Elections 2010 Dr. Slaa alikuwa anaongoza Kwa 61.6% - Marando

Ukisoma sheria za uchaguzi zinasemaje utapata jibu.

Matokeo yote yanabandikwa vituoni kuanzia udiwani, ubunge mpaka urais. Kata inatangaza matokeo ya diwani, wilaya matokeo ya mbunge na NEC makao makuu matokeo ya rais.

NEC wanatangaza mshindi wa Urais. Hivi kubandika katika kila kituo matokeo ya Urais, huko si kutangaza matokeo?
 
ni kweli tutakuona kwenye maandamano au kazi yako kuchonga hapa jf, nipe data people's power ngapi umeshiriki na uliplay role gani?
muulize maana kuogea ni rahisi ila vitendo shuhuli maana hiyo siku ya kuandama kwenyewe huyo slaa yuko na wife wake wanajivinjar
 
Source: Mwanahalisi: Jumatano, Novemba 3-9, 2010

NEC inatuhumiwa kuhujumu matokeo ya Uchaguzi kwa lengo la kukinyima ushindi CHADEMA.

Madai hayo yamo katika barua ambayo CHADEMA kiliwakilisha jana NEC kulalamikia utaratibu mzima wa kutangaza matokeo.


Katika barua hiyo, Mwanasheria wa CHADEMA, Mabere Marando anasema NEC inatumiwa na CCM kuhujumu matokeo hayo ili CCM kionekane kinashinda. "Wamepanga kupora ushindi wetu, ndiyo maana kila ambapo CHADEMA imeshinda, CCM wamekataa kusaini karatasi za kura" alisema Marando.


"Hata pale ambapo kura za madiwani na wabunge zimetangazwa, matokeo ya kura za urais hayatangazwi". Marando alisema NEC inafanya hivi kwa makusudi kwani maeneo ambayo CHADEMA haikuwa imeweka mkazo, matokeo ya madiwani, wabunge na ya urais yanatangazwa haraka . . . .


. . . . . Lakini hata katika maeneo ambayo CCM imeshinda, Marando alisema matokeo yanayotangazwa na NEC hayaendani na yale yaliyotangazwa vituoni. "Huu ni Uchakachuaji". . . .


. . . . . Marando alisema hadi juzi Jumatatu matokeo ambayo tayari walikuwa wamekusanya kutoka katika maeneo mbalimbali ya Nchi, yanaonyesha Mgombea Urais wa CHADEMA Dk. Willibrod Slaa anaongoza kwa wastani wa asilimia 61.6%..


Aidha taarifa hizo zinasema Dk. Slaa amepanga kuwakilisha ushahidi MZITO unaoonyesha uchakachuaji mkubwa wa kura za Urais ulivyofanyika. Ushahidi huo ni pamoja na matokeo halisi ya vituoni ambayo yanapishana na yale ya NEC.


Hatua zilizochukuliwa ni:


1. Kwenda NEC - kupeleka barua

2. Tunakwenda kueleza Nchi wahisani ambazo zimefadhili shughuli za Uchaguzi
3. Tunakwenda kuwaeleza wananchi kilichotokea kwa kuwaonyesha ushahidi kamili.

Malalamiko haya yanakuja siku chache baada ya lori lililoingia nchini likitokea zambia kukamatwa mjini Tunduma likiwa limesheheni karatasi za kupigia kura zilizowekewa alama ya vema kwa Kikwete. NEC ilikanusha.


Lakini katika kituo kimoja cha kupigia kura wilayani Musoma, lilikamatwa Lori lililokuwa na karatasi za kupigia kura na tayari zilikuwa na zimewekewa alama ya vema upande wa Kikwete. NEC haikutoa maelezo kuhusu tukio hilo.


My take:

Kama hizi taarifa ni za uhakika, basi hakuna maana ya zoezi zima la uchaguzi na ni dharau kubwa sana kwa Watanzania. Bahati mbaya mshindi wa Urais akishatangazwa, huwezi kuupinga ushindi huo mahakamani.

Ni vema sasa jumuiya zote za kiraia zinazotetea haki za kidemokrasia na za binadamu, wanachama na wapenzi wote wa haki na wana CCM wanaokerwa na hili kupaza sauti zao na kupinga kwa nguvu zote uzandiki huu. Arusha, Mbeya, Mwanza, Kawe, Ubungo na Iringa wameonyesha njia.

Inawezekana, mambo mazuri yana gharama na si lazima gharama hiyo iwe ni kumwaga damu bali kupaza sauti na kukataa kutawaliwa na watu ambao watanzania hawajawachagua kwa haki.

Nina wasiwasi sana na Marando anapompeleka Dr Slaa na CHADEMA?
 
Siasa za mfa maji hizo. Acha kutapata. Ni ndoto za mwendawazimu kuamini kuwa eti Dk. Slaa angeweza kumshinda JK. Huo ni upunguani kwelikweli.
Hivi Unategemea Marando- malaya wa kisiasa aseme nini. Kaivuruga NCCR na kuikimbia huku nyuma NCCRimeanza ku-gain power. Sasa amekwenda Chadema. Unategemea asemeje Wakili Mkuu wa kutetea wezi, mafisadi na wanyang'anyi wa haki za watu.
Marando huyuhuyu aliemtetea Mzungu aliyemtumia mbwa wake kumnajisi mwanamke wa Kitanzania. Tokeni kabisa na upuuzi wenu.
Kama mtu unatoa nukuu, zitoe kutoka kwa watu decent na sio watu wachafu wa aina ya Mabere Nyaucho marando.
Angesema Lisu, mimi ningenyanyua masikio yangu na kutafakari na sio kichaa wenu Nyaucho. Akome kabisa kuleta uchochezi hapa.

Jackob, hilo ndo tatizo lenu watu wa CCM, hamtaki kukubali ukweli, na huwa hamuongelei hoja, kwa mfano, jana Dr. Slaa amesoma barua iliyotoka kwa msimamizi wa uchaguzi, Mwanza akiwataka wasimamizi wasaidizi wahakikishe wanaisaidia CCM ishinde, kwa muujibu wa maagizo ya wakuu wa chama, KIKWETE, ROSTAM, LOWASA, RIDHIWANI, GACHUMA na wengine 25. Kilichofuata ni RIDHIWANI na KINANA kumkosoa DR. SLAA na kusema ni muongo, badala ya kusema MSIMAMIZI WA UCHAGUGI MWANZA ALIEYEANDIKA BARUA kuwa ndo muongo.
Najua Jackob, wewe ni mbumbumbu wa sheria, sio kosa lako, so kwa kukusaidia ni kwamba mtu yeyote ana haki ya kuwakilishwa mahakamani, ili kuhakikisha kuwa anahukumiwa kwa kufuata sheria. mf. mtu akiiba kuku, asihukumiwe kunyongwa, hapo bila shaka umenielewa?. So, acha proffesional life ya Marando tuongelee hili la matokeo kuchakachuliwa. na tuanze na hili.... jimbo la monduli,lina kura nyingi za uraisi kwa KIKWETE, 27,000 zaidi ya kura zote za ubunge, ina maana kuna watu walipiga kura za uraisi peke yake bila ubunge? TUACHE UVIVU WA KUFIKIRI.
 
Dr.Slaa ameishatamka ya kwake jana inatosha. Kuanzia sasa chadema kama chama cha siasa kilimweka Dr Slaa kuwania kiti cha urais ndicho kinapachwa kuongoza mapambano hayo. Kwa kuanzia kiweke wazi hizo takwimu anazozisema Marando kuwa zinampa ushindi Dr Slaa wa asilimia 61. Kwa upande wa NEC nanyi muwe wasikivu. Isingelikuwa vyema mkatumbukiza nchi yetu katika migogoro kwa kushindwa kutumia busara ya kawaida. Kinachotakiwa zipokee hizo takwimu za chadema, zifanyie kazi kwa kushirikisha wote wahusika, baada ya tathmini hiyo ikionekana chadema wanasema uongo wananchi na jumuia ya kimataifa itawasuta. Ikionekana madai yao ni ya kweli yafanyiwe kazi na hiyo itaipa NEC heshima kubwa.
 
Nendeni kanisani mkalalamike, waislamu oyeee, ccm oyee, tutaonana 2015. Udini wenu haukufanya kazi kikamilifu
Ndugu zangu Waislam kwa kweli tunatia aibu wakati mwingine. Kuna maswala ya kidini na maswala yanayotuhusi sisi wote kama waislamu na wakristo. Kwani wanaodhulumiwa ktkt nchi hii ni wakristo peke yao ambao wako ktk chama cha CHADEMA. Kwani waislamu pekee yao ndo wako ktk chama cha CCM, mbona kuna wakristo wako ktk CCM.Mbona mie nilimpigia Slaa nikiwa kama ni Mwislamu!! Lowasa ambae tunamlilia hapa kuharibu kula yuko CCM nae ni Mwislamu? Lewisi Makame anaeendelea kuharibu kila kitu nae ni Mwislamu. Tujalibu kutoa hoja na tusiangalie ni nani katoka dini gani. Kwani wanao msapoti Kikwete wote ni waislamu? Kusini Songea kuna wakristo kibao ambao wamempigia Kikwete. Utasemaje mwenzangu.
 
mimi natbiri kifo cha chadema kama watu hawa wenye recod ya kuua vyama mnawapa nafasi kama hizi
 
Unayejiita CCM Umejiunga jana tu, utadhani founder wa hii forums. Mwanamke anaupeo mdogo wa mawazo kulinganisha na mwanaume, lakini nimegundua Mke wangu amekuzidi kwa upeo. Wewe hata haki zako huzijui.

Du...sauti ya mabadiliko hiyo......Huu ukombozi una mambo!!!
 
kuna haja ya kuangalia upya utaratibu mzima wa kutangaza matokeo yote, kwa maana kwamba wakati wa kumtangaza mshindi wa udiwani kwenye kata, matokeo ya ubunge, na rais yatangazwe pia palepale ili kujua nani kapata nini katika sehemu husika kabla hayajapelekwa jimboni, na vivyo hivyo jimboni kabla ya kupelekwa tume taifa.

tatizo lenu wengi wenu siasa mmejifunza hapa jf na hamkutaka kushiriki mchakato wa uchaguzi japo tuliambiana tukashiriki japo kuwa mawakala ili kulinda kura za dr slaa na chadema. Baada ya kazi ya kuhesabu kura fomu 3 za matokeo yaliyosainiwa na wasimamizi wa vituo na mawakala wa vyama zilibandikwa katika vituo nilivyoshiriki kusimamia katika jimbo la ubungo zikionyesha matakeo ya udiwani, ubunge na urais. Na ninaamini kuwa huo ndio utaratibu uliotumika nchi nzima ndio maana chadema inaweza kujua kura zake zimeibiwa.

Sasa kutangazwa vituoni gani mnakotaka ndugu zangu, uchangiaji wenu duni unaonyesha ni kwa namna gani tunahitaji kujifunza siasa na uchaguzi kabal ya kurukia hoja za kuvuruga amani na utulivu uliopo kwa visingizio vya kuibiwa kura.

Tokea mwaka 1992 ulipoanzishwa mfumo wa vyama vingi vya siasa, vyama vya mbali mbali vya siasa ikiwemo chadema vimekuwa vikidai kuandikwa upya kwa katiba ya jamhuri ya muungano wa tanzania; tume huru ya uchaguzi n.k lakini watanzania kwa wingi wao wamekuwa wakiwashangaa viongozi wa vyama vya upinzani wanaodai mambo hayo na kutoshiriki katika maandamano ya kudai vitu hivyo ndio maana wizi wa kura umeweza kuwepo hata baada chaguzi kuu 3 yaani zile za 1995, 2000, 2005.

Kama kweli tumekasirishwa sana na wizi wa kura wa 2010 inatakiwa kuelekeze nguvu zetu katika kuandikwa kwa katiba mpya, tume huru ya uchaguzi n.k.tutumie elimu tulizonazo, uwezo wa kushawishi n.k kufikisha ujembe kwa watanzania wengi zaidi namna katiba mbovu inavyochangia katika kushamirisha ufisadi, umaskini n.k. Kufanya fujo, vurugu na matendo mengine kama hayo hakutakuwa na tija yoyote na uchaguzi wa 2015 tutaibiwa kura tena.
 
Hapo manota hata nchi kubwa haiweki vikwazo kwa nchi kama maslahi yao bado yapo msifikirie kuwa UN au mataifa makubwa wanakazi ya kuhangaika na nchia kama Tanzania mna nini nyie wanaenda IRAQi kuna mafuta, congo kuna mafuta, zimbabwe madini.

Ok Marando nimemuelewa lile lori mbeya lilikuwa na namba za tanzania au wapi? nanni alilikamata kwanini aliliachia? au lipo kituo gani mbeya tukalione.
Chadema mnataka mabidiliko lakini mmezidi uwongo msije kuwa kama CCM? nahofu sana
 
Hiyo Tallying anayosema Makame ni ipi? au ni ile hesabu ambazo tayari wanayo na wanataka kuhakikisha kuwa CHADEMA hawaivuki??

Kwa kuwa ameshakubali kuna irregularities ni vyema akajiuzulu haraka pamoja na vibaraka wenzake wote ili watu neutral wafanye majumuisho ya kura zote kama zinavyo-reflect vituoni...
 
Rasta! Na Botswana, Namibia iliwacost nini? Huko kwenye utulivu bila kumwaga damu. Tusiige mifano isiyofaa. Na mbona mifano yako imelala hapa hapa tu? Japan, Australia na Uswisi imewacost nini kujenga amani. Fikiri kama mtu mzima.......AMANI KWANZA

Mkuu usisahau kuwa pasipo haki hakuna Amani. Amani inajengwa haiokotwi. Mnapenda sana kutumia hicho kama kisingizio. Nenda kaulize hizo nchi kama hazikupigana vita!! Zilipigana lakini sisi tujiulize mtu uibiwe eti kwakuwa hutaki kuvunja amani usijitee? Hilo haliwezekani HAKI YETU TUTAIPIGANIA KWA NJIA YOYOTE ILE.
 
Rasta! Na Botswana, Namibia iliwacost nini? Huko kwenye utulivu bila kumwaga damu. Tusiige mifano isiyofaa. Na mbona mifano yako imelala hapa hapa tu? Japan, Australia na Uswisi imewacost nini kujenga amani. Fikiri kama mtu mzima.......AMANI KWANZA

Weweeee amani bila HAKI ni utumwa.... unataka kuturudisha enzi za ukoloni wewe:A S-baby::A S-baby::A S-baby:
 
Ndugu zangu Waislam kwa kweli tunatia aibu wakati mwingine. Kuna maswala ya kidini na maswala yanayotuhusi sisi wote kama waislamu na wakristo. Kwani wanaodhulumiwa ktkt nchi hii ni wakristo peke yao ambao wako ktk chama cha CHADEMA. Kwani waislamu pekee yao ndo wako ktk chama cha CCM, mbona kuna wakristo wako ktk CCM.Mbona mie nilimpigia Slaa nikiwa kama ni Mwislamu!! Lowasa ambae tunamlilia hapa kuharibu kula yuko CCM nae ni Mwislamu? Lewisi Makame anaeendelea kuharibu kila kitu nae ni Mwislamu. Tujalibu kutoa hoja na tusiangalie ni nani katoka dini gani. Kwani wanao msapoti Kikwete wote ni waislamu? Kusini Songea kuna wakristo kibao ambao wamempigia Kikwete. Utasemaje mwenzangu.

kaka/dada hicho ndicho kilichofanya nimtukane huyo jamaa kwa kuwa haelewi kama uislamu hoyee kwanini hawakumpa lipumba akaleta mabadili vyakula kupanda bei ovyo anaona kama wakristo ndio wanaonunua kwa bei ghali pekee haliwahusu waislamu. hata mtoto chekechea anajua kuwa kikwete na CCM yake wanaipeleka nchi pabaya na kama mtu una akili za kuzaliwa namaanisha zili za kupambanua mambo ijapokuwa hukwenda shule utaona ugumu wa maisha ulivyo na ndio maana sio waislamu wote wanapenda kikwete arudi madarakani na ccm yake narudia tena huyo jamaa ni mngese sana na nadhani hana hata akili za kuzaliwa mpambafu kabisaa
 
Ndugu zangu Waislam kwa kweli tunatia aibu wakati mwingine. Kuna maswala ya kidini na maswala yanayotuhusi sisi wote kama waislamu na wakristo. Kwani wanaodhulumiwa ktkt nchi hii ni wakristo peke yao ambao wako ktk chama cha CHADEMA. Kwani waislamu pekee yao ndo wako ktk chama cha CCM, mbona kuna wakristo wako ktk CCM.Mbona mie nilimpigia Slaa nikiwa kama ni Mwislamu!! Lowasa ambae tunamlilia hapa kuharibu kula yuko CCM nae ni Mwislamu? Lewisi Makame anaeendelea kuharibu kila kitu nae ni Mwislamu. Tujalibu kutoa hoja na tusiangalie ni nani katoka dini gani. Kwani wanao msapoti Kikwete wote ni waislamu? Kusini Songea kuna wakristo kibao ambao wamempigia Kikwete. Utasemaje mwenzangu.

Alifu Bee Tee Thee Jim He Khe Dali Dhali Re Ze Sini Shini Swadi Dhwadi .........Lam........????:smile:
 
Shule Jamaa wamekwenda. si mbumbumbu kama kiwete. hiyo ndo njia.
there is not freedom without cost. let us free ourselves from ccm oppression.
Change never by siting and singing we will overcome. change costs. dare not how much will cost us. w
we need respect: ccm must respect the decision of millions of Tanzanians who decide to go for change.
Katika historia ya dunia nzima hakuna mageuzi yaliyokuja bure bure tu!! kuwa namageuzi ya kweli lazima tukubali cost yoyote itakayo tupata. nawapa mfano mzuri mdogo.. wazanzibar iliwacost 2000 leo hii wanaheshimiana. wakenya 2007 ilwakost leo hii kuna utulivu. Kwa hiyo ndugu zangu tusife moyo. tusiogope vitisho. haki utafutwa, haki hupiganiwa. hata damu ikimwagika, lakini wajue kuwa ni hao hao Kikwete na wenzake ambao watakuwa chanzo. lete the world see. let the world witness and know that Kikwete is the DICTATOR:
huko anakojivunia kuwa watamsaidia wakuuwa watanzania, nako kumesha gawanyika. tutapata support kubwa mno. Kila mtanzania aliye na macho ya kuona na masikio ya kusikia ameyaona na amesikia jinsi gani kikwete na wenzake ambao wanajiita wasomi lakini bado wanatumika kukandamiza haki za watu. hii ni Karne ya 21. lazima ujue hivyo baba. soma maandiko, ujue alama za nyakati. Watanzania tujue kuwa hata French revolution haikutokea tu. they paid for it.
Watanzaia tuamke.


Mtu ameshindwa hataki kushindwa, huyo ina maana alikuwa na lake jambo. Haimsaidii kitu kwenda kwa waandishi wa habari km ana ushahidi aupeleke NEC wakafanye reconciliation. MATOKEO YA MITAANI HATUYATAKIIIIIII, KUWENI WAPOLE MMESHINDWA, HAMNA JIPYA KILA UCHAGUZI SABABU NI HIZO HIZO, HIZO CHANGES KWA WAKATI HUU WATANZANIA WAMEZIKATAA JARIBUNI WAKATI MWINGINE WA 2015 KAMA WA TZ WATAKUWA WAKO TAYARI.
 
Nashauri mtoke kwenye Internet, muone waTanzania wa kawaida wanaendelea na magumashi kama kawaida. Ukiingia Jambo Forum unaweza kuona kama nchi italipuka muda wowote. This place hypes kila kitu, hata upuuzi.

For my health sake. Napumzika humu ndani. Joto na jazba za siasa zikipungua--InshaAllah tutaendelea kuchangia mada.
 
Labda mimi akili yangu haina akili vizuri, lakini swali linalonisumbua ni je kwa nini matokeo ya urais hayatangazwi majimboni ilihali katika kila kituo, jimbo kuna wawakilishi wa vyama na wanapewa nakala za matokeo?????????????????

Halafu Makame anakuambia matokeo wanayotangaza sio yale yaliyoko vituoni,,,, ni yaliyohakikiwa na NEC... What a shame.... wanatudanganya kama watoto????? Hii haikubaliki:nono:
 
Back
Top Bottom