRTY MOUTH NA KUSEMA JK KAKOSEA KUWAPA USHAURI....JUST A PIECE OF AN ADVICE... ww ushindwe kuweka utaifa mbele unaleta HYPOCRICY MBELE....

==>> Hapa umechemsha kupindukia...na utafeli ushangae.... sikukudhania uko hovyo hivyo Slaa...

===>> ooohh God... I knew Upadri hujakushindwa bure.... ni Mipango ya Mungu...alikujua....

===>> Narudia Watz wazalendo wanaojua kupima mambo kwa kina TUTAKUDHARAU UTASHANGAA...

===>> Hv ww Slaa ww JK kwako hafanyi jema hata moja....ukome..uchu wa madaraka utakumaliza.... unapenda sana sifa ww...

===>> I dought perhaps ur thinking & reasoning capacity has gone with age....


===>> I*m against u Slaa... to me ur a failure to hell....

ww si Mzalendo hata tone.... Aisee... ptuuuu....!!!

Jenga hoja maana hizi adrenalin unazomwaga hapa zitafanya watu waache kukuchukulia serious!
 
JK aliPAYUKA hadharani na ikaonekana kwamba kagame yuko pamoja na hao waasi.
Haiwezekani watu wakawa wanagombana muda wote halafu mtu unakuripuka unakuja unasema kaeni meza moja mpatane badala ya wewe unayesema hivyo kuchukua hatua ya kuwapatanisha.
Otherwise wasingegombana.

JK take action ya kuwapatanisha acha mboyoyo mingi haisaidii chochote

jk hakupayuka hadharani: " nilitoa ushauri wa pk akutane na mahasimu wake ktk kikao cha marais AU. ushauri ambao niliutoa pia jwa kabila na museveni.
museveni aliniunga mkono lakin pk alikaa kimya"
alisema ni kawaida kukutana na kushayriana mambo mbalimbali kwa UWAZI kila yanapotokea.
Tanzania inapenda mahusiano nema na Rwanda na majirani zetu.
Tanzania itakuwa ya mwisho kuishambulia rwanda lakini hatutapuuza nadai yake.
kama amirijeshi mkuu kauli hiyo sio hatarishi.
 
Hajakosea in the short run kagame apigane nao mpaka hao wapinzani wake watoweke na hilo halitokei museveni alshindwa hatimae alijariibu mazungumzo
Na kagame no short cut ni kuongea tu
Kama sudan ziliongea zikapostans
Taliban nao pia wapo mezani na usa
Anataka kukaa na urais wa maisha hivo hataki sulihu
Na walokimbia rwanda sio wote wauaji ni ppropaganda ya kagame tu
Kikwete ahsante hakika uko na busara hata wakenya 2006 walikind na busaara zako zilisaidia kumaliza mauaji
 
Hili taifa sasa kweli linawanasiasa wa kuchumia tumbo kweli slaa anaweza kuwasaliti watanzania wote ambao tumeungana kumlaani kagame na kumsapoti jk,

sikutegemea wala sikudhani kama kwa matusi ya kagame kwa nchi na rais wetu kama angetokea mtu ampongeze au aungane na kagame,

huyu mzee ni mnafiki kumbe ndiyo maana hata kanisani alishindwa amekosa utaifa kwa kiwango cha juu,

Hofu yangu ni kwa wanasiasa vijana anaowaongoza, je anawafundisha nini hapo hakuna kitu utaifa tena kesho akichaguliwa kwa nini asiliuze hili taifa,kumbe utu uzima siyo dawa tena yawezekana ikiwa ni mzigo kama huo utu uzima hautatumika vema,

kuanzia leo mtu ambaye namuona anafaa kugombea urais kwa chadema ni bora ya mbowe japo hana elimu lakini anastaha ya mambo lakini huyu mzee buere kabisa.
 
Kwa nini kikwete asingemwambia privately Paul kagame...au anafikiri kagame hajui kutatua migogoro kwa njia ya amani? Kagame alimuona Jk kama anamfanyia dharau,that is why alimaua kuporomosha matusi.

angekaa kimya au angemjibu kulekule ktk kikao.
angesema tu" Mr jk kwa hili hapana.
 
atakama slaa yupo ryt....ila kagame ni gaidi....
 
Jenga hoja maana hizi adrenalin unazomwaga hapa zitafanya watu waache kukuchukulia serious!


## Ur sick of unknown infections... ww una viroja* huna hoja* kuhusu hili....shukuru Mungu CDM gave u
job...utamlamba Slaa hata masab..rii....

== Kwa hili Slaa ni KIHIYO, HOVYO, BURE like his hawara Josephine.... huwezi ona au sikia wazi wazi Rais anatukanwa na Nyani toka nje ... na nyie MNAKENUA TU... na I heartly & physically embarassed & touched
with Slaa na Kagame anayemsapoti....basi Slaa aende Rwanda anafanya nn hapa..??

== Rwanda wameshakuwa mzigo kwetu...HAWANA SHUKURANI PIMBI WALE...
...TUMEWABEBA SANA WAKIMBIZI WAO...
TUMEWALINDA NA KUWAPA KILA KITU...NA TUKAWARUDISHA KWAO....

...MAHAKAMA YA ARUSHA tulikubali iwe pale wamalize matatizo yao.... but Kagane akaja kumuua Prof. wetu
Mwakyusa.... kisa kuwatetea kisheria watuhumiwa....
...Kagame anaua wazi wazi sehemu mbali mbali duniani
wapinzani wake kwa risasi....

Sasa kakua anavuka mipaka na Kumtisha Rais wa nchi
ambaye YEYE KAGAME ALIJIFUNZA JESHI BURE HAPA KWETU....HAWA WATU HAWANA SHUKRANI NI FISI WOTE.....

MUSEVENI kasoma na kujifunza jeshi hapa Tz leo yuko against us...pimbi yule mnafiki kama Slaa..

Uhuru Kinyesikinyata alikuja hapa kabla ya Uchaguzi analilia Ikulu kwa JK kuomba Msaada..leo pimbi kabisa...

JK TWENDE MBELEE KOMAA NAO TU WEMA UMEZIDI BABA RAIS WETU, HAKUNA KURUDI NYUMA TUSIWATENDEE MEMA TENA...NA HATUTISHIKI NA HAWA WANAFIKI..OPPORTUNISTS....HATA YESU HAWA HAWA WANADAMU WALIMSULUBU KWA MEMA YAKE....KOMAA NAO NA TUMEANZA NA M23 NA TUTAMFIKIA KAGAME TU...MUUAJI KABISA YULE...
 
Kinadharia ushauri wa Kikwete unaweza kuonekana kama mzuri lakini haukuwa na action plan au road map ya utekelezaji kushauri bila action plan ni sawa na kuropoka hasa unapomshauri mkuu wa nchi nyingine.

Kama Kikwete ataanzisha vita na Kagame binafsi nitakuwa wa mwisho kwenda vitani, kwa sababu naamini Kikwete hakuwa sahihi kuwaambia Rwanda wakutane na waasi alichotakiwa ni ku-mediate mkutano kwa kuwakutanisha mahasimu na sio kuwaambia wakutane, kwanza wakutane wapi na nani awe mlalamikaji na mlalamikiwa.

I agree with you 100%. Jk amekuwa ktk nafasi nzuri ya kufanya ivyo: kwanza akiwa waziri wa mambo ya nje kwa miaka 10 na zaidi ktk kipindi cha mauaji 1994. Tunahitaji ushahidi beyond doubt alichokifanya kutatua mgogoro huo. Pili, JK yupo madarakani sasa miaka 6 atueleze nini amefanya ktk kupatanisha wanyarwanda. Kama kauli iyo alitoa na hajawai kujiusisha rasmi na mgogoro huo, itaniwia vigumu kuamini alichokifanya kama kilikuwa sahihi.
 
AHAAAA hapo mkuu ndiyo hasa nilikuwa namaanisha yaani mtelezo kwa mtelezo sasa sijui nani atamtelezea mwenzake, msimamo umeshatoka wa nchi na raisi alisema hayo mbele ya hadhara ya waheshimiwa , kingine ambacho ni ziada ya hili ni kuwa usije ukakuta muheshimiwa ana ajenda na mataifa mengine kwa rwanda. nalisema hili nikiwa na hoja moja kagame tangu siku nyingi alikataa kuwa pamoja na hao FDRL ki masikilizano na baadhi ya mataifa yalimuunga mkono akiwamo baba wa taifa , iweje leo mtu anafufua kitu kilichozikwa siku nyingi , hapo ndipo naanza kuikubali hoja ya dr.slaa kwa upande mwingine utofauti wa kikwete na kagame usije kutuingiza katika vita. lakini kama nchi tuwe wamoja kwa hili

mbona baba wa taifa alizika hoja ya g55 ya serikali tatu na leo imeibuliwa na chadema na inashika nafasi?
ni suala la muda tu. kama mmeshindwa kuwapiga basi ungana nao mjenge rwanda.
jk is right at the moment and slaa will ve right if time persist.
 
Jenga hoja maana hizi adrenalin unazomwaga hapa zitafanya watu waache kukuchukulia serious!
Ben sote sisi ni vijana tunandoto za kufika mbali tangu mwanzo wa haya maswala tupo kitu kimoja katika ishu za kitaifa tofauti zetu ni kwenye post za vyama vyetu,kiukweli mzee tunamheshimu sana ila katuchafulia siku kweli kapotoka na leo ni jumapili anapaswa kuungama,

nini hiki kafanya da! Huu ujinga sasa upinzani hauko hivyo ben tumshari mzee hasira kila sehemu zitatugombanisha na kutugawa aache mambo yake.
 
Nyerere alichafanya ni kila aliyemuona tishio kisiasa, "he was either liquidated or exiled". Baada ya hapo ilikuwa haiwezekani ku-organise uasi dhidi ya nyerere kwa sababu kuanzia padri, shehe, mwalimu mkuu mpaka daktari wa muhimbili alikuwa ni askari kanzu wa nyerere. Na hii ndiyo maana ya "authoritarian government". Nyerere hakufanya maamuzi kwa kuwashinda watu kwa hoja kwa sababu wenye hoja m-badala walikufa au walifukuzwa. Na kila mtanzania wa kawaida aliyekuwa na mawazo tofauti aliogopa kuyasema mawazo yake. Na ndiyo maana Nyerere aliwahi kuitwa "haambiliki".
Kuhusu JK kukutana na wapinzani, anafanya hivyo na kuna ushahidi wa hilo. Tatizo ni kwamba wapinzani wakishakutana na JK wanataka JK afanye wanayoyataka wapinzani. Kama yana maslahi kwa taifa JK anatakiwa afuate mawazo ya wapinzani. Na kama yana maslahi kwa chama fulani, JK anayo haki ya kuyakataa mapendekezo ya wapinzani.

Sasa nakuuliza wewe Ben Saanane: nini mtazamo wako binafsi kuhusu huu mgogoro wa Tanzania na Rwanda? na jee mtazamo umebadilika kutokana na kauli ya Dr. Slaa? au umebaki ule ule wa awali.
Sawa kabisa mkuu umenena mimi nimemfuatilia sana Ben Saanane kuhusu hii issue ya Kagame na Kikwete.

Mwanzo alikuwa ana msapoti sana Kikwete sasa hivi kaja na lugha nyingine lakini mimi hanisumbui nishamuelewa

yeye ni "double face" kaja mkuu wake wa kazi kabadilika ninacho mshauri awe na mawazo huru upinzani sio kupinga

kila kitu ni hayo tu.
 
kila siku tuna sema slaa hana uzalendo mnakataa.hawa viongozi wapo kwa ajili ya kutugawa.
sasa majuzi watanzania wote humu jf tulisimama pamoja,kupinga kauli za kagame lakini leo kuna watu wameanza kulegeza sauti eti kisa slaa kaongea.
na anapotugawa inamana anampa nguvu adui.anasahau msemo wa kizaramo genda ubwele.
hata yeye huyo slaa hakutumia busara kumlaumu kikwete wakati hili suala bado ni tete.

Mnanichekesha nyinyi....Magamba na Uzalendo wapi na wapi?Hivi Kati ya Slaa na wale wapiga deal za Unga,EPA,Meremeta,KAGODA,Richmond,IPTL,Fedha za Uswisi,Smart Partnership,nk ni nani Mzalendo?Otherwise wenzetu sijui Uzalendo mnauelewaje?
 
Wewe kila siku kwa jirani wanagombana alafu watoto wake wanakimbilia kwako, unawaweka mahali na kuwapa msosi, hivi unadhani haitafika muda uende umwambie jirani aache ugomvi?? JK kuwaambia wakae means diplomacy, sasa sijui watu walitaka aende amwambie nakuletea jeshi ukawapige vizuri au piga kwelikweli... Angesema hivo si ndio watu wangemuona mwehu kabisa... Ile nayo ni nchi ya East Africa, lolote linalotokea lazima wengine nao watoe comments, nini maana ya EA Community kama mtakaa mnaangalia tu, mbona Kenya walivyokua na mapigano ndani kwa ndani Tz ilitoa comment vilevile, its just the way it has to be, sasa Dr. Slaa lazima atafute pa ku-criticize kwa sababu ni Upinzani maana title tu mpinzani sidhani kama itafika siku wapatane, ila JK was right, ukimya muda mwingine ni ujinga, Africa nzima ilikaa kimya hadi Ghadhafi akafa sasa Libya iko wapi?
 
## Ur sick of unknown infections... ww una viroja* huna hoja* kuhusu hili....shukuru Mungu CDM gave u job... utamlamba Slaa hata masab..rii....

== Kwa hili Slaa ni KIHIYO, HOVYO, BURE like his hawara Josephine.... huwezi ona au sikia wazi wazi Rais anatukanwa na Nyani toka nje ... na nyie MNAKENUA TU... na I heartly & physically embarassed & touched with Slaa na Kagame anayemsapoti....basi Slaa aende Rwanda anafanya nn hapa..??
Ha ha haa kumekucha!
 
Nadhani Dr. Slaa hapa kakurupuka naye anasema mbona yeye kashindwa kushughulikia mambo yake ya ndani?? Mimi kwa uelewa wangu hii aimzuii kuongelea amani ya east afrika...mimi nadhani si kila kitu tupinge usalama wa east afrika una maana usalama wa tanzania...

J.K alikua sawa tu mtutu ukishindikana haina budi kurudi mezani.

I stand to be corrected

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums

Hata mi nilipoanza kusoma sikuona maana, ila lilipoingia suala la mwangosi nikapata na hasira. JK amekuwa na dharau anaona wanaokufa ni kama digidigi polini. Kwa nini hajaunda tume arusha na kwa nini kamuhanda muuaji alimpandisha cheo???? Maana yake JK is a killer na huwa hataki mazungumzo iweje leo wengine awashauri vitu ambavyo yeye anaenda kinyume?
 
Back
Top Bottom